Ibn Unuq
JF-Expert Member
- Oct 9, 2020
- 5,507
- 10,079
Kama Mungu ana uwezo wote, kwa nini asizuie dhuluma kabla hazijafanyika?Fanya jukumu lako uliopewa hivi umeshawai kujiuliza aliye uwawa au kuzulumiwa ataipata je Haki yake hali haliyakuwa Aliye mzulumu naye amesha kufa.
Kama ana huruma, kwa nini anaruhusu mtu aishi maisha yote kwa mateso huku akitumfariji kwamba atamwadhibu yule mtesaji siku akifa?
Je, hiyo ni haki ya kweli kumuacha mtu abake, alawiti, au aue watu vitani?
Kwa nini asizumzui mtu mapema kabla hajafanya hayo yote?
Kama Mungu ni mjuzi wa yote na ni wa haki, kwanini aliona ubakaji huo kabla haujatokea na hakuchukua hatua?
Na kama ananguvu kuliko vyote kwanini ashindwe kuzuia mtu asiye na hatia kuteseka na maumivu ya kubakwa?
Hivi Kulawitiwa na kubakwa mpaka kufa nalo ni jaribu la kiimani la kimungu kwa anayetendewa?
Kama Mungu ni mwenye huruma bhasi angezuia hicho kitendo kabla hakijatendwa.
Kama Mungu aliamua kutokuzuia, basi aliiruhusu dhuluma itendeke.
Je, mahakama inayochukua hatua mapema baada ya mtu kufanya ubakaji na ulawiti ni bora zaidi kuliko Allah anayeangalia na kukaa kimya?
Haki ya kweli ni ya kuchelewa au ni ya kuchukua hatua mapema?
Je, wewe ukimuona mtu anataka kubaka utachelewa kufuata haki?
Je, wewe ni bora kuliko Allah wako anayechelewa?
Kama ana subiri, basi aidha amekosa huruma, au anatenda mchezo wa kutesa watu kisha baadaye aje kuwahukumu kwa kushindwa kukwepa mateso aliyoyaleta.
Na huo si upendo – ni squid game ya kimungu.