Nimewapiga wachawi—kipigo cha mbwa koko!

Nimewapiga wachawi—kipigo cha mbwa koko!

Sasa mbona walifanikiwa kukufikia hadi kukugandamiza?
Hujui kwamba kuna watu wanagandamizwa mpaka wanakufa? Mimi sikufa. Na kwa kutamka Jina la Yesu usifikiri waliondoka wanacheka. Walipigwa kipigo cha mbwa koko.
 
Hujui kwamba kuna watu wanagandamizwa mpaka wanakufa? Mimi sikufa. Na kwa kutamka Jina la Yesu usifikiri waliondoka wanacheka. Walipigwa kipigo cha mbwa koko.
So, kuokoka kumekusaidia usife, sio usifikiwe na kuingiliwa na wachawi
 
Ungeandika kifupi tu kwamba ulipuuzia kuomba wazee wa ngwasuma waka kudaka
Niliowalenga sio Wakristo. Wala goal sio kufundisha umuhimu wa maombi kabla ya kulala. Goal ni kuwaonyesha wanaobeza Ukristo kuwa Jina la Yesu lina nguvu na linapita majina ya mitume wote.
 
Kama Shetani anaweza kutumia sauti yangu mwenyewe ili kuwaza mabaya, hapo nina uhuru gani wa kuchagua mema na mabaya?

Na kama Mungu anaruhusu Shetani aitumie akili yangu kunidanganya, je hiyo siyo dhuluma ya kiakili kutoka kwa Mungu?

Je, Mungu anayeweza kuacha Shetani aitumie sauti yangu mwenyewe kunipotosha, bado anabaki kuwa wa haki?
Utakuwa na Maswali mengi ya kumlaumu Mungu
Solution uliyonayo ukiishi kwa Neno lake Utaweza kuepukana na mawazo ya shetani
 
Maswali ya Kumlaumu Mungu hayakusaidii kwa sasa cha kwanza haukuwepo umezaliwa juzi juzi
 
Kama Mungu ana uwezo wote, kwa nini asizuie dhuluma kabla hazijafanyika?

Kama ana huruma, kwa nini anaruhusu mtu aishi maisha yote kwa mateso huku akitumfariji kwamba atamwadhibu yule mtesaji siku akifa?

Je, hiyo ni haki ya kweli kumuacha mtu abake, alawiti, au aue watu vitani?
Kwa nini asizumzui mtu mapema kabla hajafanya hayo yote?

Kama Mungu ni mjuzi wa yote na ni wa haki, kwanini aliona ubakaji huo kabla haujatokea na hakuchukua hatua?

Na kama ananguvu kuliko vyote kwanini ashindwe kuzuia mtu asiye na hatia kuteseka na maumivu ya kubakwa?

Hivi Kulawitiwa na kubakwa mpaka kufa nalo ni jaribu la kiimani la kimungu kwa anayetendewa?

Kama Mungu ni mwenye huruma bhasi angezuia hicho kitendo kabla hakijatendwa.
Kama Mungu aliamua kutokuzuia, basi aliiruhusu dhuluma itendeke.

Je, mahakama inayochukua hatua mapema baada ya mtu kufanya ubakaji na ulawiti ni bora zaidi kuliko Allah anayeangalia na kukaa kimya?

Haki ya kweli ni ya kuchelewa au ni ya kuchukua hatua mapema?
Je, wewe ukimuona mtu anataka kubaka utachelewa kufuata haki?
Je, wewe ni bora kuliko Allah wako anayechelewa?

Kama ana subiri, basi aidha amekosa huruma, au anatenda mchezo wa kutesa watu kisha baadaye aje kuwahukumu kwa kushindwa kukwepa mateso aliyoyaleta.

Na huo si upendo – ni squid game ya kimungu.
Kuna vingi tumefichwa
 
Next time waambie Malaika Wawa arrest, then Kwa Mamlaka uliyonayo amrisha wajitokeze mbele Yako.

Wakijitokeza vunja nguvu zao Kwa jina la Yesu, amrisha Ulinzi kwenye Nyumba Yako, hakuna Spirit aina yoyote kutoka nje kuingia hapo (Unazuia wasipate usaidizi Toka nje).

Wanyoe Nywele, Waongoze Sala ya Toba, waambie wakupeleke walipoweka Mikoba yao ya Kichawi, kama ni Kwao ongozana nao kukishakucha.... Teketeza Vifaa vyao vya Kichawi na Utakua umewasaidia.

Wachawi hawawezi kuacha Uchawi wao wenyewe Kwa matakwa Yao kwani Watauwawa na wenzao, wengi wanatamani kuacha lakini wanashindwa coz ni Yesu pekee anayeweza kuwasaidia kuwatoa huko bila wao kupata Madhara yoyote....!

Wakati mwingine Mtumishi wa Mungu wasaide Wachawi kuokoka.... Kwa uwepo wako hawawezi kushambuliwa na wenzao....!

NB:
Usisahau kuwanyoa Nywele baada ya maombi.
Lazima uziombee hizo Makorokoro Yao ya Kichawi then Uchome moto.
Wazo zuri
 
Huyo Yesu wako angalilitoa pepo CCM madarakani kwanza . Hata Gwajima kajificha na Yesu wake vichakani , anatoka usiku usiku Kama popobawa 😃😝😝
CCE99DA1-5510-4280-B063-B073E4A895A2.jpeg
 
walikuja usiku, muda mfupi baada ya mimi kujilaza kitandani. Wakaanza kunikandamiza
Ukute kumbe ulimeza nguna ya nguvu kabla hujalala hlf unadai umekabwa😆😆😆usiku jitahidi ule light foods uone kama utakabwa
 
Ungeandika kifupi tu kwamba ulipuuzia kuomba wazee wa ngwasuma waka kudaka
Hili andiko unalielewaje:
"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.(Efe 6:12). English version kushindana kwetu sisi ni "we wrestle..." Kilichotokea usiku huo ni Live wrestling." Nikaibuka mshindi kwa KO.
 
Ukute kumbe ulimeza nguna ya nguvu kabla hujalala hlf unadai umekabwa😆😆😆usiku jitahidi ule light foods uone kama utakabwa
Hivyo ndivyo shetani anavyowadanganya watu. Anawapiga halafu anawaambia walimeza nguna ya nguvu!! Lengo lake shetani hataki ajulikane kuwa source ni yeye. Watu wakijua watampinga.
 
Utakuwa na Maswali mengi ya kumlaumu Mungu
Solution uliyonayo ukiishi kwa Neno lake Utaweza kuepukana na mawazo ya shetani
Uadilifu wa kweli hauna dini bali una utu. Kama mtu anafanya mazuri kwa sababu anaambiwa afanye, siyo mwema, huyo ni mtiifu tu.

Lakini anayefanya mema kwa sababu anajua ni sahihi kufanya hivyo huyo ana maadili ya kweli.

Mfano mimi siamini Mungu, lakini sibaki, sichukui wake za watu, sisaliti marafiki, sitapeli, sipigi watu, sidhulumu na Naweza kudhibiti tamaa zangu za mwili.

Unajua kwanini? Kwa sababu najua kwa akili zangu ya kwamba huo ni uovu/ubaya hivyo sihitaji kuambiwa na dini ili nijue kufanya hivyo ni vibaya.
 
Niliowalenga sio Wakristo. Wala goal sio kufundisha umuhimu wa maombi kabla ya kulala. Goal ni kuwaonyesha wanaobeza Ukristo kuwa Jina la Yesu lina nguvu na linapita majina ya mitume wote.
Vip ukimuomba Mungu directly wachaw watapigwa pia au adi jina la Yesu pekee?
 
Kuna vingi tumefichwa
Ukweli hautaki kufichwa fichwa, ukweli hutafuta njia za kutokea.

Kama kweli kuna siri kubwa, lazima watu wenye akili na moyo wazi waendelee kuichunguza badala ya kukubali fikra za kufichwa fichwa tu.

Kwanza nani huyo anaficha ukweli? Pili amua wewe kama wewe binafsi kuutafuta ukweli kwa bidii, bila kufuata fuata tu vichwa vya watu wengine ambao nao wanaamini wamefichwa.

Vipi kama huko kuamini mmefichwa ndiyo kutokujua kwenyewe?

Kama unasema umefichwa kitu lakini hujui nini, nani, au kwa nini – basi hujui chochote.

Na kama hujui chochote lakini unaamini tu kwamba kuna siri hiyo si hekima, ni hofu ya mtu asiye na data.

Labda kufichwa siyo kwa sababu ya watu bali ni kwa sababu wewe hujajitahidi kutafuta ukweli kwa akili binafsi.
 
Ukweli hautaki kufichwa fichwa, ukweli hutafuta njia za kutokea.

Kama kweli kuna siri kubwa, lazima watu wenye akili na moyo wazi waendelee kuichunguza badala ya kukubali fikra za kufichwa fichwa tu.

Kwanza nani huyo anaficha ukweli? Pili amua wewe kama wewe binafsi kuutafuta ukweli kwa bidii, bila kufuata fuata tu vichwa vya watu wengine ambao nao wanaamini wamefichwa.

Vipi kama huko kuamini mmefichwa ndiyo kutokujua kwenyewe?

Kama unasema umefichwa kitu lakini hujui nini, nani, au kwa nini – basi hujui chochote.

2Na kama hujui chochote lakini unaamini tu kwamba kuna siri hiyo si hekima, ni hofu ya mtu asiye na data.

Labda kufichwa siyo kwa sababu ya watu bali ni kwa sababu wewe hujajitahidi kutafuta kwa akili binafsi.
Kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom