Nimechanganyikiwa na Simu ya mtarajiwa wangu

Nimechanganyikiwa na Simu ya mtarajiwa wangu

stata mzuka

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2012
Posts
4,834
Reaction score
1,765
Habari zenu wakuu...!! Poleni na Swaum (Mlioko kwenye mfungo)

Kwanza kabisa mie humu sio muanzisha Uzi mara nyingi huwa ni mchangiaji tu japokuwa kuna mambo mengine huwa nayamaliza mwenyewe ila hili la sasa hivi nimeona nije humu!

Ni hivi,,safari yangu ya mahusiano wa kimapenzi nikiwa najitambua ni wasichana wawili tofauti na ktk vipind tofauti, huyu wa kwanza tulikuwa nae mtaani na nilidumu nae 2yrs and half na nilifikia hatua ya kumtambulisha kwa wazazi wangu lkn wazazi walimkataa katakata hasa mzee wangu nikaona isiwe tabu kugombana na wazazi kisa m/mke (hapo baada ya kuomba ushauri kwa watu tofauti hadi watu wa dini).

Maana ilifikia hatua wazazi wanasema watasusa na kutohudhuria shughuli yeyote baada ya kuona nilikomalia sana, kifupi nilikuwa nampenda kuliko maelezo na niliumia sana hasa huyu Binti ndio aliumia zaidi lkn now she is ok na mara chache huwa nawasiliana nae.

After 1yr nikawa na mahusiano na Binti mwingine ambaye tulisoma shule moja japo nilimtangulia madarasa mi niko Advance ye yuko o'level,,tulipotezana ye kwenda kusoma Ulaya chuo lkn nashkuru mitandao hii ilituunganisha tukawa friends alivyokuja likizo tukaonana mwisho wa siku nikampa ombi langu nataka kumuoa akasema it's ok ngoja nikirudi (ulikuwa mwaka wake wa mwisho) nitaongea na wazaz niwaambie nimepata mchumba.

Wazazi, dada na kaka zake waligoma wakasema amalize kwanza masters then ndio afanya mpango wa kuolewa kwani bado mdogo (25yrs) anakimbilia nini kuolewa.

Baada ya vuta ni kuvute Binti kukomalia kweli ikabidi wazazi wakubali kwa Shingo upande mi nikafuata process zote za kutoa posa na mahari juu ambayo ndoa tulishapanga ni mwezi wa9.

KUBWA lilijitokeza hadi kuomba ushauri ni jana kunipigia Simu anasema dada yake kajifungua anataka kwenda America kumsaidia for 1 month then arudi na dada mtu huwa nawasiliana nae lkn hakunigusia hilo jambo ye Binti anasema hayuko tayari kwenda lakin baba yake anataka aende maana huyo mchumba wangu ndio wa mwisho kuzaliwa kwao.

Na hivi nilinavyozungumza dada yake anamfanyia mpango wa invitation aende huko. Binti anawaambia wazazi wake kuna mambo mengi ya kufanya sasa hivi maana bado mwezi mmoja na Nusu ndoa na huku upande wetu mawifi zake wanataka waende kumchukulia vitu like nguo za harusi, kifupi nimeshindwa hata kuwaambia wazazi kwani nimechanganyikiwa kwakweli.

1.WASI WASI wangu unakuja kuwa ni atarudi kweli au ndio kwenda kusoma masters huko?
2.Sura yangu nitaiweka wapi kama asiporudi (God forbird)


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Tulia kaka, hili tukio lipe muda ili upate majibu sahihi, usitafute majibu ya hili utaumiza kichwa bure.

Kaka muda gani tena ndugu yangu na mtu soon zinaanza process za kwenda huko ikiwa wazaz wameshatoa Go ahead? Kikubwa nafikiri sina mamlaka hajawa Mke wangu na hilo nimemuambia wazi kwani bado yuko chini ya wazaz wake!


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Yaani unashindwa kuwaambia wazasi wako ambao wana influence kwa wakwe zako unakimbilia kutuambia hapa?

Kwa kifupi wazazi wa mtarajiwa wanakudharau na hiyo ndoa wataiongoza kwa remote.
Au hawakutaki?

Huu ndo muda wa kuonesha uanamme wako.
 
Yaani unashindwa kuwaambia wazasi wako ambao wana influence kwa wakwe zako unakimbilia kutuambia hapa?

Kwa kifupi wazazi wa mtarajiwa wanakudharau na hiyo ndoa wataiongoza kwa remote.
Au hawakutaki?

Huu ndo muda wa kuonesha uanamme wako.

Ni jana nimepigiwa Simu usiku so sijaenda bado kwa wazazi kuwapa taarifa.
Wangenidharau lkn wasingekubali nimuoe Binti yako japokuwa walikaa miezi6 kunichunguza ndio posa ikakubaliwa.
Mkuu nitaonesha uanaume kivp labda maana Binti hayuko mikononi kwangu so any thing inaweza tokea like kurudishiwa mahari. Msimamo wangu nimekataa asiende huko.


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Huo ni mpango tu ili binti yao asiolewe na wewe kwenda huko ni kisingizio na sababu kama alikuwa ana maanisha ndoa na wazazi walikubali.wasingeridhia yeye kwenda Usa na anajua kuna maandalizi yote

Hilo hata mimi nina wasiwasi nalo lakini la kujiuliza kwanini wamepokea mahari?
Point yao ni kwenda na kurudi kwa mwezi mmoja!


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
usikubali aondoke huyo bibie wanafanya ujanja aondoke usimuoe...... kwani unamiaka mingapi utake kuoa now jamani ? mimi naona kama unalazimisha ndoa nilivyosoma mtiririko wa maelezo yako.... kingine be carefully kwa sababu huyo binti kwa age hii anafanyiwa maamuzi na wazazi ni tatizo ... wazazi wa huyo bint wataingilia hadi ndoa zenu kiukweli kama ingekuwa ni mimi nisingeendelea na process za ndoa kwa sababu zifuatazo:
  • binti ajitambui bado
  • inaonekana binti hayupo tayari kuolewa sema wewe yawezekana umelazimisha
  • binti anahitaji ndoa kwa status lakini bado akili yake ni changa
  • binti na wewe wote ni watoto wa mama sidhani kama kuna hata mmoja wapo anahitaji ndoa
  • bado nawaona mnaakili za kitoto achana na ndoa hiyo
  • ndoa yenu itashikiliwa na mihimili ya wazazi na ndugu kuliko ninyi wenyewe.
  • nahisi kama mtaachana soon...
 
Mmmh,
hapo ni mtihani;
Ngoja waje wenye uelewa mzuri wa haya mambo.

Mtihani sio kidogo dada yangu,Mhaya mambo mengine unaweza kuchanganyikiwa hivi hivi unajiona!


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
ningekuwa mimi,ningemuacha aende na ningewaeleza wazazi wangu kila kitu,then ningesubiri kuona movie inavyoenda,asiporudi then ningejua sikuwa nimepangiwa na mungu kuwa nae,niliyepangiwa atakuja tu,bora hata hiyo ya kwako,watu wanaachwa mataa siku ya harusi yenyewe.
NB: my slogan "dnt take luv too seriously"
 
Labda chozi la yule binti alokataliwa na wazazi wako ndo linalipwa, na wewe unakataliwa na wazazi wa mtarajiwa wako...labda Karma...

Ila tuliza moyo, kama ndoa ipo ipo tu, hata aende wapi...atarudi.
 
usikubali aondoke huyo bibie wanafanya ujanja aondoke usimuoe...... kwani unamiaka mingapi utake kuoa now jamani ? mimi naona kama unalazimisha ndoa nilivyosoma mtiririko wa maelezo yako.... kingine be carefully kwa sababu huyo binti kwa agehii anafanyiwa maamuzi ni tatizo ... wazazi wa huyo bint wataingilia hadi ndoa zenu kiukweli kama ingekuwa ni mimi nisingeendelea na process za ndoa kwa sababu zifuatazo:
  • binti ajitambui bado
  • inaonekana binti hayupo tayari uolewa sema wewe yawezekana umelazimisha
  • binti anahitaji ndoa kwa status lakini bado akili yake ni changa
  • binti na wewe wote ni watoto wa mama sidhani kama kuna hata mmoja wapo anahitaji ndoa
  • bado nawaona mnaakili za kitoto achana na ndoa hiyo
  • ndoa yenu itashikiliwa na mihimili ya wazazi na ndugu kuliko ninyi wenyewe.
  • nahisi kama mtaachana soon...

Tarehe 27/10 natimiza 28
Kwa huyu Binti sidhani maana kama kuna mtu ambaye anahitaji ndoa ni yeye nafikiri kuliko mimi.
Mimi kuwa na 28 sidhani kama bado ni mtoto maana najitambua na nahitaji ndoa kwakweli.


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Pole sana mkuu,hapo kunahitaji umakin wahali ya juu yan mwezi m1 kabla ya ndoa halafu anasepa kwenda abroad!!!Hilo nisuala zito wala usisite kuwa muwazi kwa familia yako ili kuepuka Hasara ya pesa na muda.Akioondoka tu nawe sitisha mchakato wa maandalizi ya ndoa la sivyo......
 
ningekuwa mimi,ningemuacha aende na ningewaeleza wazazi wangu kila kitu,then ningesubiri kuona movie inavyoenda,asiporudi then ningejua sikuwa nimepangiwa na mungu kuwa nae,niliyepangiwa atakuja tu,bora hata hiyo ya kwako,watu wanaachwa mataa siku ya harusi yenyewe.
NB: my slogan "dnt take luv too seriously"

Mmmmhh mkuu hapo kuficha itakuwaje sasa asiporudi siku yenyewe na Wajue alishaondoka before na vile vile after Ramadhan ndio mawifi zake wawil wanaenda kumchukua kwa ajili ya maandalizi yake.

Sasa hapo kukaa kimya ni heri Shari au Nusu Shari?


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Tatzo lipo pale pale, mwnzo mulitaka kulazimisha ndoa na huyo mchumba wako wa kwanza ikashindikana kutokana na wazazi wako kupinga, huyu nae pia mumelazimisha wakati upande wa binti hawajawa tyari

Sasa ushauri wangu kwako ni utulize munkari wa ndoa alafu utafakari unachofanya maana utakuja kulazimisha alafu mbeleni uje ujute zaidi ya sasa
 
Back
Top Bottom