Nimewapiga wachawi—kipigo cha mbwa koko!

Shetani kabla ya kuwa shetani alikuwa malaika mkuu mbinguni. Baadaye akaingiwa na kiburi, akataka kuwa kama Mungu. Yeye pamoja na theluthi moja ya malaika walioasi wakatupwa duniani. Kwa sasa wanasubiri kutupwa motoni milele. Hao ndio wanaoitwa mapepo. Na ndio wanaosababisha mambo mengi maovu duniani pamoja na kuwashawishi watu wasimwamini Mungu. Na wanafanya kazi pamoja na wachawi. In fact wachawi bila nguvu za giza yaani bila msaada wa mapepo hawawezi kufanya lolote.
Kwanini Mungu hakumtupa shetani na wenzake hukoJupiter au Neptune, akamleta humu duniani aturubuni sisi wanadamu?
 
Angetupwa huko Jupiter, ungejuaje nguvu ya Jina la Yesu. Usimuogope shetani, ni mbwa koko. Tumia Jina la Yesu kumkemea
 
Waliingia ili Yesu awaaibishe hadharani kwa ushuhuda huu. Kama wasingeingia nisingeandika ushuhuda huu ambao umewawezesha maelfu kujua nguvu ya Jina la Yesu dhidi ya shetani, mapepo na wachawi.

Ni kama wakati ule wana wa Israeli walipokuwa wanavuka bahari ya Sham. Ulinzi wa Mungu ulikuwa juu yao lakini majeshi ya Farao yaliwafuatia na kuingia katika njia aliyoipasua Musa. Matokeo yake unayajua. Maji yaliwafunika wakaangamia kwa maji. Ni ushuhuda mpaka leo.
Majeshi ya farao hayakuwafikia maana Mungu aliwazingira nyuma na mbele kasome vizuri hapo, yaani wakaingia mpaka wanakukaba kabisa sema ulilala bila kuomba
 
mkuu hayo uliyopitia mm niliyapitia miaka kadhaa hapo nyuma nilipokua tanga..

kwa mara ya kwanza na mm niliamini uchawi upo, ashukuriwe Mungu huyu kwa kutupatia jina lenye nguvu na mamlaka ya kumfukuza shetani...nilikemea kwa jina la YESU na kutumia damu ya YESU kuwafurusha kabisa wachawi na hawakuwahi tena kuja kunijaribu

nimefurahishwa pia na majibu yako mazuri, endelea kutoa elimu nzur ya ufalme wa Mungu na Mungu atakubariki sanaa

NB:YESU anakaribia kurudi, tuzidi kutangaza injili watu watubu dhambi zao na kumrudia MUNGU
 
Angetupwa huko Jupiter, ungejuaje nguvu ya Jina la Yesu. Usimuogope shetani, ni mbwa koko. Tumia Jina la Yesu kumkemea
Siyo fare alivyofanya angetutenganisha na shetani, kama aliweza kuwaweka samaki, papa ma nguva baharini na si wanadamu duniani.

sioni kwanini shetani asingepelekwa hata Mars au hata Mercury aungue na joto la huko mpaka kiama.

Sasa sisi katuleta duniani, shetani naye duniani, halafu anamuacha anaturubuni, kisha anatuambia tusimsikilize na hatumuoni wala kumfahamu, angalau basi angempa shetani mwili mwekundu au blue ili tuwe tunamkimbia tukimuona.

Bado sioni fair yeye Mungu kutuchanganya sisi wanadamu na Shetani humu Duniani.
 
Hujitambui tu wewe ni nani mbele ya shetani. Wewe ni kama Polisi wa Usalama barabarani. Haogopi gari linalokuja mbele yake, hata liwe kubwa namna gani, amepewa mamlaka ya kulisimamisha, tena kwa mkono mmoja tu.

Mungu anakupenda, amekupa mamlaka ya kumkemea shetani kwa Jina la Yesu.

Ni kweli humuoni, lakini akikukandamiza usiku husikii?

By the way, usimlaumu Mungu. Jilaumu mwenyewe. Uliambiwa usile tunda, ukala. Ungetii amri ya Mungu sasa hivi ungekuwa bado unaishi katika bustani nzuri ya Eden.

