Proof of God

SatCitAnanda

JF-Expert Member
Dec 11, 2022
643
1,090
(Usomaji wa dakika 25)

PRAISE OUR LORD JEHOVAH!!!

PRAISE JESUS!!!

Whatever name you have for him (him being a symbol for Order), we all recognize him.

It took me being a Mum and going through crap to come to this realization.

Ikanibidi nikubaliane na maneno niliyasikia kwa Dr. Jordan Peterson kuwa "the pathway to enlightenment is barred by the necessity of passage through hell, and no one wants to go there, otherwise the whole world would be enlightened."

Sasa nikuulize,

Je, unachukizwa na uovu na maumivu katika ulimwengu huu? Vita, umaskini, utumwa, jeuri, chuki na mengineyo?

Hata kwenye jamii tunazoona zina amani na maendeleo kuliko zingine bado wanakumbwa na viwango fulani vya uhalifu, familia kuvunjika, matumizi ya madawa ya kulevya, magonjwa ya akili n.k.

Bado hatujaongelea magonjwa, ulemavu, kifo, na ushindani usio na huruma tunaoona kwa viumbe hai (Mfano wanyama kula wanyama wengine n.k).

Haya yote ukiangalia kijuujuu utasema yanaonyesha dhihaka kwa wanaodai kuwa ulimwengu umeumbwa na Mungu mwenye haki na upendo.

Sasa ngoja nikwambie,

Huwezi kukataa uwepo wa Mungu kwa misingi ya uovu na mateso uliopo ulimwenguni, isipokuwa kwa viwango vya maadili thabiti visivyotia shaka (objective moral standards).

Kama ambavyo hatuwezi kusema mstari umepinda bila kuulinganisha na ulionyooka,
basi kitendo, mtu au hali haiwezi kulaaniwa kuwa sio haki/sawa bila kuulinganisha na haki kamilifu.

Sasa Je, viwango vyetu vya mema, kweli na haki vinatoka wapi?

Kama viwango hivi ni vya kibinafsi, kama mapendezi yetu binafsi ya nguo, chakula na burudani,
basi kwa bahati mbaya hatuwezi kutumia viwango hivi kukosoa wengine au kutetea malalamiko yetu juu ya ulimwengu, na hivyo hukumu yetu juu ya uwepo wa Mungu na wema Inaporomoka.

Lakini tukiona kuwa kuna viwango vya maadili vilivyoandikwa mioyoni mwetu ambavyo vimesimama vyenyewe, vimekamilika na vinaishi milele, ambavyo vinatoa hatia kwa matendo kama uuaji, wizi, ukandamizaji n.k, na vinatudhihirishia kuwa upendo ni bora kuliko chuki, Basi tunabaki na swali kuwa Huu utambuzi uliosimama imara kuelekea kweli unatoka wapi??

Hizi hisia za kuwa na wajibu kimaadili na utambuzi wetu wa mema na mabaya unatoka wapi?

Mantiki ya wakana Mungu inayojipinga yenyewe

Ndo hapa kwenye swala la chanzo cha ufahamu wa binadamu (consciousness) na viwango vya maadili ambapo falsafa ya wakana Mungu inafeli mitahani ya uaminifu na ukweli.

Kama wakana Mungu wanakataa uwepo wa Mungu na uwepo wa lengo la kimungu nyuma ya uumbwaji wa ulimwengu, na wanaona binadamu ni mashine za kibayolojia tu bila roho wala nafsi, basi athari za uelewa huu ni kifo cha kimantiki cha falsafa yao (logically self destructive).

Kama falsafa ya ukana Mungu ni ya kweli, basi mawazo yetu, viwango vyetu na maoni yetu tunayoshikilia kwa nguvu ikiwemo uhalali wa hoja za kimantiki, uwepo wa kweli za kisayansi na kihisabati, vyote hivi vinabaki tu kuwa matokeo ya kiajali ya kemia ya ubongo wetu, na mienendo isiyo na mpango wala akili ya atomi (atoms) ya milli yetu.

Hivyo tunakuwa tunajidanganya kwamba tunao uwezo wa kupima mashauri/hoja na kuamua Kati ya mashauri yanayopingana, na ni dhahiri bila uwezo huo hatuwezi kutafuta ukweli wala kupata maarifa.

Hoja zetu zote na mahitimisho yetu yote yanabaki kuwa matokeo yasiyotegemewa ya msururu wa visababishi vya kimwili/kifizikia (physical causes) visivyokuwa na mpangilio wala mantiki ambavyo hatuwezi kuvidhibiti.

