CCM Wana miaka 70 hawawezi kuwaza hayo.
CCM IPO tayari kuuwa watanzania wote ilimradi wabakie madarakani,wapo tayari kutumia mbinu yeyote
WARAKA WA TEC: Kuna Watu Wanaiharibia Serikali.
Kuna “vita” imeanzishwa kulishambulia Kanisa Katoliki nchini. Vita hiyo inaiumiza serikali kuliko walengwa wa vita hiyo. Nashauri tuiache serikali ijiharibie na uwezo huo inao. Tafakari haya yanayosemwa na watu wasiojisikiliza wakati wanaongea:
1. BANDARI: Kwa hiyo miaka yote TEC wanakwepa kodi, wanauza madawa ya kulevya na mambo mengine machafu, na serikali zooooote zilizopita ziliwaacha mpaka awamu hii ya sita?!
2. VURUGU ZA UCHAGUZI MKUU: Kwa hiyo TEC ndiyo iliyoharibu uchaguzi, ikaua watu, ikaharibu mali, ikazima internet nk?
3. MATAMKO YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI: Kwa hiyo SADC, AU, EU, State Department na Balozi zooote zilizosema uchaguzi ulikosa viwango, wote hao ni Wakatoliki au walishinikizwa na TEC?!
4. UTEKAJI: kwa hiyo, wakatoliki ndio walioagiza watu watekwe, wakampiga na Fr Kitima, wakateka mapadre na kuwadhalilisha au TEC hao hao wakafunga midomo ya viongozi kutokemea vitendo hivyo?
5. WASIOJULIKANA: Kwa hiyo hawa TEC ndio wasiojulikana ambao wanaogopwa na serikali kiasi cha kutofungua midomo kuwakemea?
6. MAANDAMANO: Kwa hiyo TEC ina nguvu ya kuwahamasisha vijana wa dini zote, vyama vyote, jinsia zote kuingia barabarani? Kwa hiyo TEC ina nguvu kuliko serikali na wazazi?
7. RUSHWA NA UFISADI: kwa hiyo TEC ndiyo inanyamazia ripoti za CAG, inagawa rushwa ndani na nje ya vyama wakati wa uchaguzi? TEC ndiyo inawalipa wanaotumia mitandao kuitukana serikali na sasa imewalipa ili waitukane TEC?
TEC ndiyo inayoagiza watu wale rushwa bila hofu ya TAKUKURU?
8. MAUAJI YA RWANDA: Kanisa Katoliki Rwanda lilihukumiwa kwa dhambi mbili. Kwanza, baadhi ya mapadre na maaskofu kuunga mkono serikali ya Habyalimana katika kuwabagua Watusi. Pili, baadhi mapadre na maaskofu kukaa kimya wakati hayo yanaendelea. Kundi la kwanza lilienda mbali na kushirikiana na polisi (kwa kuwaonyesha walipo Watusi) ili wauawe. Sasa Je TEC yetu imefanya lipi kati ya hayo mawili ili iwaombe radhi watanzania? Inaunga mkono serikali katika kuvitesa vyama vya upinzani?! Je iko kimya kama TEC ya Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari?!
Nijuacho mimi, TEC kwa ukubwa wake, ikikaa kimya ni taabu, Ikisema ni taabu. Haya sasa, waondoeni wakatoliki wooote kila mahali na funga midomo yao, tuone kama matatizo yetu yatayeyuka kama umande!
Jamani, Tutafute watu wazuri na wabobevu wa kuwasema TEC. Hawa waliojitokeza, wanawasafisha TEC wakati si lengo lao kuwasafisha.
NARUDIA: Kuna kitu hakikwenda sawa tarehe 29/10/2025. Yawezekana halikuwa lengo hilo lakini kikatokea. Kusema SAMAHANI haiondoi wala kupunguza heshima yetu. Kama taifa, tunalazimika kuishi na hali tusiyoweza kuibadilisha.
Baba wa Taifa aliwahi kutuadithia kisa cha dereva wa Ikulu aliyekuwa anapiga “rivasi” akamkanya mtoto wake na kumuua. Aliumia lakini akaendelea na msafara na kurudi baadaye kwa mazishi. Uzalendo una gharama.
Ugumu wa moyo haujawahi kuleta amani wala suluhisho. Serikali yetu siyo malaika. Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza PhD