Tanzania Kushirikiana na Morocco Katika Michezo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Morocco hapa nchini Mhe. Zakaria El Goumiri kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Morocco katika Sekta ya Michezo.​

Kikao hicho kimefanyika Septemba 13, 2023 katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salam ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro amewasilisha salamu za pole kwa nchi hiyo kufuatia Tetemeko la Ardhi lililopita katika nchi hiyo. Na kumhakikisha Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Balozi Zakaria El Goumiri amepokea salamu za pole kutoka Tanzania, ambapo pia amesema nchi yake itaiunga mkono Tanzania katika ujenzi wa miondombinu ya michezo ili kuendelea kukuza vipaji vya wanamichezo ambao watakuwa ni hazina kwa mataifa hayo kwenye timu za taifa.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Saidi Yakubu ambaye amesema ushirikiano wa Tanzania na Morocco katika sekta ya michezo ni wa kihistoria na kila mara nchi hizo mbili zimekuwa na mechi za kirafiki katika nyakati tofauti na hivi karibuni timu moja kutoka nchi hiyo itakuja nchini kucheza na timu mojawapo.

F55LQc2WAAAfiH8.jpg
F55LREzXgAAnSXM.jpg
F55LRsdXEAAAnYP.jpg
F55LSUUXkAAKRyr.jpg
 
Nawaza au tetemeko la ardhi huko Morocco ni kama ile vita ya Ukraine na Urusi mana kuna namna Ukraine mambo yanaenda kama kawaida hadi kushiriki michezo kimataifa
 
Uwanja wa Dodoma umeishia wapi?

Maana naona kunaibuka Hexagon mara tutasikia pentagon kigoma mara msambaba pemba!
 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Morocco hapa nchini Mhe. Zakaria El Goumiri kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Morocco katika Sekta ya Michezo.​

Kikao hicho kimefanyika Septemba 13, 2023 katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salam ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro amewasilisha salamu za pole kwa nchi hiyo kufuatia Tetemeko la Ardhi lililopita katika nchi hiyo. Na kumhakikisha Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Balozi Zakaria El Goumiri amepokea salamu za pole kutoka Tanzania, ambapo pia amesema nchi yake itaiunga mkono Tanzania katika ujenzi wa miondombinu ya michezo ili kuendelea kukuza vipaji vya wanamichezo ambao watakuwa ni hazina kwa mataifa hayo kwenye timu za taifa.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Saidi Yakubu ambaye amesema ushirikiano wa Tanzania na Morocco katika sekta ya michezo ni wa kihistoria na kila mara nchi hizo mbili zimekuwa na mechi za kirafiki katika nyakati tofauti na hivi karibuni timu moja kutoka nchi hiyo itakuja nchini kucheza na timu mojawapo.

View attachment 2747928View attachment 2747929View attachment 2747930View attachment 2747931
wee waziri mwenzako yupo msibani wewe unazungumzia michezo!!!!!! upo serious kweli????...huendi mbinguni!!
 
Back
Top Bottom