Hata hivyo ukiokoka, Yesu atakapokuja atatupeleka mbinguni. Mbinguni shetani hataingia. Shetani ameandaliwa moto wa milele. Ila ukikataa kuokoka utatupwa motoni pamoja naye. Huko utajua rangi yake kama ni mweusi au wa bluu.
 
Lakini unadhani ni fair kuhukumiwa kwa makosa ua wazazi wako?

Mfano baba yako labda kateleza kakwapua serikalini pesa, kakamatwa, kashitakiwa na kuhukumiwa.

Ni vyema wewe nawe uhukumiwe kwa makosa yake tena?

Adam na Eva hawakutii sauti ya Mungu, wakala Tunda, mimi na wewe kwanini bado tuna hukumiwa kwa dhambi zao?

Kwanini Mungu asiturudishe Eden sisi ambao hatujala hilo tunda, tuliotii na kuisikia sauti ya Mungu isemayo msile hilo tunda na tukaacha?

Adam na Eva wabebe hukumu yao nasi tupewe nafasi huko Eden, tuki haribu tufukuzwe, lakini naona Mungu kamkazia Adam na Eva na uzao wake wote.

Unadhani ni fair?

Na tunaambiwa ni mwenye huruma na upendo, atuhurumie siye, au atusamehe atupende na kuturudisha bustanini huko Eden.
 
Siasa peleka huko kwenye jukwaa la siasa. Hapa tunashuhudia nguvu ya Jina la Yesu dhidi ya wachawi. Amen?
Kwani Yesu haijui siasa ? Au nguvu zake zinashindwa na wanasiasa ? Hiyo biblia yako unajua kuwa iliandikwa na wanasiasa wa Roma ? Au hujui , Kama hujui niambie nikuwekee documentary ya BBC
 
Sauti 3
Ya Mungu
Ya Kwako Na Ya Shetani

Sauti ya maadili mazuri. Wewe kama wewe ni sauti ya nafsi yako yani wewe
Na ikitokea shetani katumia sauti yako
Utajiuliza kwa nn mimi huwa sisemagi hivi na hii sio kawaida yangu kuwaza mabaya
Kama Shetani anaweza kutumia sauti yangu mwenyewe ili kuwaza mabaya, hapo nina uhuru gani wa kuchagua mema na mabaya?

Na kama Mungu anaruhusu Shetani aitumie akili yangu kunidanganya, je hiyo siyo dhuluma ya kiakili kutoka kwa Mungu?

Je, Mungu anayeweza kuacha Shetani aitumie sauti yangu mwenyewe kunipotosha, bado anabaki kuwa wa haki?
 
Mimi navyofikiria alikuwa anajua
Sasa utasemaje kwamba alikuwa hajui akati yeye anajua Future
Unapokubali kuwa Mungu alijua future unakubali pia kuwa uovu unaoendelea duniani ni sehemu ya mpango wake.
Sasa hiyo siyo free will, hiyo ni preplanned system.

Sababu kama Mungu alijua Shetani ataasi na bado akamuumba, hiyo inaonyesha alitaka hilo litokee.

Sasa swali linalokuja ni Je, Mungu pia atawajibika kwa uovu alioujua kabla hajauumba, ambao alipanga utufikie kupitia Shetani?
 
Nimejiuliza Tuu,,, Hayo Mapepo Yamewezaje Kuingia Nyumbani kwako tena Hadi Chumbani kwako hadi kitandani kwako.

Tena wakapata Mamlaka ya Kuuchezea Mwili wako hadi ulipostuka na kuanza kuwakemea.

Hadi hapo naona Ulinzi wako wa kiroho(kama Unavyodai) sio Mkubwa sana.
 
Majeshi ya farao hayakuwafikia maana Mungu aliwazingira nyuma na mbele kasome vizuri hapo, yaani wakaingia mpaka wanakukaba kabisa sema ulilala bila kuomba
Na Ayubu naye hakufikiwa? Na je, Petro aliyeambiwa "rudi nyuma yangu shetani" ?
 
Ayubu ni Mungu aliruhusu na sharti maalumu la kutokugusa uhai wake, vipi na wewe kukabwa na wachawi Mungu aliruhusu wakukabe?

