Jagina
JF-Expert Member
- Jan 29, 2019
- 11,505
- 5,378
Kama hukubaliani na andiko hilo. Na hili je?
Luka 10:17–19
Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.
Hapo wanaposema "wanatutii kwa Jina lako," ni nani anaambiwa kama si Yesu?
Aliyesema "nimewapa amri ya kukanyaga nyoka" ni nani kama si Yesu?
Wewe kama unabishi, acha sisi tuendelee kulitumia Jina la Yesu kuyachapa mapepo.
Huyo aliyeandika ni Luka na yeye ameanza Luka1;1 kuandika kuwa hizo ni hadithi alizosikia kwa watu mitaani akaamua kumwandikia Theophilus , si wewe wala Mimi . Pia Hao waliozichapisha wanasema hakuna uthibitisho wa Luka kuandika hizo hadithi ndio ikaandikwa Injili Kama alivyotuhadithia Luka.
Usifikiri kuwa nakataa Mimi Tu Laa! ni Hao waliochapisha hizo biblia ndio wanasema hivyo. Siye Mimi. Ukitaka ushahidi wa biblia nitakuwekea