Nimeamua kuwa Atheist

Nimeamua kuwa Atheist

Naelewa misingi ya imani ni ndani ya box la imani tu na sio fikra huru , hivyo siwezi pinga chochote kanisani wala msikitini au kwenye majukwaa ya dini ambayo yamefungamanishwa na misingi ya kiimani tu
Unadhani kuwa atheist ndio upo huru kifikra? Mfano mleta mada anasema kafanya tafiti kuhusu Mungu na kafikia uamuzi kuwa hakuna Mungu na kaamuwa kuwa atheist, lakini kwa kuamua kwake kuwa atheist atajikuta analazimika kupinga uwepo wa vitu vingine mbali na Mungu kwa sababu ni atheist na si kwa sababu amefanyia utafiti hivyo vitu.
 
Angekuwepo na mimi na wewe tunajua hilo , wala kusingekua na haja ya wewe kuniambia kuwa yupo .

Hivyo kama unajua yupo ni haki yangu kukuhoji uwepo wake , ila sio lazima wewe uthibitishe huenda umeropoka tu
Msingi wa hiyo hoja yako ni ipi wenye kukufanya useme kwamba angekuwepo kusingekuwa na haja ya kuambiwa yupo?

Kwamba kila mtu angejua yupo au kwamba angekuwa anaonekana wazi kwa kila mtu? Hebu eleza msingi wa hiyo hoja ni nini?
 
Kabla ya kukujibu wewe unaonaje?
 
Unadhani kuwa atheist ndio upo huru kifikra? Mfano mleta mada anasema kafanya tafiti kuhusu Mungu na kafikia uamuzi kuwa hakuna Mungu na kaamuwa kuwa atheist, lakini kwa kuamua kwake kuwa atheist atajikuta analazimika kupinga uwepo wa vitu vingine mbali na Mungu kwa sababu ni atheist na si kwa sababu amefanyia utafiti hivyo vitu.
Unaelewa maana ya imani?
 
Huo ndiyo ukweli mkuu. Kila mtu anazaliwa bila kujua mambo ya dini au Miungu.
Ila mazingira utakayokulia ndiyo yataamua unakuwa muislam au mkristo, budha nk
Sasa kuna tofauti ya kutokujua mambo ya Mungu na kujua kuwa hakuna Mungu, atheist sio kwamba hawajui mambo ya Mungu bali wanapinga madai ya kuwepo Mungu na kuhitimisha kwa kudai hakuna Mungu kwa hoja kwamba hakuna uthibitisho.

Kwahiyo utaona hapo ni suala lenye kuhitaji ufahamu, Sasa hapo unafananishaje na mtoto anayezaliwa haelewi lolote?
 
Sijui vipi niweke nieleweke.

Ila nahisi Kuna Atheist wa mkumbo kama mimi nilivyohitaji kuwa.

Na Kuna real atheist,sasa pengine hawa real one wako real pia ila hawa wa mkumbo Kuna muda kwenye real life uhisi Kuna vitu haviko sawa wanajikaza tu.

Unamkataa Mungu jamiiforum haafu in real life sio kweli
 
Kabla ya kukujibu wewe unaonaje?
Mimi nimeshaeleza huko nyuma kwamba suala la kukubali uwepo wa Mungu msingi wake ni imani na ndio maana wale wenye kukubali kuamini na kufuata maamrisho inaaminika kuna malipo kwa kufanya hivyo, sasa wewe kiujumla unapinga kila chenye kuitwa kuwa ni imani na hapo ndio penye tatizo kwa sababu madai ya kuwepo Mungu unayapinga si kwa sababu ni kwamba sio imani sahihi bali ni kwa sababu ni imani.
 
Sijajua una lenga kitu gani na maandiko haya🤔
 
CARD YA MWISHO KABISA YA WAABUDU MUNGU NI VITISHO VYA MOTO WA JEHANAMU NA HUKUMU YA MWISHO WA KUSADIKIKA.

Faraja yao wao ni kwenda huko ktk mbingu za kusadikika ambako wanaimba na kusujudu wengine watangonoka na mabikra 70 WHAT A SHAME kwa wafia dini
 
Ni mtu ambaye anafahamu masuala ya Mungu na ndio maana anapinga madai ya kuwepo huyo Mungu, huwezi kupinga kitu ambacho hauna ufahamu nacho kabisa.
Kufahamu sio tatizo hata mimi nafahamu Mungu zaidi ya 10000 duniani kote na wala si amini uwepo wa hata mmoja
 
Sijui vipi niweke nieleweke.

Ila nahisi Kuna Atheist wa mkumbo kama mimi nilivyohitaji kuwa.

Na Kuna real atheist,sasa pengine hawa real one wako real pia ila hawa wa mkumbo Kuna muda kwenye real life uhisi Kuna vitu haviko sawa wanajikaza tu.

Unamkataa Mungu jamiiforum haafu in real life sio kweli
Upo sahihi sana mkuu, ndio maana baadhi yao wamekuwa wakishikilia sana masuala ya uthibitisho ili ukishindwa kuthibitisha naona kwao huwapa faraja.
 
Upo sahihi sana mkuu, ndio maana baadhi yao wamekuwa wakishikilia sana masuala ya uthibitisho ili ukishindwa kuthibitisha naona kwao huwapa faraja.
Wala hakuna faraja , watu wanataka kuujua ukweli , ukiona mtu anataka mpaka uthibitisho ujue alisha amani mpaka basi ila kuna vitu kavitilia mashaka akaacha kuamini
 
Basi achana nayo, wewe elezea tu msingi wa hoja yako yenye kufanya useme Mungu angekuwepo usingehitaji kuambiwa kuwa yupo.
Mama samia yupo hivyo sina haja ya kuomba uthibitisho wa uwepo wake nitaonekana kichaa dhana ya Mungu ni tata na hasa ukichukulia vitabu vinavyosemakana ni vya kwake ndio kuna mikanganyiko kibao
 
Sijui una lenga nini ndio maana nimekuuliza ila mtoa mada hataki kuamini tena kitu bila uthibitisho sasa hapo cha kujadili ni kipi?
Kama hivyo ndivyo alivyoamua ni haki yake ila siku zote uthibitisho sio ndio wenye kufanya jambo kuwepo na ndio maana kuna mambo yalipingwa sana huko zamani kwa sababu hayakuwa na uthibitisho wa kisayansi, ila baada ya miaka mingi mbele leo hii yana uthibitisho hivyo kutokuwepo kwa uthibitisho haiondoi uwepo wa kitu.
 
Back
Top Bottom