Mtu kutokupenda chakula flani wala hakuna ubaya wowote sema wanaochukia ugali wanawaona wanaokula ugali kama hawana akili, kwamba wao kuacha kula ugali ni ujanja na akili kubwa na wala ugali hawana akili, hapo ndio unashangaa.
Mtu haelezi madhara ya kiafya ya kula ugali bali anaponda tu ugali mbaya, wala wala ugali hawana akili halafu mtu huyo anajutanabaisha kwamba ana akili.
Ugali ni wanga, hauna kitu kingine zaidi ya wanga, mtu anaponda ugali eti hauna maana lakini anakwambia anapenda wali, unajiuliza huyu ndio alisema ana akili, maana ugali na wali, chips, mikate, tambi,na wanga nyingine zote ni wanga katika forms tofauti tofauti.
Stupidity is still common in Tanzania. Mtu ambae ameenda shule anajua samaki, nyama, maharage, mazao jamii ya kunde, maziwa nk vyote ni kutoa protini mwilini, wali, ugali, tambi na aina zote za nafaka ni kutoa wanga mwilini. Acha MCC waendelee kutawala tu.