Nimewapiga wachawi—kipigo cha mbwa koko!

Next time waambie Malaika Wawa arrest, then Kwa Mamlaka uliyonayo amrisha wajitokeze mbele Yako.

Wakijitokeza vunja nguvu zao Kwa jina la Yesu, amrisha Ulinzi kwenye Nyumba Yako, hakuna Spirit aina yoyote kutoka nje kuingia hapo (Unazuia wasipate usaidizi Toka nje).

Wanyoe Nywele, Waongoze Sala ya Toba, waambie wakupeleke walipoweka Mikoba yao ya Kichawi, kama ni Kwao ongozana nao kukishakucha.... Teketeza Vifaa vyao vya Kichawi na Utakua umewasaidia.

Wachawi hawawezi kuacha Uchawi wao wenyewe Kwa matakwa Yao kwani Watauwawa na wenzao, wengi wanatamani kuacha lakini wanashindwa coz ni Yesu pekee anayeweza kuwasaidia kuwatoa huko bila wao kupata Madhara yoyote....!

Wakati mwingine Mtumishi wa Mungu wasaide Wachawi kuokoka.... Kwa uwepo wako hawawezi kushambuliwa na wenzao....!

NB:
Usisahau kuwanyoa Nywele baada ya maombi.
Lazima uziombee hizo Makorokoro Yao ya Kichawi then Uchome moto.
Hahhahha Hayo Hayawezi kutokea.

Kwa sababu hayo ni mambo halisi na sio kama yale maigizo ya madhabahuni Wajinga Wakitapeliwa bila Huruma.

Akiyafanya hayo aje aandike Uzi hapa na Asisahau kuchukua japo 'tu video tuwili kwa ajili ya ushahidi
 
Hiyo ni Sleep paralysis inatokana haswa na mtindo mbovu wa maisha.

Kutokuwa na utaratibu maalumu wa kula, Uchovu mwingi, Stress, Kulala chali na kuchelewa kulala ni moja ya visababishi.
Ila mm nikichelewa kulala Huwa hawaji😄, nikiwahi kulala huja tunasumbuanaga sana, naamini ni wachawi...unakuta tunakemea ila sauti hazitoki ghafla wanakuachia sauti inatoka kwa nguvu...utasikia Tokaaa kwa jina la Yesu..ila tayari unakuwa umeteseka mda Fulani walikushikilia😂. Alafu kuna baadhi ya watu mnagombana kwenye harakati za utafutaji ridhiki wakati wa mchana...unashangaa usiku unagandamizwa😀...maisha bila kuokoka ni bure haloo...unaweza hama nyumba Yako uliyoijenga😃
 
Asante kwa ushuhuda mzuri.
 
Wakati ule nipo boarding schule niliwahi experience hii kitu mara kadhaa.

Nilikua napenda kulala deka ya juu, siku moja likanikandamiza bhana, nikalipiga mateke mangumi nk liniachie, ofkoz jina la yesu lilitumika pia, linaniachia.... Asee sitak kusema kwamba ilikua illusion au nn ila nliona kama kivuli kikitoka pale kwangu, kikaenda bwen ya pili tunayopakana, dakika 1 ni nyingi, naskia mwingine akipiga kelele za kuweweseka... Nilipata woga sana nikasema silalu nione likirudi.

Mara ya pili ilikua mtihani wa mwisho tumebak only form two schule nzima, tukaamua tuchague bweni moja tulale wote make hatukua wengi sana. Usiku wake tumwpiga story adi sa7 mmoja baada ya mwingine akalala, me na jamaa angu hatujalala story za hapa na pale zinaendelea... Tukaanza skia kwenye kona kule mtu anaweweseka, mara anahamia mwingine, yani ikawa kwa kupokezana hivi...

Ikafika muda yule jamaa angu nae akalala, sasa mimi niko macho kabisa yani, na akili yangu ilisema silali maana na mm linaweza kunijia... Asee... Likanikaba bhana.... Nikamuita jamaa make ni deka ya jirani na jins tumezibananisha yuko karibu tu, lkn wapi.... Nikapambana kwa kurusha mateke na mangumi... Likaniacha... Sekunde chache namskia na jamaa nae anapiga makelele ya kuweweseka ikabidi nimuamshe. Nikamsimulia akasema nae ndo alikua anaota hivyo.

Nikatoka nje kukojoa, nje kuna limti likubwa sana la zamani kama mita 30-50 hivi, ile nafika pale nje nikaona sehemu ya ule mti imenesa as if kuna nyani kaurukia hivi... Oya.... Nlitoka nduki kmmke.... Nkatafta ndoo ya kukojolea tu.

Asbh yake kila mtu story ni hiyo kwamba alikabwa. Wenyewe wanaita sleep paralysis lkn ile ni ya kipekee asee... Sio kawaida
 
Kuna mengn ni Majinamizi
Ndio zao
Kuna sk nilikuwa naangalia TV mchana
Nikasinzia
Kilichonikuta ndio hicho
Nikajikaza nifungue macho
Nikaona mtu kavaa nguo nyeupe juu kwenye Corner
 
Mkuu mi nafikiri umechanganya mtu wa kum-quote.
 
Duuh, asante sana storyteller kwa ushuhuda huo. Nimependa ulivyomalizia: "Wenyewe wanaita sleep paralysis lkn ile ni ya kipekee asee... Sio kawaida"

Wanasayansi kwa hilo wamekwama, mambo ya wachawi hawawezi kuya-prove. Endelea na ujasiri huohuo tu. Shetani ni kama mbwa koko, akikutisha ukaogopa ndio atakuonea zaidi. Ulivyoona sehemu ya mti imenesa ilitakiwa usiogope. Ungekemea tu kwa Jina la Yesu. Ukisema tu: "shindwa katika Jina la Yesu" hiyo ni dawa tosha.
 
Kuna mengn ni Majinamizi
Ndio zao
Kuna sk nilikuwa naangalia TV mchana
Nikasinzia
Kilichonikuta ndio hicho
Nikajikaza nifungue macho
Nikaona mtu kavaa nguo nyeupe juu kwenye Corner
Na wengine wanaona mijitu ya ajabu ajabu barabarani wanapoendesha magari au pikipiki. Na hii imesababisha ajali nyingi. Sasa wanaosema ni sleep paralysis, barabarani nani anaendesha gari amelala? Shetani ni muongo. Anafanya maovu mengi lakini hataki ajulikane kuwa yeye ndiye chanzo, maana watu wakijua watampinga. Hata wanaoenda kwa waganga wanadanganywa. Wanaambiwa jirani ndio mbaya wako kumbe sio jirani ni shetwani mwenyewe. Tumeishatambua hila zake tuendelee kumpinga kwa Jina la Yesu atakimbia.
Yak 4:7-10
Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
 
1 Pet 5:8
Mwe na kiasi na kukesha, maana adui yenu ibilisi huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mtu ammeze.
 
Wacha kujipakazia , mchawi gani akujie wewe ili apate nini kwako ? Umeshiba maharage mengi na ugali usiku , gesi imekujaa unakuja kutumwagia upepo JF, Yesu haäwezi kuwaambia watu watumie jina lake. Huo ni ushirikina
Shetani anajua mimi ni tishio kwake, kwa sababu namnyang'anya watu aliowateka, ndio sababu anawatumia maajenti wake(wachawi) kujaribu kuniangamiza. Lakini hawawezi. Yesu wangu ni ngome imara.

Kuhusu Yesu kuwaambia watu watumie Jina lake, soma mstari huu:
Marko 16:17
Nazo ishara hizi zitafuatana na wanaoamini: Kwa Jina langu watatoa pepo wachafu; watasema kwa lugha mpya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom