Nimewapiga wachawi—kipigo cha mbwa koko!

Hii ni habari ya kweli kabisa. Uongo mimi nauchukia kama ukoma.

Kama huamini kuna wachawi, sikiliza vizuri: Hivi majuzi, walikuja usiku, muda mfupi baada ya mimi kujilaza kitandani. Wakaanza kunikandamiza kwa nguvu sana. Mgandamizo ulikuwa mzito, utafikiri mtu ameweka juu yangu mifuko mitano yenye saruji. Sio mzaha, nakwambia.

Sijawahi kuhisi uzito huo kamwe. Haraka sana nilitambua ni wachawi wanaotumiwa na mapepo kujaribu kunidhuru. Nikaanza kuwakemea kwa Jina la Yesu - kwa sauti ndogo, lakini yenye mamlaka watoke na kuniachia. Instantly, waliniacha na mgandamizo ule ukatoweka. Jina la Yesu lina nguvu sana. Ukilitamka, wachawi wanapigwa kipigo kikali sana na kukimbia. Hii ni mojawapo ya faida za kuokoka. Unatembea kifua mbele bila kuogopa wachawi.

Yakobo 4:7-10
"Basi mtiini Mungu. Mpingeni ibilisi, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Itakaseni mikono yenu ninyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu ninyi wenye nia mbili. Huzunikeni, na muomboleze, na kulia. Kicheko chenu na kigeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni. Jinyenyekezeni mbele za Bwana, naye atawainua."
Tuwekee kapicha namna ulivyowatembezea kichapo.
Bila hivyo ni kachai
 
unaishi wapi nduguyefu kwenye wachawi kiasi hicho?
 
Adui wanaozungumzwa ni wanadamu. Mapepo tunatakiwa kuyatandika mboko za ukweli. Na si kwa nguvu zetu. Ni kwa kutamka tu: "Kwa Jina la Yesu, shindwaaa"

Ukitamka hivyo, yanapigwa sana. Kumbuka wale walioenda kumkamata Yesu. Alipowaambia: "Ni mimi hapa." Wakarudi nyuma, wakaanguka chini - puu! Ni mapepo hayo yalipigwa mweleka! Jina la Yesu linawapa vipondo vya uhakika 😀
Mbona naona mnamtukuza na kumsifu na kumuomba sana Yesu
kuliko aliyekuwa akimuomba Yesu pindi anapopatwa na matatizo au mimi ndiyo sijaelewa? Na mnieleweshe Yesu alikuwa alikuwa akimuomba nani.
 
Ulimwengu wa Kiroho ni hatari Sana. Kuna madaraja unapanda kadri unavyo endelea. Kuna daraja la Kiroho ukifika ndiko utajua kumbe Kuna mengi Sana duniani.
 
Aisee
Kama Mungu alijua shetani atakua chanzo cha uovu kabla hajamuumba ila akamuumba hivyohivyo basi uovu na kuteseka kwa binadamu ni mpango wa mungu mwenyewe.

Huwezi kuanzisha mchezo ambao unajua mwisho wake utakua uharibifu kwa wengi, halafu ukajiita mwenye upendo na haki.

Na kama kweli hakujua matokeo, basi si mungu wa kila kitu.
Lakini kama alijua na bado akaumba basi Shetani si tatizo kuu, bali tatizo ni mungu mwenyewe.

Kama Mungu yupo basi hana sifa ya upendo mkuu, hajui yote na hana nguvu kupita vyote.
Na kama hana sifa hizo baso hayupo - hizo zinabaki kuwa hadithi mlizojitungia kichwani tu.

Nikiweka sahihi ujue nimemaliza, huna cha kutetea tena.
Ibn Unuq.
 
Kwa kifupi Dunia ni kama chumba cha mitihani lazima yawepo mambo ya kuchagua
lililo Amriwa na kukatazwa na Mungu na mlango wa kuingilia chumba hicho ni kuzaliwa na wakutokea ni kufa,

Na Shetani ni katika majibu yasiyo sahihi na mafundisho ya Manabii ndiyo majibu sahihi,

Hadi hapo siwezi kumlaumu Mungu maana anachagua viumbe watiifu
Nimetowa mchanganuo wakiakilitu

ukitaka maandiko haya hapa
katika Sura Al-Mulk (67:2) ya Quran. Inasema:

"Yeye ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni, ni nani miongoni mwenu aliye bora katika matendo. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe." kwa sasa Watu wengi tunajua baya najema wakijilaumu ni sisi wanadamu siyo Mungu .
 
Ikiwa Allah ni mjuzi wa yote ajuaye mwanzo na mwisho kwanini autunge huo mtihani huku akijua baadhi ya wanafunzi wataushindwa huo mtihani?
Kama hakujua kuna watu watashindwa basi si mjuzi wa yote na kama alijua kuna watu watafeli si mungu wa haki.

Je huo mtihani ni wa haki, au ni mchezo wa kutafuta watu wa kuwachoma moto?
 
Kabisa
Kuna vitu nikiwaambia watu wanasema movie zinabichanganya
Siri

Hao wanakuwa hawana nguvu kwenye ulimwengu wa Roho. Ni mateka kwenye ulimwengu wa Giza. Nipoanza kupata nguvu kwenye ulimwengu wa Roho nikashangaa kumbe hata ulimwengu wa Giza Wana utawala wao unaoanzia kwenye Kijiji au mtaa. Kwa hivyo kadri unavyopata nguvu ya Kiroho kupitia maombi ya Kufunga ya muda mrefu utashangaa mkuu wa anga ya mtaa anakitafuta, hivyo hivyo mpaka Taifa. Kulingana na nguvu uliyonayo. Mambo ya Rohini ni very interesting.
 
Ikiwa Allah ni mjuzi wa yote ajuaye mwanzo na mwisho kwanini autunge huo mtihani huku akijua baadhi ya wanafunzi wataushindwa huo mtihani?
Kama hakujua kuna watu watashindwa basi si mjuzi wa yote na kama alijua kuna watu watafeli si mungu wa haki.

Je huo mtihani ni wa haki, au ni mchezo wa kutafuta watu wa kuwachoma moto?
Amekupa Akili na ameacha fursa ya maombi umuombe na hukumuomba uhuru wa maamuzi unatutia kiburi.
 
Hiyo ni hoja ya kawaida ya kidini ya kutaka mtu alazimike kumuabudu Mungu kwa hofu ya Jehanum bila uthibitisho wa uwepo wake.

Kama Mungu alijua kabla ya kuniumba ya kuwa nitatumia akili aliyonipa kuchagua kutomuomba na akajua nitakwenda motoni kwa hilo - kwa nini aliamua kuniumba?
 
Mpaka wanakukaba walikuta umelala bila kuomba!
Ukiomba kabla ya kulala hawasogelei kabisa! Wanapita mbali na nyumba yako.
Hata hivyo hongera kwa kutumia Silaha ipitayo silaha zote duniani JINA LA YESU!
 
Hao wanakuwa hawana nguvu kwenye ulimwengu wa Roho. Ni mateka kwenye ulimwengu wa Giza. Nipoanza kupata nguvu kwenye ulimwengu wa Roho nikashangaa kumbe hata ulimwengu wa Giza Wana utawala wao unaoanzia kwenye Kijiji au mtaa. Kwa hivyo kadri unavyopata nguvu ya Kiroho kupitia maombi ya Kufunga ya muda mrefu utashangaa mkuu wa anga ya mtaa anakitafuta, hivyo hivyo mpaka Taifa. Kulingana na nguvu uliyonayo. Mambo ya Rohini ni very interesting.
Ni interesting kwel
 
Hiyo ni hoja ya kawaida ya kidini ya kutaka mtu umuabudu Mungu kwa hofu bila uthibitisho.

Kama Mungu alijua kabla ya kuniumba kwamba nitatumia akili aliyonipa kuchagua kutomuomba na akajua nitakwenda motoni kwa hilo - kwa nini aliamua kuniumba kabisa?
Fanya jukumu lako uliopewa hivi umeshawai kujiuliza aliye uwawa au kuzulumiwa ataipata je Haki yake hali haliyakuwa Aliye mzulumu naye amesha kufa.
 
Kweli kabisa Set free...
Mimi pia huliita jina la Yesu na hunisaidia
..ila sijaokoka nipo na imani yangu ya kanisa Katoliki..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom