Sio hivyo kaka,kuna maana gani kuwa na rais lets say kutoka chadema wakati bunge linatawaliwa na ccm?
Natambua uhuru wa watu kushift ideology zao, lakini suala la msingi wanadhamira za dhati kweli? Wanashift kwa ajili ya maslahi ya nani?? Maslahi binafsi au ya chama? Wakishindwa wakati huu, watavumilia kuendelea kuwa upinzani au ndiyo watarudi walipotoka?Kwanza tuanze na ni tendo la demokrasia kuwa na vyama vya upinzani, pili people are entitled to shift their ideologies therefore partisan disalgnment is part of that democracy.
Cha kujiuliza kwa nini upinzani inachukua hii mitumba ambayo imeshindwa in the first place huko ilipotoka wakati wanaelewa kuna fouls kwenye campaign and all the shenanigans associated na chama cha majambazi. Mi nadhani yeyote anaetokea CCM kipindi hichi ana nia na mageuzi bali tumbo lake. CCM ingempa guarantee hiyo iwapo angetueliwa, sasa kipindi hiki (baada ya kuwashinda huko CCM) ndio wanakimbilia upinzani as a backup plan.
To simplify the 'lot', Tambwe Hizza is a perfect example of these group. Maslahi ni binafsi hapo amna lolote in my opinion.Natambua uhuru wa watu kushift ideology zao, lakini suala la msingi wanadhamira za dhati kweli? Wanashift kwa ajili ya maslahi ya nani?? Maslahi binafsi au ya chama? Wakishindwa wakati huu, watavumilia kuendelea kuwa upinzani au ndiyo watarudi walipotoka?
Nakubaliana na wewe kabisa. Nadhani umefika wakati sasa wananchi wawe na nguvu kubwa ya kuwaadhibu wawakilishi wao. Wengi wa wawakilishi kiukweli kabisa wanawaza matumbo yao. Hawa watu wapo upinzani na hata kwenye chama cha siasa. Lau wananchi wangeweza kuwawajibisha vyema watu hawa siasa isingekuwa chaka kama lilivyosasa. Maana kwenye siasa kuna kila aina ya uchafu hasa kwenye nchi nzetu.Siasa ni mchezo wa ubinafsi ,individualism, maslahi binafsi na makundi. Huwezi kuondoa hizi vices kwene siasa, ndio maana mara kadha wa kadha tunashuhudia mivutano tu lakini nia ya msingi ya kuwatumikia wananchi ikikanyagwa bila aibu. Matokeo yake ndio hivo maendeleo sufuri.
Mkandara kwa siasa za vyama vingi vya upinzani, kuing'oa CCM madarakani ni ngumu saaana. Huu ni ukweli ingawa tukiutamka kinadharia watu wanaona hao ndiyo walewale lakini kivitendo ukweli ukweli huu haufichiki. Kiukweli upinzani unahitaji wenye ushawishi mkubwa na dhamira ya dhati ya kutetea maslahi ya Watanzania ambayo kwa muda mrefu yamekuwa hayapewi kipaumbele. Lakini nguvu ya upinzani haitakiwi itokane na political failures. Wengi wa hawa watu hawana msimamo. Ni watu ambao wakiwa upinzani wanasikilizia hali ya upepo kwenye chama Tawala. Sio watu wa kuaminika. Wapo watu hukohuko kwenye upinzani, wamekuwepo muda mrefu na wanadhamira ya dhati licha ya ufinyu wa raslimali lakini lengo kuu kwao hasa ni mapinduzi. Hawa watu wanakili kwa moyo kwa dhati hasa na hata matamshi ya ulimi wao yanatanguliwa na dhati hiyo. Upinzani unatakiwa ubebe sera na usimamie unachokiamini bila ya kujali idadi ya watu wenye dhamira hiyo. Ni bora kuwa na kundi la watu wachache wenye dhamira madhubuti na ya ukweli kuliko wengi ambao wamejaa ubinafsi, chuki, tamaa na ukigeugeu.Wakuu zangu hakuna sheria yeyote inayoweza kumkataza mtu asijiunge na chama kingine kwa sababu tu alikuwa CCM. Na tukifuata imani yenu nadhani asilimia 100 ya viongozi wote wa Upinzani pamoja na wanachama wake wengi walitokea CCM na sii ajabu walikihama chama baada ya kukutana na wakati mgumu kama hawa tunaowabeza hapa.