Kesi ya Petro iko tofauti kabisa, Petro ni fikra zake, vipi kuhusu wewe
 
Nimejiuliza Tuu,,, Hayo Mapepo Yamewezaje Kuingia Nyumbani kwako tena Hadi Chumbani kwako hadi kitandani kwako.

Tena wakapata Mamlaka ya Kuuchezea Mwili wako hadi ulipostuka na kuanza kuwakemea.

Hadi hapo naona Ulinzi wako wa kiroho(kama Unavyodai) sio Mkubwa sana.
Ni kweli siku hiyo sikuomba. Nilijisemea moyoni mwangu: "ngoja nilale kidogo ntaomba baadaye!" Hilo lilikuwa somo kwangu nisimpe Ibilisi nafasi, kama Maandiko yanenavyo. Na kwamba tunapaswa kukesha kwa kuwa shetani ni kama simba angurumaye, anazunguka zunguka akitafuta mtu wa kummeza.

Hata hivyo nimeishaeleza kwamba ilikuwa hivyo ili shetani aaibike. Ningemzuia kwa maombi siku ile asingefanya aliyoyafanya na huu ushuhuda nisingeuandika. Kwa ushuhuda huu wanaochezewa na mapepo na wachawi wametambua jinsi ya kuyafukuza. Hivyo ni faida kwamba waliingia ili wengi wapone.

Usisahau pia, unaweza ukaomba lakini Mungu akamruhusu shetani akujaribu kama ilivyokuwa kwa Ayubu. Watoto wa Ayubu walikufa, na yeye akapatwa na magonjwa mazito directly kutoka kwa shetani, maana Mungu alimruhusu auguse mwili wake isipokuwa roho.

Vile vile kama shetani asingeingia, nisingepata uzoefu wa jinsi anavyowatesa watu na kutafuta kuwachinja na kuwaua. Kwa ujuzi huo nimekuwa mwalimu mzuri.

Nadhani umeona sasa kuwa tukio hilo lilikuwa special tena kwa utukufu wa Mungu. Okay?
 
Ayubu ni Mungu aliruhusu na sharti maalumu la kutokugusa uhai wake, vipi na wewe kukabwa na wachawi Mungu aliruhusu wakukabe?

Kesi ya Petro iko tofauti kabisa, Petro ni fikra zake, vipi kuhusu wewe
Soma post #155 ina majibu ya kina
 
Ni kweli siku hiyo sikuomba. Nilijisemea moyoni mwangu: "ngoja nilale kidogo ntaomba baadaye!" Hilo lilikuwa somo kwangu nisimpe Ibilisi nafasi, kama Maandiko yanenavyo. Na kwamba tunapaswa kukesha kwa kuwa shetani ni kama simba angurumaye, anazunguka zunguka akitafuta mtu wa kummeza.
Kwaiyo tunapaswa kukesha Na Tusilale ili shetani asije kutuchezea??

Hata hivyo nimeishaeleza kwamba ilikuwa hivyo ili shetani aaibike. Ningemzuia kwa maombi siku ile asingefanya aliyoyafanya na huu ushuhuda nisingeuandika. Kwa ushuhuda huu wanaochezewa na mapepo na wachawi wametambua jinsi ya kuyafukuza. Hivyo ni faida kwamba waliingia ili wengi wapone.
Kwani wanaokabwa usiku wote huwa hawafanyi maombi?? Au ni kwamba wanaofanya maombi huwa hawakabwi?umefanya utafiti??
Usisahau pia, unaweza ukaomba lakini Mungu akamruhusu shetani akujaribu kama ilivyokuwa kwa Ayubu. Watoto wa Ayubu walikufa, na yeye akapatwa na magonjwa mazito directly kutoka kwa shetani, maana Mungu alimruhusu auguse mwili wake isipokuwa roho.
Umemgusa Ayubu. Haya nakuuliza Ayubu Alifanya nini juu ya majaribio yale ya shetani kwake??
Vile vile kama shetani asingeingia, nisingepata uzoefu wa jinsi anavyowatesa watu na kutafuta kuwachinja na kuwaua. Kwa ujuzi huo nimekuwa mwalimu mzuri.
Shetani Huchinja na Kuua watu??
Kwa namna gani physical au spiritual?
Nadhani umeona sasa kuwa tukio hilo lilikuwa special tena kwa utukufu wa Mungu. Okay?
Siasa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom