I have said this before and I will say it again, majina ya vyama vya wapinzani should only be on paper lengo lao liwe 1 permanently getting rid of CCM. Hii haitawezekana kama wapinzani watapondana na kurushiana maneno kila wakati.
Kwa nini unatilia mashaka kuhusu wanaCUF ndugu?
Mkuu nadhani hapa unapotosha kidogo..Mimi na wewe hatufahamu kilichotokea baada ya vyama hivi kufikia maafikiano kisha wakageukana..Ni baada ya kugeukana, sijui kama CCM ilihusika au laa ndipo vyama hivi zilianza mashambulizi baina yao wenyewe kwenye hizi chaguzi ndogo. Nakumbuka ni Chadema waliweka mgombea Mbeya vijijini dhidi ya CUF....Chadema pia waliweka mgombea somewhere huko usukumani dhidi ya TLP na Mrema akapiga kelele sana. CUF na TLP nao wakaweka wagombea wao huko Tarime na sehemu mbili nyingine za Chadema.Mara kadhaa nimeona wapenzi/washabiki/wanachama wa CUF wakikishambulia CHADEMA kuliko vyama vingine ikiwemo hata CCM!
Mfano mzuri ni uchaguzi mdogo wa Mbeya Vijini ambapo CUF kiliweka pingamizi dhidi ya mgombea wa CHADEMA, Shitambala. Pamoja na mgombea huyo kujitoa bado CUF kiliendelea kukilaumu CHADEMA ambacho kilikuwa nje kuliko CCM ambayo walibaki nayo kuchuana. Humu JF tumeona thread zikidai kuwa CUF ina sifa kadhaa ukilinganisha na CHADEMA! Sijui kwa nini walinganishe na CHADEMA badala ya TLP, NCCR, etc?
Swali la kujiuliza: Hivi CUF ni chama cha upinzani kwa CHADEMA tu?
Tusubiri vitendo, sio maneno tu ndugu yangu! CCM Zenj na CUF ndio wanalala ndani ya net moja sasa hivi! Madaraka matamu acha mchezo bwana!Mi ninavyoamini haukuna ugomvi wala upinzani kati ya CUF na CHADEMA ni CCM tu hao wanaojaribu kuzusha zusha na kuleta uchonganishi kwa makusudi ya kudhoofisha vyama hivi ambavyo vinashirikiana vizuri katika kujenga siasa za ushindani, sijapata kuona hitilfu wa switafahamu za hivyo baina ya vyama hivi, tungewaomba nyinyi CCM mtazame ya kwenu zaidi kuliko ya wenzenu, yenu mengi tu hamuyaoni, mnaghushi, mnaiba, mnafanya kila ufisadi...hamuoni kuwa huu ni ugomvi kati yenu na wananchi mnaojidai wamekuchaguweni kwa kukubali ilani yenu...?
Shughulikeni na hayo kwnza ya CUF na CHADEMA hamuyawezi wakati ya CCJ hata hayajakaa vizuri yanawakosesha usingizi.
Profesa Lipumba: Ah, Ushirikiano bado upo. Kwa mfano, ushirikiano wetu na TLP na NCCR Mageuzi bado mzuri sana. Lakini bado hatujajiweka vizuri pia katika Bunge.
Wabunge wetu bado wanaendelea kushirikiana, kambi ya upinzani bado inaendelea kuwapo kwa hiyo hatujayaweka mambo haya uzuri kwamba kanuni zetu ziwepo. Halafu pale tatizo jingine (CHADEMA) wameshafikia maamuzi kwamba hawawezi kushirikiana na vyama vingine.
Hilo ni wazi kwamba wao (CHADEMA) kushirikiana na NCCR-Mageuzi wanaona kwamba hilo ni jambo haliwezekani au kushirikiana na TLP ni jambo ambalo haliwezekani. Sasa katika hali hiyo ya kutoaminiana, sintofahamu hiyo inakuwa mbaya.
source
Haki Sawa kwa Wote
Kama anakubali JK anafanya vizuri kila kitu, anafanya nini upinzani? Au hajui analosema??
Mkuu NN, kwa kweli upinzania Tanzania unasikitisha sana. Huyo Mrema na Cheyo wameshadhihirisha kwamba wao ni mamluki wa CCM na walijifanya ni wapinzani ili kuhakikisha wanavuruga juhudi zozote za upinzani kujiimarisha ili kuiondoa CCM madarakani. Kwa hali hii ya CCM kuwapandikiza mamluki miongoni mwa wapinzani, itawachukua wapinzani miaka mingi ijayo kuweza kujiimarisha na kuweza kupambana na CCM, nilikuwa naupinga sana ule usemi kwamba CCM itatawala Tanzania milele lakini sasa naona una ukweli kutokana na njama za CCM kufanya kila wawezalo ili kuudhoofisha upinzani.QUOTE]
Halafu mnasema wapinzani waungane what is common amongst you ? CCM wamefurahi kila mtu leo mkutanoni anasema hata upinzani unamkubali inabidi waelewe kuwa Mrema sio mpinzani hata siku moja
Mkuu kwani CCM wakifanya jambo jema huwezi kuwasifia?Halafu mnasema wapinzani waungane what is common amongst you ? CCM wamefurahi kila mtu leo mkutanoni anasema hata upinzani unamkubali inabidi waelewe kuwa Mrema sio mpinzani hata siku moja
Mkuu kwani CCM wakifanya jambo jema huwezi kuwasifia?