Nimeamua kuwa Atheist

Nimeamua kuwa Atheist

Uthibitisho kwa muktadha wa maongezi haya ni kwa kutumia mantiki, kuangalia hoja kimantiki, kuangalia truth table kimantiki, kuangalia contradictions.

Hoja ya Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, aliyeumba ukimwengu huu unaoweza kuwa na mabaya, ina contradictions nyingi zinazoonesha kuwa Mungu huyo hayupo, katungwa tu katika hadithi za watu, hadithi zenye makosa mengi ya kimantiki, ndiyo maana hoja ya kuwapo Mungu huyo ina contradictions nyingi kama

1. Epicurean Paradox/The Problem of Evil.
2. The incompatibility of God's perfect knowledge and human perfect freewill.
Naweza kukubaliana nawe ikiwa tutaelewa kwa dhati mipaka ya Mungu na hizo sifa ambazo sisi tunampa, ya kuwa muweza wa yote, aliyeumba ulimwengu ambao unaweza kuwa na mabaya, huo ni ufahamu siyo kuhusu Mungu. Mungu kuwa ana uwezo wote katika ukamilifu wake wa kiungu, Mungu hawezi kuumba kitu kizito kitakachomteza nguvu, huyo si Mungu, ana kanuni alizoziweka katika uumbaji wake ambao sisi wanadamu tuna elimu ndogo tu juu ya mambo hayo, siku zinavyosogea tunapata ufahamu kiasi kuhusu huu ulimwengu wetu. Hizo nadharia za Epicurian Paradox/ The problem of evil (uwezo wote, ujuzi wote, wema wote) na uwepo wa uovu, haya mambo hayahitaji njia ya mkato yanahitaji uelewa katika maelezo, ingekuwa imani ni kitu rahisi basi hakuna binadamu angepewa hiari ya kuchaguwa na hapo ndipo kwenye mtihani.
 
Kwenye maelezo hayo (yako), kwa upande mmoja ni masimulizi ya biblia na kwa upande mwingine ni uelewa wa mambo na elimu ya vitu. Hili la mwisho ni muhimu zaidi katika kuelewa biblia, ambayo ni msingi wa mafundisho mengi ya dini, na kwa kweli neno Mungu.

Sasa basi, neno upendo maana yake ni nini? Ujuzi maana yake ni nini? Na uwezo maana yake ni nini?

Aidha, kwa nini unafikiri kutokea kwa uovu ni kushindwa au kutokuwepo kwa Mungu mwenye upendo, uwezo na ujuzi wote?

Unalielezeaje jambo la baba anaemwadhibu mtoto wake, ana au hana upendo, ana uwezo au hana uwezo, ana ujuzi au hana ujuzi?

Upendo, uwezo, ujuzi ni nini hasa?
 
Mungu hagupo, kuna hadithi kuhusu uwepo wa Mungu.

Ukibisha, thibitisha Mungu yupo.
 
Kwenye maelezo hayo (yako), kwa upande mmoja ni masimulizi ya biblia na kwa upande mwingine ni uelewa wa mambo na elimu ya vitu. Hili la mwisho ni muhimu zaidi katika kuelewa biblia, ambayo ni msingi wa mafundisho mengi ya dini, na kwa kweli neno Mungu.

Sasa basi, neno upendo maana yake ni nini? Ujuzi maana yake ni nini? Na uwezo maana yake ni nini?

Aidha, kwa nini unafikiri kutokea kwa uovu ni kushindwa au kutokuwepo kwa Mungu mwenye upendo, uwezo na ujuzi wote?

Unalielezeaje jambo la baba anaemwadhibu mtoto wake, ana au hana upendo, ana uwezo au hana uwezo, ana ujuzi au hana ujuzi?

Upendo, uwezo, ujuzi ni nini hasa?
Baba anayemuadhibu mtotobwake hana uwezo wote, hana ujuzi wote, hana uoendo wake.

