Nimechanganyikiwa na Simu ya mtarajiwa wangu

mwambie hutaki aende kama akikataa jua changa la macho. ushauri wa mtu mzima
 
Habari zenu wakuu...!! Poleni na Swaum (Mlioko kwenye mfungo)

Kwanza kabisa mie humu sio muanzisha Uzi mara nyingi huwa ni mchangiaji tu japokuwa kuna mambo mengine huwa nayamaliza mwenyewe ila hili la sasa hivi nimeona nije humu!

Ni hivi,,safari yangu ya mahusiano wa kimapenzi nikiwa najitambua ni wasichana wawili tofauti na ktk vipind tofauti, huyu wa kwanza tulikuwa nae mtaani na nilidumu nae 2yrs and half na nilifikia hatua ya kumtambulisha kwa wazazi wangu lkn wazazi walimkataa katakata hasa mzee wangu nikaona isiwe tabu kugombana na wazazi kisa m/mke (hapo baada ya kuomba ushauri kwa watu tofauti hadi watu wa dini).

Maana ilifikia hatua wazazi wanasema watasusa na kutohudhuria shughuli yeyote baada ya kuona nilikomalia sana, kifupi nilikuwa nampenda kuliko maelezo na niliumia sana hasa huyu Binti ndio aliumia zaidi lkn now she is ok na mara chache huwa nawasiliana nae.

After 1yr nikawa na mahusiano na Binti mwingine ambaye tulisoma shule moja japo nilimtangulia madarasa mi niko Advance ye yuko o'level,,tulipotezana ye kwenda kusoma Ulaya chuo lkn nashkuru mitandao hii ilituunganisha tukawa friends alivyokuja likizo tukaonana mwisho wa siku nikampa ombi langu nataka kumuoa akasema it's ok ngoja nikirudi (ulikuwa mwaka wake wa mwisho) nitaongea na wazaz niwaambie nimepata mchumba.

Wazazi, dada na kaka zake waligoma wakasema amalize kwanza masters then ndio afanya mpango wa kuolewa kwani bado mdogo (25yrs) anakimbilia nini kuolewa.

Baada ya vuta ni kuvute Binti kukomalia kweli ikabidi wazazi wakubali kwa Shingo upande mi nikafuata process zote za kutoa posa na mahari juu ambayo ndoa tulishapanga ni mwezi wa9.

KUBWA lilijitokeza hadi kuomba ushauri ni jana kunipigia Simu anasema dada yake kajifungua anataka kwenda America kumsaidia for 1 month then arudi na dada mtu huwa nawasiliana nae lkn hakunigusia hilo jambo ye Binti anasema hayuko tayari kwenda lakin baba yake anataka aende maana huyo mchumba wangu ndio wa mwisho kuzaliwa kwao.

Na hivi nilinavyozungumza dada yake anamfanyia mpango wa invitation aende huko. Binti anawaambia wazazi wake kuna mambo mengi ya kufanya sasa hivi maana bado mwezi mmoja na Nusu ndoa na huku upande wetu mawifi zake wanataka waende kumchukulia vitu like nguo za harusi, kifupi nimeshindwa hata kuwaambia wazazi kwani nimechanganyikiwa kwakweli.

1.WASI WASI wangu unakuja kuwa ni atarudi kweli au ndio kwenda kusoma masters huko?
2.Sura yangu nitaiweka wapi kama asiporudi (God forbird)

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app

hii ndiyo tabu ya kuoa kwenye familia za hizo zako!!
ona sasa ata baba mkwe hakujali kasahau km unataka kuoa mwanaye, pole sana kaka.
 
Ni kweli mkuu ndoa ambayo haina baraka haifai lakini kumbuka sikulazimisha,,ingekuwa nimepeleka posa halafu wamekataa ingekuwa kweli lakini hadi tukaitwa majibu yamekubaliwa na wakapanga mahari juu so, sidhani kama nililazimisha mkuu.

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app

Mkuu sijawahi kuona watu ambao wana nia njema wakakaa na barua kwa miezi 6.Hilo pekee lilikuwa linatosha kabisa kukupa picha kuwa una lazimisha.Wasingeweza kuikataa posa mkuu caz ingekuwa si busara kwahyo walikubali basi tu lakini walikuwa na mpango wa kumrudisha shule binti yao.

Kuwa mpole,kama ipo ipo tu na utamuoa.Let it go and let her go to school
 
Ni shiida kaka alafu wazazi wakishaamua basi ukipinga kivivu unaachiwa laana.Mimi ningekushauri swala la ndoa lipe muda kidogo aende huko ulaya labda mpaka miez sita ipite ndio uanze kukomalia tena.

Kama ni wako basi atazidi kuwa wako,ni suala la muda tu.

Wazazi wengine sio waelewa,ila mkuu nasikia laana inakupata kama kweli umefanya kosa ila kama ujafanya aukupati!?
 
Kama unatafuta baraka za wazazi mbona unataka kuzipotezea za wazazi wa mkeo mtarajiwa?

We endelea tu kuzitafuta hadi utajikuta unazeeka bila mke!

Ha ha mkuu ilo nalo neno wazazi wengine sio waelewa
 
Kijana pole sana.

Kuna mtu humu nimemsahau ana signature inasema "mwenye hekima hujifunza hata kwa mjinga". Sasa we mwenzangu watu wanakwambia mambo ya msingi wewe unashupaza shingo tu. Ni ukweli ulio wazi kuwa wewe hujakomaa kiakili kutokana na uwezo wako wa kufanya maamuzi kuonekana kuwa ni mdogo. Hakuna aliyesema usiheshimu wazazi ila unatakiwa ujue wewe ni mtu mzima unaetakiwa kuachana na wazazi wako uambatane na mkeo. Hilo wewe katu huliwezi; hata wazazi wakiridhia uoe na ukaoa bado kwa jinsi unavyowachukulia wana uwezo wa kuendesha ndoa yako.

Nina rafiki alikutana na mkaka wakaanzisha mahusiano. Ndani ya miezi mitatu toka wafahamiane wakapeana mimba. Kijana akasema wafunge ndoa haraka iwezekanavyo kwani hapendi kabisa wazo la kuwa mtoto wa kabla/nje ya ya ndoa. Binti kupeleka taarifa kwao wazazi wakaweka ngumu, waka-loby mpaka kwa mashangazi na mama wakubwa kuwa wamwekee ngumu. Kijana nao kwao ikawa hivyo. Hoja za wazazi ni kuwa vijana hawafahamiani vizuri na kuwa wameshtukizwa hivyo binti ajifungue kwanza halafu wao wapate muda wa kutosha kufanya maandalizi ya sherehe. Ukapita mwenzi mzima wa malumbano lakini kwa kuwa vijana lao lilikuwa moja wazazi wakanyoosha mikono wakaanza maandalizi. Huu ni mwaka wa 6 wako pamoja na watoto wawili na wanaishi kwa furaha na wazazi wa pande zote ingawa mwanzo haukuwa mrahisi.

Pili, umeambiwa humu kuwa hao wazazi wa binti watakupa shida ukimuoa binti yao kwani bado wanamuendesha binti yao. We unasema wana haki kwa sababu hujamuoa. Haki wanaitoa wapi wakati weshapokea mahari? Dalili ya mvua ni mawingu kaka.

Kama msimamo wako kuhusu wazazi hauyumbishwi basi acha ubinafsi, muache binti nae aheshimu wazazi wake kama ulivyoheshimu wa kwako.

Hakuna umri sahihi wa kuoa bali mtu sahihi na wakati sahihi.
 
Kama Mke wangu kweli hatowapenda wazazi wangu au kutowaheshimu kama wazazi wake hapo hakuna mjadala nitaacha tu huyo Mke bila hata mzazi kuniambia, lakini sio niache Mke bila sababu ya Msingi eti kuwa mzazi amesema hilo halipo.
Umri sahihi wa kuoa upo na mtu sahihi wa kuoa pia upo lakini unaposema umri sahihi wa kuoa sikubalianj na hicho kitu mkuu.

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Mkuu sijawahi kuona watu ambao wana nia njema wakakaa na barua kwa miezi 6.Hilo pekee lilikuwa linatosha kabisa kukupa picha kuwa una lazimisha.Wasingeweza kuikataa posa mkuu caz ingekuwa si busara kwahyo walikubali basi tu lakini walikuwa na mpango wa kumrudisha shule binti yao.

