Kwanini Watanzania wengi hawapendi kucheza na kuwajali wanyama wanaowafuga?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Tanzania wanyama tunaoishi nao wanateseka sana kwakweli, ni kama vile waliumbwa na shetani wakati tumeumbwa nao na Muumba wetu alietupa mamlaka tumsaidie kuwatunza, Watanzania tunasali sana na kuomba dua ila ya nini hivi vyote kama hatupo tayari kuukubali uumbaji wa viumbe vingine vilivyoumbwa na Baba wa mbinguni / Allah?

Ni mwaka unaisha sasa paka wako hujawahi hata kumpa zawadi ya samaki mzima.

Ni mwaka unaisha sasa mbwa wako hujawahi kwenda buchani umnunulie kilo ya nyama umchomee ama umchemshie.

Mbuzi ama kuku umemnunua wa kumchinja, yafaa umtendee haki walau kwenye safari yake ya mwisho umuandali malazi safi, chakula na maji viwepo, kisha kesho yake umchinje, si sawa apigwe na mvua ama upepo wa el nino, chakula umbanie na maji anywe kwenye vyombo vichafu kisha kwa unafki eti umuombe Mungu kabla ya kumchinja.

Paka ama mbwa kakuzoea hujawahi hata kukaa nae sehemu kumpeti peti, akija unamwambia tokaa, yupo kwao tayari aende wapi?

Mbwa wako kakuzoea hujawahi hata kucheza nae michezo ya kukimbizana ama mpira

Mbwa yumo kwenye banda kila siku, hujawai kutembea nae hata siku moja jioni
 
Sijawahi penda Wanyama hata mmoja ,paka ,mbwa ,wote .....labda Kwa vile utotoni sikuweza kuishi navyo ...
Pengine wazungu na ufuska wao wote wamependelewa kiakili kwa kutambua kuwa Muumba wao ndie huyo huyo alieumba wanyama na kuwapa jukumu la kumsaidia kuwatunza wanyama.

Huku Afrika hali ni tofauti, mtu katoka kanisani / msikitini lakini akikutana na mbwa anamyupia jiwa, Ujinga mtupu !
 
Sijawahi penda Wanyama hata mmoja ,paka ,mbwa ,wote .....labda Kwa vile utotoni sikuweza kuishi navyo ...
Nilishawahi kufuga Mbwa na Paka toka wakiwa wadogo hawakuweza kupigana Wala kugombana,
walicheza Pamoja, maziwa walikunywa Pamoja ilikuwa ni burudani sana kuwatizama

Watu wengi waliokuwa wanakuja home walikuwa wanashangaaa sana ule urafiki wa mbwa na Paka😁
 
Nilishawahi kufuga Mbwa na Paka toka wakiwa wadogo hawakuweza kupigana Wala kugombana,
walicheza Pamoja, maziwa walikunywa Pamoja ilikuwa ni burudani sana kuwatizama

Watu wengi waliokuwa wanakuja home walikuwa wanashangaaa sana ule urafiki wa mbwa na Paka😁
Ni kweli kabisa mbwa na paka wakikua nyumba moja huwa wanazoeana bila shida.

Ila mbwa na paka ambao hawajazoeana wakikutana, hapo panaweza kuchimbika,
 
Kwaio kwa mfano case ya mbuzi, you mean, chakula nikakinunulie chakula tena?
Ni mnyama alieumbwa na Mwenyezi Mungu kama ulivyoumbwa wewe isipokuwa wewe ulipewa jukumu la kumhudumia kwasababu umebarikiwa uwezo mkubwa kiakili.

Nyasi saf za kutosha siku moja kwajili ya Mbuzi ni haki yake kwenye safari yake ya mwisho, na sio chakula tu bali anywe maji safi na malazi yake kama banda lisafishwe.
 
1. Tz watu wengi hawana disposable income(kipato-kodi) kubwa, tunasikia watu wengi wanaishi chini ya dola 5, dola 1 moja kwa siku. Kutunza mnyama ni jukumu na lina gharama zake, wenzetu mambele wana disposable income kubwa kwahiyo wana uwezo wa kutunza mifugo vizuri.... sio kuwalisha makombo.

2. Tuna tamaduni ya kuhusisha mifugo na uchafu, unakuta mtu hataki kugusa mbwa anaona kinyaa, hii ipo kwa watu wengi.... yaani pets na livestock sisi tunaona ni kama pests

3. Tusichokijua ni kwamba ukiishi na mnyama yeyote kuanzia akiwa kachanga, kuna biological process inaitwa imprinting, yaani anabond na wewe anakuona kama kiongozi/mzazi.... mahusiano kati ya binadamu na wanyama yanawezekana.

4. Kulingana na point ya 3, wabongo tushazoea kila mnyama ana kazi yake, ukiachana na wanaoliwa, mbwa ni wa ulinzi, paka wa kufukuza panya.... mambele kuna livestock, wanafugwa ili waliwe... na kuna pets, wanafugwa ilimradi tu kama company
 
1. Tz watu wengi hawana disposable income(kipato-kodi) kubwa, tunasikia watu wengi wanaishi chini ya dola 5, dola 1 moja kwa siku. Kutunza mnyama ni jukumu na lina gharama zake, wenzetu mambele wana disposable income kubwa kwahiyo wana uwezo wa kutunza pets vizuri.... sio kuwalisha makombo.
Hapana kwa hilo ninakupinga, wenzetu majuu wapo ambao waliochoka mbaya lakini kwenye suala la wanyama huwa wanajali kiasi cha kumuona ni mwanafamilia, mtu anaweza akawa kachoka mbaya lakini hawezi kuuza mbwa ama paka wake, binafsi mbwa ama paka wangu hata ulete milioni 5 siwezi kuzichukua nafsi itanisuta kwa usaliti.
2. Tuna tamaduni ya kuhusisha mifugo na uchafu, unakuta mtu hataki kugusa mbwa anaona kinyaa, hii ipo kwa watu wengi.... yaani pets sisi tunaona ni pests
Hii inachangiwa na uvivu wetu pia wa kutojali mazingira ya wanyama, banda la mbwa hujasafisha miaka unatagemea nini hapo hata kama unampeleka josho, hawa ni wanyama inabidi uwe dedicated angalau kwenye usafi wao, kusafisha banda kila mwezi si mbaya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom