Shishye
JF-Expert Member
- Feb 26, 2009
- 269
- 1
Na uzoefu unaonyesha kwamba CCM haiwezi kutoka pale ilipo kutokana na kwamba Viongozi wengi wa vyama vya upinzani ni wepesi sana kurubunika na hela za Mafisadi kama tulivyoona hivi karibuni na bado naamini tutaendelea kuwaona.
CCM haiwezi kutoka kwa hiari, italazimishwa kutoka tu pale wanyonywaji tutakapoamka na ku-realize hali halisi ilivyo. Haishangazi baadhi ya wapinzani wananunuliwa na mafisadi maana ni strategy za CCM kuwadhoofisha. Wapinzani wenyewe njaa kali kama maskini yeyote mwingine wa nchi hii, na sisi wenyewe ndio wakwanza kuwatia majaribuni kwa kisingizio cha mafisadi. Kama hatuwaungi mkono kupambana na maovu, lazima wakate tamaa na kukubali kurubuniwa. Wanasema 'if you can't beat them, join them'. Tumewaona wengi ndio, na tutawaona wengi ndio, lakini mapambano yataendelea hadi siku iliyokubalika na mabadiliko yatatokea.