Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kuhamia Dodoma

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
32fe85f9-585c-43ed-9a35-d02b623e05cd.jpg


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Prof. Elifas Tozo Bisanda, ametanabaisha ya kwamba makao makuu ya OUT yanatarajiwa kuhamia jijini Dodoma baada ya kupata eneo na fedha kutoka serikalini kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).

Prof. Bisanda, ametanabaisha hayo wakati akihutubia mkutano mkuu wa 42 wa Bunge la wanafunzi (USRC) wa OUT, Machi 23, 2023 mjini Babati mkoani Manyara.

“Kupitia fedha za HEET tulizopata, Dodoma tunajenga jengo lenye vyumba vya maabara za Sanyansi pamoja na makao makuu ya OUT. Tutaanza na ujenzi wa ofisi za viongozi wakuu wa chuo wakati tukiangalia namna ya ujenzi wa majengo ya ofisi nyingine kadri serikali yetu itakavyoendelea kutuwezesha na sisi pia kujiongeza kadri tutakavyoweza kupitia wadau mbalimbali.” Amesema Prof. Bisanda.

Out2.jpg

Aidha, Prof. Bisanda, aliendelea kusema kuwa OUT ipo katika manunuzi ya jengo la iliyokuwa shule ya sekondari Biafra linalotumika kama kituo cha Mkoa wa Kinondoni wa OUT jijini Dar Es Salaam.

“Tumeomba msaada wa fedha za manunuzi ya majengo hayo serikalini na sasa tunasubiri kupatiwa fedha hizo. Tunawashukuru sana Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiambatana na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda walitembelea majengo hayo mnamo tarehe 12/12/2022.

Makamu wa Rais aliridhia maamuzi ya OUT kununua majengo hayo na kuiagiza Wizara kuhakikisha inaipatia OUT fedha za manunuzi hayo. Tunafuraha kuona Wizara yetu inalifanyia kazi suala hili na tunatarajia fedha zitapatikana hivi karibuni." Alimaliza kusema Prof. Bisanda.

Out.jpg

Akizungumzia mkutano wa Bunge la wanafunzi, Prof. Bisanda amesema, bunge la serikali ya wanafunzi (USRC) ni chombo muhimu sana kwa mustakabali wa OUT na anachukulia kuwa mwanafunzi ni mteja lazima apatiwe heshima na nafasi ya juu anapotaka huduma muda wowote aipate.

Makamu Mkuu wa Chuo alipokea risala ya wanafunzi yenye maombi mbalimbali na kuyatolea majibu na mengine kuyaelekeza kwenye vitengo vya chuo kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

Akizungumza katika mkutano huo, Rais wa serikali ya Wanafunzi na Spika wa bunge hilo, Felix Lugeiyamu, amesema serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUTSO), imekuwa ikishirikiana na uongozi wa OUT kwa kuchangia na kushiriki moja kawa moja katika maedeleo ya chuo.

“OUTSO imenunua jenereta kwa ajili ya Kituo cha mkoa wa Mara, imenunua mashine ya kudurufu na komputa kwa ajili vituo vya Pemba, Songwe, Pwani na Geita. Haya tunayafanya kwa ajili ya kuimarisha huduma zinazotolewa katika vituo vya mikoa laikini pia kuhakikisha tunatengeza mazingira mazuri ya kujifunzia na kufundishia.” Alisema Rais Lugeiyamu.

Aidha, aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha miaka miwili ya masomo serikali hiyo imeweza kulipa ada jumla ya shilingi 36,580,000 fedha za Tanzania kwa wanafunzi 68 walioshindwa kuendelea na masomo kwa kushindwa kujilipia ada. Lengo lao kwa mwaka ujao wa masomo ni kulipia wanafunzi 150.

Katika kukazia hayo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Fedha, Mipango na Utawala Prof. George Sylivanus Oreku alithibitisha kwamba OUTSO ni mdau mkubwa na muhimu katika maendeleo ya OUT.

Alisema "Hakika aliyoyasema ndugu Rais na Spika wenu ni kweli kabisa na kila mwaka wamekuwa wakichangia mahitaji mbalimbali pale panapokuwa na upungufu. Wamekuwa wakichangia vifaa vya TEHAMA, viti, meza na kulipia ada ya wanafunzi wenye uhitaji kila mwaka.

Nawapongeza sana OUTSO kwa mfano huu mzuri na pale mtakapohitimu masomo yenu muendeleze mambo haya katika jamii mnapoishi au kufanya kazi.

Prof. Oreku alihitimisha kwa kuwaambia kwamba OUT itasaidia kutoa fedha za kufanya uchaguzi katika maeneo yote ya vituo ambayo kwa sasa hayana vituo. Miongoni mwa vituo hivyo ni Tunduru na Kahama ambavyo awali vilikuwa ni vituo vya uratibu na kwa sasa vimepewa hadhi ya kuwa vituo vya mikoa ya OUT.

Naye, Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Huduma za Ushauri wa Kitaalamu, Prof. Deus Ngaruko, amesema kuanzisha Chuo Kikuu kinachotoa elimu kwa njia za Huria na Masafa ni jambo kubwa mno la kujivunia katika nchi yetu.

Pamoja na ugumu uliopo katika kuendesha chuo kama hiki katika ukanda ambao watu wake wamezoea elimu ya darasani, OUT imepiga hatua kubwa sana ya maendeleo. Ni chuo cha kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Tunapongeza sana serikali yetu kwa kuanzisha chuo hiki na kuendelea kukiwezesha kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake. Hivi karibuni tumeona Kenya nao wanakusudia kuanzisha Chuo Kikuu Huria katika nchi yao.

“Huria maana yake ni ule uhuru wa mwanafunzi kujisomea, gharama yake kubwa ipo kwenye kuwaelewesha watu kuwa hawatakiwi kufuata chuo ila kinawafuata wao. Huria maana yake ni kuwa huru, achague muda wa kusoma, mahali na gharama. Naomba waheshimiwa Wabunge wa USRC muupate uelewa huu na mtusaidie kuufikisha uelewa huu wa Watanzania wenzetu wa mijini na vijijini.” Amesema Prof. Ngaruko.
 
Hiki chuo ni kumbe ni noma sana, nilikuwa napitia mahali nimeona ni chuo bora cha kwanza Africa kwa miaka mitatu mfululizo kwa vyuo vinavyotoa elimu kwa mfumo wa masafa na cha 13 kidunia!!

Kinalea (mentor) vyuo vya Laweh kipo Ghana na Open University ya Botswana!! Nimekielewa mtu wangu, wacha wahamie Dodoma viongozi walipo!!
 
1. Yale Makao Makuu ya Kule Mkoa wa Pwani wameachana nako?
2. Ununuzibwa Generator, photocopier nayo Ni Mafanikio?
NB: Tunaandaa Taifa la wahitimu nusu mkate kupitia Chuo hili. Samahani ikiwa nimewaudhi Wahitimu toka chuo pendwa
 
Rais wa Serikali ya wanafunzi, anakuaje spika wa bunge la chuo??
How??
 
Ina maana na sisi wafanyabiashara tuhamishie biashara zetu dodoma?? Mbona kila kitu cha serikali chahamia dodoma?
 
Ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi.

Kama OUT wanafanya shughuli zao vyema kabisa DSM ikiwa makao makuu ya chuo, hakuna mantiki yoyote ya kuhamia Dodoma.

Utasiki makao makuu ya Mamlaka ya Bandari Tanzania THA nayo kutokana na siasa watahamishia makao makuu ya THA Dodoma kwa ajili ya kuwaridhisha wanasiasa na sio kuongeza huduma bora kwa wateja wake.
 
Ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi.

Kama OUT wanafanya shughuli zao vyema kabisa DSM ikiwa makao makuu ya chuo, hakuna mantiki yoyote ya kuhamia Dodoma.

Utasiki makao makuu ya Mamlaka ya Bandari Tanzania THA naye kutokana na siasa watahamishia makao makuu ya THA Dodoma kwa ajili ya kuwaridhisha wanasiasa na sio kuongeza huduma bora kwa wateja wake.
DP Makao Makuu yapo Dubai
 
Ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi.

Kama OUT wanafanya shughuli zao vyema kabisa DSM ikiwa makao makuu ya chuo, hakuna mantiki yoyote ya kuhamia Dodoma.

Utasiki makao makuu ya Mamlaka ya Bandari Tanzania THA nayo kutokana na siasa watahamishia makao makuu ya THA Dodoma kwa ajili ya kuwaridhisha wanasiasa na sio kuongeza huduma bora kwa wateja wake.

Siyo kweli hiki ulichosema!! Nilichosikia mimi ni kwamba serikali imekiunga Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na kuwa mnufaika katika mradi wa mageuzi ya kiuchumi kupitia elimu ya juu!!

Mradi huu unaijengea OUT maabara saba za kikanda yaan Pwani, Mtwara, Njombe, Kigoma, Dodoma, Mwanza na Arusha.

Hapo ndipo mabadiliko yakatokea, ilipokuwa ijengwe makao makuu (Bungo Kibaha Pwani) patajengwa kituo kikubwa cha utafiti licha ya kuwa na maabara ndani yake, hiki kituo kitakuwa funga kazi!!

Majengo ya maabara ya Dodoma yatajengwa na ofisi za kutosha kuwa makao makuu!! Hiki ndicho nilikipata kutoka katika chanzo changu!! Hivyo hakuna wastage ya pesa ni maboresho tuu
 
Back
Top Bottom