Swala sii kujiunga ama kupokelewa kwao isipokuwa ni kitu gani wanakileta Upinzani badala ya wanategemea nini kutoka vyama vya Upinzani!. Binafsi nitathamini kile wanachokileta ktk chama kuliko kile wanachokitegemea kutoka ktk chama kwani hawa wa kuja hawakushika mpini wa shoka..Na sidhani kama vyama vya Upinzani ni wajinga kiasi hicho yaani wampe mtu uongozi pasipo kuchunguza uwezo wake kuongoza au hata kukipatia chama ushindi.
Wapo wana CCM walioshindwa kwa mbinu chafu na hakika Ukiwatazama soko lao ktk jimbo ni kubwa sana kuliko wale waloishinda, hivyo vyama vya Upinzani vinaweza kutumia penyo (makosa) kama hizi kuchukua majimbo ambayo hadi sasa hawana mgombea mwenye nguvu ya ushawishi. Na hakika wengi wanaokimbilia vyama vya Upinzani baada ya kushindwa CCM ni opportunist, yet again kwa siasa za Bongo - who isn't!..
Ni viongozi wa vyama vya Upinzani wanaoweza kutoa maamuzi ya mwisho nini nafasi ya huyu kiongozi na sii kiongozi aliyejiunga kuweka masharti yake ya kujiunga..Chadema we don't shake hands with devils - Unatakiwa kukiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kuwa mfuasi wa itikadi na utakubali maamuzi ya viongozi wako kulingana na itikadi..Hivyo kwa yeyote anayejiunga he or she is just a believer (member of the party) like many others..
Mimi naamini kabisa kwamba huu ndio wakati wa CCM kuvurugika, ni wakati wa wanaCCM wengi kusoma alama za nyakati kwamba muda wao wa siasa za mwalimu umekwisha, huu ni wakati wa Ufisadi kwa kwenda mbele hivyo chaguo ni lako..Na maadam ni wao wanakuja batizwa na kuukana Ufisadi sidhani kama watapata nafasi ya kuvuruga ibada za vyama hivi zinazoongozwa na kulaani Ufisadi..
Kwa kawaida vituko, kashfa, rushwa na mizengwe kwenye chaguzi za Tanzania imekuwa ni kawaida. Mara nyingi yule anayeweza kucheza siasa za rafu kwenye chaguzi za ndani ya CCM yeye ndio huibuka mshindi. Kwahiyo kwa wale wasioweza rafu, wanaoamini kwenye uadilifu na ukweli kwao kuweza kuongoza kupitia chama tawala ni kitu ambacho hakiwezekani au ni kigumu saaana. Sina hakika km yupo/wapo wana CCM ambao wamepitishwa kwenye chaguzi zao bila kufanya mizengwe hata kidogo. Matokeo yakitangazwa kwenye chaguzi hizo, mambo mengi hujitokeza. Wengine huamua kuunda makundi na kimya kimya kuunga mkono wagombea wa upinzani na wengine huamua kuhama chama kabisa. Na hapa ndio kwenye mjadala.
Hivi karibuni wagombea wengi wa CCM wamelalamikia kuchezewa rafu na wengine kuahidi kuhama vyama. Na hii sio mara ya kwanza wapo wengi huko nyuma waliowahi kufanya hivyo km mh Njelu Kasaka, (CCM-CUF-CCM) na wengineo. Lakini pia suali la msingi la kujiuliza, linabaki nini hasa lengo la vyama vya upinzani??? Je, lengo ni kuwa na uwakilishi mkubwa bila kujali aina ya watu waliopo upinzani au lengo ni kukidhi haja ya maendeleo ya Watanzania? Km lengo ni kuleta maendeleo kwa Watanzania basi lengo hilo linakinzana na aina ya watu wanaohamia kwenye vyama hivi si kwa sababu ya sera za upinzani bali ni kwa sababu wanadhani wanawaadhibu chama Tawala. Ndugu wanaJF, kwa mtindo huu, je kuna dhamira ya dhati kutoka kwa baadhi ya Watanzania wenzetu kujikomboa katika ufisadi na umasikini uliokithiri??