PostGE2025 Nimeogopa sana! Kete yao ya mwisho ni udini

PostGE2025 Nimeogopa sana! Kete yao ya mwisho ni udini

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
WARAKA WA TEC: Kuna Watu Wanaiharibia Serikali.

Kuna “vita” imeanzishwa kulishambulia Kanisa Katoliki nchini. Vita hiyo inaiumiza serikali kuliko walengwa wa vita hiyo. Nashauri tuiache serikali ijiharibie na uwezo huo inao. Tafakari haya yanayosemwa na watu wasiojisikiliza wakati wanaongea:

1. BANDARI: Kwa hiyo miaka yote TEC wanakwepa kodi, wanauza madawa ya kulevya na mambo mengine machafu, na serikali zooooote zilizopita ziliwaacha mpaka awamu hii ya sita?!

2. VURUGU ZA UCHAGUZI MKUU: Kwa hiyo TEC ndiyo iliyoharibu uchaguzi, ikaua watu, ikaharibu mali, ikazima internet nk?

3. MATAMKO YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI: Kwa hiyo SADC, AU, EU, State Department na Balozi zooote zilizosema uchaguzi ulikosa viwango, wote hao ni Wakatoliki au walishinikizwa na TEC?!

4. UTEKAJI: kwa hiyo, wakatoliki ndio walioagiza watu watekwe, wakampiga na Fr Kitima, wakateka mapadre na kuwadhalilisha au TEC hao hao wakafunga midomo ya viongozi kutokemea vitendo hivyo?

5. WASIOJULIKANA: Kwa hiyo hawa TEC ndio wasiojulikana ambao wanaogopwa na serikali kiasi cha kutofungua midomo kuwakemea?

6. MAANDAMANO: Kwa hiyo TEC ina nguvu ya kuwahamasisha vijana wa dini zote, vyama vyote, jinsia zote kuingia barabarani? Kwa hiyo TEC ina nguvu kuliko serikali na wazazi?

7. RUSHWA NA UFISADI: kwa hiyo TEC ndiyo inanyamazia ripoti za CAG, inagawa rushwa ndani na nje ya vyama wakati wa uchaguzi? TEC ndiyo inawalipa wanaotumia mitandao kuitukana serikali na sasa imewalipa ili waitukane TEC?

TEC ndiyo inayoagiza watu wale rushwa bila hofu ya TAKUKURU?

8. MAUAJI YA RWANDA: Kanisa Katoliki Rwanda lilihukumiwa kwa dhambi mbili. Kwanza, baadhi ya mapadre na maaskofu kuunga mkono serikali ya Habyalimana katika kuwabagua Watusi. Pili, baadhi mapadre na maaskofu kukaa kimya wakati hayo yanaendelea. Kundi la kwanza lilienda mbali na kushirikiana na polisi (kwa kuwaonyesha walipo Watusi) ili wauawe. Sasa Je TEC yetu imefanya lipi kati ya hayo mawili ili iwaombe radhi watanzania? Inaunga mkono serikali katika kuvitesa vyama vya upinzani?! Je iko kimya kama TEC ya Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari?!

Nijuacho mimi, TEC kwa ukubwa wake, ikikaa kimya ni taabu, Ikisema ni taabu. Haya sasa, waondoeni wakatoliki wooote kila mahali na funga midomo yao, tuone kama matatizo yetu yatayeyuka kama umande!

Jamani, Tutafute watu wazuri na wabobevu wa kuwasema TEC. Hawa waliojitokeza, wanawasafisha TEC wakati si lengo lao kuwasafisha.

NARUDIA: Kuna kitu hakikwenda sawa tarehe 29/10/2025. Yawezekana halikuwa lengo hilo lakini kikatokea. Kusema SAMAHANI haiondoi wala kupunguza heshima yetu. Kama taifa, tunalazimika kuishi na hali tusiyoweza kuibadilisha.

Baba wa Taifa aliwahi kutuadithia kisa cha dereva wa Ikulu aliyekuwa anapiga “rivasi” akamkanya mtoto wake na kumuua. Aliumia lakini akaendelea na msafara na kurudi baadaye kwa mazishi. Uzalendo una gharama.

Ugumu wa moyo haujawahi kuleta amani wala suluhisho. Serikali yetu siyo malaika. Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza PhD
Mawazo ya MUNGU si sawa na ya mwanadamu.
Hii ishu ya bakwata itapotea kama majivu ndani ya wiki hii, wala sina wasiwasi hata kidogo na UJINGA huu unaonendelea najua D9 ni zaidi ya Moto wa gesi
 
Hii ya udini wamefeli... sababu hata wao wasilaumu wanawagawanya. Hii ni karne ya 21, huwezi beba watu ufala kirahisi. Kila mwenye akili anajua BAKWATA haiwakilishi muslims
 
Trust me, waanzilishi wa vurugu ikifika December 9 ni hao Mashekhe wamepanga kuchoma makanisa.
1763625514963.jpg
 
Nimeogopa sana! Nimeogopa kupita kiasi... Banda yote kushindikana sasa wanataka kutumia kete ya dini! Mungu atusaidie sana
Walianza na figisu za kawaida
Wakaja na siasa majitaka
Wakaanza kurubuni wapinzani
Wakaanza kubambikia kesi
Wakawa wanateka
Wakawa wanateka na kupoteza watu
Wakawa wanaua.. Na kilele cha mauaji kikawa tar 29.10. Mpaka tar 3 November 2025.

