Abood ageuka mbogo Mgogoro wa ardhi baina ya Kidondolo na Chuo Kikuu cha Sokoine

Stayfar

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
1,070
2,226
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe, Abdulaziz M. Abood asikitishwa na kuendelea kwa mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa mtaa wa Kidondolo na Mamlaka ya Chuo Kikuu cha Sokoine {SUA}, ambao umeendelea kukua kila baada ya muda na kusababisha taharuki kwa baadhi ya wananchi wa mtaa huo kwa kuhofia kuchukuliwa maeneo yao jambo ambalo kwao wanaona haki yao inapokwa.

Mhe Abood ameonesha kuchukizwa na kitendo cha mgogoro huo kuendelea hadi sasa wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi wa Kata ya Magadu iliyopo ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mkoani Morogoro Machi 27 Mwaka huu kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kididimo ambapo wananchi hao walieleza kero hiyo.

Mhe Abood amesema kuwa, mipaka halali baina ya Mamlaka ya Chuo hicho na wananchi hao unafahamika tangu mwaka 1965 Chuo hicho kilianzishwa rasmi ambapo wananchi waliendelea na shughuli zao za kawaida ikiwemo kuendeleza maeneo yao kwa kujenga majengo ya kudumu ya kuishi na hakukuwahi kutolewa zuio lolote {stop order} na Mamlaka ya Chuo hicho hadi wananchi wanakamilisha ujenzi, waliendelea kushirikiana vyema na Chuo hicho.

Aidha, Mhe Abood amebainisha kuwa, mgogoro huo ulianza tangu mwaka 2013 na baadae kushughulikiwa na Mhe Abood mwaka uliofuata. Kitendo cha kujaribu kuchukua maeneo halali ya wananchi kupitia mgogoro huo, hakitakubaliwa wala kuvumiliwa kwa hali yoyote kwani, kufanya hivyo ni kupora haki ya wananchi hao ya umiliki halali wa maeneo hayo.
‘Nashangaa kuona mgogoro huu bado unaendelea na kama Mbunge nasema hivi sitakubaliana na hilo, tulishakaa na Mkuu wa Chuo miaka hiyo tukakubaliana kuhusu hilo. Mhe, Diwani haki ya kidondolo isimamie kikamilifu, haki iko wazi bila kumung’unya maneno, Sua ni waelewa na waungwana pia ila kuna wahuni na wajanjawajanja ambao wanataka kutuvuruga, kwani kuna maeneo mengi wameachia, Lukobe na maeneo mengine……..
Sasa ikitokea tena naomba nihusishwe kikamilifu kwa sababu ya wananchi, nipo kwa ajili ya kutetea na kusaidia wananchi ikishindikana tutatumia maana ya mafiga matatu, tutampeleka *Mhe. Rais
na tutamweleza ukweli.’ Amebainisha Mhe Abood.

Sanjari na hayo, Mbunge Abood ameahidi kufanya ukarabati utakaogharimu kiasi cha shilingi 7,000,000. kwenye Zahanati ya kata hiyo ili kuboresha na kusogeza huduma bora kwa wananchi hao kwa upande wa afya.

Mbunge Abood pia alitoa kiasi cha shilingi Mil. 1,457,000 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya kata ya Chama cha Mapinduzi na kiasi cha shilingi Laki 410,000. Kwa ajili ya ununuzi wa mifuko 10 ya saruji pamoja na Lori mbili za mawe ili kukarabati daraja la barabara ya Shaurimoyo ili wananchi waweze kupita vema.

Katika hatua nyingine Mbunge Abood, amemuagiza Mtendaji wa Kata ya Magadu kushughulikia usajili wa vikundi vya wajasiriamali ili waweze kupata haki ya kutumia vikundi hivyo kwenye fursa za mikopo mbalimbali inayotolewa na taasisi binafsi na 10% ya Halmashauri na hatimaye waweze kujiajili, ambapo Mbunge Abood ameahidi kulipia gharama za usajili wa vikundi hivyo kiasi cha shilingi Laki 350,000.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Mhe, Juma Kiduka amemuomba Mbunge Abood kufikisha shukrani wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha shilingi Bil. 1.7 kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji katika kata hiyo, vilevile upatikanaji wa kiasi cha Mil. 80 ambazo zimesaidia kukamilisha ujenzi wa choo na maabara Shule ya Sekondari ya Sua, ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya kata pamoja na ujenzi wa choo shule ya msingi Sua.

Naye, Dkt. Jasmine Bunga ambaye ni Mbunge Mstaafu, pamoja na kutoa pongezi kwa Mbunge Abdulazizi Abood, pia amemueleza Mbunge kuwa, kwa kiasi kikubwa kinachopelekea mgogoro wa eneo hilo ni maslahi binafsi ya watumishi wa Chuo hicho hasa baada ya kuona wananchi wananufaika kutokana na vitega uchumi na umuhimu wa eneo hilo. Ameongeza kuwa, tangu mwaka 1965 wameishi kwa amani lakini mgogoro umechochewa baada ya ujenzi wa hosteli za Chuo hicho na kuonekana wananchi wananufaika na biashara katika eneo hilo.
Vilevile Dkt. Jasmine Bunga ameweka wazi kuwa, katika kushughulikia mgogoro huo Prof. Mali alipanda miti ili kuonesha na kudhihirisha mpaka wa Mamlaka ya Chuo na wananchi, hivyo kwa nini Chuo Kikuu cha Sokoine wamekiuka na kuendelea kunyanyasa wananchi wa mtaa wa Kidondolo kwa kuwapa taharuki.

Zaidi, Prof. Bukheti Kilonzo kupitia mkutano huo wa wananchi amewashauri wawakilishi wa idara ya maji Mkoani humo pamoja na mradi mzuri wa maji, kuwepo na vioski vya huduma hiyo kuzunguka mitaa ya kata hiyo ili kutoa fursa na kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi wasiokuwa na uwezo wa kuweka maji majumbani kwao, waweze kupata maji kwa gharama nafuu, hatimaye lengo la Serikali la kumtua Mama ndoo kichwani litimie kwa ufanisi.View attachment 2947691
Kweli kipindi hiki cha Chaguzi,tutaona na kusikia mengi.Huyu Abood sijawahi kusikia akiwasemea chochote wapiga kura wake zaidi ya mabasi ya kusindikiza misiba
 
Wafanyakazi wa SUA kutetea eneo la Chuo, inakuwaje iwe maslahi binafsi?
CCM inabidi ijitathmini kupitisha majina ya wagombea Ubunge ambao watoto wao hawasomei katika Shule na Vyuo vya nchini mwetu Tanzania.
Leo hii tukianza kutetea uvamizi wa maeneo ya Vyuo Vikuu vyetu, huku idadi yetu ikiendelea kuongezeka, miaka 20 mpaka 50 ijayo, vijana wetu wa Kitanzania watasomea wapi?
Mbunge Abood aone aibu kutetea uvamizi wa maeneo ya SUA, hata kama watoto wake hawasomei Tanzania.
SUA ni rasilimali muhimu sana ya Watanzania wote.
 
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe, Abdulaziz M. Abood asikitishwa na kuendelea kwa mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa mtaa wa Kidondolo na Mamlaka ya Chuo Kikuu cha Sokoine {SUA}, ambao umeendelea kukua kila baada ya muda na kusababisha taharuki kwa baadhi ya wananchi wa mtaa huo kwa kuhofia kuchukuliwa maeneo yao jambo ambalo kwao wanaona haki yao inapokwa.

Mhe Abood ameonesha kuchukizwa na kitendo cha mgogoro huo kuendelea hadi sasa wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi wa Kata ya Magadu iliyopo ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mkoani Morogoro Machi 27 Mwaka huu kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kididimo ambapo wananchi hao walieleza kero hiyo.

Mhe Abood amesema kuwa, mipaka halali baina ya Mamlaka ya Chuo hicho na wananchi hao unafahamika tangu mwaka 1965 Chuo hicho kilianzishwa rasmi ambapo wananchi waliendelea na shughuli zao za kawaida ikiwemo kuendeleza maeneo yao kwa kujenga majengo ya kudumu ya kuishi na hakukuwahi kutolewa zuio lolote {stop order} na Mamlaka ya Chuo hicho hadi wananchi wanakamilisha ujenzi, waliendelea kushirikiana vyema na Chuo hicho.

Aidha, Mhe Abood amebainisha kuwa, mgogoro huo ulianza tangu mwaka 2013 na baadae kushughulikiwa na Mhe Abood mwaka uliofuata. Kitendo cha kujaribu kuchukua maeneo halali ya wananchi kupitia mgogoro huo, hakitakubaliwa wala kuvumiliwa kwa hali yoyote kwani, kufanya hivyo ni kupora haki ya wananchi hao ya umiliki halali wa maeneo hayo.
‘Nashangaa kuona mgogoro huu bado unaendelea na kama Mbunge nasema hivi sitakubaliana na hilo, tulishakaa na Mkuu wa Chuo miaka hiyo tukakubaliana kuhusu hilo. Mhe, Diwani haki ya kidondolo isimamie kikamilifu, haki iko wazi bila kumung’unya maneno, Sua ni waelewa na waungwana pia ila kuna wahuni na wajanjawajanja ambao wanataka kutuvuruga, kwani kuna maeneo mengi wameachia, Lukobe na maeneo mengine……..
Sasa ikitokea tena naomba nihusishwe kikamilifu kwa sababu ya wananchi, nipo kwa ajili ya kutetea na kusaidia wananchi ikishindikana tutatumia maana ya mafiga matatu, tutampeleka *Mhe. Rais
na tutamweleza ukweli.’ Amebainisha Mhe Abood.

Sanjari na hayo, Mbunge Abood ameahidi kufanya ukarabati utakaogharimu kiasi cha shilingi 7,000,000. kwenye Zahanati ya kata hiyo ili kuboresha na kusogeza huduma bora kwa wananchi hao kwa upande wa afya.

Mbunge Abood pia alitoa kiasi cha shilingi Mil. 1,457,000 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya kata ya Chama cha Mapinduzi na kiasi cha shilingi Laki 410,000. Kwa ajili ya ununuzi wa mifuko 10 ya saruji pamoja na Lori mbili za mawe ili kukarabati daraja la barabara ya Shaurimoyo ili wananchi waweze kupita vema.

Katika hatua nyingine Mbunge Abood, amemuagiza Mtendaji wa Kata ya Magadu kushughulikia usajili wa vikundi vya wajasiriamali ili waweze kupata haki ya kutumia vikundi hivyo kwenye fursa za mikopo mbalimbali inayotolewa na taasisi binafsi na 10% ya Halmashauri na hatimaye waweze kujiajili, ambapo Mbunge Abood ameahidi kulipia gharama za usajili wa vikundi hivyo kiasi cha shilingi Laki 350,000.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Mhe, Juma Kiduka amemuomba Mbunge Abood kufikisha shukrani wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha shilingi Bil. 1.7 kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji katika kata hiyo, vilevile upatikanaji wa kiasi cha Mil. 80 ambazo zimesaidia kukamilisha ujenzi wa choo na maabara Shule ya Sekondari ya Sua, ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya kata pamoja na ujenzi wa choo shule ya msingi Sua.

Naye, Dkt. Jasmine Bunga ambaye ni Mbunge Mstaafu, pamoja na kutoa pongezi kwa Mbunge Abdulazizi Abood, pia amemueleza Mbunge kuwa, kwa kiasi kikubwa kinachopelekea mgogoro wa eneo hilo ni maslahi binafsi ya watumishi wa Chuo hicho hasa baada ya kuona wananchi wananufaika kutokana na vitega uchumi na umuhimu wa eneo hilo. Ameongeza kuwa, tangu mwaka 1965 wameishi kwa amani lakini mgogoro umechochewa baada ya ujenzi wa hosteli za Chuo hicho na kuonekana wananchi wananufaika na biashara katika eneo hilo.
Vilevile Dkt. Jasmine Bunga ameweka wazi kuwa, katika kushughulikia mgogoro huo Prof. Mali alipanda miti ili kuonesha na kudhihirisha mpaka wa Mamlaka ya Chuo na wananchi, hivyo kwa nini Chuo Kikuu cha Sokoine wamekiuka na kuendelea kunyanyasa wananchi wa mtaa wa Kidondolo kwa kuwapa taharuki.

Zaidi, Prof. Bukheti Kilonzo kupitia mkutano huo wa wananchi amewashauri wawakilishi wa idara ya maji Mkoani humo pamoja na mradi mzuri wa maji, kuwepo na vioski vya huduma hiyo kuzunguka mitaa ya kata hiyo ili kutoa fursa na kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi wasiokuwa na uwezo wa kuweka maji majumbani kwao, waweze kupata maji kwa gharama nafuu, hatimaye lengo la Serikali la kumtua Mama ndoo kichwani litimie kwa ufanisi.View attachment 2947691
Chaguzi zimekaribia.

Tujiandae kuona hasira za wabunge kuwatetea wananchi wao.

Unafiki mtupu
 
Aachane na mambo ya ardhi, atukarabatie magari ya kuzikia, ya ma makopolo, pia atuongezee na magari ya kwenda kwenye ngoma na vigodoro, na kama anaweza, atafute Kosta kama kumi, awe anatupatia kama tunaenda kusutana au kufumania.

Huo mji hauendelei kwa sababu taasisi kama SUA na mashamba ya mkonge yanauzonga, SUA basi wajenge hata commercial complex kama mlimani city, au wayatumie kufanya kilimo cha kisasa, maana yakikaa tu, yanatamanisha watu kuyavamia. They need to have a strong team of estate officers
 
Back
Top Bottom