Kitu muhimu kwanza ni kuwaelewesha Wananchi walio wengi ,kuwa upinzani kwa hapa ulipo hauwezi kuleta maendeleo yeyote kwa mwananchi na yakaonekana, wananchi wanaweza kuhoji kwa nini hamjengi zahananti ,mahospitali na kila kitu japo iwe kwa kulipa lakini kwa bei nafuu ,jawabu ni kuwa Sultani CCM anatia mguu wake na kuzuia kwa hila za kila aina.
Pili wananchi waeleweshwe kuwa wataweza kupima maendeleo ya Wananchi pindipo watafanikiwa kuwakilishwa na wabunge wengi kutoka kambi ya Upinzani kwa maana asilimia kubwa ipatikane katika upinzani kiasi ya kuweza kutumia nguvu ya kura katika kupitisha na kupinga na vilevile nguvu ya uwingi katika kuhoji na kushinikiza bungeni.
Sasa hayo ni baadhi ya mambo ambayo upinzani utatakiwa uwajulishe wananchi kila wakati na kila kwenye mikutano ili mwananchi ajue kinachoendelea na kinachowasibu wapinzani hata ikawa hawaonekani katika kuendeleza maisha ya mwananchi,maana tunawasikia pembeni wananchi wakihoji upinzani haujatufanyia chochote na kura tunawapa,kunahitaji mwananchi huyu kueleweshwa ili kuilinda kura yake isirudi au isipotee kwa kukata tamaa,ni lazima aeleweshwe na aelewe.
Ikiwa kama nipo upande wa uwananchi ningependa Vyama vya upinzani kuwa na msimamo uliomkali rightwing,fundametalist,ngangari,usiotetereka usioyumba wala kuyumbishwa ,yaani hakuna mchezo wala kulegeza kamba ,tunaposema CCM ni mafisadi basi tuwachanganye wote ,hakuna kumuona mmoja ni afadhali kuliko mwengine,hilo napenda uwe msimamo wa Upinzani,kama upinzani ukisema serikali iliyopo madarakani inawalinda mafisadi basi ijumuishe vyombo vyote vya serikali bila ya kukibakisha hata kimoja,kwamba vyote havitendi sawa na kama kipo kinachodai kutenda sawa lakini utendaji wake haufuatwi ,ningeomba upinzani udai kujiuzulu kwa huyo anaesema maneno hayo ,kama tuliiimbia serikali ipambane na madawa ya kulevya na Saidi Mwema akasema kuwa mambo hayo si rahisi na kuna maneno aliongezea nimeyasahau,basi upinzani udai kuwa Saidi mwema ameshindwa kazi hafai na aondoke katika cheo hicho, kama kasi ya mauaji ya albino imezidi na Waziri husika haonekani kupambana na hali hiyo ,upinzani umvalie njuga na kumuumbua kila kona ya Tanzania hii kuwa ameshindwa kazi haina haja ya Raisi wala Waziri Mkuu kumtetea ,halikadhalika katika ujambazi ,na hivyo hivyo katika elimi na hivyohivyo katika afya ,Vyama vya upinzani ni lazima vipambane na vituo hivi vya serikali katika kudai hali ya maisha bora kwa kila Myanzania ,ni lazima nyenzo hizi zikandiwe na vyama vya upinzani bila ya kuvipa nafasi ya kupumua ,kwa lugha nyingine vipambane katika mazingira ya wizara na shughuli zake zinazoonekana hazipo hazionekani mbele ya wananchi ,kuna maji,umeme ,zahanati,walimu wenye taaluma,ulinzi wa raia ,tunaona majambazi wanatoka toka wanakotoka mpaka wanafika katikati ya jiji na kufanya ujambazi na kisha wanatoka ndani ya mji wakiwa hai ,hii inamaana security ni mbovu na ni ndogo.natumai nimeeleweka.