Mpaka hapo wakazani wameshafanikiwa kuuza hofu.. Lakini wali ndio kwanza kama wamechokoza nyuki

Pengine walifadhiliwa mabilioni ili wakirudi kwenye power walipe fadhila kupitia rasilimali za wote..Sasa kitisho ni dhahiri. Wanaona wazi hawana pa kuchomokea
Kulinda maslahi yao na ya wafadhili wao ni wao kubakia kwenye power.. Hii ndio salama yao
Waliokwisha onja utamu wa maliasili lukuki za taifa hawako tayari kupokonywa tonge mdomoni.. Wako tayari kufanya lolote na chochote alimradi tu waendelee kuzifaidi

Hii kete ya udini ndio kete ya mwisho na hatari kuliko nyingine zote! Wameanza kea kasi kubwa na ya ajabu kupenyeza hiyo sumu kwenye jamii kupitia wachache wasiojutambua

Tunahitaji kudra kubwa za Mwenyezi Mungu tusije kufika wanakotaka kutufikisha.... 😭😭😭🚯
udini si kete ya watawala Tz, udini ni tatizo lipo for years! Toka zama za waasisi.

Kama watu wanahisi ni kete ya CCM wanajidanganya sana, Labda mmesahau uchaguzi wa 210 na ulienda vipi? na hio ni juzi tu hapa.

Risiti ya Mwl Nyerere hii hapa kuhusu udini

View: https://www.threads.com/@muya51/post/DQ9prVWDKj5/media?xmt=AQF0kziQ8yWkJ4R3Nb7EQDxIcv-5UMFdhFyqLHjzBEku2xs6-pBunPoC0_byAYnCgtYsvEdi
 
Mwisho was iku walimuombea kura kanisani

Na walituliza watu baada ya serikali kuwa madarakani licha ya mauaji na wizi wa kura! Kwanini hawayafanyi hayo leo hii?

Pili compare haya matamko uliyo weka leo na haya sasa! Tazama content zake.

Tazama risiti hizi hapa chini


View: https://www.youtube.com/watch?v=TAVwIU9qXas

1763627396165.png


Hapa chini akihimiza maridhiano baada ya rafu na mauaji ya uchaguzi 2020! kipi kimebadilika sasa hivi? Kwanini sasa hivi hoja uponyaji na nchi kuendelea mbele + kutoa ushirikiano kwa serikali haina mashiko kwao kwao kwa sasa?

View: https://www.youtube.com/watch?v=R76EVJWY4f4&t=111s
 
Hapana. Usiogope.

Acha inyeshe tujue panapovuja. Hii itatusaidia kuziba palipo na uharibifu.

Haya mambo yamekuwa yakiendelea chini kwa chini, na sasa imebidi yabubujike kila mtu aone tulipofikia kama nchi.
Sasa mabomu au kuchinja kukitokea hakuna tena wa kuuliza imekuwaje tena.

Ukweli ni kwamba haya mambo tulijuwa yapo, lakini unafiki wa kiTanzania wa kujifanya tu sisi ni tofauti na wengine ndio umetufikisha hapa.

Sasa ni kichaa gani atakayeweza kusema hatuna tatizo hili hapa kwetu?
Sahihi tatizo lipo kama unavyo sema.

Kimsingi wito wa haki kama zao la amani ni dhihaka kwa kwa waislam wengi. Nitakumbusha hali nchi iliyopitia hapo nyuma. Miaka iliyopita palikuwa na wimbi la vijana kujiunga na vikundi vya kigaidi na kufikiria kufanya vitendo hivyo hapa nchini na kwingineko, sababu kubwa nyuma ya movement hii ni madai ya haki.

Pengine watu wanaweza wasielewe na kujua, ma-sheikh wamefanya kazi kubwa sana kwa miaka kadhaa hapo nyuma kuongea na vijana waache fikra hizo na kwamba amani ya nchi ni kipaumbele kuliko naadhi ya haki wanazo dai! au zinazo koswa.
Sasa leo hii ikitokea wito wa haki kwanza ndio amani ni kama kidonda kinatiwa chumvi hivi.
 
Mshana clip kama hio isikupe matumaini yoyote, huyo na wale walio toka jana lao ni moja. Waweza chukua maneno yangu au kuyaacha.
Nitayachukua🙏🏿✌🏿💪🏿
 
Back
Top Bottom