Nimechanganyikiwa na Simu ya mtarajiwa wangu

Nimechanganyikiwa na Simu ya mtarajiwa wangu

Hao wazazi walitaka kusikia maoni yako kuhusu hili? Au waliamua tu kwa kua wana mamlaka juu ya binti yao? Hapa ukiacha imani busara inataka nini?
Na kama unaamini binti anakusikiliza, una wasiwasi gani ilhali kasema atarudi?

Nimeshatoa mahari tayari
Lakini babu kumbuka kuna Mila, tamaduni na Imani,,,hivi ni vitu vitatu tofauti.
Unazo sema wewe ni Mila kuwa ukishatoa mahari tayari ni Mke sasa hapo inapingana na Imani yangu na yake.
Vile vile kuna tamaduni ambazo m/ume akishajitambulisha tu kwa wazazi wa m/mke anaweza kumchukua na kuishi nae kama Mke wake bila ndoa.

Sasa hapa lazima tuwe na mitazamo tofauti kwa kila mmoja wetu.

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Nashkuru sana mkuu ni wazo zuri pia lakini bora kusingekuwaa tarehe ya kupanga ndoa!

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app

Harusi zinahairishwa tuu mbona, utalazimisha mwishowe yatakua makubwa kuliko uyaonavyo sasa.
 
Duh brother pole kwa mitihani mizito,better step up and make a decision Kama mme sasa,Hamna kwenda mpaka ndoa ifungwe na HAKIKISHA unakomaa kweli kweli
 
Lakini dada yangu umesoma tokea mwanzo Uzi huu?
Kikubwa Binti bado yupo kwao bado hajaja nyumbani kwangu.
Na kuhusu msimamo wangu nimeshamwambia siitaki hiyo safari na yeye akiwa mmoja wapo anaafikiana na mimi.

Sasa wasiwasi wako unakuja vipi nikamchukue kwa nguvu kisa tu nimeshatoa mahari au ki vpi?

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app

Angekua ameafikiana na wewe asingekubali kwenda angeungana na msimamo wako kama mmewe mtarajiwa.
 
Ankali unasemaje kuhusiana na hili? Let's assume kuwa mleta mada ni Muislamu.

SWALI:

Wakati mwanamke nishamposa na nimeshamtolea mahari nina haki yoyote ile ya kumwambia kitu mfano asitoke kila wakati na je yeye ana haki yoyote ile kwa kumwambia mchumba wake kitu chochote kile? - Ni haki kumchezea mkeo mwili wake wote? Natumai nitapata jibu zuri.

JIBU:

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kumdhibiti mke baada ya kumtolea mahari. Mambo ya kijamii na hasa ya ndoa ni nyeti sana kwa kiasi ambacho Uislamu umeyapatia kipaumbele kusije kukatokea mushkeli ambao hautarajiwi.
Unapomposa msichana na pengine kutoa mahari kwa sababu ya kukubaliwa posa yako bado huwa kisheria hajawa mke wako hivyo huna udhibiti. Bado mwanamke huyo yuko katika udhibiti na amri ya wazazi wake.

Jambo ambalo unaweza kufanya ni kuweza kukubaliana wakati wa posa pamoja na wazazi wake kuhusu hilo na yeye mwenyewe kuridhia. Ile haki ambayo umepatiwa ni kuweza kumtembelea na kukutana na mkeo mtarajiwa nyumbani kwao sio katika faragha bali akiwa na aliye maharimu wake.

Yote haya ni kuweza kudhibiti watu hao wawili wasiwe ni wenye kuingia katika maasiya. Kutoa mahari si dhamana kuwa utamuoa bali zipo ndoa nyingi zilizovunjika kwa sababu moja au nyingine. Katika muda huo, ima mwanamke au mwanamme anaweza kuivunja hiyo ndoa kisheria bila ya wasiwasi wowote.

Ama kuhusu mkeo ni ruhusa kabisa kuchezea naye mwili wake wote kama alivyo yeye mwenye ruhusa kuuchezea mwili wako wako. Kitu kinacho katazwa ni kufanya mapenzi kupitia sehemu ya nyuma (liwati).

Chanzo: Akishatoa Mahari Anayo Haki Kumuamrisha Au Kumkataza Jambo Kwa Aliyemchumbia? | Alhidaaya.com

kopi kwa Kongosho, Asprin na snowhite kwa taarifa.

Mkuu EMT mambo ya kiislam naxhelea kuyasemea maana ni mbumbumbu kabisa wa taratibu hizo..mi nimeassume mketa mada ni mfuasi wa taratibu za kimila tu kwenye kuoa...
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
Dogo hebu skiza.....

Mahari ushatoa, right?
Ilifuata na kutimiza matakwa na masharti ya ukweni, sawa?
Imepokelewa kwa taratibu zote, si ndio?

Na hapo bado hujajua kuwa huyo ni mkeo???? Hapo kilichobakia si ni ndoa kwa maana ya taratibu za kidini? Au?? Taratibu za kimila si ushaoa???

Ok, sasa hebu nambie, ukishaoa, mkeo anakusikiliza wewe au baba yake na nduguze??

Ukishajua hayo..... na mkeo kama anakuheshimu kama mwanaume wako, atakusikiliza wewe. Ushanielewa?

Laiti ingekuwa mimi...... Hakuna safari ambayo ingefanyika bila kibali changu. Period.

Ushauri mdogo: Kama unaburuzwa namna hii katika kipindi hiki cha mwanzo kabisa cha mahaba..... mkijazoeana, sio kwamba tu atakuomba ruhusa ya kwenda kwa shoga yake, bali atakutaarifu kuwa atalala kwa shoga yake kwa siku tatu..... na hutakuwa na jinsi zaidi ya kukubali.

Huu sio mfumo dume, Kaizer hommie, nimekuwa mnoko sana au huu ushauri umetoka kwa Bwana??

Mkwe Fixed Point, hatutamfanyia unaa kijana wako wallah, kuwa na amani....

CC: Fidel80, RR , Baba V, kiwatengu, Dark City, Kwa Taarifa.

Jna lako limeandikwa mbingubi mtumishi Asprin kwa neno hili kuu
 
Last edited by a moderator:
Ki vp labda mkuu?
Maana alikataa kuendelea ili nimuoe vile vile ye mwenyewe hataki kwenda huko ingekuwa labda anahitaji kwenda hapo sawa ningeweza labda kukuelewa!!

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
Ni kwamba yeye mwenyewe hana mamuzi yake binafsi, anaamuliwa na wazazi wake kama tu ilivyokuwa kwako unaamuliwa na wazazi wako. hata kama yeye anataka wazazi hawataki basi inabidi uwe mpole tu na ukubali matokeo, si ndo ilivyokuwa kwako kwa yule mdada wa kwanza? wewe ulikuwa unataka lakini wazazi hawataki.....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwanza shukuru Mungu kwamba hii "safari" yake ya kwenda USA imetokea kabla ya harusi. Fikiria kama baada ya mwezi tangu umuoe ndio angeibuka na hii safari ya "mwezi mmoja" halafu kila siku anakupiga kalenda dada bado hali yake si nzuri hivyo naongeza muda wa kuwepo huku halafu baada ya miezi michache anakwambia "nimepata shule huku hivyo nimeamua kusoma" hapo ndio ungechanganyikiwa zaidi. Mwache aende lakini sioni tatizo la wewe kuona shida kuwaambia Wazazi wako nini kinachoendelea kuhusiana na mkeo mtarajiwa. Pole sana na kila la heri.
 
Mpaka sasa najuiliza kwanini huyu JK hakukuteua kuwa mjumbe wa kamati ya rasimu ya katiba mpya? Nondo kama hii Papa Francis akiisoma ataruhusu mapadre wa kutoka kwenye chama chetu waoe..... na kina snowhite tutawawowa tena na tena na tena.

Baada ya kusema hayo hom boi wangu hebu naomba unambie hii sredi inadiskashen makitu gani???

Nje ya Mada: Mwenyekiti napenda kukufahamisha kuwa Khantwe amenishinda naomba kibali chako nikamatemo shemeji yako mpya. Tafazali nichaguliemo kwa PM mabazazi wasione. (Am sore Kongosho, nalazimika kudumisha mila hapa)

Hapo kwa Khantwe hebu subiri kidogo niitishe faili lake
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ushaonja apo kweli? Usikute mzuka wako ukaonjee ndani ndio mana una mzuka sana wa kuoa au asije kukuponyoka bila kuonja.

Zingatia, chakula huonjewa jikoni sio mezani! Hahahaaaa!!!!
 
Wakati mwingine kama mnapendana sana haya mambo ya Wazazi si vizuri kuyafuata 100%. Mnamuomba Mungu awasaidie kwenye ndoa yenu na kuendelea na maandalizi ya harusi yenu.

Ni kwamba yeye mwenyewe hana mamuzi yake binafsi, anaamuliwa na wazazi wake kama tu ilivyokuwa kwako unaamuliwa na wazazi wako. hata kama yeye anataka wazazi hawataki basi inabidi uwe mpole tu na ukubali matokeo, si ndo ilivyokuwa kwako kwa yule mdada wa kwanza? wewe ulikuwa unataka lakini wazazi hawataki.....
 
Hiyo ni kazi ndogo mbona ahirisha shughuli mpaka vumbi litakapotulia in the name of "sababu zilizo juu ya uwezo wako" Miaka miwili kitu gani bana!
By the way una haraka gani?
 
Dogo hebu skiza.....

Mahari ushatoa, right?
Ilifuata na kutimiza matakwa na masharti ya ukweni, sawa?
Imepokelewa kwa taratibu zote, si ndio?

Na hapo bado hujajua kuwa huyo ni mkeo???? Hapo kilichobakia si ni ndoa kwa maana ya taratibu za kidini? Au?? Taratibu za kimila si ushaoa???

Ok, sasa hebu nambie, ukishaoa, mkeo anakusikiliza wewe au baba yake na nduguze??

Ukishajua hayo..... na mkeo kama anakuheshimu kama mwanaume wako, atakusikiliza wewe. Ushanielewa?

Laiti ingekuwa mimi...... Hakuna safari ambayo ingefanyika bila kibali changu. Period.

Ushauri mdogo: Kama unaburuzwa namna hii katika kipindi hiki cha mwanzo kabisa cha mahaba..... mkijazoeana, sio kwamba tu atakuomba ruhusa ya kwenda kwa shoga yake, bali atakutaarifu kuwa atalala kwa shoga yake kwa siku tatu..... na hutakuwa na jinsi zaidi ya kukubali.

Huu sio mfumo dume, Kaizer hommie, nimekuwa mnoko sana au huu ushauri umetoka kwa Bwana??

Mkwe Fixed Point, hatutamfanyia unaa kijana wako wallah, kuwa na amani....

CC: Fidel80, RR , Baba V, kiwatengu, Dark City, Kwa Taarifa.
Mkwe, mwanangu ni kidume ambacho kinajua nini kinataka......... haburuzwi....
Jana tu nilikuwa naongea nao maana karibia wanafunga shule, nikawauliza watakaa hapa home likizo yote wiki sita? maana mimi na dad wao hatuna likizo. Nikawaambia waende kwa bibi yao angalau kwa wiki mbili....... mdogo akasema hapana, labda niwapeleke kwa mamao mdogo ili wakaone wenzao, mkubwa akasema hataki kwenda huko, anataka kwenda sehemu ambayo ata-have fun. mpaka mwisho nikawaambia wajipange wakubaliane wataenda wapi ndo waje wanipe majibu.
Kwa hiyo mkwe Matesha akileta za kuleta tu itakula kwake na nyie wazazi wake
 
Bwana mdogo Stata Mzuka, katika umri na uzoefu wangu, hilo ni changa la macho, unaingizwa mjini aka king, kaa chonjo saa mbaya!!! Akili ya kuambiwa changanya na yako!!!
 
hili nalo neno. wazazi sasa wanajuta kwanini waliweka kauzibe yule wa kwanza...
Unafikiri wazazi wanashida? hao naona hata mtoto wao akikaa bila kuoa watafurahi tu........ yeye ndo ana shida ya kupata mke, atumie akili yake na siyo kusingizia wazazi
 
Siko desperate
Nitajifanya mjinga sawa sasa si bora ni muambie wakati hajaondoka bado?

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app

Wewe tulia, suprise ni kitu kizuri kwake, atapata somo. Unaweza ukamwambia sasa akasema poa tu
 
Wakati mwingine kama mnapendana sana haya mambo ya Wazazi si vizuri kuyafuata 100%. Mnamuomba Mungu awasaidie kwenye ndoa yenu na kuendelea na maandalizi ya harusi yenu.

Ndo nilimwuliza labda baba alikuwa na sababu ya msingi....
mdada alikuwa mchawi, jambazi, au alishawahi kutembea naye....... yaani yale mambo yasiyofaa kabisa, lakini eti hamtaki tu! hapo mimi siwezi kusikiliza kabisaaaaa, na namwomba Mungu nisije kufanya hivi kwa mwanangu yeyote.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Dogo hebu skiza.....

Mahari ushatoa, right?
Ilifuata na kutimiza matakwa na masharti ya ukweni, sawa?
Imepokelewa kwa taratibu zote, si ndio?

Na hapo bado hujajua kuwa huyo ni mkeo???? Hapo kilichobakia si ni ndoa kwa maana ya taratibu za kidini? Au?? Taratibu za kimila si ushaoa???

Ok, sasa hebu nambie, ukishaoa, mkeo anakusikiliza wewe au baba yake na nduguze??

Ukishajua hayo..... na mkeo kama anakuheshimu kama mwanaume wako, atakusikiliza wewe. Ushanielewa?

Laiti ingekuwa mimi...... Hakuna safari ambayo ingefanyika bila kibali changu. Period.

Ushauri mdogo: Kama unaburuzwa namna hii katika kipindi hiki cha mwanzo kabisa cha mahaba..... mkijazoeana, sio kwamba tu atakuomba ruhusa ya kwenda kwa shoga yake, bali atakutaarifu kuwa atalala kwa shoga yake kwa siku tatu..... na hutakuwa na jinsi zaidi ya kukubali.

Huu sio mfumo dume, Kaizer hommie, nimekuwa mnoko sana au huu ushauri umetoka kwa Bwana??

Mkwe Fixed Point, hatutamfanyia unaa kijana wako wallah, kuwa na amani....

CC: Fidel80, RR , Baba V, kiwatengu, Dark City, Kwa Taarifa.

Hii mada nilijaribu kuikimbia mzee mwenzangu ila naona inanirudia......

Hapa kuna matatizo mengi ila makubwa ni mawili...

1. Wazazi wa binti ni wapuuzi.... Huwezi kula mahari ya watu halafu ukajidai kwamba una mwali ambaye yuko huru. Enzi zetu, binti akishalipiwa mahari anakuwa mzigo mzito kwa wazazi na walihakikisha haraka iwezekanavyo anaenda kwa wakwe zao. Nawashangaa hawa wazazi wanaojifanya hamnazo!

2. Kijana na familia yake wanaelea juu ya maji. Sikutegemea kijana (na kama anawazazi + wazee) aanze kulia lia wakati yuko kwenye maandalizi ya ndoa.

Labda kwa mwanasheria wetu EMT, endapo huyo binti akichomokea ughaibuni na ndoa ikashindikana, dogo na familia yake wanaweza kudai fidia kutoka kwenye familia ya msichana?

Ngoja nikanawe uso kwanza,

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Wazazi wakati mwingine wanafanya makosa kwa kuingilia maamuzi ya watoto wao ambao taari ni watu wazima, na mengine huweza kuwaathiri watoto kwa kipindi kirefu katika maisha yao.

Back
Top Bottom