Hakuumba ulimwengu huu.

Mungu mnayemsema yupo mnasema ana uwezo wote, ujuzi wote na uowndo wote.

Mpaka hapo umefanya makosa kuwalinganisha.

Unafanya hesabu za cross multiplication wakati upande mmoja una infinity. Hesabu haiwezi kuwa sawa.
 
Nimefanya tafiti yakinifu nimekuja kugundua Mungu hayupo. Ni story tu za kutupa matumaini hewa.

Nimeamua kuwa Atheist. Nitaupa muda nao ukizingua namrudia Yesu.

Dhulma, uonevu, usaliti na ukatili umetamalaki sana.

Bora kuamini nature na kuwa mwema kwa viumbe hai hata visivyonekana.

Ni maamuz yangu binafsi.
unakuwa mwema kwa viumbe hai ili iweje??
 
Dhulma, uonevu, usaliti na ukatili umetamalaki sana.

Bora kuamini nature na kuwa mwema kwa viumbe hai hata visivyonekana.

Hii kwenye kamali wanaita double chance kitendo cha wewe kuamini katika nature na kuwa mwema kwa viumbe hata visivyoonekana kwenye game of chess♟️, umepush king 👑 kwa mantiki hiyo hata ikitokea kuwa Mungu anayezungumziwa yupo basi wewe utakuwa salama no matter what.!
 
Kwanza kabisa, kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo.

Narudia tena, kisichopo, hakithibitishiki kuwa hakipo.

Kwa sanabu hakipo, na kama hakipo, hakithibitishiki kuwa hakipo, uthibitisho unaendana na kilichopo.

Tunaweza kujenga hoja kama za proof by contradiction kuonesha contradiction zinazoonesha kitu fulani hakiwezi kuwapo. Katika hii dhana ya Mungu (mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote) hayupo, nimeelezea sana Epicurean Paradox mpaka michoro nimeiweka hapa. Google Epicurean Paradox, soma, ielewe, kama una swali kuhusiana an Epicurean Paradox lilete hapa.

Zaidi.

Mzigo wa uthibitisho unamuangukia yule anayesema kitu kipo.

Ndiyo maana Polisi wakija nyumbani kwako, wakisema una madawa ya kulevya, wao wanaosema una madawa ya kulevya wanatakiwa wafanye msako mpaka wayapate, wathibitishe yapo.

Hawakwambii wewe unayesema huna madawa ya kulevya uthibitishe huna madawa ya kulevya.

In principle, we cannot prove a negative, but we can show contradictions that shows the impossibility of a negative.

Swali la kuuliza hapa, ni kuwauliza wanaosema Mungu yupo, wathibitishe Mungu yupo.

Unasema Mungu yupo?

Kama unasema hivyo, thibitisha Mungu yupo.
unataka wakuthibitishie Mungu yupo ili iweje???
 
Dhulma, uonevu, usaliti na ukatili umetamalaki sana.

Bora kuamini nature na kuwa mwema kwa viumbe hai hata visivyonekana.

Hii kwenye kamali wanaita double chance kitendo cha wewe kuamini katika nature na kuwa mwema kwa viumbe hata visivyoonekana kwenye game of chess♟️, umepush king 👑 kwa mantiki hiyo hata ikitokea kuwa Mungu anayezungumziwa yupo basi wewe utakuwa salana no matter what.!
imani hainaga 50 fifty au double chance ni hakuna hakuna au ndiyo ndiyo

hili swala la kusema n bora uamin kuwa yupo alafu usmkute

kuliko kuamini hayupo ukamkuta
ni upagani.
 
Imani ni dhana pana, waneni husema imani chanzo chake ni kusikia pia waebrani 11. pale anakwambia imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo na ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

Kwa mujibu wa mtoa mada yeye anasema haamini tena uwepo wa MUNGU bali anaona bora kuamini katikabl nature na kuwa mwema kwa viumbe wote hata wasioonekana, kitendo cha kuwa mwema kinamuweka kwenye position nzuri sijui kama unapata point yangu

kwa ufupi Mungu ni anapenda matendo mema na mtoa mada anaangazia kuwa mwema kwa viumbe wote, weka mbali imani ukishakuwa mwema tayari unayo imani ndani yake.
 
Nijiulize kitu ambacho kimethathibika kwa waumini wengi nikiwemo mimi? Haya mambo sio dhahania, inakupasa kushiriki ili kuyaelewa! Tofauti na hapo utajiona uko sahihi sana!
sasa mkuu we huoni mgogoro hadi hapo?

ushiriki ili uyaone ---
 
Nimefanya tafiti yakinifu nimekuja kugundua Mungu hayupo. Ni story tu za kutupa matumaini hewa.

Nimeamua kuwa Atheist. Nitaupa muda nao ukizingua namrudia Yesu.

Dhulma, uonevu, usaliti na ukatili umetamalaki sana.

Bora kuamini nature na kuwa mwema kwa viumbe hai hata visivyonekana.

Ni maamuz yangu binafsi.

Kusema “Mungu hayupo” si tafiti, ni msimamo wa imani mbadala. Biblia ilishasema:

“Mpumbavu husema moyoni mwake, Hakuna Mungu.”
(Zaburi 14:1)

Kama dhulma na uovu vinakufanya useme Mungu hayupo, basi unathibitisha kinyume chake—kwa sababu huwezi kuita kitu uovu bila kipimo cha haki.

“Ole wao waitao uovu kuwa wema, na wema kuwa uovu.”
(Isaya 5:20)

Yesu hakuwahi kuahidi dunia isiyo na maumivu, bali alisema: “Katika dunia mtapata dhiki.” (Yohana 16:33)

Na kusema “nikimhitaji Yesu nitamrudia” ni hatari, maana: “Hamtaniona, kwa maana hamjui siku wala saa.” (Mathayo 25:13)

Kuwa mwema kwa viumbe ni jambo jema, lakini wema bila Mungu hauna msingi wa kudumu: “Hakuna mwenye haki, hata mmoja.” (Warumi 3:10)

Huu si uhuru wa akili—ni kubadilisha imani ya Mungu kwa imani ya nafsi.

Mungu anataka kuaminiwa kwa imani tu, hajataka athibitishwe kwa logic na akanushwe kwa falacy, kwani ufahamu wetu upo kinyume na uhalisia wake. Sisi ufahamu wetu unataka uwe kwenye mipaka ya wakati na mahali, wakati Mungu yupo kinyume na hicho.

watu kwa nyakati hii wapo kwenye mkanganyiko kuna dini nyingi , wanajuaje wameamini upande sahihi?
 
kwa dhehebu ambalo elon yupo , we unaona kapotea au lah?
Usiniulize maswali ya kicengecenge babu!!..kama una bichwa zito tafuta mwingine wa kukuelewesha,mi silipwi kukuelewesha
 
Imani ni dhana pana, waneni husema imani chanzo chake ni kusikia pia waebrani 11. pale anakwambia imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo na ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

Kwa mujibu wa mtoa mada yeye anasema haamini tena uwepo wa MUNGU bali anaona bora kuamini katikabl nature na kuwa mwema kwa viumbe wote hata wasioonekana, kitendo cha kuwa mwema kinamuweka kwenye position nzuri sijui kama unapata point yangu

kwa ufupi Mungu ni anapenda matendo mema na mtoa mada anaangazia kuwa mwema kwa viumbe wote, weka mbali imani ukishakuwa mwema tayari unayo imani ndani yake.
kama humuamini Mungu unakuwa mwema au unatenda wema ili iweje?? na ulijuaje huo ni wema?? na uovu ni upi ?? na kulingana na nn uuite huo n wema na huu n uovu ???
 
Back
Top Bottom