Michezo ya Asia ya Hangzhou 2023 kuhimiza Asia kuelekea maendeleo ya pamoja, uwazi na mafungamano

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111456721132.jpg


Michezo ya 19 ya Asia inayofanyika mjini Hangzhou, China ni jukwaa kubwa zaidi la michezo barani Asia, na inafanyika kwa mara ya kwanza baada ya kusimamishwa kwa muda kutokana na changamoto ya COVID-19. Kwenye hotuba ya ufunguzi wa michezo hiyo, Rais Xi Jinping wa China alikumbusha kuenzi kauli mbiu ya Kamati ya Olimpiki ya Asia yaani “kusonga mbele daima” (Ever onward), na kufungua mustakbali zaidi ya njia ya Asia kuelekea maendeleo ya pamoja, uwazi na mafungamano.



Michezo ya Asia ni moja ya michezo mikubwa zaidi ya bara la Asia na duniani, ambayo maandalizi yake yana utatanishi mwingi hasa kutokana na wingi wa washiriki wa michezo hiyo ambao kwa mwaka huu ni wanamichezo 12,000, mbali na watu wanaojitolea zaidi ya 1,200, pamoja na wenyeji, watalii na watazamaji kutoka sehemu mbalimbali za Asia.



Wengi wa watu wanaofuatilia michezo hiyo, walisubiri kwa hamu kutazama sherehe ya ufunguzi wa michezo hiyo, kwani mara zote China inapokuwa mwenyeji wa shughuli kubwa za michezo kama hii, sherehe ya ufunguzi inakuwa na mvuto wa kipekee. Maonyesho yake sio kama tu yanatoa burudani, bali pia yanaonesha historia na teknolojia mbalimbali za kisasa za usanifu na ujenzi. Kwenye sherehe ya ufunguzi ya safari hii iliyoshuhudiwa na watu elfu 50, pia imekuwa na umaalum huyo. Kwenye eneo maarufu la Ziwa Magharibi la mji huo (Xihu Lake), uwanja mkuu michezo ulikuwa ukionekana kama ua zuri la yungiyungi linaloelea kwenye maji, na kuwa burudani nzuri kwa wale walioangalia kutoka nje wakati sherehe ya ufunguzi ikiendelea ndani.



Mbali na maajabu ya kiteknolojia yaliyotarajiwa na wengi kama vile taa za kisasa zinazotumia nishati kidogo, maonesho mbalimbali ya historia kwa mtindo wa 3D na wakimbiza mwenge wa kielektroniki, michezo hii inakuwa moja ya michezo mikubwa ya kwanza duniani kutokuwa na upigaji mkubwa wa fataki. Hatua hii inaonesha juhudi za waandaaji, sio tu kuzingatia usafi wa hewa bali pia kueneza mwamko wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, wakati ambapo dunia inakabiliwa na changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabia nchi.



Michezo hii pia imekuwa na umaalum wa China au tunaweza kusema umaalum wa Asia, kwa kuingiza michezo ya kielektroniki yaani E- Sports, ambayo mashabiki na wataalamu wa michezo katika sehemu nyingine za dunia, hawaichukulii michezo hii sawa na michezo inayoshindanisha uwezo wa mwili wa binadamu. Lakini michezo hii imekuwa ni michezo muhimu kwa watoto na vijana wa nchi zote za Asia, na imekuwa ni sekta kubwa yenye thamani kubwa kama ilivyo soka kwa nchi za Ulaya magharibi. Kwa mara ya kwanza wapenzi wa michezo ya kielektroniki wa Asia, wana nafasi kwenye michezo hiyo, kwani kutakuwa na medali.



Mbali na hayo michezo hii pia imeonyesha mshikamano kati ya nchi mbalimbali za Asia, kwani mbali na kutuma jumbe za wanamichezo kushiriki kwenye michezo hii, viongozi wakuu wa baadhi ya nchi za Asia wameweza kuja kushiriki kwenye sherehe ya michezo wa michezo hiyo.
 
Back
Top Bottom