Nimeamua kuwa Atheist

Nimeamua kuwa Atheist

Ila mkuu hii hoja ya uthibitisho kuwepo kwa Mungu ni atheists tu naona huileta hii hoja kama kutaka waonekane wao ndio wako sahihi ila kimsingi haikupaswa hata kuwa suala la kujadili. Kwa sababu msingi wa uwepo wa Mungu upo kwenye kuamini kuwepo kwake na ndio maana hata yale matendo(maamrisho) anayotenda mwenye kuamini huwa na malipo yake kwa sababu hamuoni huyo Mungu na hakuna uthibitisho ila kakubali kukubali kuwa yupo na anatekeleza maamrisho kwa imani.
Wapi wameileta ?
 
Kila mtu aamini anachokiamini,anayeamini Mungu yupo aishi kwa kumuamini Mungu na asiyeamini uwepo wa Mungu nae aishi maisha aliyo yachagua,

Hua sioni mantiki yeyote ile ya watu kubishana kuhusu uwepo wa Mungu au kutokuwepo, coz haya mabishano hayatokuja kua na mwisho wala kupata mshindi au mshindwa,

Kuna watu humu JF miaka na miaka wapo kwenye haya mabishano ya uwepo wa Mungu au kutokuwepo kwa Mungu,

Kwanini utumie nguvu na muda wako kubishana au kujadili hii issue? Wewe amini unachokiamini kisha piga kimya,

Hakuna haja ya kupangiana namna ya kuishi hasa kwenye mambo ya kiimani,

Sijaona hata mantiki ya mleta mada kuutangazia umma kuhusu uamuzi wake,

Kila mtu afuate anachokiona ni sawa kwake,tukutane mwisho wa safari kwa wenye kuamini.
Well said!
 
Wakristo ni wengi sana manabii na mitume wengi pia ila kuna waongo na wakweli! Kuwajua ndio mpaka uwe ndani ya imani!
Imani zote ni imani tu hazina uthibitisho wa imani ya kweli wala ya uwongo , hiyo ya kusema imani yako ndio sahihi na inapaswa kufuatwa ni ego za kimani na kampeni zake tu
 
Tunaomwamin Mungu tunajua hizi ni siku za mwisho, so watu Kama wew mnaopinga uwepo wa Mungu mtazidi kuongezeka
 
Madai ya kutaka uthibitisho wa kuwepo Mungu ni atheists ndio huleta madai hayo, wao ndio hufanya hitimisho kwa kusema hakuna Mungu kwa sababu hakuna uthibitisho.
Wanadai tu bila nyie kudai yupo?
 
Imani zote ni imani tu hazina uthibitisho wa imani ya kweli wala ya uwongo , hiyo ya kusema imani yako ndio sahihi na inapaswa kufuatwa ni ego za kimani na kampeni zake tu
Kama ni hivyo kusingekuwa na huu ubishani wa kuhusu imani ya kuwepo Mungu, kwa maana wasioamini wangeacha tu hii imani kama ilivyo.
 
Kama ni hivyo kusingekuwa na huu ubishani wa kuhusu imani ya kuwepo Mungu, kwa maana wasioamini wangeacha tu hii imani kama ilivyo.
Hakuna anaewafuata kanisani au misikitini kuwataka uthibitisho wa uwepo wa Mungu , unajua kwanini?
 
Dhuluma ,uonevu mfanye ninyi binadamu lawama umpe Mungu.
Vaa viatu vya mungu.ungekuwa wewe ungefanya nini?
 
Wanadai tu bila nyie kudai yupo?
Sie tudai huku tukijua na kueleza kuwa ni imani hayo madai yetu, sasa shida inakuja kwenu mnapokuja kusema mnataka uthibitisho hamtaki imani na mwishoni mnahitimisha hakuna Mungu kwa sababu hakuna uthibitisho.

Hapo ndio mie nawashangaa atheists.
 
Kama ni imani tu wala hakuna uthibitisho, hivyo basi hakuna sababu ya kutaka na mimi niamini, kuamini ni haki yako wala hakuna anaekunyima kufanya hivyo .
 
Back
Top Bottom