Yaani, kama hatuna nafsi/roho, na hatuna muunganiko wa kiroho na Muumba ambaye ni chanzo cha mantiki na kweli, basi bongo zetu na kazi zote za kiakili zimefungwa kwenye mchakato wa visababishi vya kimwili (physical determinism) hivyo kudunisha na kushusha hadhi kama sio kuua kabisa mawazo yote.

Yaani hatutawezi kuwa na uhakika kama mawazo yetu yoyote yanapatana na ukweli, kimaadili au kisayansi, kwasababu tumeishafungwa na kusetiwa kibayolojia kuyawaza , iwe ya kweli au uongo. Mawazo haya yanakuwa hayana umuhimu kuliko sauti ya upepo kwenye miti!!.

Kwa hatua hii ya kudunisha (discredit) mawazo yote, wakana Mungu wamejiua kifalsafa.

Mawazo yao yote kuhusu kweli za kimsingi yanajikataa/yanajiua.

Kwa maneno mengine, hatukubali kweli ya kauli yoyote ile kama itathibitika kuwa ni hitimisho la visababishi visivyo na kimantiki, kama vile uvimbe kwenye ubongo.

Na kama falsafa ya ukana Mungu ni kweli basi mawazo yetu YOTE, msururu WOTE wa kutafuta sababu/hoja, ikiwemo sheria zetu za kutafuta mantiki, VYOTE vina visababishi vya kimwili visivyo na mpangilio.

Mahitimisho yote ya wakana Mungu yanakuwa hayana maana yoyote kama mauzauza yanayotolewa na komputya isiyo na programu.

Yaani, mchakato wote usiopangwa wa ulimwengu (unguided cosmic evolution) hauwezi kutoa hitimisho lililokamilika na linaloridhisha kuelezea uwepo wa maisha na ulimwengu, pamoja na kutoa viwango vya maadili thabiti.

Huu Mchakato wa ulimwengu usiopangwa (usio na lengo wala mwisho) hauwezi kufanya hivyo kwasababu elimu na majaribio yote ya kisayansi yanategemea hoja za kimantiki ambazo uwepo na uhalali wazo haziwezi kutetewa na dhana za ukana Mungu.

Ndio maana NI KOSA kutoa hoja kwamba kwamba hizi sayansi za asili (fizikia n.k) ndo zitatoa KWELI kuhusu ulimwengu na sisi wenyewe zaidi ya DINI.

Sasa kama sisi ni wakaaji wa bahati mbaya tu wa ulimwengu usio na mpango wala lengo, na hatuwezi kuona na kushikilia maana, kweli na umuhimu wowote wa mawazo yetu na maisha yetu, tunawezaje kutetea hukumu yetu dhidi ya uovu na mateso, na kuitumia kama fimbo kuchapia imani juu ya Mungu?

Unaweza kujitetea kwa kusema kuwa hata kama tumetokea bahati mbaya bado tuna uwezo wa kuthamini maisha na kuyapa maisha yetu maana, hivyo tunapata msingi usio wa kidini wa maadili na chuki juu ya uovu kwahiyo sio ajabu wakana Mungu wanapokasirika juu ya uovu wanaoshuhudia.


Pingamizi hilo linakwepa mtanziko (dilemma) ufwatao.

Je, kuthamini na kuheshimu maisha unapaswa kuwa wajibu wa kimaadili unaojidhihirisha wenyewe, na kuwa ukweli ambao kila mtu anapaswa kuutambua , na kuwa sheria ambayo kila mtu anapaswa kutii?

Au ni maonyesho ya hisia zetu za kibinafsi?

Kama kauli ya kwanza ni sahihi, basi hiyo inadhihirisha kwa hakika kuwa akili na mawazo yetu yana mahusiano na kweli flani/ulimwengu flani wa kiroho ulio nje yetu na nje ya ulimwengu wa kimwili,

La sivyo, kama tulivyoona, hatuwezi kukwepa mantiki ya ukana Mungu iliyojifunga kimwili (physically deterministic) na inayojiua yenyewe (self destructive).

Kwa maneno rahisi, hatutaweza kuona ubaya wa tendo au wazo lolote isipokuwa kwa viwango vya maadili tunavyoangazia viwe na sifa ya kusimama thabiti na milele,
ambavyo uwepo wake (viwango hivyo) hauwezi kuelezewa kama hakuna kingine kinachoishi zaidi ya muda, nafasi, na mata (time, space & matter).

Hii ndio hoja hasa iliyokwenye kiini kabisa cha hoja ya maadili kuhusiana na uwepo wa Mungu na wema.

Ukitafakari kwa kina utagundua kuwa, viwango vya mema na mabaya vinavyosimama thabiti na milele, ambavyo huishia kutupa hisia za kuwa na wajibu kimaadili, zina sifa zipitazo maumbile (transcendent) kwasababu hazitegemei muda, saa, eneo, tamaduni, matabaka na hata uwepo wa mwili.

Kwa mfano, kwa namna flani itabaki milele kuwa kubaka ni kosa, kutesa mtoto ni kosa, kumfanya binadamu mwenzio kuwa mtumwa ni kosa, na matendo haya ni maovu na yanastahili adhabu. Na hii ni kweli tuwe maskini au tajiri, hai au mfu, popote tulipo.. Hata ikitokea ulimwengu upotee kesho, bado ukweli wa madai haya ya kimaadili utabaki umesimama.

Kweli na haki vitabaki kweli na haki hata kama hakuna atakayebaki kuutambua.

Ukweli na wema una mizizi ndani ya Muumba na unaangaza sifa zake muhimu na zisizobadilika milele.

Kama kweli tukitaka kuchukulia hisia zetu za kimaadili kwa uzito, na hivyo kuthibitisha kweli tunaguswa na kuumizwa na uovu iliopo, tunapaswa kutambua kuwa kweli na wema ni wa milele na haubadiliki, na tuna wajibu wa kuutii bila masharti.

Sifa hizi za umilele, ipitayo maumbile na ya lazima, zinaashiria kuwa sheria za maadili zilizoandikwa kwenye mioyo yetu zina Uungu ndani yake (divine).

Utambuzi wetu wa kweli, mema na mabaya, una uhusiano na akili zetu na mapenzi yetu (will), kwasababu tunazitambua dhana hizi na kuitikia kupitia akili zetu.

Kupitia ukweli huo, ni busara kuhitimisha kuwa sheria za maadili zenye sifa ya Uungu zina uhusiano na akili yenye Uungu inayoishi milele (eternal divine intelligence), tunayoiita Mungu.

Ukweli unaotuweka huru

Kitendo cha wewe kuchukizwa na kuumizwa na ukatili, uongo, ukosefu wa haki n.k na tamaa yako ya kutamani kuponya wagonjwa, kulinda wasio na hatia, kufariji wanaoomboleza n.k ni Ushahidi Mkubwa kuwa sisi sio maroboti ya kibayolojia tunaoelea bila matumaini kwenye ulimwengu usio na maana.

Uhakika wa maoni yetu yenye nguvu na uzito wa hisia zetu zinadhihirisha wazi mwanga ulio ndani yetu ambao unaangaza akili zetu na kulainisha mioyo yetu,
Lakini pia unatupa changamoto ya kutambua chanzo chake cha kimungu, na changamoto ya kushirikiana kwenye harakati za kuurudisha ulimwengu kwenye usawa wake, kuanzia sisi wenyewe.

Mwandishi C.S. Lewis (1898 - 1963) (mkana Mungu aliyegeuka kuwa Mkristo) aliandika:

The defiance of the good atheist hurled at an apparently ruthless and idiotic cosmos is really an unconscious homage to something in or behind that cosmos which he recognizes as infinitely valuable and authoritative: for if mercy and justice were really only private whims of his own with no objective and impersonal roots, and if he realized this, he could not go on being indignant.The fact that he arraigns heaven itself for disregarding them means that at some level of his mind he knows they are enthroned in a higher heaven still."

Yaani anasema ukaidi wa mkana Mungu juu ya ulimwengu usio a huruma ni heshima kutoka ndani yake kabisa juu ya kitu kilicho ndani au nje ya ulimwengu, ambacho anakitambua kuwa kina thamani na mamlaka, kwasababu kama huruma na haki vingekuwa ni mshtuko wake wa kibinafsi, usio na malengo wala mizizi nje yake mwenyewe, na angelitambua hilo, asingeendelea kuwaka hasira. Kitendo cha yeye kuzishtaki Mbingu zenyewe kwa kupuuzia huruma na haki inayonyesha kuwa kwa kiwango fulani kwenye akili yake mwenyewe anatambua kuwa sifa hizi zimesimikwa kwenye Mbingu za juu.

Uwepo wa uovu hutolewa kama ushahidi na wanafalsafa wengi wa kikristo wa kutokuwepo kwa Muumbaji mwenye akili na upendo.

Lakini kwanini iwe hivyo?

Je, uwepo wa majengo yaliyoundwa vibaya ni uthibitisho kuwa hamna wabunifu wazuri? Au kuwa vifaa vilivyounda majengo hayo vilijikusanya vyenyewe?

Je, uwepo wa ukatili na chuki unaashiria kutokuwepo kwa wema na upendo na hivyo kubadilisha uwepo wake?

Bila shaka hapana.

Kwahiyo tuutazamaje huu mzozo baina ya pande mbili zenye ushahidi unaojidhihirisha wazi baina ya Mungu mwenye upendo na Ulimwengu?

Kwanza tutambue uwepo wa ubunifu wenye akili kwenye asili. Kila tutakapogeuka, kwanzia nyuki wanaotengeneza asali, sisimizi wanavyojipanga kwenye Kazi zao, ndege wanaotengeneza viota, kuzaliana kwa wanyama na mimea, kinga za mwili, mfumo wa chakula, programu za kibayolojia yaani DNA, mfumo tata wa hata seli mdogo kabisa isiyo na vitu vingi.

Sayansi za kisasa zinadhihirisha kuwa tunaishi kwenye ulimwengu uliopangwa, ambao sheria zake na muundo wake unaweza kujadiliwa kwa lugha ya hisabati. Ndio maana baba waanzilishi wengi wa sayansi ya kisasa waliamini katika Muumbaji.

Kwakuwa tayari tuna uthibitisho wa Ubunifu wenye akili pamoja na hali ya kuhuzunisha ya ulimwengu, na tumeona hali hizo mbili hazibatilishi uwepo wa Muumbaji, basi lazima hali hizo zitakuwa zinaendana na kuelezea ukweli wa mambo.

Hali hizo zinapatanaje?

Wengi tuliokulia kwenye utamaduni wa kisasa usio na dini tulikubali kabisa bila kuchunguza kwa kina kuwa sayansi ya kisasa imeikataa Biblia.

Hasa kwenye zile sura za mwanzo zinazoelezea kupotea kwa paradiso na kuanguka katika dhamibi kutoka kwenye kutokuwa na kosa, ilishindikana kupatanisha simulizi hizo na mafundisho ya Darwin kuhusu binadamu kutoka kwenye unyama mwitu kuja kwenye ustaarabu.

Pia hatukupenda jinsi simulizi hilo lilivyoashiria kuwa dini/Mungu huchukizwa na uhuru na utambuzi. Ilionekana kama Mungu ni dikteta flani anayetaka watu vilaza wasiojua mambo kama watoto na wabaki kutii mamlaka kipofu.

Hilo pamoja na kusoma maandishi ya wakana Mungu iliweka ukuta wa kibaguzi kuelekea Ukristo kwenye mioyo yetu.

Unaweza kuvunja ukuta huo namna hii,

Mengi tunayojua kuhusu binadamu wa zamani ni kupitia vitendea kazi vyao (artefacts) visivyo bora kama vyetu.

Watu hukimbilia kudhani kuwa wazee wetu walikuwa duni kimaadili na kiakili kuliko sisi, na kwasababu hiyo pekee ni lazima tukatae maelezo ya Biblia kuhusu chanzo cha uovu.

Hili ni linafanya kosa la kuhusianisha maendeleo ya teknolojia na maendeleo ya kiakili na kimaadili wakati hakuna ulazima wa uhusiano wa baina yao.

Wanazi wa Ujerumani (karne ya 20) walikuwa na teknolojia ya kisasa kuliko Waingereza wa karne ya 19 lakini hakuna anayeweza kupendekeza kuwa Wanazi walikuwa wastaarabu zaidi.

C.S. Lewis aliyetajwa mwanzo anaadika kuwa "Kati ya dhamibi kubwa ya ushirika tunayofanya jamii za kisasa ni kuwapima wazee wetu kwa vitu walivyotengeza. Tunasahau ni wao waligundua mambo yote ya muhimu : moto, lugha, nguo, familia, kufuga wanyama, ukulima, meli, mashairi n.k. Kwahiyo sayansi haina chochote cha kusema, iwe kwa kukubali au kukataa, kuhusu fundisho la kuanguka katika dhambi."

Sio hivyo tu, bali tuna sababu mbili kuu za kulichukulia kwa uzito na kukubali fundisho hilo.