Kuwa mpole,kama ipo ipo tu na utamuoa.Let it go and let her go to school

Mkuu kwangu mimi hiyo ilikuwa it's not big deal kwasababu wazazi wake walikuwa hawanijui wala hawaijui familia yangu sasa sidhani kama kuna mzazi akurupuke tu akubali posa hajui huyo mkwewe ana maadili gani wakimuozesha kwa Jambazi je?

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kwangu mimi hiyo ilikuwa it's not big deal kwasababu wazazi wake walikuwa hawanijui wala hawaijui familia yangu sasa sidhani kama kuna mzazi akurupuke tu akubali posa hajui huyo mkwewe ana maadili gani wakimuozesha kwa Jambazi je?

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app

Mkuu anayeolewa ni binti sio wazazi hivyo mpaka mmeenda kupeleka barua ni kwasababu binti aliwaambia kuwa kuna ugeni unakuja na binti amesha kubaliana na wewe hata kama ni jambazi.Unless kama wazazi hawamwamini mtoto wao,wanamuona kuwa hajakomaa kuweza kufanya huo uchunguzi.

Kwahiyo ishu hapo haikuwa kwamba walikuwa wana kuchunguza ila ni kwamba walikuwa wanafanya delaying mechanism kukunyima mke.Ila mimi nafikiri wana nia njema tu kwa binti,laiti angekuwa kamaliza masters wala wasinge leta zengwe
 
"Hakuna umri sahihi wa kuoa bali mtu sahihi na wakati sahihi."

Umri sahihi wa kuoa upo na mtu sahihi wa kuoa pia upo lakini unaposema umri sahihi wa kuoa sikubalianj na hicho kitu mkuu.

Sijakuelewa. Mwenyewe umesema ndugu yako alioa at 23, wewe unataka kuoa at 28 na mwanzo ulitaka kuoa at 25 kama sikosei. Kuna waliooa at 30s na wengine 40s. Kwa hiyo hakuna umri kwa maana ya namba ambao bila huo au ukipita huo huwezi kuoa. Cha kuzingatia kuliko vyote ni kupata mtu sahihi na kuoa kwa wakati sahihi.
 
Nashkuru sana mkuu kwa mchango wako,,,naomba uniambie kidogo hilo Zengwe ulilivuka vipi? By the way, wazazi wake nitawalaumu kufa kwa kukubali mahari na tarehe ya ndoa pia.

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
ha haaaaa, inawezekana pia wazazi wa yule binti mwingine nao walikulaani kwa kupoteza muda wa mtoto wao na kumtambulisha kwa ndugu, na huwezi kujua wazazi wa mdada nao walishatamba saaana huko kilabuni kuwa binti yao karibu anaolewa halafu ghafla unaacha kumwoa sababu tu wazazi wamekataa.......
Zengwe langu liliisha kwa kufanya maamuzi magumu..... nilijua mimi binafsi nini ninakitaka...... nikamsomesha bibi yangu (mzaa mama) ambaye baba alikuwa anampenda saaanaaa ili aongee na mkwe wake. Baba alipoona kafwatwa na mama mke wake akasema nifanye ninalotaka ila yeye hahusiki. nikaingia. Amini usiamini mpaka babangu anafariki tulikuwa marafiki saaanaaaa na hata huyo mume aliyekuwa anabisha kuolewa naye walikuja kuwa washkaji sana tu.......
 
Labda chozi la yule binti alokataliwa na wazazi wako ndo linalipwa, na wewe unakataliwa na wazazi wa mtarajiwa wako...labda Karma...

Ila tuliza moyo, kama ndoa ipo ipo tu, hata aende wapi...atarudi.

Inawezekana ikawa ndo payback ya hapa hapa duniani.
mm niko kwenye situation kama yako ya kwanza mchumba kukataliwa ila sijapata nguvu ya kumove on.nimesha waambia wazazi kuwa haya wanayofanya kuna siku hili swala litakuja kujitudia ktk familia
 
Daah sina hata cha kusema, but naamini wengi wamekushauri humu vizuri tu. Mkabidhi tu Mungu hili suala, yeye anajua kipi ni bora kwako.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ahsante mkuu

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Wazazi, dada na kaka zake waligoma wakasema amalize kwanza masters then ndio afanya mpango wa kuolewa kwani bado mdogo (25yrs) anakimbilia nini kuolewa.

Baada ya vuta ni kuvute Binti kukomalia kweli ikabidi wazazi wakubali kwa Shingo upande mi nikafuata process zote za kutoa posa na mahari juu ambayo ndoa tulishapanga ni mwezi wa9.

KUBWA lilijitokeza hadi kuomba ushauri ni jana kunipigia Simu anasema dada yake kajifungua anataka kwenda America kumsaidia for 1 month then arudi na dada mtu huwa nawasiliana nae lkn hakunigusia hilo jambo ye Binti anasema hayuko tayari kwenda lakin baba yake anataka aende maana huyo mchumba wangu ndio wa mwisho kuzaliwa kwao.

Na hivi nilinavyozungumza dada yake anamfanyia mpango wa invitation aende huko. Binti anawaambia wazazi wake kuna mambo mengi ya kufanya sasa hivi maana bado mwezi mmoja na Nusu ndoa na huku upande wetu mawifi zake wanataka waende kumchukulia vitu like nguo za harusi, kifupi nimeshindwa hata kuwaambia wazazi kwani nimechanganyikiwa kwakweli.

1.WASI WASI wangu unakuja kuwa ni atarudi kweli au ndio kwenda kusoma masters huko?
2.Sura yangu nitaiweka wapi kama asiporudi (God forbird)

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app

Rudia mwanzo mkuu nilishasema hili kuwa hawajanikataa

Hahaha, mtu mzima unashindwa kusoma hata picha!
 
ulipomtolea mahali alishakuwa wako. wazazi wake hawana mamlaka ya kumpangia cha kufanya bila kuwasiliana na wewe. wanataka kumtorosha tu huyo.
 
ha haaaaa, inawezekana pia wazazi wa yule binti mwingine nao walikulaani kwa kupoteza muda wa mtoto wao na kumtambulisha kwa ndugu, na huwezi kujua wazazi wa mdada nao walishatamba saaana huko kilabuni kuwa binti yao karibu anaolewa halafu ghafla unaacha kumwoa sababu tu wazazi wamekataa.......
Zengwe langu liliisha kwa kufanya maamuzi magumu..... nilijua mimi binafsi nini ninakitaka...... nikamsomesha bibi yangu (mzaa mama) ambaye baba alikuwa anampenda saaanaaa ili aongee na mkwe wake. Baba alipoona kafwatwa na mama mke wake akasema nifanye ninalotaka ila yeye hahusiki. nikaingia. Amini usiamini mpaka babangu anafariki tulikuwa marafiki saaanaaaa na hata huyo mume aliyekuwa anabisha kuolewa naye walikuja kuwa washkaji sana tu.......

Hongera mkuu lakini we ulifikia hatua nzuri mpaka mzazi amekuambia hahusiki it means kakupa Go ahead litakalo kukuta ni wewe na nina Imani hata ndoa yako alihidhuria, hapo hapo ukumbuke wazazi ni tofauti na kila mzazi ana misimamo yake kwangu mimi alinisusa kabisa nimewafuata hadi wazee wenye hekima waliomzidi umri lakini alisema BIG NOOOO...!!

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
ha haaaaa, inawezekana pia wazazi wa yule binti mwingine nao walikulaani kwa kupoteza muda wa mtoto wao na kumtambulisha kwa ndugu, na huwezi kujua wazazi wa mdada nao walishatamba saaana huko kilabuni kuwa binti yao karibu anaolewa halafu ghafla unaacha kumwoa sababu tu wazazi wamekataa.......
Zengwe langu liliisha kwa kufanya maamuzi magumu..... nilijua mimi binafsi nini ninakitaka...... nikamsomesha bibi yangu (mzaa mama) ambaye baba alikuwa anampenda saaanaaa ili aongee na mkwe wake. Baba alipoona kafwatwa na mama mke wake akasema nifanye ninalotaka ila yeye hahusiki. nikaingia. Amini usiamini mpaka babangu anafariki tulikuwa marafiki saaanaaaa na hata huyo mume aliyekuwa anabisha kuolewa naye walikuja kuwa washkaji sana tu.......

hili nalo neno. wazazi sasa wanajuta kwanini waliweka kauzibe yule wa kwanza...
 
Back
Top Bottom