MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 847
Wakuu macho_mdiliko na Rwabugiri nawapa asante kwa maoni yenu. Kama kuna kitu kinachonikera kikweli kweli ni misimamo na maoni ya watu kama MwanaFaslsafa1. MwanaFalsafa1 anadai kuwa CCM ina nguvu kubwa vijijini na ndiyo maana ni rahisi sana kwao kushinda iwe kwenye ubunge au uraisi, je kwa nini wameweza kushinda nafasi zote za Ubunge mjini Dar es Salaam. Kwa nini yeye MwanaFalsafa1 licha ya kuwa na uelewa kuliko hao wa vijijini bado anakaa pembeni na eti kuwashauri wengine namna ya kuiondoa CCM.
Yaonekana MwanaFalsafa1 anaridhika na uongozi wa CCM nchini uliojaa ubabaishaji, ufisadi na ulaghai wa kiwango cha juu na kama ni hivyo kwa nini ashauri namna ya kuiondoa CCM ? Na kama haridhiki na hali hii kwa nini akae pembeni kusubiri watanzania wengine (yeye anawaita wapinzani lakini mimi nawaita wazalendo wenye uchungu na taifa lao) ndio walikomboe taifa ? Kama ni unafiki, hapa MwanaFalsafa1 anaonyesha kiwango cha juu kabisa kama walivyo wengi wanaotetea status quo.
MwanaFalsafa1 anatetea kuwa wizi peke yake hauwezi kuwanyima wazalendo ushindi lakini anasahau kuwa huo wizi ni sera ya CCM inayolindwa na dola. Hiyo asilimia 80% ni idadi ya walioweza kupiga kura kama ilivyotangazwa na dola kwa mdomo wa kinachoitwa tume ya uchaguzi. Je, ni asilimia ngapi ya watanzania walinyimwa fursa ya kupiga kura ama kwa shahada zao kununuliwa, vitisho vya dola, rushwa, wizi, udanganyifu, ulaghai na uzembe wa wasimamizi wanaoteuliwa na CCM.
Tuache kudanganyana hapa, ama umepiga kambi kwenye bonde la kashfa na harufu ya uvundo si tatizo tena kwako au uko kando na unakerwa na hiyo harufu kiasi cha kusogea mbali. MwanaFalsafa1 ameamua kulifanya hilo bonde kuwa makao yake ya kudumu na kwa kuwa katiba inalinda kuwepo kwa bonde haoni kasoro yoyote na kuwepo kwake. NI lini tutakuwa wakweli kwa nafsi zetu na kutambua nguvu halisi alizonazo hili zimwi la CCM. Kila siku tunashuhudia haya mambo hadi kwa jirani zetu lakini hatujifunzi, tuna nini ?
Huu ni ulaghai - CCM ingetaka kuona upinzani wenye nguvu, hivi sasa tungekuwa na katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na dola inayofanya kazi bila uonevu, upendeleo na kwa maelekezo ya CCM. Kwa hali hiyo vitendo tulivyovishuhudia Busanda havingepata nafasi.
MwanaFalsafa1, unajua hatari ya kila chama kuunda kikosi cha vijana,
je, umesikia walichokuwa wanafanya vijana wa CCM huko Busanda ?
Ndiyo maana nikasema kila mpenda maendeleo awe mwana-CCM au la ata penda kuona upinzani ukiendelea hapo umeshindwaje kuelewa? Sasa kama CCM hawaja fanya hivyo ndiyo maana nikasema mwana-CCM MPENDA MAENDELEO.
Acha kumisquote watu Mag3. Wapi nimesema kikosi cha vijana? Mimi naongelea umoja wa vijana ambao wata jiunga na mchakato wa siasa. Mimi nime ongelea vijana wenye vipaji kushirikishwa kwenye siasa sasa wewe hiyo kikosi cha vijana umetoa wapi? Soma vizuri uelewe hapa umeboa kabisa kwa sababu hauja fikiri kabla ya kuandika.
Baadhi ya mambo kwenye post yako umeandika bila kutafakari. it is obvious you wrote with passion rather than ration.