Sababu ya kwanza ni ukweli kuwa binadamu tuna kanuni za maadili zilizoandikwa ndani yetu tunazoshindwa kuzitoa, lakini pia ajabu tunashindwa kuzitii.

Tunakataa uovu na kulalamika kuhusu uwepo wake lakini sisi wenyewe tumetiwa doa nao.

Tunakasirishwa na tabia mbaya na mawazo na matendo yasiyo na fadhili ya wengine lakini wenyewe tunashindwa "kumpenda jirani yetu" kama tunavyotakiwa na tunatenda isivyofaa pia.

Na zaidi, kadri tunavyohisi kuwa sheria za maadili zinatia mkazo kwenye akili zetu, ndivyo tunavyozidi kutambua jinsi tunavyofeli kuishi kulingana na matakwa ya sheria hizi.

Je, hii haiashirii kuwa kuna Mchakato wa kuzorota Uliotokea kwenye akili na mioyo yetu sisi binadamu?

Sababu ya pili
ya kutodharau simulizi la biblia kuhusu anguko la binadamu katika dhambi ni la kihistoria.

Jamii nyingi za zamani kwanzia Wagiriki, Waroma, Waskandinavia, Wachina Wana simulizi za upotevu wa paradiso wakati fulani uliopita.

Mshairi wa Kigiriki Hesiod (735 BC) aliimba kuhusu
" a past golden age when ‘The immortals formed a golden race on earth.’ "

Mwanahistoria wa Kiroma Tacitus (55 – 120 AD) aliandika:

"The first race of men, free as yet from every depraved passion, lived without guile and crime, and therefore without chastisements; nor was there need of rewards, when of themselves they followed righteousness."


Je imetokea tu kwa bahati mbaya kuwa a tamaduni za paradiso iliyopotea nje ya Biblia?

Au inaashiria kuwa ni dhahiri kuna anguko lilitokea lililopelekea kuzorota kwa hali ya binadamu, kipande cha kumbukumbu kilichoacha chapa kwenye akili ya binadamu, ikidhihirishwa kwenye nyimbo, mashairi na simulizi.

Mbali na ushahidi wa kimaadili, kitamaduni na kihistoria, sababu nyingine inayodhihirisha uhalali wa simulizi la biblia kuhusu uovu jinsi ilivyo falsafa yenye kusadikika kiasili.

Karne na karne Wanafikra wa kikristo wametambua kuwa upendo wa kweli unahusisha muungano wa hiari Kati ya wawili waliojitoa kila mmoja kwaajili ya mwenzake kwa ajili ya kufurahishana na kufurahia maisha na baraka zake.

Kwahiyo hata Muumbaji alipoumba binadamu wa kwanza aliwapa uwezo wa kuchagua kwa mapenzi yao (free will), ili wazawa wote washiriki pamoja naye (Muumba) maisha yake, upendo wake, furaha yake, uzuri wake pamoja naye na pamoja na kila mmoja.

Tatizo la uwezo huu wa kuchagua kwa mapenzi yako (free will) ni kuwa unaweza kuchafuliwa na kutumiwa isivyofaa.

Uhuru wetu wa ndani wa kuweza kuwa na uhusiano na Muumbaji na wengine kwa maelewano na upendo unaweza kutumiwa kufanya kinyume kabisa na kilichodhamiriwa, yaani tunaweza kuamua kumkataa Muumbaji na kuishi kivyetu.

Na ndicho kilichotokea kwa binadamu. Wazee wetu waliamua kutotii na kuleta madhara makubwa kwao na kwa vizazi vyao.


Mwanzo 2:16-17 BHN
Mwenyezi-Mungu alimwamuru huyo mwanamume, “Waweza kula matunda ya mti wowote katika bustani;

lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, usile, maana siku utakapokula matunda ya mti huo, hakika utakufa.”

images (67).jpeg


Swali la kwanza, kwanini Muumba awape katazo ambalo hawakuwa na uwezo wa kulielewa kimantiki kwakuwa walikuwa kama watoto wasiojua mema na mabaya?

Sababu si kama nilivyowaza mwanzo, kuwa Muumba anataka tuwe kama watoto wakitii kama maroboti kila dai na sheria, bali Muumba alitaka kupima Free will ya uumbaji wake huu mpya ili kuzifanya kamili tabia zao na uhusiano wake nao.

Kwakuwa Muumbaji ndiye chanzo cha wema, kweli, upendo na kweli inayosimama milele, tunalazimika kumpa upendo, imani na utii wenye furaha na bila masharti.

Tunafanya hivi si tu kutoka kwenye moyo wa shukrani kwasababu ya zawadi ya uhai, lakini pia kwasababu kuchunguza na kuitikia shaka Hekima na Malengo ya Muumba kunaashiria ukosefu wa busara wa hali ya juu.

Yeye kama Muumba ndiye chanzo mwanzo na mwisho cha uwezo wetu wa kusababu kimantiki.

Ndiye chanzo cha kweli, upendo na wema.

Tunawezaje kuhalalisha kufikiri kwamba tunajua zaidi yake, au kipi ni bora kwetu, au kipi kitatupa furaha?

Sisi kwa mtazamo wetu finyu wa nafasi na muda (time& space) tunaanzaje kuhukumu matendo na amri za mwenye hekima yote, ujuzi wote na uwezo wote anayeishi kwenye umilele? (Isaiah 57:15)

Kwa viumbe wasiokamilika kimaadili na wanaoishi kwenye ulimwengu ulioharibika na wenye mateso, ni ngumu kumpenda na kumuamini Muumba kama inavyotupasa, hasa tunapopata majaribio na hali ambazo ni ngumu kugundua uwepo wake au kutambua Malengo yake.

Wazee wetu wa kwanza waliishi kwenye mazingira yaliyokamilika, wakimuamini Muumba na kutii sharti ambalo halikuonekana kuleta mateso ya aina yoyote, ndiomaana kitendo kile cha kuasi kilileta maafa makubwa! Na hii inatuleta kwenye ukweli mwingine tunaopata kwenye simulizi hili.

Ndani ya yale mazingira yaliyokamilika ya wazee wetu wa kwanza, njia pekee ya wao kupata utambuzi juu ya "uovu" na hivyo kuona utofauti wake na wema, ilikuwa kupitia kuleta huo uovu wao wenyewe na kuishi matokeo yake.

Kwahiyo lile onyo la Muumba halikuwa tu njia ya kujaribu free will, lakini onyo lenye upendo ili kuwalinda na kuhakikisha masilahi ya hawa watoto wapya wa Muumba.

Kiumbe kumuasi Muumbaji wake ni sawa na mmea kukataa kukua kuelekea jua. Matokeo huwa ni kuharibika kwa mahusiano na kutengana kwa kiumbe huyo na chanzo cha uhai, kweli, upendo na furaha ya milele.

Ndio maana tangu wazee wetu wajitenge na chanzo hicho kupitia kutotii hapo zamani, chuki , magonjwa na kifo viliingia ulimwenguni kwanzia kwa wanyama hadi kwenye ulimwengu asili (nature).

(Mwandishi wa makala hii anasema kuwa safari kutoka ulimwengu wa ukana Mungu wa Bertrand Rusell hadi kwenye mtazamo wa kibiblia wa chanzo na tatizo la uovu ilikuwa ni safari ndefu sana, kiakili na kihisia. Anatumai kushiriki nawe safari hii kumekuvutia na kutaamsha hamu yako ya kujua ukweli)

[Binafsi niseme nakubaliana na uelewa huu, ambao katika kiini kabisa unafanana kwenye dini zote hata kama kwa juu masimulizi yanatofautiana (poteto potato),

ikiwemo za Wahindu ambao ambao uelewa wao ni kuwa Mungu/Muumba ni Ufamahu Mkuu wa ulimwengu (the super-consciousness) na viumbe hai ni visehemu/vipisi vya Ufahamu huu Mkuu, kama matone ya maji yanayotoka kwenye bahari,

viumbe wakiwa matone na bahari ikiwa Muumba,

na asili ya ufahamu huu ni ukweli/uwepo, ufahamu na upendo/ amani (Sat-Chit-Ananda).

Sisi tukiwa visehemu vilivyojitokeza vya huyu Muumba tuna sifa zake kwa kadri fulani, mfano kama alivyo na sifa ya kujitegema (supremely independent) nasi tuna viwango vya kujitegemea, kwahiyo sio kuwa katupa Free Will ila Free Will ni asili yetu.

Kwahiyo kama Muumba huyu ana asili ya upendo, ni asili yetu/lazima kumpenda. Na tukitimiza takwa hili kiasili tu tunajiunga naye na kukwepa ule mzunguko wa kuzaliwa na kufa (reincarnation).

Kinyume chake tusipotimiza hilo takwa la asili tunajikuta kwenye mzunguko huo tena na tena.

images (68).jpeg


Sasa tusipokuwa na free will Upendo unajidhihirishaje? Unaweza kuuishi (experience) upendo kama tu una nguvu ya kuchagua kwa mapenzi yako (Free Will).

Bhagavad Gita verse 9.6 -

"Understand that as the mighty wind, blowing everywhere, rests always in the sky, all created beings rest in Me.”

Watafakuri Wahindu wanaelezea hilo andiko kutoka kwenye kitabu hicho cha Wahindu, kuwa kinaelezea jinsi sifa za Muumba za kujua yote na uweza yote zinavyoapatana na Free will yetu - kuwa tuna uwezo wa kufanya lolote lakini ndani ya mfumo uliokoma (limited).

Mfano unaweza kuchagua kuongea, kutukana au kunyamaza. Lakini huwezi kuimba kama kasuku au kuwasiliana na sauti kama wanyama wanavyowasiliana.

Tumepewa miili na Muumba wetu yenye ukomo wa uwezo lakini tuna nguvu ya kuchagua chochote kwa mapenzi yetu kadri ya mfumo huu tuliopewa.

Ndomaana sisimizi akikutana na mti anabadilisha muelekeo lakini tembo anaweza kuamua kuuparamia na kuuangusha kisha kuendelea na uelekeo huo huo.

Wanaohoji swala la Free Will huwa wanalazimisha aidha tuwe na Free will kamili (absolute) au tusiwe nayo kabisa. Absolute Free will ni sifa ya Muumba sio yako.

Muumba ni kama mvua inayonyesha pote na kusababisha mazao, lakini mvua haiamui mazao gani yatakayoota.

Uwezo wa Free will umetupa nafasi ya kufidia upendo wa Muumba kwa mapenzi yetu wenyewe na kuanzisha safari ya kurudi kwake.]

AMEN?

Karibu.
 
Kukaidi agizo la Muumba na kula tunda ni jambo zuri au baya?
Kama ni jambo baya je freewill maana yake ni kuwa binadamu aliumbwa na uwezo wa kutenda baya hata kabla ya kula tunda la ujuzi wa mema na mabaya?
Kama si baya je binadamu alikula tunda bila uelewa kuwa anafanya jambo baya?
 
Kukaidi agizo la Muumba na kula tunda ni jambo zuri au baya?
Kama ni jambo baya je freewill maana yake ni kuwa binadamu aliumbwa na uwezo wa kutenda baya hata kabla ya kula tunda la ujuzi wa mema na mabaya?
Kama si baya je binadamu alikula tunda bila uelewa kuwa anafanya jambo baya?
Na kwanini shetani apewe nafasi ya kupiga story na mwanadamu ????
 
rne na karne Wanafikra wa kikristo wametambua kuwa upendo wa kweli unahusisha muungano wa hiari Kati ya wawili waliojitoa kila mmoja kwaajili ya mwenzake kwa ajili ya kufurahishana na kufurahia maisha na baraka zake.

Kwahiyo hata Muumbaji alipoumba binadamu wa kwanza aliwapa uwezo wa kuchagua kwa mapenzi yao (free will), ili wazawa wote washiriki pamoja naye (Muumba) maisha yake, upendo wake, furaha yake, uzuri wake pamoja naye na pamoja na kila mmoja.

Tatizo la uwezo huu wa kuchagua kwa mapenzi yako (free will) ni kuwa unaweza kuchafuliwa na kutumiwa isivyofaa.
Sure thing, free will ni muhimu ili kuuexperience upendo
 
Kukaidi agizo la Muumba na kula tunda ni jambo zuri au baya?
Kama ni jambo baya je freewill maana yake ni kuwa binadamu aliumbwa na uwezo wa kutenda baya hata kabla ya kula tunda la ujuzi wa mema na mabaya?
Kama si baya je binadamu alikula tunda bila uelewa kuwa anafanya jambo baya?
Kumkaidi Muumba ni kama mmea kukataa kuota muelekeo wa jua. What happens?

Hawakuwa wanajua ubaya ni nini na njia pekee ya wao kujua ubaya/uovu ni kwa kuuleta wenyewe duniani.

Wakati wanapewa katazo hawakujua kifo ni nini, ndomana ni kukosa busara kuhoji maamuzi ya Mungu, kama kuhoji kwanini hadi sasa hivi miaka elfu imepita bado hajarekebisha mambo wakati cha moto tumeshakiona.

Ndio waliumbwa na uwezo wa kuamua kutotii i.e walipewa free will, otherwise wangekuwa marobot ya kibayolojia.

Wahindu wanaamini uovu na wema ni asili ya ulimwengu, ambapo uovu ni matokeo ya kutojua (ignorance) na wema ni matokeo ya hekima (wisdom),

na kadri ya matendo yako utapata adhabu na thawabu, na utaendelea kwenye mchakato wa kuzaliwa na kufa (reincarnation), utazidi kujisogeza au kujirudisha nyuma kutoka kwa Mungu, hamu yetu kubwa maishani ikiwa ni wokovu kutoka kwenye mchakato huu na kufika kwa Mungu, na mwishowe kwa Mungu hakuna uovu wala wema, hizi ni sifa za huku kwenye ulimwengu uliofungwa (conditioned).

Wahindu wana "the pie philosophy of Brahmann".

Inasema "As the diameter of a circle increases by one unit, the circumference of the circle increases 3.14 times. Similarly, as your knowledge of Brahmann (God) increases by one unit, your Ignorance of Brahmann will increase 3.14 times.

So let me just declare that I trust the Supreme Intelligence, whatever the truth is.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Shetani aliutoa wapi ushetani wake? Ni kwanini aliaminiwa na mwanadamu kwenye jambo kubwa na muhimu kwenye maisha ya mwanadamu?
Watafakuri wa kikristo wanasema free will ilianza kufanyiwa kazi huko huko kwenye dimensions zingine 😂 i.e malaika walichagua kuasi.
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Watafakuri wa kikristo wanasema free will ilianza kufanyiwa kazi huko huko kwenye dimensions zingine 😂 i.e malaika walichagua kuasi.
Ili uchague ubaya lazima uujue. Inamaana Hivi viumbe viliufahamu ubaya kabla havijauchagua.
 
Kutokutii si ni jambo baya? Mtoto anayekosa utii anafanya jambo zuri au baya?
Kuonesha Mungu ana Hekima kubwa kukuzidi wewe anajitetea hivi, kwa kukuuliza swali wewe mtoe Majibu.

"Warumi 9:20-21
[20]La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi?
[21]Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?"

Tupe majibu sasa hata kama ni wewe ndie ungekua mfinyazi (mbumbaji/mtengenezaji) kile ulichokibumba/ kukitengeneza kinaweza kuanza kulalamika mbona wewe si fundi mzuri umenitengezeza nikiwa na kasoro nyingi ? sitaki niongezee kitu fulani niwe vizuri nitakavyo ???

Utakubali mtu wako wa udongo atoe lawama ??? 🤣
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kuonesha Mungu ana Hekima kubwa kukuzidi wewe anajitetea hivi, kwa kukuuliza swali wewe mtoe Majibu.
Hahaha...

Amejitetea kwanini?

NOTE: Kuna uwezekano mkubwa mafungu haya hayamaanishi Kujitetea.
 
Hahaha...

Amejitetea kwanini?

NOTE: Kuna uwezekano mkubwa mafungu haya hayamaanishi Kujitetea.
Jibu swali umeulizwa, mbona unachembembe chembe za ubishi pro max 🤣🤣🤣
 
Si maandiko ya neno la Mungu hayo, nimeweka na kifungu sasa uzushi unatoka wap?
Kifungu hakina shida ila namna ulivyotafsiri. Ni mazingira yapi yalimfanya Mungu ajitetee? Kwanini ajitetee?
Binafsi sioni utetezi ila karipio kwa wanaokosoa uumbaji wa Mungu. Mfano mtu mfupi kuona kakosewa kuumbwa.
 
Kifungu hakina shida ila namna ulivyotafsiri. Ni mazingira yapi yalimfanya Mungu ajitetee? Kwanini ajitetee?
Binafsi sioni utetezi ila karipio kwa wanaokosoa uumbaji wa Mungu. Mfano mtu mfupi kuona kakosewa kuumbwa.
Kalipik na kwako na wewe unaesema kwanini Mungu utuwekee shetani?, kawanini uweke me na Ke?, kwanini uweke Tunda la ujuzi wa mema na mabaya ?

Just the same with all of your questions.
 
Kalipik na kwako na wewe unaesema kwanini Mungu utuwekee shetani?, kawanini uweke me na Ke?, kwanini uweke Tunda la ujuzi wa mema na mabaya ?

Just the same with all of your questions.
Duh! Hayo umetoa wapi? Embu rudi huenda hukunielewa. Yote niliyouliza ni kutaka kujua iwapo ubaya ulikuwepo kabla ya dhambi kutokana na uchaguzi wa kutokutii kwa binadamu na shetani.
 
Back
Top Bottom