Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Upelelezi umemshinda nini?

Jibu hili swali bwana mrema..

1. Kadi ya ccm ulisharudishaga? Na kama bado utarudisha lini? Na mtu mwenye unachama ktk vyama 2 anaitwaje?

2. Just for curiosity ...unaweza kustaafu kazi ya ushushu ukishikilia nafasi nyeti za juu kitengoni kwenu(usalama wa taifa)? yaani kama ya marehemu kombe
 
Mkuu Shiumiti Cheo cha naibu waziri mkuu kiliwahi kushikwa na Salim A Salimu
Thanks bwana Ngongo...... itakuwa ilikuwa mwaka 1984 au 1985 hivi wakati Hayati Sokoine katutoka...
THANKS KAKA....KWELI UNA KUMBUKUMBU..
 
mrema kwa kuchanganya habari ndio mwenyewe.mimi ushauri wangu viongozi wote wa kubwa wa vyama vya upinzani wagombee ubunge kwenye majimbo yao.wakishapata nguvu bungeni ndio waangalie swala la kusimamisha mgombea mmoja lakini kwa sasa hivi watakuwa wanajenga na kubomoa wenyewe tu.
 
hii inaonesha ni jinsi gani hivi vyama vya upinzani au viongozi wake walivyokua awana muelekeo maalum. sasa bwana mrema anataka wengine wasigombee kuwa ili chama chake kiwe na nafasi ya kupambana na CCM basi waungane kama ni hivyo let me guess yeye vilevile ndio awe chairman wa hivyo vyama vikiungana kwa sababu ameshaanza kujipamba yeye ndio aliyechukua kura nyingi so far katika uchaguzi na kwa mujibu wake yeye ndie alitakiwa achukue urais wakati yupo CCM, yeye ndio mwenye experience high office position. embu punguza mdomo bwana Mrema, agenda ya TLP inasimamia nini tena aieleweki.

Mungu Ibariki Tanznania
 
Thanks bwana Ngongo...... itakuwa ilikuwa mwaka 1984 au 1985 hivi wakati Hayati Sokoine katutoka...
THANKS KAKA....KWELI UNA KUMBUKUMBU..

Hivyo si Naibu bali "kaimu" ,Mrema bado anakuwa Naibu wa kwanza kwani kikatiba hadi sasa cheo hicho hakipo.Salimu alikaimu kwa muda cheo cha uwaziri mkuu.
 
Leo hii ndio Mrema anayaona haya?..

Hivi ameshindwa kukumbuka kwamba Upinzani walianza vizuri sana kuwa pamoja ktk maswala mengi lakini mara tu Uchaguzi wa Kiteto ulipofika ni wao waliwageuka Chadema.. Mgombea wa Chadema ndiye alikuwa na nafasi kubwa zaidi kwani mgombea wao ndiye alichukua nafasi ya pili uchaguzi wa mwaka 2005....Hakuyaona hayo!.

Baada ya Kiteto, tukaenda Tarime, ambako Wangwe alikuwa mshindi mwaka 2005, je, ni nani alotakiwa kuungwa mkono kama sio tena Chadema!..Yale yale wao wakazua kila ubaya kwa Chadema na hasa hawa viongozi wa juu wa vyama vya Upinzani macho yao sii ktk majimbo ila ni nani atakuwa Jemedali mkuu siku ya siku itakapo fika..Kweli huwezi pigana vita bila Jemedali lakini mbona CCM wanaweza tuma tingatinga wao ktk kila Uchaguzi na haihusiani kabisa na nani atakaa meza kubwa siku ya siku!...

Imeshindikana kote kutokana na uongozi wa juu wa vyama hivi kwa sababu kila mmoja wa hawa viongozi anataka yeye awe meza kubwa nina hakika kabisa kuwa Mrema, Lipumba na Cheyo hawa wanajiona wao kuwa bora na wenye CV kubwa kuliko Mbowe au mtu yeyote toka Chadema, pamoja na kwamba wote wapo meza kubwa..
 
Tatizo la viongozi wetu wa upinzani wanamipango mizuri sana kabla ya uchaguzi. Lakini uchaguzi unapofika kila mtu na lwake na kashifiana wenyewe kwa wenyewe.

NAJUUUUUUUUUUUUUTA KUUPENDA UPINZANI
 
Hivyo si Naibu bali "kaimu" ,Mrema bado anakuwa Naibu wa kwanza kwani kikatiba hadi sasa cheo hicho hakipo.Salimu alikaimu kwa muda cheo cha uwaziri mkuu.

Mkuu Mchizi Bwana Mrema aliwahi kuwa Naibu waziri mkuu na si Kaimu waziri mkuu.

Augustine Mrema alizaliwa mwaka 1945, huko mkoa wa Kilimanjaro Tanzania, katika kijiji cha Kilaracha kilichopo katika Wilaya ya Moshi vijijini akiwa mzaliwa wa pili katika familia ya watoto watano ya Mzee Lyatonga Mrema.

Elimu
Mwaka wa 1955 -1963 alianza masomo yake ya darasani mpaka shule ya kati katika Wilaya aliyopo huko huko mkoani Moshi vijijini. Ilivyofika mwaka wa 1964 mpaka 1965 Mrema alijiunga na Chuo cha Ualimu cha Mtakatifu Patrick. Tangu 1966 bwana mrema alikuwa mwanachama mkubwa wa CCM.

Baada ya kumaliza mafunzo yake ya Ualimu na kupata kazi Mrema alianza kuchukua mafunzo yake ya sekondari ambapo mwaka wa 1968 alifanya mtihani wake wa kidato cha nne, wakati huo mitihani ikitoka Chuo Kikuu cha Cambridge cha nchini Uingereza.

Mwaka wa 1970-71 alijiunga kwenye mafunzo maalumu ya siasa na uongozi katika Chuo cha Kivukoni na mwaka wa 1980 na 81 alienda nchini Bulgaria ambako alifanikiwa kutunukiwa Diploma ya sayansi ya Ustawi wa jamii na Utawala.

Kazi na Kujiendeleza Kielimu
Augustine Lyatonga Mrema baada ya hapo alifanya kazi mbalimbali za kijamii na kichama kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Pacific mwaka 2003 ambako ametunukiwa Shahada ya Sanaa katika Sayansi ya Jamii.

Bwana Mrema alianza kazi mwaka 1966-69 kama mwalimu akifundisha shule mbalimbali za mkoa wa Kilimajaro, ilopofika mwaka 1972 na 1973 aliteuliwa kuwa mratibu wa elimu wa Kata.

Mwaka 1974 na 1980 Augustine Lyatonga Mrema alichaguliwa kuwa mwalimu wa siasa katika wilaya mbalimbali kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi.

Mwaka wa 1980 na 1982 bwana Mrema alichaguliwa kuwa Mwalimu wa Chuo kikuu cha usalama wa Taifa na mwaka 1982 hadi 1984 bwana Mrema aliteuliwa kuwa Kaimu mkuu wa usalama wa Taifa kwa mkoa wa Dodoma, mwaka 1983 hadi 1984 aliteuliwa tena kuwa Katibu wa kikosi cha ulinzi na usalama makao makuu Dodoma.

Shughuli za Kisiasa
Mwaka wa 1985 Mrema alirudi katika Jimbo lake na kugombea Ubunge huko alipata ushindi mkubwa tu, lakini hata hivyo aliwekewa pingamizi na Mahakama Kuu ya Kilimanjaro na wakati kesi ikiendelea Mrema alipelekwa katika mkoa wa Shinyanga, Wilaya ya Kahama kuwa Afisa Usalama wa Taifa katika wilaya hiyo, ilipofikia mwaka 1987 alishinda rufaa yake na kurejeshewa ubunge wake.

Aligombea ubunge kwa mara nyingine mwaka 1990 na akafanikiwa kutetea jimbo lake tena safari hiyo kwa kishindo na akarudi bungeni kwa mara ya pili.

Baadae akateuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kwa mwaka wa 1990 hadi 1994, na wakati huohuo mwaka 1993 hadi 1994 aliteuliwa tena kuwa Naibu Waziri Mkuu cheo ambacho hata hivyo hakikuwepo kwenye Katiba ya nchi.

Ilipofika mwaka 1994 alibadilishwa Wizara hiyo na kuhamishiwa katika Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo.

Kujiengua na Chama Tawala
Mh. Mrema alijiengua na CCM mwaka 1995 na kujiunga na Chama cha NNCR - Mageuzi ambako huko alienda kuwa Mwenyekiti wa Taifa na mgombea Urais kupitia chama hicho.

