Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Pamoja chief..you are welcome.. kuna elim pana sana huku katika ukristo sijui ni kwanin wachungaji wame concerntrate kwenye vitu common common hiv vya kila siku ambavyo pia hawavichimbui kwa ndani, lakin kuna mambo mengi mnoo huku. The doctrine is soo wide about the bible.. the bible explain about earth speherical shape, kuna biblical archeology, huku current days event prophecy ambazo hiz ziko very deeply elaborated katika the study called Eschatology.

Alot of things kwakwel
Unaonaje ukifungua kanisa ila muhasibu ni mimi
 
Ilikuwa ni siku chache kabla sijatimiza miaka 18. Nilipelekwa Tanga, kijiji kimoja kipo karibu sana na mpaka wa kwenda Kenya. Kabla ya kuingia huko kijijini ndani kuna ki mji kinaitwa Duga. Ilikua sio mara yangu ya kwanza kupelekwa huko kwa mambo ya kimila na jadi.

Lakini hii ya safari hii ilikua kidogo yakutisha. Kijiji chenyewe kipo ufukweni kabisa na kina mito miwili inapita, mmoja Kaskazini mashariki ya kijiji, huu mkubwa kiasi na mmoja mdogo unapita kusinii ya kijiji. Kwa hio kijiji ni kama kimezungukwa na maji, maana mashariki yake ni bahari ya hindi, Kaskazini mto na kusini mto. Magharibi tu ndio kuna njia ya kwenda mpaka barabara kubwa ya lami, ambayo ipo kama kilomita 3 au 4 kutokea hapo kijijini.

Safari hii ilikua ni nzito kidogo kwa sababu niliambiwa unaweza kukaa kijijini huko wiki moja au mbili, itategemea na "babu" huko ataamua kama mambo yako tayari au bado.

Nilifatana na Baba na Mama yangu kwenye gari la nyumbani mpaka hapo barabara kuu kutokea Tanga, hapo nikakuta vijana wawili wakubwa kwangu, wananingoja na baiskeli mbili, moja ya kunipakia mimi na moja ya kupakia mizigo yangu.

Mizigo yangu kweli ilikua mingi, yangu binafsi lilikua ni begi kubwa na racksack ya mgongoni, lakini kuna maboksi kama matatu makubwa yalikua ya mama akanambia haya yote mkabidhi babu yako mkifika.

Basi tukaagana pale, wao wakanambia ukimaliza kazi yako watakuleta hapa barabarani utapanda gari za kuja Tanga, sisi utatukuta Tanga, tutakuja baada ya wiki mbili, kama utakua umemaliza kabla ya wiki mbili ukifika Tanga tusubiri. Wakaondoka zao, na mimi nikapakiwa kwenye baiskeli kama abiria, na nyingine ikafungashwa ile mizigo yetu yote, ikatangulia.

Hatukuchukua muda sana, tukafika kijijini, moja kwa moja mpaka kwa babu yangu. Babu yangu tunajuana sana, na alikua ni sahiba yangu sana, ni mtu ma story ya kizamani na mimi nilikua mdadisi sana. uzuri wa babu alikua hakwepi swali lolote utalomuuliza na alikua hamumunyi maneno, anakujibu mpaka likuingie. Nilikua namshangaa sana, kwani hakuna swali lilililokua gumu kwake.

Hata niwe na swali, mwenyewe naliona gumu kweli, nikimuuliza babu ananijibu huku ananisifia "swali zuri sana hilo", ananijibu kiurahisi kabisa, mengine huwa anachukua muda kuyajibu, mtindo wake wa kuibu ulikua kama anakusimulia hadithi, anaweza akatoka kabisa nje ya swali ulilomuuliza lakini atakuhadithia mpaka utalipata jibu. Mara nyingi akikujibu basi lazima utakua na maswali mengine mawili matatu ya kuuliza. Kwa ufupi alikua anaelewa kufungua "kichwa" kwa mujibu baba yangu.

Tutaendelea baadae.
Safi.
 
Inaendelea kutokea post namba 1.

Babu akatupokea pale, tukakumbatiana kwa futraha, mara na bibi nae akaja aliposikia nimefika, akanambia "aah, sasa mume wangu ndio kaingia, sio hiki kizee, sina habari nacho tena". na yeye bibi akanikumbatia akanipiga mabusu ya ngubu ya shavuni, akanambia twende ndni mume wangu, nimekutayarishia chumba chako.

Nyumba ya babu yangu ilikua ni kubwa sana kwa maisha ya kijijini, ina vyumba self contain vitatu, umeme utafikiri upo mjini. maana umeme umepita hapo hapo kijijini kwao, wenyewe wanasema huu unakwenda Kenya, unagtokea Hale. Kwa ufupi hauhisi kabisa kama upo kijijini mpaka utoke nje ya boma lake. babu alikua na nyumba hiyo yake kubwa na nyingine ndogo ndogo za vyumba viwili au kimoja zimetapakaa pote kumzunguka. Nyingi zilikua za kufikia wageni wanaokuja kwa matatizo yao kwa babu yangu, babu alikua mganga wa jadi, tena anaesifika kweli. Kwake hapakosi wageni, mpaka mawaziri utawakuta huko. Kila mmoja na shida yake.

Babu toka nimefika alikua haniwachi peke yangu, ana nyumba moja ipo karibu na kwake hiyo mwenyewe ndio ofisi yake, ina chumba kizuri tu, cha kufanyia shughuli za ke na wageni wake, na kama ina baraza kubwa ndipo wanapoisubiri wageni wanaokuja kumuona, na ina vumba viwili vidogo ndani, mwenyewe anavoiita "operation rooms". Babu alikua anaongea na kuandika Kingereza na Kijerumani kwa ufasaha kabisa. Kabla ya kaumua kurudi kuishi kijijini alikua ni fundi mekanika, tena fireman, wa idara ya vifaa na magari ya serikali hapo Tanga. Alikua ni mtu anaejulikana sana Tanga na anaheshimika sana. Ni mcheshi sana, kutwa anatabasamu, akikasirika humjui kabisa, wewe kutwa kucha unamuona ni mtu wa furaha tu.

Itaendelea.
Uko vizuri
 
Inatokea post namba 43.


Usiku huo ulikua hauna matukio yoyote, nililala usingizi mnono kabisa, isipokua niliamka alfajiri sana, kutoka kwenye ndoto iliokua ndefu kidogo.

Wakati najitayarisdha kuamka sawa sawa, nikasikia kwa nje sauti ya babu "hodi, hodi, hodi bwana mkubwa bado umelala? Amka tusali bwana. Fanya haraka bibi yako kanipa kahawa na visheti nikuletee".

Nikaamka nikiwa fresh kabisa, usingizi ulikua umenitosha kabisa na zaidi. Kutoka nje nikamsalimia babu nikaenda kwenye mto nikatawadha nikarudi, njiani nikakutana na mwanafunzi wa babu na yeye kishaamshwa na babu.

Babu akanambia kunywa kahawa wakati tunamsubiri mwenzako arudi tusali. Akanitilia kikombe cha kahawa, akanambia kuna visheti pia, nikamwambia visheti baadae babu, tukisha sali. Mwanafunzi aliporudi akakimu sala, tukasali pamoja.

Tulipomaliza kusali, tukatia kikombe cha kahawa tukaanza kunywa na visheti. Kimya kimya, baada ya kama dakika kumi, mwanafunzi wa babu akaaga, akasema atarudi baada ya muda si mrefu.

Alipoondoka tu, babu akaniuliza, vipi umelalaje pangoni? Nikamwambia nimelala hata sijijui kabisa. Babu akacheka. Nikaendelea, isipokua babu nimeota ndoto moja siielewi elewi, sasa hivi ndio inanijia kichwani. Babu akasema, kama unaweza nielezee ndoto yako. Nikaanza kumuelezea.

Nimeota kuna mtu kaja, lakini sura yake siikumbuki, anasema yeye kaja kwa ajili yangu. Yeye anafanya kazi na wewe babu kwa miaka mingi sana, na mimi inabidi nianze kuijua hiyo kazi kupitia kwako na yeye atakua ananisaidia katika hio kazi. Hapo babu sijamuelewa kazi ipi, kabla sijamuuliza ikawa nimeamka.

Babu akacheka, akasema "si nilikwambia wewe ndio mrithi wangu?". Nikamwambia, babu mimi nirithishe mali zako, kazi zako mimi siziwezi. Babu akacheka, akasema mali nikiondoka kabla ya wanangu watarithi wanangu, wacha tamaa. Nikacheka. Babu akaendelea, akanambia kazi zangu ni nyepesi sana Bwana Mkubwa, wewe unachotakiwa kufanya, akija mtu ana shida yake yoyote usithubutu kumwambia hapana au hujui. Usichokijua chochote niulize mimi. Kuanzia ukiondoka hapa wenye matatizo wataanza kukufata, usiwatoe njiani hata siku moja. Wewe wasikilize, nipigie simu, na yule aliekuja ni ruhani wangu, ana akili sana na anajua mambo mengi sana. Saa zingine atakutatulia matatizo ya watu bila wewe kunambia mimi. Lakini yatakujia mambo madogo madogo tu, yale makubwa mpaka ufikie miaka 35 mpaka 45 babu, usiogope. Mpaka wakati huo utakua umeshazowea.

Babu akaendelea, kama umemsikia na umekumbuka ina maana ushafunguka wewe. Huna haja ya kukaa hapa muda mrefu, tutatimiza ada ya siku chache kabisa za kukaa, nazo ni siku tatu. Lakini siku zijazo mwenyewe utataka uje pangoni hapa, utakua na mambo mengi ya kufanya. Leo usijitie dawa yoyote, kakoge maji ya chumvi halafu kakoge maji ya mtoni, ukimaliza njoo tumalizie kahawa.

Nikaenda nikaogelea baharini, nikakuta kuna kama watu watano wapo baharini wanaogelea kwa mbali kidogo na mimi, lakini nikaona wao hawajavua nguo, wapo maji yanawafika tumboni. Sikuwatazama sana nikatoka baharini nikaenda mtoni, nikakoga maji ya mto. Kamba walikua wamejaa tena wameshakua wakubwa wengine, nikatoka.

Nikamwambia babu, kamba naona wamekua wakubwa tayari, akanamabia, hao wa kuanzia kesho babu, kesho kwenye dimbwi lile kubwa hakuna pakukanyaga. Ndio msimu umeanza, kesho ndio watakua kamba wazuri. Tena mbele huko kuna wale wakubwa kabisa, nao kesho wataanza kuvunwa kwa wingi. Babu akaniuliza hujakutana na watu wanavuna kamba huko? Nikamwambia sijakutana na mtu babu isipokua nimeona watu wanaogelea baharini lakini kama wamesimama tu maji yameishia tumboni. Babu akacheka, akanambia wewe macho yashagfunguka hayo. Hao hata mimi niliwaona nilipokua nakuletea kahawa. Babu sasa utayoyaona usiogope, utaona mambo na viumbe vingi ambavyo kwa macho ya kawaida huwezi kuviona. Wale uliowana sio watu, wale ni viumbe vingine kabisa wamekuja kwa umbo la binadam tu.

Nikacheka, nikamwambia babu, mambo yenu nyinyi wazee, ya kiajabu ajabu tu. Babu akanmbaia yashakua yako sasa, usiogope tu. Lakini usiwe na wasi wasi bwana mkubwa, wewe una kinga zote kuanzia utotoni, hii tunakufanyia kama ada tu, wewe ulikua huna sababu ya kuja kama sio ada kukuleta.

Babu akaag, akaondoka zake, ile anaondoka tu akaja yule mwanafunzi wake, kumbe hajaenda mbali alikua anangoja babu aondoke tutu arudi. Kukaa kidogo akaja na yle mwingine na kapu lina chupa ya chai, akasema leo bibi yako kaanza kukupikia kuanzia usiku, kuna mikate ya sinia humu na rosti la kamba. Nikamwambia, lete, maana najisikia njaa, kweli, tukaanza kula weote pale. Bibi yangu alikua anasifika kwa kupika. Wale vijana wakasema wewe usiondoke mapema huku tufaidi vyakula vya bibi yako. Huwa anavifaidi babu yako tu ukiwa haupo, sisi hatuvioni. Nikacheka.


