Nimefikia uamuzi wa kuchanachana vyeti vyangu vyote vya Kitaaluma baada ya kuona sifaidiki na elimu niliyosoma

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
Salaamj Wana JF.

Naitwa DJ. DON NALIMISON Ni Mtanzania mwenye asili ya Kimarekani. Yaani baba Mzazi ni raia wa Marekani na mama Mzazi ni raia wa Tanzania. Nimezaliwa 28.06.1980 wilayani Kahama , SHINYANGA, Tanzania.

Nimefikia uamuzi wa kuchanachana vyeti vyangu vyote vya Kitaaluma baada ya kuona sifaidiki na elimu niliyosoma, zaidi Ni kuwekewa vikwazo vya kuwa maskini na serikali ya Tanzania.

Vyeti nilivyochana Ni pamoja na Elimu ya msingi(Kahama Primary school-1996) kwa jina la utotoni MASHAKA KISANDU. Vyeti vya Elimu ya Sekondari(Kishimba Sekondari-iv, Kahama 2002). Cheti Cha Uandishi wa habari(Royal college of Journalism-2003). Vyeti vya Advanced Sekondari (Tabora Sekondari-Private Candidate-2007 na Kahama sekondari-2008), Cheti za induction course(Chuo Cha ualimu Tabora-2007). Cheti Cha degree ya kwanza Cha Chuo Kikuu Cha Sebastian Kolowa(SEKUCO/SEKOMU)-2012. Vyeti vya vyuo vya Utunzaji wa kumbukumbu. Hivi vyote nilisoma kwa jina Langu la zamani la DEOGRATIUS PIO KISANDU kabla sijaapa nakuwa DEOGRATIUS NALIMI KISANDU. Na haya yote yamefanyika baada ya kuapa na kuwa DON NALIMISON kwa mujibu wa Sheria.

Hivyo Sasa sihitaji Ajira ya Serikali Wala Ajira kwenye makampuni. Serikali ilinifunga jela miaka mitatu 2018-2020 kuonesha elimu yangu haifai. Hivyo nimechana vyeti vyote na kubadili jina jumla Maisha yangu yote na sitasikiliza ushauri wa Majeshi yote Wala ushauri wa Serikali. Nachotaka nikutimiza ndoto zangu kwa jina Langu DJ. DON NALIMISON nasivinginevyo.

Tanzania Ni Nchi chafu Sana, kuanzia viongozi mpaka Majeshi. Wananchi wanapata kiburi Cha kufanya unyama kwangu kupitia Majeshi. Sitaki kupewa jina lolote na serikali maana Ni na uelewa wa kutosha kuliko vigogo wa serikali wasio kuwa na lolote kwangu.

Leo nimenyimwa kitambulisho Cha Taifa kwa jina Langu la DON NALIMISON eti mpaka nioe TAKATAKA za Serikali na CCM.

Nawatakia Maisha mema wote mnaotegemea vyeti vya taaluma ili muwe na Maisha mazuri maana Mimi Vyeti havijanisaidia.

Wenu,
DJ. DON NALIMISON
Screenshot_20211113-151344.png
 
Vuta picha unapoambiwa eti ujiajiri wakati huna mtaji, bodi ya mikopo ikikudai fedha za ufadhili, una familia na ndugu wakikutegemea na cheti hakikupi majibu ya matatizo unayoyapitia! Na ajira hamna! ndipo unapoona miaka zaidi ya 15 ulioitumia kwenda chuo ni hasara tupu! I feel for you Brother!!!
 
Back
Top Bottom