Mrema ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Part (TLP) aligombea urais mara mbili hiyo ilikuwa mwaka 2000 kupitia (TLP), na akagombea tena 2005 kwa mara ya tatu kupitia chama hicho cha TLP.

Source: "http://sw.wikipedia.org/wiki/Augustine_Lyatonga_Mrema"
 
Mrema wee kampumzike Kiraracha uachie siasa wanaoweza. Eti kama ni urithi wa jimbo basi TLP inatakiwa kurithi Biharamulo. Sasa kama mwendo ulikuwa ni hivyo kwa nini walisimamisha kule Tarime. Hizi siasa za kurithisha jimbo kwa chama kilichopoteza mbunge kwa kifo zilianza lini. Kila mtu anao uhuru wa kushiriki katika siasa aidha kukampeni, kugombea/kupigiwa kura au kupiga kura. Haya sasa mambo ya urithi yanatoka wapi?

Umechoka katulie zako, waachie wengine maana muda wako naamini umekupa mkono. Still bado una haki ya kugombea, kukampeni au kupiga kura ila naamini umepishana tayari na alama za nyakati.
 
Kwanza Watanzania , hasa wale waliomshabikia sana Mrema mwaka 1995 (nami nikiwemo) katika azma yake ya kuwania urais tumshukuru sana Mwenyezi Mungu hilo halikutokea. Kama angeukwaa urais:

1. Hadi leo angekuwa bado rais, katiba ingebadilishwa naye kuwa rais wa maisha.

2. Wote wale waliomuunga mkono awali, na hasa wasomi, angewashtukia na kuwasweka jela na pengine hata kuaawa. angeitumia sana ile sheria ya kuwela wati kizuizini bila kufunguliwa mashitaka.
 
Haya ni maoni yangu kama upinzani wa Tanzania utataka kuimarika na hatimae kushika nchi siku moja. Baadhi ya mambo nina uhakika yata kuwa yamesha semwa na hata wao wenyewe kuyajua. Maoni yangu ni kama yafuatayo:

1.Asilimia kubwa ya Watanzania wapo vijijini(rural areas) na si mijini(urban areas). CCM ina nguvu kubwa vijijini na ndiyo maana ni rahisi sana kwao kushinda iwe kwenye ubunge au uraisi. Upinzani kila siku una lalamikia wizi wa kura kwa hiyo ngoja nitoe mfano. JK kaingia madarakani na zaidi ya 80% ya kura. Je kama ni wizi wangeiba kiasi gani hicjo mpaka ifike idadi hiyo na watu wasione? Ukiondoa malalamiko kidogo yaliyo tokea je hayo madai ya wizi wa kura ungetosha kupunguza asilimia za JK mpaka upinzani ushinde? Ukweli ni kwamba upinzani hauja wahi kushinda uraisi.

2.Jengeni hoja zenu wenyewe badala ya kuipinga tu CCM. Kila siku tuna wasikia upinzani wakisema CCM haija fanya hiki au CCM haija fanya kile, ni nadri sana kusikia upinzani kusema CCM tuta fanya hiki au kile. Kama siasa zenu ni za kupinga tu CCM basi ni bora kuendelea kuchagua CCM. Wananchi wata penda zaidi kusikia mtawa fanyia nini badala ya kusikia tu CCM ime shindwa kuwa fanyia nini.

3.Msianze kampeni wakati uchaguzi unapo elekea tu. Kila mwisho wa uchaguzi ni mwanzo wa mwingine. Jinadini miaka yote mitano ili wakati wa uchaguzi ukifika ham hangaiki kutafuta jinsi ya kuwa fikia wananchi wote. Elezeeni sera za chama chenu. Katika hili niwape pongezi Chadema na operesheni Sangala. Nadhani ni wachache sana hata kwa sisi tulio bahatika kuwa na access tu information tunao jua sera za upinzani. nime zoea tu kusikia kasoro ya sera za CCM ila sera zenu wenyewe hatuzi sikii.

4.Uraisi si njia pekee ya kui punguzia CCM nguvu. Kuna Bunge. CCM wana nguvu kwa sababu sera zozote wanazo tunga iwe kwa faida yao wenyewe au kwa faida la nchi ni lazima zita pitishwa na Bunge la CCM. Nadhani ingekua bora kwa upinzani kuji tahidi kwa sasa kuongeza idadi ya wabunge wao badala ya kung'ang'ania uraisi.

5.Viongozi wa upinzani msiwe ving'ang'anizi. Wengi wa wagombea uraisi kutoka upinzani ni wale wale tokea mwaka 1995. Wananchi nao wana wachoka kwa maana kila siku mna shindwa na mnaonekana kutokuwa na jipya. Jengine utamaduni wa kupokezana. Ukiona umeshindwa siyo vibaya kuwaachia na wengine.

6.Nguvu kubwa moja wapo ya CCM ni umoja wao wa vijana na jinsi wanavyo andaa viongozi wao wa baadae. Upinzani nao ushirikishe vijana wengi zaidi katika nafasi za uongozi katika chama. Leo hii viongozi wangapi wa upinzani mkiachia ngazi kuna vijana wa kuchukua nafasi zenu ambao wamesha anza kuandaliwa. Naona vijana wengi katika vyama vya upinzani wanaishia tu kuwa katika umoja wa vijana ila hatuwaoni wakiingia kwenye uongozi haswa wa vyama vyenyewe, sasa sijui huwa wanaishia wapi. Kuna vijana wengi sana wenye vipaji na uwezo na si wote wataenda CCM, ni kazi kwenu kuwa recruit hao vijana.

7.Badala ya kulalamika CCM wezi fanyeni tathmini ya ni jinsi gani mna kubalika. Mnaweza kufanya polls na survey mbali mbali kujua hali ya vyama vyenu. Na mfanyi zaidi utaiti kwenye sehemu ambazo hamna nguvu siyo sehemu ambazo mnajua matokeo yata onyesha mna pendwa sana. Kila baada ya uchaguzi fanyeni tathmini ni wape mmekosea na wapi mme fanikiwa na kwanini. kila baada ya miaka mitano angalieni mafanikio mliyo yapata na wapi pana hitaji nguvu zaidi.

8.Chungeni sana kauli zenu haswa muwapo mbele za watu. mara nyingi mnatoa kaulu au kufanya vitu ambavyo baadae mnakuja kuji contradict nyie wenyewe na mna poteza credibility. Mfano mzuri ni Zitto Kabwe na swala la Dowans.

9.Unganeni katika kuongeza nguvu zenu. Kutokana na hali halisi hamna cham kimoja cha upinzani kinacho weza kugawa rasilimali zake zote katika kila jimbo. Mkiungana na kuachiana majimbo kutokana na mgombea yupi au chama kipi kati yenu kina uwezo wa kushinda idadi yenu itaongezeka bungeni na hata kuwa tishio katika uchaguzi wa uraisi.

10.Shawishini watu wenye vipaji mbali mbali kujiunga nanyi. Kuna watu wengi wanao weza kutoa mchango mkubwa hata kama si wa kipesa. Kuna wasomi, kuna watu wanajua kuendesha kampeni, kuna watu wanajua kupanga mikakati, kuna watu wanajua kuandika hotuba nk.

Mtanzania yoyote mpenda maendeleo ata taka kuona upinzani wenye nguvu awe mwana-CCM au la. Checks and balances katika nchi yoyote ni muhimu.
 
Last edited:
Haya ni maoni yangu kama upinzani wa Tanzania utataka kuimarika na hatimae kushika nchi siku moja. Baadhi ya mambo nina uhakika yata kuwa yamesha semwa na hata wao wenyewe kuyajua. Maoni yangu ni kama yafuatayo:

1.Asilimia kubwa ya Watanzania wapo vijijini(rural areas) na si mijini(uraban areas). CCM ina nguvu kubwa vijijini na ndiyo maana ni rahisi sana kwao kushinda iwe kwenye ubunge au uraisi. Upinzani kila siku una lalamikia wizi wa kura kwa hiyo ngoja nitoe mfano. JK kaingia madarakani na zaidi ya 80% ya kura. Je kama ni wizi wangeiba kiasi gani hicjo mpaka ifike idadi hiyo na watu wasione? Ukiondoa malalamiko kidogo yaliyo tokea je hayo madai ya wizi wa kura ungetosha kupunguza asilimia za JK mpaka upinzani ushinde? Ukweli ni kwamba upinzani hauja wahi kushinda uraisi.

2.Jengeni hoja zenu wenyewe badala ya kuipinga tu CCM. Kila siku tuna wasikia upinzani wakisema CCM haija fanya hiki au CCM haija fanya kile, ni nadri sana kusikia upinzani kusema CCM tuta fanya hiki au kile. Kama siasa zenu ni za kupinga tu CCM basi ni bora kuendelea kuchagua CCM. Wananchi wata penda zaidi kusikia mtawa fanyia nini badala ya kusikia tu CCM ime shindwa kuwa fanyia nini.

3.Msianze kampeni wakati uchaguzi unapo elekea tu. Kila mwisho wa uchaguzi ni mwanzo wa mwingine. Jinadini miaka yote mitano ili wakati wa uchaguzi ukifika ham hangaiki kutafuta jinsi ya kuwa fikia wananchi wote. Elezeeni sera za chama chenu. Katika hili niwape pongezi Chadema na operesheni Sangala. Nadhani ni wachache sana hata kwa sisi tulio bahatika kuwa na access tu information tunao jua sera za upinzani. nime zoea tu kusikia kasoro ya sera za CCM ila sera zenu wenyewe hatuzi sikii.

4.Uraisi si njia pekee ya kui punguzia CCM nguvu. Kuna Bunge. CCM wana nguvu kwa sababu sera zozote wanazo tunga iwe kwa faida yao wenyewe au kwa faida la nchi ni lazima zita pitishwa na Bunge la CCM. Nadhani ingekua bora kwa upinzani kuji tahidi kwa sasa kuongeza idadi ya wabunge wao badala ya kung'ang'ania uraisi.

5.Viongozi wa upinzani msiwe ving'ang'anizi. Wengi wa wagombea uraisi kutoka upinzani ni wale wale tokea mwaka 1995. Wananchi nao wana wachoka kwa maana kila siku mna shindwa na mnaonekana kutokuwa na jipya. Jengine utamaduni wa kupokezana. Ukiona umeshindwa siyo vibaya kuwaachia na wengine.

6.Nguvu kubwa moja wapo ya CCM ni umoja wao wa vijana na jinsi wanavyo andaa viongozi wao wa baadae. Upinzani nao ushirikishe vijana wengi zaidi katika nafasi za uongozi katika chama. Leo hii viongozi wangapi wa upinzani mkiachia ngazi kuna vijana wa kuchukua nafasi zenu ambao wamesha anza kuandaliwa. Naona vijana wengi katika vyama vya upinzani wanaishia tu kuwa katika umoja wa vijana ila hatuwaoni wakiingia kwenye uongozi haswa wa vyama vyenyewe, sasa sijui huwa wanaishia wapi. Kuna vijana wengi sana wenye vipaji na uwezo na si wote wataenda CCM, ni kazi kwenu kuwa recruit hao vijana.

7.Badala ya kulalamika CCM wezi fanyeni tathmini ya ni jinsi gani mna kubalika. Mnaweza kufanya polls na survey mbali mbali kujua hali ya vyama vyenu. Na mfanyi zaidi utaiti kwenye sehemu ambazo hamna nguvu siyo sehemu ambazo mnajua matokeo yata onyesha mna pendwa sana. Kila baada ya uchaguzi fanyeni tathmini ni wape mmekosea na wapi mme fanikiwa na kwanini. kila baada ya miaka mitano angalieni mafanikio mliyo yapata na wapi pana hitaji nguvu zaidi.

8.Chungeni sana kauli zenu haswa muwapo mbele za watu. mara nyingi mnatoa kaulu au kufanya vitu ambavyo baadae mnakuja kuji contradict nyie wenyewe na mna poteza credibility. Mfano mzuri ni Zitto Kabwe na swala la Dowans.

9.Unganeni katika kuongeza nguvu zenu. Kutokana na hali halisi hamna cham kimoja cha upinzani kinacho weza kugawa rasilimali zake zote katika kila jimbo. Mkiungana na kuachiana majimbo kutokana na mgombea yupi au chama kipi kati yenu kina uwezo wa kushinda idadi yenu itaongezeka bungeni na hata kuwa tishio katika uchaguzi wa uraisi.

10.Shawishini watu wenye vipaji mbali mbali kujiunga nanyi. Kuna watu wengi wanao weza kutoa mchango mkubwa hata kama si wa kipesa. Kuna wasomi, kuna watu wanajua kuendesha kampeni, kuna watu wanajua kupanga mikakati, kuna watu wanajua kuandika hotuba nk.

Mtanzania yoyote mpenda maendeleo ata taka kuona upinzani wenye nguvu awe mwana-CCM au la. Checks and balances katika nchi yoyote ni muhimu.

Very Well Written! I support 100%
 
Umewasaidia mawazo mjarabu kabisa. Laiti wangeweza kukusikiliza wasingekosa kupiga hatua moja au tatu mbele.
 
Kazi ya kuiondoa Tanzania kutoka kwenye uongozi wa CCM uliojaa ubabaishaji ufisadi na ulaghai wa kiwango cha juu ni ya Watanzania wote. Naomba Watanzania wote tuondokane na ile kasumba ya kuketi na kuangalia kama tuko kwenye jumba la sinema. Kila mtu ajiulize ni nini wajibu wake kwenye hii 'vita' na 'apigane' kwa vitendo. Tuache kulalama kwa mdomo huku tumejiegemeza kwenye viti uvivu.
 
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/3036-nini-hatima-ya-upinzani-tanzania-37.html

I am an Alien from outer space. I reside in Galaxy but have been assigned to follow various developments in this planet and provide you with alternative solutions.

1. Opposition Politicians you must come out clean and put the interest of the country at hear before your personal interests. YOU MUST agree to sit on one table and come out with agreed policies and election manifesto for election. You must form one party. If u do that Tanzanians will support you.

2. Prof. Lipumba, Mbowe, Mbatia, Mrema etc, its time now to iron out your differences. Come out clean and put the interest of Tanzanians as a priority. Form a large party now and more than 50% of Tanzanians will support you. If you dont do that, winning the election will be a dream. You must network people in villages to a big extent. You also need to find the best candidate with clean records to stand out in elections. Its not necessary for all of you to stand for an presidential elections.

Going to SATURN PLANET, I will be back again.
 
Na ccm kununua shahada wapinzani wafanyaje ikiwa waliokamatwa wakinunua wanaachiwa bila hatua zozote kuchukuliwa?
 
Kazi ya kuiondoa Tanzania kutoka kwenye uongozi wa CCM uliojaa ubabaishaji ufisadi na ulaghai wa kiwango cha juu ni ya Watanzania wote. Naomba Watanzania wote tuondokane na ile kasumba ya kuketi na kuangalia kama tuko kwenye jumba la sinema. Kila mtu ajiulize ni nini wajibu wake kwenye hii 'vita' na 'apigane' kwa vitendo. Tuache kulalama kwa mdomo huku tumejiegemeza kwenye viti uvivu.

Mkuu hapo umemaliza yote, ikiwa kila mtanzania ataamka akafanya sehemu yake, bila kusubili nani amfunge paka kengele tuta fanikiwa.

Hata hivo tunaposema wapinzani wafanye hivi, wameshindwa.. hivi wapinzani ni akina nani? kwani wanatoka sayari ya jupita ama wanatokea nchi jirani kwa ajli ya kutuletea ukombozi?

Kama tunaona kwamba ili kujinasua mikononi mwa mafisadi wa CCM ni kwa njia ya kuwa wapinzani, basi wote tujiunge upinzani, na tufanye sehemu yetu, si tukae nyuma ya pazia tubaki kuwa nyooshea vidole wachache wanao thubutu! Ni kazi yetu wote na hakika tukishirikiana tutawashinda!
 
Nakubaliana na wote waliosema kila Mtanzania ana takiwa kufanya sehemu yake. Lakini je na hao upinzani siyo Watanzania? na wao hawana nafasi ya kucheza? ukombozi Watanzania tunaweza kuji letea wenyewe lakini nani wa kutu saidia kuweka mazingira ya ukombozi? Si serikali na bunge? Ukweli usio pingika ni kwamba chama ndiyo kina ingia madarakani kutuongoza kwa hiyo vyama vyote vina a big role to play for Tanzania. Kila nchi ina watawala na watawaliwa na ni kazi yetu Watanzania kuhakikisha every potential mtawala(including vyama vya upinzani) vipo katika mstari. tupendi tusipende nchi ni lazima iongozwe na chama kimoja au kingine na hivi vyama vina nafasi kubwa katika kuleta maendeleo ya Watanzania.
 
Kazi ya kuiondoa Tanzania kutoka kwenye uongozi wa CCM uliojaa ubabaishaji ufisadi na ulaghai wa kiwango cha juu ni ya Watanzania wote. Naomba Watanzania wote tuondokane na ile kasumba ya kuketi na kuangalia kama tuko kwenye jumba la sinema. Kila mtu ajiulize ni nini wajibu wake kwenye hii 'vita' na 'apigane' kwa vitendo. Tuache kulalama kwa mdomo huku tumejiegemeza kwenye viti uvivu.

Hata hivo tunaposema wapinzani wafanye hivi, wameshindwa.. hivi wapinzani ni akina nani? kwani wanatoka sayari ya jupita ama wanatokea nchi jirani kwa ajli ya kutuletea ukombozi?

Kama tunaona kwamba ili kujinasua mikononi mwa mafisadi wa CCM ni kwa njia ya kuwa wapinzani, basi wote tujiunge upinzani, na tufanye sehemu yetu, si tukae nyuma ya pazia tubaki kuwa nyooshea vidole wachache wanao thubutu! Ni kazi yetu wote na hakika tukishirikiana tutawashinda!

Wakuu macho_mdiliko na Rwabugiri nawapa asante kwa maoni yenu. Kama kuna kitu kinachonikera kikweli kweli ni misimamo na maoni ya watu kama MwanaFaslsafa1. MwanaFalsafa1 anadai kuwa CCM ina nguvu kubwa vijijini na ndiyo maana ni rahisi sana kwao kushinda iwe kwenye ubunge au uraisi, je kwa nini wameweza kushinda nafasi zote za Ubunge mjini Dar es Salaam. Kwa nini yeye MwanaFalsafa1 licha ya kuwa na uelewa kuliko hao wa vijijini bado anakaa pembeni na eti kuwashauri wengine namna ya kuiondoa CCM.

Yaonekana
MwanaFalsafa1 anaridhika na uongozi wa CCM nchini uliojaa ubabaishaji, ufisadi na ulaghai wa kiwango cha juu na kama ni hivyo kwa nini ashauri namna ya kuiondoa CCM ? Na kama haridhiki na hali hii kwa nini akae pembeni kusubiri watanzania wengine (yeye anawaita wapinzani lakini mimi nawaita wazalendo wenye uchungu na taifa lao) ndio walikomboe taifa ? Kama ni unafiki, hapa MwanaFalsafa1 anaonyesha kiwango cha juu kabisa kama walivyo wengi wanaotetea status quo.

MwanaFalsafa1 anatetea kuwa wizi peke yake hauwezi kuwanyima wazalendo ushindi lakini anasahau kuwa huo wizi ni sera ya CCM inayolindwa na dola. Hiyo asilimia 80% ni idadi ya walioweza kupiga kura kama ilivyotangazwa na dola kwa mdomo wa kinachoitwa tume ya uchaguzi. Je, ni asilimia ngapi ya watanzania walinyimwa fursa ya kupiga kura ama kwa shahada zao kununuliwa, vitisho vya dola, rushwa, wizi, udanganyifu, ulaghai na uzembe wa wasimamizi wanaoteuliwa na CCM.

Tuache kudanganyana hapa, ama umepiga kambi kwenye bonde la kashfa na harufu ya uvundo si tatizo tena kwako au uko kando na unakerwa na hiyo harufu kiasi cha kusogea mbali.
MwanaFalsafa1 ameamua kulifanya hilo bonde kuwa makao yake ya kudumu na kwa kuwa katiba inalinda kuwepo kwa bonde haoni kasoro yoyote na kuwepo kwake. NI lini tutakuwa wakweli kwa nafsi zetu na kutambua nguvu halisi alizonazo hili zimwi la CCM. Kila siku tunashuhudia haya mambo hadi kwa jirani zetu lakini hatujifunzi, tuna nini ?

Mtanzania yoyote mpenda maendeleo ata taka kuona upinzani wenye nguvu awe mwana-CCM au la. Checks and balances katika nchi yoyote ni muhimu.

Huu ni ulaghai - CCM ingetaka kuona upinzani wenye nguvu, hivi sasa tungekuwa na katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na dola inayofanya kazi bila uonevu, upendeleo na kwa maelekezo ya CCM. Kwa hali hiyo vitendo tulivyovishuhudia Busanda havingepata nafasi.
MwanaFalsafa1, unajua hatari ya kila chama kuunda kikosi cha vijana,
je, umesikia walichokuwa wanafanya vijana wa CCM huko Busanda ?

Back
Top Bottom