Nimewatengenezea SOLDRAX: App ya kucheza na marafiki michezo ya Karata (Arubastini & LastCard) pamoja na Draft style zilizo maarufu Tanzania

kali linux

JF-Expert Member
May 21, 2017
1,996
5,054
Hello bosses and roses,

Kwa muda mrefu nmekua nafikiria namna ya kutumia tech kukuza na kuendeleza mwenendo wa maisha uliozoeleka hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla sababu Systems na Apps nyingi tunazotumia zimetengenezwa kufuata mazingira na utamaduni wa nchi za Ulaya, Amerika na Asia. Mfano mdogo ni hizi board games kama karata na draft, sana sana karata ni ngumu sana kupata apps unazoweza kucheza mchezo kama arubastini.

Miaka kadhaa ilopita nilitengeneza game la karata kwa hii michezo ya arubastini na Lastcard lkn kutokana na u-busy wa kazi ikawa ngumu kumaintain hio project.

Leo hii nawaletea App ya Soldrax ambayo utaweza kucheza na kushindana na marafiki zako katika michezo ya ARUBASTINI, LASTCARD, BRAZILIAN & SPANISH CHECKERS (aina hizi ndizo tunazocheza sana Hapa Tanzania)

Vile vile nitakua naorganize leagues kila baada ya muda fln ambapo washindi watazawadiwa pesa tasilimu na zawadi nyingine.

App inapatikana Google Playstore kwa jina la Soldrax, au bonyeza link hii Download Soldrax from Google Playstore kuipata moja kwa moja.

Kitu nilicholenga hapa ni watu kucheza dhidi ya watu, hivyo functionality ya mtu kucheza na BOT haipo kwa sasa (I hate&love AI).

Kwa sasa mtu anaweza kuhost match ya mchezo anaotaka kisha akatuma match ID kwa mwenzake na wakajoin na kuanza match. Au mchezaji mmoja anaweza kumualika mwingine moja kwa moja kwenye profile ya mhusika.

Vile vile app inakuruhusu kuangalia users waliopo online au waliokuwepo online muda mfupi ulopita kisha unaweza kuwa-alika (invite) kwenye mchezo wako.

Kama kawaida maoni yenu yanakaribishwa, kwenye app kuna link za Telegram, Instagram na Whatsapp so unaweza kunifikia moja kwa moja na kutoa recommendation, ushauri, critics, malalamiko etc...

Hapa chini ni baadhi ya screenshots.

Screen Shot 2023-03-22 at 12.02.17.png
Screen Shot 2023-03-22 at 12.01.29.png

Screen Shot 2023-03-22 at 12.09.56.png
Screen Shot 2023-03-22 at 12.08.02.png
Screen Shot 2023-03-22 at 12.03.40.png
Screen Shot 2023-03-22 at 12.02.41.png

Pia kuna group la telegram Soldrax Telegram Group na kuna channel SOLDRAX Channel humo utaweza kukutana na players wengine ukawa unaweza kuwaalika kwenye mechi zako au kushare Match ID kwenye group na wengine wakajoin.

Hii ni moja kati ya projects tano nlizopanga kufanya maalum kwa ajili ya culture ya Afrika mashariki na kati hasahasa Tanzania, napenda kutumia JF kudeliver mambo kama haya sababu JF imenipa karibu asilimia 40 ya wateja biinafsi nlofanya nao kazi, na pia kuna followers wangu huwa wananifuatilia kwenye mabandiko yangu ya tech na kuja PM lakini wanajiuliza kazi zangu ziko wapi? Kiufupi nadeal na internal systems ambazo ni mara chache kuwa exposed publicly lkn kwenye Apps kama hizi dipo naweza onyesha ujuzi wangu kwenye vitendo.

Karibuni....

kali linux
 
Nimeipakua! Interface ipo pouwa sana!

App ni nzuri ila ni nzito sana, labda inaweza ikawa kifaa changu cha kizamani

Sijacheza mchezo hata mmoja, huwezi cheza offline na inategemea opponent alie tayari, hapa ungeipa uwezo wa ku cheza na computer kama hakuna opponent online
 
Asante kwa feedback mkuu.

Uzito unaweza sababishwa na mengi lkn nnachoweza kusema ni kwamba App inatumia recent technologies so kama ni kifaa cha zamani utaweza kuona lagging mahala, pia package size ni ndogo, less than 4 mb. Lkn ntazidi kuboresha perfomance ya app

Kuhusu kucheza na BOT(computer) nafikiria kuongeza hio part japo lengo langu kubwa lilikua ni human to human interaction. Na ndio maana nikacreate Telegram group ambapo mtu unaweza join humo na kutuma ID ya game lako ili watu wakujoin, au pia unaweza muinvite directly mchezaji aliopo online sababu app inakuruhusu kuona watu waliopo online. Au unaweza kuwa na rafiki yako akakupa username yake mka-linkup na kucheza.
 
Ahaa! Sawa sawa! Ila part ya BOT iweke itasaidia kucheza offline maana unaweza kua sehemu ambayo network c rafiki kama kilangelanje ukajikuta upo bowadi
 
Back
Top Bottom