Itaendelea.
Simba.
Asante.
 
Inatokea post namba 67.

Nimekaa kaa muda nikajihisi kama kiusingizi, nikaingia pangoni ndani, nikarekebisha mto wangu wa mchanga nikafunika shuka juu ya mchanga, nikachukua mkebe wangu wa pete nikauweka chini ya shuka, pale pale nilipoukuta mwanzo, nikaiweka bakora pembeni hyangu nikajilaza, ukanipitia usingizi mzito sana.

Katika kulala nikaota kaja mtu ambae sura yake simuoni, ananisemesha, ananambia mimi ndio mwenye hiyo pete ulioivaa, leo saa 9 kamili uwe nje ya pango upande wa mtoni kuna uwanja mzuri, nataka kuongea na wewe. Ndoto ndio ilikua hivyo tu, haina jambo lingine zaidi.

Baada ya muda, nikaamshwa na wanafunzi wa babu, wakanambia bibi yako kishafanya mambo, amka umoge tule. Nikaamka, nikaenda mtoni nikajiingiza kwenye maji, leo nikakwepa kabisa sehemu ya dimbwi la kamba, maana nilipopita nawaona wamejazana hasa. Nikaokoga voizuri nikarudi. Vijana wa babu wakanambia tuweke mambo, leo kuna supu ya kamba hapa na pilau la kamba, Bibi kasema hii ni kwa ajili yako tu. Nikawaambia kama ipo supu, kwanza nitakunywa supu, chakula baadae maana nililala mpaka nikae muda kidogo mwili uchangamke. Ile kabla hawajanitilia supu, babu akaja.

Bwana mkubewa leo nimekija kula na wewe, nasikia vimeletwa vitu sio vya kawaida huku, unanitia wivu bwana. Niakcheka, nikamwabia wewe unavifaidi peke yako hivi. Babu akasema, biboi yako sasa hivi anajitutumua kwa ajili yako, hana nguvu kama za zamani lakini si haba, kwa kula tu, hana hiana.

Tukatia supu tukanywa wote, supu nzuiri kweli kweli, bibi yangu kusema kweli anajua kupika, ilikua na chumvi kwa mbali na ina pili pili manga kwa wingi. Yaani sijawahi kunywa supu ya kamaba nzuri kama ile.Babu nae akaisifia, akasema, hii hata mimi sipikiwi, naona bibi yako leo kaamua. Tukamaliza supu, vijana wa babu wakasema sasa hivi hata pilau haiingii tena mpaka baadae. Tukaamka tukatawadha tukasali woyte pamoja, Babu akasema leo nitakutembelea usiku baada ya kusali isha, kuna wageni wengi wacha nikawaone. Leo babu siku yako ya mwisho kulala pangoni. Ukitembelewa na watu usiogope ni kawaida ya hapa. Nikamwambi nishatembelewa babu. Akasema najua, tutaongea zaidi usiku, leo tegemea kutembelewa sana mpaka kesho. Akatuaga akaondoka zake, akawaambia na wanafunzi wake, twendeni, kuna wageni wengi leo. Mwacheni huyu Bwana Mkubwa, kishapazowea huku.

Kweli nilishpazowea kiasi nilihisi kama kero wakiwepo wanafunzi wa babu, nilikua nataka niwe peke yangu sehemu ile, walipoondoka nikatazama saa, nikaona saa 9 bado dakika tano, nikaona goja niende uwanja wa pembeni kama nilivyoota, karibu ya mto.

Itaendelea.
Asante.
 
Naona wewe ndio umekwepa swali.

Naona umeingiza dini, uchawi, kuswali yote katika andiko lako fupi kabisa. Vyote hivyo vinahusiana nini na hii mada?

Umeielewa mada lakini?

Nakushauri, tulia usome mada, ni elimu kubwa sana hii. Uliza kwa unayoyasoma hapa, sio ya kubuni kichwani mwako tu, hutoelewa kitu.

Kuna watu wamenitumia pm kuniuliza kama hiki kisa cha kweli. Napenda kuwafahamisha kua hiki kisa ni cha kweli kwa asilimia 98, labda kuna vionjo vya hapa na pale katika kuandika na fahamu zetu haziwezi kua na kumbukumbu ya mia kwa mia wakati wote, pia kiuhadithia moia kwa mia ni kazi ngumu sa, Kwa hio maelezo ya muhimu yoe ni ya kweli. Kuonana na vumbe visivyoonekana ki kawaida ni kweli, kua babu yangu yuko huko ninapohadithia ni kweli.

Nawahakikishia hakuna ninachozidisha wala kupunguyza isipokua vionjo vichache sana. Pia ieleweke mimi sio mwndishi wa hadithi na jaribu kukifanya hiki kisa kama cha kaiwada lakini naamini si kawaida kwa wengi wenu.

Pia naamini kuna wengine wana visa vya ukweli vingi na vya kusisimua sana lakini hawawezi kuvieleza kwa sababu moja au nyingine. Hata mimi kuyaeleza haya na mengine ya maisha yangu ninafanya juhudi kubwa sana.

Sio wepesi kama nilivyodhani na kuna nguvu kubwa sana inanizuwia, sema nipo namtaalamu, Arsis, siuna shaka wala wasi wasi kabisa.

Kwanza sikuelewa kama Arsis anaongia kunisoma JF, akanambia chochote ninachokifanya yeye anaelewa, kwa sababu yupo kariubu sana na mimi kuliko ninavyofikiria, akanitahadharisha, kama hataki niandike nisingeweza kuandika habari zake.

Sema Arsis, ni muelewa sana, amenikumbusha kua maandiko yangu yawe kwa njia ya kusaidia wengine kuelewa asioyaelewa. Wakiwa wana maswali wajibu kwa kadiri ujuavyo kwa faida yao, sio yako.

Wana JF mnaonisoma hayo ni kwa uchache sana, mengine, nakariisha sana maswali wakati wowote, nipo kwa ajili ya jamii.

Haya ninayoyaandika hapa hayahusiani kabisa na ushirikina. Mimi ni "braza men kwedli kweli" tena yule wa kujirisha sana, Tanzania na duniani, sema majukumu mengine yamenipiga breki kali sana. Na utu uzima umenijia naona niyaeleze niyajuayo labda itakua faiada japo kwa mooja wetu mwengine.

Karibuni muulize mnapokua na swali au maswali, lolote lile, linalohusiana na hiki kisa au lisilohusiana.
Nataka kujua hizo post kutoka #1 inakuja 7,mara 97,mara 108. Ni kwa maagizo ya mtaalam?. Au ni vipi brother Arsis ?
 
Kuna kisa kimoja Cha kweli kabisa naomba Arsis anipe ufafanuzi na Tiba:
Baba yangu ni mgonjwa (maradhi ya akili) wa muda mrefu sana. Maradhi haya yalimpata 1996 nikiwa na umri miaka ..... Kwa kipindi hicho alikua mjasiliamali mdogo huko kijijini na alikua anamalengo ya kuamia mjini Kwa wakati huokwa ajili ya kujitanua kibiashara.

Ugonjwa ulimpata akiwa polini anapasulisha mbao Kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mjini, ghafla akapatwa na hayo maradhi akiwa uko poloni!

Sasa huu ugonjwa una mkangnyiko kutoka na ulivyotokea tunaamini amefanyiwa ushirikina. Kwa kipindi hicho chote watitembea sehem mbalimbali walishindwa baadae wakampeleka hospital akawa anatumia Sindano Kila baadae ya miezi 3. Kuanzia 1998 Hadi 2012 hivi ikawa zile dawa hazisaidii akawa tena Yuko serious sana.

Mwaka 2020 nikazunguka nae Mimi bila mafanikio nikampeleka milembe akapatiwa dawa ambapo hizi dawa alizopewa sasa ni mtihani sana Kwa sababu anatakiwa ameze Kila siku asubihi 3na jioni 1, Hadi Maisha yake yatakapofika mwisho. Kikubwa zaidi zinaua nguvu za kiume.
Kikubwa zaidi sana ni yeye kutotumia dawa hizo na hili hata alipokua anatumia Sindano hilokua ni changamoto kubwa sana. Hii inatokana na kutojitambua kama yeye ana maradhi ya akili.

Sasa hali hapo zamani ilipokua inataka kumtokea alikua anafaham kua siku zijazo atapatwa na hilo tatizo hivyo kama anapesa alikua anampatia mama anamwambia hii ni Ada ya Chama hata kama nikikuomba vipi usinipatie na anaweza akampatia na Pesa nyingine. Sasa Ile hali ikimjia tu anakua na huruma na ukarimu mkubwa sana mtu akija dukani kununua kitu anampatia vingine zaidi au kama Kuna mtu anapita nje anmwita anampatia ama Pesa au Mali kutoka dukani ni hivyo. Ile Pesa aliyokupatia akirudi kwenye hali yake yakawaida anakumbuka vizuri ikipungua hata 100 atakuambia.

Kwa ufupi ugomvi unatokea na hasira zaidi pale anapodai zile Pesa anakua na vitisho vikali na hata kutia kukupiga au kukupiga kabisa. Nilisoma Kwa namna hyo Hadi nikamaliza.

Kwa ufupi Hadi Leo baba yupo ni mgonjwa naomba Arsisi aniambie huu ugonjwa nini chanzo chake na unatibika na kama unatibika anifahamishe wapi atapata tiba.

Nina mengi ya kuongea athari tunazozipata au tuzazopitia kutokana na huu ugonjwa wa baba kama famiia na ukoo Kwa ujumla.
 
Kuna kisa kimoja Cha kweli kabisa naomba Arsis anipe ufafanuzi na Tiba:
Baba yangu ni mgonjwa (maradhi ya akili) wa muda mrefu sana. Maradhi haya yalimpata 1996 nikiwa na umri miaka ..... Kwa kipindi hicho alikua mjasiliamali mdogo huko kijijini na alikua anamalengo ya kuamia mjini Kwa wakati huokwa ajili ya kujitanua kibiashara.

Ugonjwa ulimpata akiwa polini anapasulisha mbao Kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mjini, ghafla akapatwa na hayo maradhi akiwa uko poloni!

Sasa huu ugonjwa una mkangnyiko kutoka na ulivyotokea tunaamini amefanyiwa ushirikina. Kwa kipindi hicho chote watitembea sehem mbalimbali walishindwa baadae wakampeleka hospital akawa anatumia Sindano Kila baadae ya miezi 3. Kuanzia 1998 Hadi 2012 hivi ikawa zile dawa hazisaidii akawa tena Yuko serious sana.

Mwaka 2020 nikazunguka nae Mimi bila mafanikio nikampeleka milembe akapatiwa dawa ambapo hizi dawa alizopewa sasa ni mtihani sana Kwa sababu anatakiwa ameze Kila siku asubihi 3na jioni 1, Hadi Maisha yake yatakapofika mwisho. Kikubwa zaidi zinaua nguvu za kiume.
Kikubwa zaidi sana ni yeye kutotumia dawa hizo na hili hata alipokua anatumia Sindano hilokua ni changamoto kubwa sana. Hii inatokana na kutojitambua kama yeye ana maradhi ya akili.

Sasa hali hapo zamani ilipokua inataka kumtokea alikua anafaham kua siku zijazo atapatwa na hilo tatizo hivyo kama anapesa alikua anampatia mama anamwambia hii ni Ada ya Chama hata kama nikikuomba vipi usinipatie na anaweza akampatia na Pesa nyingine. Sasa Ile hali ikimjia tu anakua na huruma na ukarimu mkubwa sana mtu akija dukani kununua kitu anampatia vingine zaidi au kama Kuna mtu anapita nje anmwita anampatia ama Pesa au Mali kutoka dukani ni hivyo. Ile Pesa aliyokupatia akirudi kwenye hali yake yakawaida anakumbuka vizuri ikipungua hata 100 atakuambia.

Kwa ufupi ugomvi unatokea na hasira zaidi pale anapodai zile Pesa anakua na vitisho vikali na hata kutia kukupiga au kukupiga kabisa. Nilisoma Kwa namna hyo Hadi nikamaliza.

Kwa ufupi Hadi Leo baba yupo ni mgonjwa naomba Arsisi aniambie huu ugonjwa nini chanzo chake na unatibika na kama unatibika anifahamishe wapi atapata tiba.

Nina mengi ya kuongea athari tunazozipata au tuzazopitia kutokana na huu ugonjwa wa baba kama famiia na ukoo Kwa ujumla.
Poleni sana, kwenye kisa chako umesema amezunguka sana je huko mlipozunguka ni kwa waganga?
 
Inatokea post namba 1384

Vionjo vya Arsis 3 Kumwokoa Msukule 1 G.

ilishangaa sana. Kilichhonishangsza ni Jini Bakora. Kwa mara ya kwanza nikajua kumbe anakuja sehemu kama mtu kabisa na hatujui kua ni jini. Siku ile nikafikiri huyu huyu ndio Arsis nini anacheza na akili yangiu? Siku nyingine kabisa nikataka kumuuliza Arsis katika maongezi yetu pale oshen rod, akanijibu kabla sijuliza. Arsis aliua ana ajabu moja ya kunijibu kabla sijauliza. Hua anaanza kama kunipa elimu hya kitu fiulani, huku ananijibuj nilichpotaka kuuliza. Mfano siku hio alikua ananielekeza.aina za majini na majina yao Kiarabu, Kingereza, kiindoneshia.Akanielekeza majini wanaoweza kujibadili na wasioweza, akachomeka na "na jini Bakora" anaweza kujibadili tena jini mkubwa sana. Akija hapa hata jini mwenzake asie na ujuzi anakua hamjui kama huyu jini, atajua huyu binadam mwenye kuoza majini. Nakumbuka siku hio nikataka kumuuliza kwanini ananitajia majina ya majini "kiindonesia", akasema bila kumuuliza. Mke wa mzee Ali ana rouhan ya kiindonesia, ana elimu sana lakini hajibadili kabisa ingawa anaweza. Nikamuuliza, kwanini Arsis. Akacheka, akasema, ameshika sana dini hataki kutumia elimu yake vibaya.

Hayo ya siku ingine jamani. nisiharibu kis, ngoja nimalizie hatraka haraka.

Yule kijana akapelekwa kubvaa, kweli walijua kumchagulia nguo, wakaambiwa wasimtie mafuta mazuri, wkati anavaa wakapewa majani wafukize chumbani kwake, yalikua makjani na mizizi mikavu ilipotiwa kwenye moto, moshi una harufu kama bangi sema huu mzito na unalaia, koo na macho yanawasha washa.Kutoka kapendeza sana na katoka kipara hajulikani kama huyu ndio alikua kama zimwi. Alikua kashika cap yake mpya mtoto wa babu mkononi, nikajua ni mtoto wa babu kampa, maana mtoto wa babu anapenda kweli cap, mwenyeqe anaziita base ball cap, lakini babu alimkataza kuvaa za mtumba. Babu yangu alikua wote anatukataza kabisa kuvaa nguo za mitumba, anasema kama hauna nguo vaa hata kaniki moja au shuka, usivae kafa ulaya. Ukimuuliza kwanini anakwambia nuksi tupu.

Wakaja tukaka nao, lakini ndio haongei, haoneshi kasoro yoyote ile, anasikia, anaguna, anacheka, antabasamu, anajua watu wote. Kuna vijiti kama saizi ya kidole hivi alipewa na jini bakora awe anaweka mdomoni, anatafuna tafuna. kikiisha aweke kingine. Nilijua baadae sana kazi yake ni nini.

kwenye mabasi huko kila mtu anahamu ya kurudi ndani, maana hawajui nini kinaendelea lakini wamepata fununu kijana yupo ndani.

Babu yake akasema muiteni mama'ke, mama'ke akaletwa, akaanza kulia, akamkimbilia mwanae na yeye yule kijana akawa anatabasamu tu, akasimama wakakumbatiana na mamake kama vile anasema sikuachi tena, mama vilio hapo na mtoto vilio na wengine wenye roho ndogo kama Mzee Ali na yeye akaanza kutokwa na machozi na mafua membamba yanamdondoka.

babu: kawaitewni wote na wale wachawi waaje hapa tuagane.


Wakaitwa watu wakajazana kila. anaeingia analia, anakwenda kumkumbatia, wanamsemesha wanawatazama tu kama hawaamini wanachokiona, yeye anatabasamu tu. Anajua kila mtu, kuongea ndio hawezi na kakaa kama zuzu fulani hivi walipokwisha kuwepo wote. babu akasema kwana ztusome Qur'an hgalafu kila mtu aseme lake kisha tuagane. Wakaitwa vijana wa kusoma Qur'an wakasoma, wakamsalia mtume mara mia moja. Walipomaliza.

Babu: jamani mimi naitwa Maruki, sijui kwanini, msiniulize, Huku anacheka. Mimi sio uweo wangu huu kua na ni mtu wa tiba, na yaliotokea yote sio uwezo wangu. Ni Allah katukutanisha na kutujaalia kuokoa wengi sana. Sio huyu tu. waapo huko vijana wengine sita, wengine wadogo sana kuliko huyu. Wapo kama mazimwi kwa hatua tofauti tofauti bila makosa yoyote. Mkitaka kujua ulizeni hawa mbwa, watawaambia sababu zao. Ni sababu zaa kijinga kabisa. Sana sana gtamaa ya utajiri. Haya nyinyi semeni, utajiri unawasaidia nini?

Lakini AlhamduliLlah qote qale na wengine wapo Mwnaza na Tabora, wengi zaidi, walioweza kuokolewa wameokolewa, ambao hali zao mbaya sana, wamekufa na wao, lakini kidogo sana. Hawa mbwa wakiona huwezi kufanya kazi zao vizuri wanakuwacha ufe tu, wanakulisha uchafu maisha yako yote, hao wanakupeka sijui wapi huko, mbwa hawa, mtawauliza wenyewe, mimi naweza kuwaua sasa hivi, lakini itakua hakuna faida. Bado wengine, hawa mbwa , huyu wanawafanyisha kazi bar na kujiuza miili yao. sasa watakua vizuri na hawa mbwa watalipia gharama zao zote. Huyu mshenzi na wenzake wana mali nyingi sana Tanzania nzima, msimuone hivi huyu ni wakala wa shetani wa kichawi. Huyu kunywa damu kwake ni kama wewe na mimi tiunavyokunywa juisi a machungwa. Hatoki kwake asubuhi bila kunywa damu, na yule mbwa wake malaya kishaanza na yeye kunywa damu kama mamake.. Leo umekunywa nini wewe mbwa? Sema,tusikie.

babu ndio nikajua kumbe kuna siku anakua mkali. Alimuuliza kwa kwa ukali kabsa, sauti ikawa inatoka ananguruma, kimoyomoyo nikajisema huyu sasa hivi ni simba. ataua sasa hiuvi, simwingilii kabisa. Yule mama akaendelea, imemwagwa yote ikachomwa moto. kumgtazama babu alivyomkazia macho, nikajiua leo babu kakasirika, hata sura ilikua inaonesha, nikajisemea leo ukimchokoza, simba anakuumiza kama sio kukuua.

Babu: Huyu kapagtikana siku kumi nyuma, tukaanza kazi dakika hio hio, huyu ni mjukuu wangu. wanza tushukuru Mwenyezi Mungu, huyu kijana wetu kupatikana salama. Mimi sisemi zaidi, ni mengi na waliyafanya haya ili huyu mbwa mkubwa wao awe kiongozi mkubwa, kumbe hawajui kila mwizi qna siku arubaini. Mbwa hawa. Maneno aseme mwenyewe.. Haya sema...

Mama Yule; Akaanza kuwaambia ndugu wote kilichotokea mwanzo mpaka mwisho, waliokua wanalia, waliokua wanasema huyu hatufai kwenye ukoo.

babu: Kila mwenye swali lake amuulize huyu na mbwa na hawa wengine. Aliepotolewa na mwanae, mume, mke, dada amuulize huyu mbwa. Huyu kila wiki anaua huyu. Maisha ya mtu kwao hawa ni kama panya tu. Nyie mnaopoteza watoto wachanga, hawa ndio wakuwashika. Mbwa hawa wengine wapo hai waroro lakini hawafai kabisa, wanawapelekea matajiri wakichawi wawaingilie, We mbwa mnaanza kuwaingilia watoto wa umri gani, akmuuliza yule mzee mchawi. Akajibu kuanzia wachanga wa mwaka mmoja tunajaribu, tunawamwagia usoni wankula yote ile na wenzao wanakuja kuwasafisha kwa kuilamba, ndio furaha yao. Mzee yule akanyanyka akmpiga kofi yule jamaa mpaka akaemnda chini, babu akamwabia mwache mbwa huyu. Mtawauliza we nyewe huko, mimi nilitaka mjue uaalimu wao. hayua fanyeni haraka kila mtu aende kwao.

Maswali yakawa kibao, mwengine anauliza umejifunza vipi ,anajibu. Umeanza lini? anajibu, wanagapi ushawafanya hivi ?Akajibu hawana idadi ni wengi sana hatuweki hesabu, ni mwiko kuweka hesabu. Huuyu binti yako kaanza lini hii kazi yako? KUanzia mdogo, huyu ndio kashika kazi zangu zote, mimi sana sifanyi tena nafundisha tu. Mmoja akauliza, kwanini tusikuue? Akasema nimemrishwa kwanza mimi na qenzangu hawa na wengine hamuwajui, turudishe mali zote kwenu na kwa watu tuliowazulumu. Za huyu binti yangu na za huyu na huyu. Baada ya hapo niueni. Sina sababu ya kuishi tena.

Babu: hakuna atakae kuua, na nyinyi na wale mbwa wengine ambao hajauliwa muishi kama mlivyotesa wenzenu. mwengine akasema mimi nipeni huyo binti awemtumishi wangu, mali hio.

EWote tukacheka. Wahuni whawakosekani sehemu.

Watu wakaanza kuuliza wana mali ngapi? yule mama aksema nyingi sana. Akataja nyumba ake zaidi ya kumi na sita, Mwanza huko, mpaka capri pint ana majumba kakodisha, magorogfa Dar. Ana bar kibao zimejaa misukule. Tanzania nzima mpaka nchi za jirani. Mzee Ali akuliza Dubai na Ulaya hamna mali? Wakasema wanazo lakoini huko zina masharti makubwa kuna wakubwa wengine huko, lazima wao wapate aidi, Hatupendi sana huko,

Akataja nyumbani ana masanduku ya noti, kama ishirini na biti yake anayo mengi zaidi, yeye anapenda sana kuweka pesa. Hata godoro lake ni la noitti tupu na mito yake ni maiti za watoto wachanga. Watu wakaanza kunong'ona. wakauliza ziote zao au za wanaushirika wengine ? akajibu zikifika kwako ni zako peke yako, hazina ushirika. Wanapeana faida wakiwa kwenye ushirika na wale wapya tu. Akasema wale wapya lazima wawe na sisi wa zamani ndio biashara zao zipate wateja ziingize mali. wale wanaume wawili mmoja kamuingiza yeye kwenye uchawi, yule kijana ni mtoto wa dadake, mamake alikuwepo pale akasema sio mwanangu kuanzia leo, naahidi mbele ya watu. Yule mwanammme mtu mzima ni shemeji yake ambae mkewe alishakufa siku nyingi, kumbe ni yeye alimuua kichawi, huyo hakufanywa msukule walimtoa kfara ya damu kwa ajili alikua na mdomo sana. Kwa mujibu wake.

ykongewa we.

Babu akasema sasa uamuzi ni wenu ndugu. Huyu kijna atabaki na mimi, nitaondoaka nae kesho aendelee na dawa mpaka akae sawa. Mtaalamu wa damwa hapa kasema huyu wiki tu ataongea.

Mama Yle: hatukumuharibu kwa sababu tulitaka kivuli chake kiwe kiima kisiwe na athari yoyote, kusema andesema kwa sauti ya mwengine, Na aliekua apewe kivuli ni yule kija alaiekwenda kumnunulia nguo. Yaani wote ni ndugu kwenye ukoo.

babu; nani mnamuamini kwene ukoo wenu, wote wakasema yule mzee.

Babu, sasa tunakupa wewe majukumu mazito, mali zao zote hawa watakwend kuwagaia, na kila aliedhulumiwa ndugu au mtoto na hawa au washirika wao, mali zao ziwalipa. Na kabisa walipe gharama zenu nyote mpaka kufikia hapa. Msiwe na wasiwasi hawa ni matajiri wakubwa woe, nyinyi hamjui, mimi nafahamu siri zao zote. Hapa hawa wote wapo chini ya ulinzi wakibwa zao wameuliwa na wengne wamedhibitiwa majeshi mengi na mkubwa yapo kazini. bqabu akaendelea; Huyu kototo, mtoto, mamake na kijana yoyote wa kike na kiume wa kwenye ukoo wa baki nae kwa jili ya tiba. Mama yao akawachagua, hawa ndio wanapatana sana. Wale vikjaja wakakubali kubaki.
Babu: leo hii wakachukue vigtu vyao kama vipo hoteli waje hapa haraka sana, Nyinyi wengine kama mtasafiri hata leo, Hawa wagtakua chini ya mzee wenu, hawafanyi chochote boila yeye.

Mzee: Mimi sitaki hata kuwaona sutra zao.
Babu; Iabidi ustahamili mpoaka mpate haki zenu, mkiziwacha ndio zinachululiwa na wachawi wengine au zinapote hivihivi, hawa hawawe zitena kufanya lolote bila amri yako kuanzia leo, hata kazi yoyote hawawezi kufanya. Yaani hawa ni afadhali mgtu awe msukule kuliko wTvyiku Hawa, mimi nakushauri kila mmoja mpe mtu mmoja awe nae maana hawa hata kuoga hawaendi bila kumarodhwa na mtu utakae wapa. Kila mmoja akaanza kuguna.


Babu akasema haya mtajua wenyewe ndugu, Mzee Ali na wewe baki,wacha waende jawa, na mkitoka hapa asirudi mtu mkifika ndio mtanijulisha safari yrnu, msiogope nyote wapo chini ya ulinzi maisha yo yote hawa mpka kufa kwao.

Wakaondoka kurudi hoteli, mimi namzee ali tukaenda na wale vijana walioambiwa wabaki kuwasaidia kumlea yule kijana na mamake. wamedhukua tu vutu vyao na b)vya yule mama wakrudi, Babu hakukaa tena alikua mwenyewe kishafanya mipango yake akaondoka nao usiku ule bila sisi kujua kwa gari lake na mwane akamapeleka. Siku ya pili anatupigia kisha fika kwake. aksma na nyinyi kipenda kuja njooni mkipenda kwenda nendeni tutawasiliana zaidi kuanzia kesho.

Kwa ufupi yulle kijana na mamake wakaa miezi miwili shmaba kwa babu mpaka akawa mzima kabisa anaongea na anafanya kazi zote, akawa hataki kuridi Mwanza, wakahamia Dar., wanaishi hapo mpaka leo.

Walipata mali nyingi sana kwa wale washenzi, wale walichwa wakawa ndio kam mental, mata)ra ya mwisho ukoo ukawatawanya, wakishia hospitali za vichaa hakuna aliekua anawataka hata kuwaona.

babu alitumiwa million kumi na yule mzee wao. Ni bossa kibwa sana Mwaza, sitaki kumtaja jina ni mtu maarufu sana na mwenye pesa zake. Zilikua ni pesa nyingi sana kwa zamani, mimi akaniwekea tanoi zangu Mzee Ali sijui.

kkazi zote za upande usioonekana zilifanywa chini ya usimamizi wa Arsis.


Kuna kisa kingine cha kukoaa msukule hii ilikua Zanzibar ni tofauti kabisa hiki. Tutakileta siku za usoni.


Tutaendelea.
Kuna huyu Mwanamuziki wa kisabato aliyefariki wiki iliyopita hapo JKCI anaitwa Marco, Ugonjwa unaosemekana kumuondoa ni ugonjwa ambao yeye hakuwa na risk yoyote. Muulize arsis kama ni kapewa ugonjwa wa kwa njia za kichawi au ni imetokea tu bahati mbaya?
 
4 Vionjo vya Arsis. Tiba ya ajabu" 1


Hiki ni kimoja ya kionjo kifupi sana cha Arsis, kasema weka wazi watu wafaidike:

Kwa wale wanaouliza kuhusu tiba jamani, kwanza tuelewane, mimi sio mganga wala sio mtu wa tiba. Mimi Nafahamiana na Arsis nafahamiana na jini Bakora na kisa nimekielezea nilivyowafahamu. Mgtu wa gtiba alikua babu yangu, mimi sijairithi hio kazi. Arsis kuna siku alinambia hivi kuhusu hapa JF.

Arsis, kuna tiba muhimu sana hapa JF. Hao wanaoitangaza sio waganga wala watu wa tiba lakini wanayo. Hiyo mimi naijuwa waliipoata wapi na kwanini waliipata. Sio kupitia kwangu lakini walipewa na jini la ukoo wa guyo mama. Ni jini lipo kwenye ukoo, ingawa alieipata hio dawa ni dawa huyo mzee lakini kwa kuelekezwa na huyoi jini bila yeye kujua.

Mimi: Dawa ipi hio.
Arsis: udongo, unatibu kila aina ya matatizo ya ngozi. ho mjukuu wao aliungua wakaoteshwa tiba mnayo kwanini hamuitumii. Mengine ukiwasoma JF utawaona. Wenyewe wameiita kivyao lakini hio jina lake ni lingine kabisa tunavyoijua sisi.

Mimi: Nipe jina niitafute.

Arsis; Hio dawa kuna watu wajanja, wameiona hapa JF sasa hivi wamebadili majina wanajiita Dokta, haijawahi kushindwa ugonjwa wa ngozi.

Arsis akanipa jina na mimi nikaifatilia, nikampigia huyoi mama akanambia ipo kariakoo, nikaifata , ninayo sijauitumia. Arfsis akanambia ndio hiohio. Usiidharau hhio, inatibu kila kitu kwenyue ngozi, mpaka saratani ya ngozi.
Mimi: Arsis, basi hao waee matajiri sasa hivi.
Arsis: Hawawezi kuytajirika kwa hio dawa, hawajui Wanaofaidika sasa wanaonunua kwao. Lbda wajukuu zao waafaidika wakijua, thamani yake, lakini wapo wapo tu, wamekua wanaiona nyumbanithamani yake, wao wanaona Mwenyezi Mungu kawapa na wao wanasaidia watu, wanaiuza kama bure jinsi ilivyo na nguvu. Labda wajukuu zao watatajirika nayo, lakini wamekaa hawana habari nayo kabisa, kwa kua wanaiona kwao kila siku hawajui kua haiatikani hovyo kama hujaoneshwa ilipo.

Mimi: hapa jamani nitawapa kisa sio cha tiba lakini kinahusiana na mali za ardhini ambazo baada ya kukosa mali za kijeriumani, Arsis akasewma yeye ana kitabu kingine kinatwa "kenz al ardh" maana yake hazina za ardhini, ndio hicho kimefannya aijue hio ytiba ya ngozi na nani anailinda chini ya Ardhi.

Nimeleta haya tiba jamani, wale wanaotaka tiba hata za kusomewa Qur'an au zingine, kuna watu naweza kuwapa namba zao. Mimi sifanyi kabisa. Mi i sio mganga wala sio mchawi. Arsis pia sio mganga wala sio mchawi, anasema yeye anatoia maarifa tu, hatoi uganga wala wal uchawi wala hafanyi utrabiri wala hafanyi ramli.

Natumai nimeeleweka, tiuchote maarifa hapa, halafu kila mtu ajue atatua vipi tatizo lake. Binafsi naweza kusaifdia ushauri na nani na wapi, kwa kua nina marafiki kama Jini bakora lakini sifanyi ano tiba wala sizijui. babu yangu ndio ilikua kazi yake ya tiba, akikuona tu, anajua umebeba hirizi, ankwambia itoe. Mimi hayo siyajui, isipokuwa najuwa watu na majini wabaya wakiepo. Sio utabiri wala ujanja wangu, nina pete ya Arsis na vijini vyake, vipo, lakini mika inapita siku hizisina kazi nao wala Arsis hawatumi kwangu.

Ahsanteni, nimeona hiki kionjp kimenijia nikiweke wazi.

Najibu maswali tu sasa mpaka nikiwa na mida nianze kionjo cha Ungujja cha msukule.
Mkuu Simba na Arsis hii dawa ya kutibu matatizo ya ngozi binafsi naomba kuifahamu kiundani au ni wapi niende ili niweze kuipata na kujifunza?
 
Ndivyo alivyonambia Arsis.

Kuhusu Arsis kuoa, niliwahi kumuuliza, hakupenda kuliongea swala hilo, Nikaliwacha kama lilivyo.
Simba.
20240827_104220.jpg

Embu muoneshe Arsis huu mmea, pia muulize una faida gani mwilini?
 
Hakuna ukweli wowote. Yesu ni Mungu aliyekuwa ndani yake na aliyafanya yote alofanya akiongozwa na roho wa Mungu. Ni jambo dogo kuelewa kama unataka. Kwa namna ambayo Arsis amewajibu maswali kupitia huyu bwana mwenye uzi pale sio huyu bwana ila Arsis mwenyewe ndio kafanya. Akipatia amepatia Arsis sio mwenye uzi. Hivyo hivyo Mungu alikaa na kufanya yote ndani ya Yesu kwa hiyo sio Yesu ila Mungu mwenyewe ndio alifanya. Je, saa hii mnamsifu mwenye uzi kwa ujuzi na hekima au huyo Arsis aliyempa hayo yote?
Naomba nikuache boss

Asante
 
Story nzuri ila uandishi una changamoto! Nataka na Mimi nitunge ya kwangu inayohusu aliens na dunia nyingine ambayo inazunguka majua mawili ambalo huko unaambiwa Kuna binadamu Wana mikono sabasaba
Binadamu ana mikono miwili na miguu miwili, hao wenye mikono saba sio binadamu
 
Ndio maana kusoma neno na kulielewa ni muhimu.. Wakati wote Yesu mwenyewe alikuwa anasema yeye fanyia kitu isipokuwa ameona kwa Baba.. Yaani hafanyi kitu pasipo Baba.. Hujiuliza kwanini hapo msalabani ndio Yesu anasema Baba yangu mbona umeniacha..

Simply ni dhambi zetu ambazo Yesu alibeba msalabani ndizo zilizo mtenga na Baba.. Nimesema huko baada ya Adam kutenda dhambi tulikosa ushirika na Mungu na ndio maana hakuwa anaongea na kila mtu bali wachache aliowachagua.. Dhambi hutenga mtu na Mungu
Naomba nikuache boss,kila mnavyojaribu kunik
Ndio maana kusoma neno na kulielewa ni muhimu.. Wakati wote Yesu mwenyewe alikuwa anasema yeye fanyia kitu isipokuwa ameona kwa Baba.. Yaani hafanyi kitu pasipo Baba.. Hujiuliza kwanini hapo msalabani ndio Yesu anasema Baba yangu mbona umeniacha..

Simply ni dhambi zetu ambazo Yesu alibeba msalabani ndizo zilizo mtenga na Baba.. Nimesema huko baada ya Adam kutenda dhambi tulikosa ushirika na Mungu na ndio maana hakuwa anaongea na kila mtu bali wachache aliowachagua.. Dhambi hutenga mtu na Mungu
Ngoja nikuache boss,kila mnavyojaribu kujibu ndivyo nakuwa na maswali mengi zaidi na mnazalisha porojo zaidi

Asante
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom