Nimewapiga wachawi—kipigo cha mbwa koko!

Hii ni habari ya kweli kabisa. Uongo mimi nauchukia kama ukoma.

Kama huamini kuna wachawi, sikiliza vizuri: Hivi majuzi, walikuja usiku, muda mfupi baada ya mimi kujilaza kitandani. Wakaanza kunikandamiza kwa nguvu sana. Mgandamizo ulikuwa mzito, utafikiri mtu ameweka juu yangu mifuko mitano yenye saruji. Sio mzaha, nakwambia.

Sijawahi kuhisi uzito huo kamwe. Haraka sana nilitambua ni wachawi wanaotumiwa na mapepo kujaribu kunidhuru. Nikaanza kuwakemea kwa Jina la Yesu - kwa sauti ndogo, lakini yenye mamlaka watoke na kuniachia. Instantly, waliniacha na mgandamizo ule ukatoweka. Jina la Yesu lina nguvu sana. Ukilitamka, wachawi wanapigwa kipigo kikali sana na kukimbia. Hii ni mojawapo ya faida za kuokoka. Unatembea kifua mbele bila kuogopa wachawi.

Yakobo 4:7-10
"Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Itakaseni mikono yenu ninyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu ninyi wenye nia mbili. Huzunikeni, na muomboleze, na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni. Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua."
Chai
 
Nimekwambia elezea mgandamizo ule ulisababishwa na nini na kwanini ulitoweka ghafla baada ya kuukemea, umeshindwa.
Ndio shida ya kutegemea chatGPT. Za kuambiwa changanya na zako. Bahati mbaya huwezi kuchanganya na zako kwakuwa huna ufahamu wa kisayansi kuhusu jambo hilo na wala huna ufahamu wa kiroho kuhusu nguvu za giza. Umebakia kupinga tu. Nakuombea, Mungu aondoe upofu uliofunika akili zako, nuru ya Kristo ikuangazie.
2 Wakorintho 4:4
Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu.

Kutoweka ghafla baada ya kukemea hakuthibitishi kuwa chanzo kilikuwa pepo. Lete aya ya Biblia inayosema mgandamizo wa usingizi unasababishwa na pepo na kwamba kukemea ndiyo tiba yake. 2 Wakorintho 4:4 haisemi hivyo; inazungumzia kupofushwa akili kuhusu Injili.
 
Typo.
Mathayo 10:1
Yesu aliwaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa uwezo wa kuwafukuza pepo wachafu na kuponya magonjwa na maradhi yote.

Sawa, Mathayo 10:1 ndiyo aya sahihi. Lakini aya hiyo inasema Yesu aliwapa mitume uwezo wa kuwafukuza pepo; haisemi kwamba kila mgandamizo wa usingizi unasababishwa na pepo. Huo ndio ushahidi unaokosekana kwenye hoja yako.
 
Biblia haisomwi na kutafsiriwa hivyo unavyodhani wewe. Ndio sababu katika Biblia hakuna aya inayokuambia kuhusu kuvinjari WhatsApp, Instagram, au TikTok; wala hakuna aya inayokuambia ukitaka kuoga uende bafuni, au ukilala usiku ujifunike shuka. Hiyo haimaanishi Biblia haina kanuni zinazotusaidia kuelewa mambo hayo; tunazitafuta kupitia mafundisho na kanuni za jumla za Maandiko. Kwa mantiki hiyo ili ujue dalili za mtu kuvamiwa au kuathiriwa na pepo, ni muhimu kwanza uisome Biblia yote kwa upana: ujue inasemaje kuhusu shetani, wachawi na pepo; ujue jinsi nguvu za giza zinavyoelezewa katika vitabu mbalimbali vya Biblia, na jinsi Yesu na mitume walivyokabiliana nazo.

Ukitafuta aya inayoonesha specific checklist ya dalili za kuvamiwa na pepo, Yesu atarudi kabla hujaipata, na utaachwa kwa sababu ya ugumu wa moyo wako.
Mathayo 22:29
"...Mnapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu."
 
Sawa, Biblia inatumia kanuni za jumla. Lakini kanuni ya jumla si ushahidi wa moja kwa moja kwamba mgandamizo wa usingizi unasababishwa na pepo. Mathayo 10:1 inathibitisha kuwa Yesu aliwapa mitume mamlaka juu ya pepo, lakini haisemi kwamba kila tukio la mgandamizo wa usingizi ni pepo.

Mathayo 22:29 pia haithibitishi madai hayo. Usiniletee aya kuhusu pepo kwa ujumla; leta ushahidi unaounganisha pepo na mgandamizo wa usingizi.
 
Kwahiyo wewe ndio Judge unayeamua huu ushahidi unafaa na huu haufai?
 
mimi si judge. Wewe ndiye uliyeleta ushahidi, hivyo ni kawaida kuulizwa kama ushahidi huo unathibitisha dai lako. Kuwepo kwa ushahidi si sawa na ushahidi kuthibitisha kila dai.
 
Hueleweki, tumia lugha yako, acha kucopy na kupaste AI
 
Umekuwa msemaji wa AI ? Au unaogopa AI kuliko Mungu wako ?
Weka ushahidi wa Aya , kwenye biblia hamna ?? au Roho Mtakatifu wako yuko likizo anaota AI?

lete ushahidi unaounganisha pepo na mgandamizo wa usingizi.
 
Chonde chonde usimnenee mabaya Roho Mtakatifu. Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu haisamehewi.
Niliyoyasema yanatosha, ni hiari yako kukataa au kuamini.
 
Roho Mtakatifu wa kanisa lipi ndiye hasemwi vibaya ? Mara hii hakuota AI ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom