Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Sawa Arsis umeelewaka.
Kuhusu Adamu kuwa mtu wa kwanza hilo halijawekwa wazi katika Qur an moja kwa moja namaanisha Quran haijasema wazi kuwa Adamu ndio binadamu wa kwanza ila kuna kitu kinaitwa dalil tul aqil yaani ishara za kiakili kupitia hiyohiyo quran unaweza ona katika surat baqarah aya ya 30 ( AL BAQARAH 2:30) inasema

"وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ۗ قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَنْ يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ ۖ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۗ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ"
"Na Mola wako alipowaambia malaika: 'Mimi ninamteua khalifa katika ardhi,' waliposema: 'Je, utamteua mtu ambaye atatenda ufisadi humo na kumwaga damu, wakati sisi tunakusifu kwa sifa zako na tunakutakasa?' Mungu alisema: 'Mimi ninajua msiyo yajua.' "

Katika aya hii utaona Allah anawaambia malaika kuwa yeye anamteua khalifa katika ardhi hapa unaweza sema adamu kateuliwa na Mola hivyo labda huenda kuna wandamu wengine hawakuteuliwa sasa twende taratibu baada ya mola kumteua adamu aya inaendelea kusema malaika waliambiwa wamsujudie baada ya yeye kufundishwa elimu na mungu kama ilivyokatika SURA YA 2:34 AL BAQARAH

"وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَى وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ"
Na tuliposema kwa malaika: 'Jinyenyekeeeni kwa Adam,' walijinyenyekea isipokuwa Iblisi; alikataa na kujikweza na akawa miongoni mwa makafiri."

Mpaka hapa utaona kuwa hakuna viumbe vilivyotajwa isipokuwa ni Malaika, Adamu na Iblis hii kwanza inatupa alert kuwa Huenda adamu ni binadamu wa kwanza.
Ingawaje madai ya kuwa Adam ni binadamu wa kwanza yametolewa na wanazuoni wa tafsir na hadith hilo halina shaka hivyo madai ya kuwa adamu sio binadamu wa kwanza yanaweza kuwa kweli au kinyume chake ningependa kusikia kutoka kwako Arsis nani ni Mwanadamu wa kwanza na ushahidi uko wapi? Asante.
Kwa haya hizi... Zinathibitisha ya kwamba hakuwa mwanadamu wa kwanza.. ila aliteuliwa.. na kabla ibilisi kuwa kafiri inaonesha kuliwa na makafiri pia.
 
Hilo la kuwa hakuna majinni wakristo, sikupingi. Tunavyoelewa sisi majinni wanaishi umri nrwfubkukiko sisi sasa qai wanaelewa hakuna dini ya Kikristo, ni mchongo wa kishetani tu, sasa jinni atakuwaje mkristo? Haiingii akilini, si atakuwa poyoyo huyo kama wewe?
Wewe dawa yako ,nikupigishwa samasoti siku moja kama mzee mmoja kwenye simulizi hii ,ili ukome ubishi
 
Yaani nimechekeaaa mbavu sina mzee na kitambo anapiga samasoti....bwana Simba Arsis je ni jini wa asili Gani huyo anapiga sarakasi?

Kuna mahali ulisema aidha huzijui sura za jini 1 yaani unaona mtu ila sura haipo au ...namna hiyo. Sasa mlivoenda kojani ulikuawa unawaonaje? Bado sura hazionekani?

Jini 1 alisoma mwaka Gani mlimano?
 
Arsis anasema yeye ni mtu, kama hutaki, vyovyote utavyotaka kumuita yeye kwake sawa tu.

Hapigi samasoti kabisa.
Hivi vijini vina vituko vingi sana, ngoja mbele kido nitaleta vituko vya majini.
Simba.
 
Vionjo vya Arsis - Majini ya Kojani- Pemba 8.

Tuliporudi hoteli, Dokta macho na sura vimemvimba kwa kulia.

Wife; Mume wangu mie nakwenda kukaa na Dokta chumbani, nakuacha peke ako ukinihitaji nipo kwa Dokta, leo si vizuri kumuacha peke yake, she needs a shoulder to lean on.

Nikamwambia, Poa. wakaenda kwa Dokta mimi nikaingia chumba chetu, noikakoga, nikapiga piga simu zangu, kumaliza tu, Mlango ukagongwa nikajua staili ysa Jini 1. Nikamfungulia, baada ya kusa,limiana...

Jini 1; Simba unawabadilisha watu kama babu yako. Mzee Ali huko baada ya wewe kupokea zile pesa kawachiwa afanye kazi zake lakini azifanye kihalali, akirudia kufanya mambo yake ya kishenzi, sasa watajuana Kamanda na wakubwa zake. Vijini vyake vimeachiwa vyote lakini Kamanda ana masharti yao ya kijini anayajua mwenyewe, ukitaka kuyajua wewe utaongea naArsis, hata mimi siyajui..

Kilichonileta hapa. ni kuwaambia msisafri leo wala kesho, kaeni siku zenu kama mlivypokusudia, na wewe leo fanya kila njia uende Kojani ukaione sherehe yao, huna cha kuogopa, na hivi mkeo analala Dokta itakua wepesi kwako, sisi wite tutakuawepo huko, kuna surprise yako.

Mimi; Hata wewe jini unajua "surprise"?

Jini 1; Hivi elimu yote ninayopata kwa Arsis nisijue ' surprise"? Mie nasoma wewe usinione hivi, mwenzako nipo form Vi Sasa hivi karibu namaliza niingie chuo kikuu.
Mimi' Chuo kipi, cha Kijini?
Jini 1; Wala, mimi mtu wewe, nasoma mlimani...

Sasa hayo mengine acha, wewe Arsis kanituma nikuombe uende Kojani, waache kinamama wapumzike, usiwe na shaka, wewe Kojani na Pemba nzima habari zako zitaongelewa na vijini vyote vya kichawi. Huna swali?

Mimi; Kuna maswali mengi sana, lakini najihisi nimechoka, hata huko Kojani sijui kama nitakwenda. Ngoja nipumzike.

Jini 1; kwani huko sasa hivi, wewe fika hata saa tatu kasorobo, shughuli yao inaanza saa tatu kamili. kamuone rafiki yako Mzee Ali anavoendesha shughuli yake. Tutakuepo huko usikose. Kwaheri.

Akaondoka zake, na mimi nikapumzika kidogo tu, wife akaja.

Wife nimemwacha Dokta apumzike kidogo tena kaniomba leo nilale nae, unaonaje?
Mimi; Njaa kali.
Wife; ndicho kilichonileta hicho, mapirika kama ya leo yale sijui kwanini yanaleta njaa?
Mimi; Kujua baadae kwanza tuitoe njaa.

Tukakaa na wife kama lisaa lizima, akakoga akabadili akaenda kwa Dokta. mimi nikakoga nikashuka chini, nikaenda pool, mara wakashuka na wao wakaja poool wapo fresh kabisa.

Wife: Dokta anasema hapo barabarani karibu tu kuna hoteli wanapika samaki wazuri na vyakula vizuri, tutaenda hapo kula?

Mimi; Amueni nyinyi.
Dokta: Bira tukachukue tuje kula hapa.
Mimi; Twendeni tutaamua hapo hapo, kama pazuri tutakula hapohapo.

Tukaenda kufika, kweli ni kama hoteli zozote za Dar, nikaagiza mapande ya nguru wa kukaanga na mchuzi wao wa nguru, ni ka a supu tu, nikala na mkate wa bofulo za Kizanzibari.

Dokta na wife waksema wao chao wanachukua watakula hoteli. nikawarudisha, wife akaja chumbani akachukua chukua vitu vyake, akasema Mume wangu tutaonana alfajiri, nipigie nikichelewa kuamka kusali.

Mimi; Poa.

EWalipotoka nikawa nawaza habari ya Kojani, niende nisiende, nikaona niende tu, si ndio fursa ya kujionea mambo ndio kufungua macho huko.

Nikatoka nikaenda kwa miguu mpaka kile kihoteli nilichokula nilion magari na vibajaji pale vinangoja abiria. Nikamuu;liza mwenye Kibajaji anaweza kunipelka kigtuo cha Kojani?
Bajaji; Kituo cha Kojani cha hapa kuendea Kojani au cha kule Kojani?
Mimi; Cha kule Kojani.
Kibajaji; Elfu kumi, nakupeleka faster tu na sichukui abiria mwingine.

Nikamwambia twende, tukaondoka, kweli alikua anakipeleka spidi huyo na vile hakuna magarri mengi njiani, faster tu tukafika, oile nashuka nielekee kwenye vingarawa, nikaona Bakora yupo, tukasalimiana.

Bakora; Mimi nilirudo mlip0oondoka nilikua namalizia kazi na yule mjinga, wtwende Jini 1 na 2 tutawakuta hukohuko. Tukaenda lakini safari hii vichochoro vya mbele huko hatukuenda njia ya mzee Ali, tukaingia kulia tukaenda sehemu kama kuna jumba la zamani na kuna uanja mkubwa, watu wamejaa, mwenye kucheza, na ndani ya hilo jengo, lipo wazzi tu kama soko fulani hivi, Kuna ngoma zinapigwa.
Bakora; huu ndio uwanja wa sherehe na hilo jengwa limejengwa miaka mingi ni kwa ajili hii, wakimaliza kazi yakea leo, siku zingine wanaletwa watu mmoja mmoja na waganga zao, wanaotaka kuaguliwa, wenyewe wanaamini hili jengo lishakua kituo cha mizimu yao yote ya Kojani, akiitwa jini hapo lazima aje.

Tukaingia ndani ya jengi kwa kusukumna na watu mlangoni, lango kubwa lakini watu wengi, tukaelekea kama nkuna jukwaa hivi. Nikamuona Mzee Ali ndio kakaa juu ya kiti katikati, tukaenda mpaka kwa mbele yake lakini sisi tuko kwa chini ya jukwaa, mwenyewe yupo bize, kachangamka huyo, sio yule wa mchana, matra aanamuagiza huyu hiki, mara jile, kuna vyetezzo hapo kama vyote. Chhenye chenye mavumba mengi hata siyajui, moshi mtupu ndani na pembeni kwa chini ndio wapiga ngoma hao.

Mzee Ali alipoangaza upande wetu akatuona, kama akapigwa ngazi kwa muda aliponiona. Akaanza kuja upande wetu, huku anapangauwau, njooni njooni Bwana Simba, Bwana bakora, pandeni nyinyi wageni wangu, wapisheni wapisheni. Tukapanda juu ndio high table tena hio.

Mzee; Jamani jamani jamni, subiri kidogo , nisikilizeni, ngoam simamisheni. Nataka kuwajulisha wageni wetu rasmi wa mwaka huu.

Pakawa kimyaa, kasoro sauti za hapa na pale za watu.

Mzee Ali; Wageni mliotoka nchi na sehemu mbali mbali, Binadam na majini na viumbe wengine wote mliohudhurria, wenyeji wa hapa Kojani na Pemba naomba niwajulishe na watu rasmi.

Huyu hapa ni bwana simba, kutokea Dar na huyu hapa bwana Bakora kutokea Tanga. Kwa leo na kila wanapokuwepo, siku yoyote mtayokutana nao, uwe jini uwe binadam, elewa kua hawa ndio wakuu wa kazi wetu, muwape heshima yao na mimi kuanzia sasa hivi kwa kua wapo wao sifanyi chochogte bila idhini yao.

Kusema hayo nikaanza kusikia minong'ono na sauti kila mmoja anauliza lake. Mmoja akasimama, alikua jukwaa kuu na sisi, nikajua ni chawi la majini. Akasema. Mimi siliafiki hilo, haijawahi kutojea na wala haitokuwa. Haiwezekani mgeni aje kuwa mkubwa wa hii shughuli. Nawaambia....

Kimyaaaa, akawa anapeka midomo haitoki sauti kabisa, akaanza kama kujishngaa, watu wakashangaa nini kinaendelea.

Bakora: Kaa chini, wewe feshuli unaeweza kufungua mdomo mbele yetu.

Ikawa kama kama kanyuliwa akakalishwa chi kwa nguvu lakini haonekani aliemkalisha chini.
Bakora; Endelea Ali.

Mzee Ali; jamani kama kuna mwenhgine anapinga apinge kabisa, lakini narudia, hawa ndio wakuu wa kazi leo na siku nyingine yoyote wanapokuwepo. Asielitaka hilo ni bora aseme wazi kama Shikh hapa chini. Kuna mwenye lake? msituchelewe tunataka kuanza kuchinja, muda unakwenda.

Bakora: haya simama wewe, useme.
Yule mzee aksimama akaanza kusema; Kwanza mnisamehe sana nilikua sijaelewa lakini nimefahamishwa, jamani naungana na Bwana Ali hapa na mimi nakiri hawa ndio wakuu wa hii kazi. Sheikh Simba na Sheikh bakora mnisamehe sana ni mapungufu ya kutokuti kaui ya mkuuw) wetu wa shughuli Bwana Ali...

Bwana Ali nisamehe sana endelea.

Mzee Ali; naona tumeliza, sasa jamani tutashuka kwenye kuchinja na wageni wote na wakuu wetu watakuja kushuhudia kafara zetu.

Akashuka akatangulia, huku ansema anzeni ngoma haya kila mmoja aendelee kama kawaida. Tukashuka watu wanatupa nafasi tukaenda mpka kama hatua 20 au 25 kutoka lile banda tukakuta ng'ombe saba wamesha fungwa wamelazwa kwa kuchinjwa, Mzee Ali akakabidhiwa bonge ya Kisu.

Mzee Ali; Wakuu naomba muanze nyinyi kuchinja.
Bakora; Wewe endelea tu na kazi yako, sio kazi yetu hio.

Mzee akaendelea, kisu kilikua kikali, mzee alai akawa anawachinja kuna mama wana mabeseni wanaikinga ile damu, beseni lijaa anapewa jingine.

mzee Ali; kama ada yetu, hawa ni ng'mbe wa... wote saba, (Bakora akanambia hilo ndio shetani lao kubwa la kichawi,) kwa hio tunaomba nyote msikate nyama mpoka baada ya nusuu damu itapokauka, na nyinyi mliochukua damu mnajua pa kuipeleka na chakufanya kama ilivo ada yetu. akaitika sawa.

Mzee Ali akatangaza, baada ya nusu saa tutarudi kuchinja wengine wote waliobakia. Tukarudi juu. ngoma zinaendelea ssa zinhgine zipo nje kwenye ng'mbe zingine zipo Juu.

Mzee Ali; Haya jamani, wale wabeba vyano vya kesho wapande juu hapa, wakapandishwa wasichana 21. Mzee Ali akasma yule mbeba chano kikuu aliechaguliwa asogee hapa kwangu, akaja binti mmoja kajazia jazia. wakati huo watu wote kimya mpka ngoma zimenyamaza bila kuambiwa, wanajua ptokali yao.

Mzee Ali; Wakuu huyu ndie binti aliechaguliwa kubeba chano kikuu mwaka huu. Mmemuafiki wakuu.
Bakora; Endelea tu na utambulisho.

Mzee Ali hawa wengine watabeba vyano vingine.

Binti mbeba chano kikuu, chano kitakua nyumba ya...utakwenda kule ukawepo kinapopambewa na usiondoke ule mpaka kesho kipokwenda kukabidhiwa, Na nyinyi wengine nendeni hukohuko wako wapambaji vyano watawapangia kila mmoja aende kapambe chano kwa nani, ile damu ya sasa hivi yote iende nyumba ya chano kikuu sasa hivi. Wakaondoka, ngoma zikjaanza hazijapigwa sana

Mzee Ali; Sasa watayarisheni ng'ombe wengine waliobakia, wakuu kuna ng'ombe wengine 20 tutaenda kuchnja ili vyanoi vingine vikamilike. Naomba twendeni.
Bakora: Tangulia sisi tunakuja, mangoma yakaanza, bakora akanambia sikioni.
Bakora: Simba wakianza kuchnja kabala hawajamaliza wewe jifiche kwa kuminya pte yako tuwe hatuonekani, mimi utaniona lakini hawa washenzi wote hawataniona, nifate twende na mimi, ndio tunaondoka sisis mpaka kesho.

Nikagfanya kama Bakora alivonambia kufika ng'ombe wa tano tu, watu wapo bize na ng'ombe, mimi nikaiminya pete Bakora akatangulia mbele yangu nikawa namfata nyuma. Tukaenda mpoaka bandari ya mitumbwi, tukakuta mtu mmoja. Tukapoanda mtumbwi wakatuvusha, tuliposika mwisho.

Bakora; Yule nilishmtayarisha atungoje bandarini, na Bajaj ile pale inatungoja, twende, wewe nenda tu uka[umzike, leo hakunza aizada ni ushetani tu uliobaki mpaka asubuhi, wataanza kupika mnayamafu yao yaliochinjwa kwa ajili ya shetani, mji mzima leo watagawana nyama, wale saba itapikwa chakula kila mtu atakula na kinachobaki watachukua wakale makwao kesho mchana, ndio chano kitapelkwa kutolea. Utakuja kuona, njoo baada ya dhuhuri tu, kazi ya chano inaanza. haichelewi. Wewe neda Simba, mimi narudi, uliwaona jamaa zako? Kina nani? Jini 1 na 2. Wapo pale niliwaambia wasijitokeze.

Mimi; Sikuwaona, kwaheri bakora,.

Tukaagana pale nikarudi hoteli, nikaingia chumbani kwangu nikakoga nikasali nikalala, usingizi haujaja mapema nikawa na maswali mengi sana lakini sipati majibu, nikasema kesho nitawauliza hawa majini na babu. Nikalala.

...
Vionjo vya Arsis - Majini ya Kojani- Pemba 9.

Nilipata usingizi mzito sana, alfajiri badala ya mimi kumwamsha wife, yeye akaniamsha mimi, kwa kugonga mlango. Nilipofungua mlango akanihug.
Wife: hey lazybones, wake upo and pray.

Kutazama saa ni wakati wa alfajiri, kiaingia kuchukua udhu, nikatoka nikakuta wife kishanitandikia msala. nikasali pale, nilipomaliza.

Wife: ytena msikiti inaonesha haupombali hapa, adhana naisikia kama panaadhiniwa hapahapa.
Mimi; Igtabidi niujue. Vipi mmelala salama?
Wife; tumepiga story na Dokta mpaka saa tisa usiku, kidogo nije kukufata. bahati yako, nimemuonea huruma Dokta, maana jana kafunguka, jamani binadam tuonane hivi hivi tunatembea na kujuana kijujuu tu, yaani haya majini na wachawi wamempa wakati mgumu sana Dokta, mimi sikuhadithii, lakini mume wangu, nashukuru Babu alikuchagua wewe kumrithi kazi zake za kutibu watu, maana umeokoa ujuzi pale, ytule ni Daktari wa Kimataifa, kasoma, ujuzi nao wa miaka mingi, kafanya reseaches chungu nzima, kakatiza masomo yake PhD bila ya kuyamaliza bila sababu yoyote ya maana. Akifikiria hilo analia.
Mimi; Anaweza kufanya PhD mpaka sasa, kinamzuia nini?
Wife: haya mambo hyalimzonga, lakini mwenyewe anashangaa kua sasa anaweza kuyahadithia kwa watu na toka alivorudi Unguja anahisi kawa mwepesi sana mambo yake kama zamani, hakuna uzito uzito. Aah, mimi nikaone mradi kapata pakuyatolea mwache ayatoe.

Wife; Lakini jana usiku sikutaka kuja kwa hayo, nisubiri hapohapo kitandani, nakuja 10 minutes, ngoja niamuage Dokta maana nilimwabia nakuja kukuamsha tu, amka mimi nakuja.

Mimi; Niamke marfa ngaoi tena, na mpoaka kusali nimesali. Akacheka.

Nikajua anachoongea.

Baada ya muda tukashuka wote kupiga breakfast.

Dokta anaonesha ingawa wamechelewa kulala lakini leo anatabasmu tu, nikajuwa wife wangu kamtoa wasiwasi kabisa. Wakati tunakula.

Wife; Sasa mume wangu mimi na Dokta tumeongea jana, tumeeona haina haja ya kufanya hasira kuondoka Pemba, bora tumalize siku zetu kama tulivyopanga wale wachawi wasitutoe njiani.

Mimi; Nililifikiria hilo, msdingesema nyinyi mimi ningewaambia hilohilo.
Wifw; Mimi wewe nakujua fikra zako zote, kingine tumeongea Dokta lakini sikwabii leo wala kesho, suprise.
Mimi; Usinambie tayari yule hata kunyonyua hajaacha.
Wigfe; Hilo nalo linawezekana, In shaa allah tutajua baada wiki tukirudi Dar.
Dokta; Nisha sitaki utani please, huyo akiwa wa kike ushanambia wajina wangu, nataka na mumeo ajue hapahapa, nipo serious.
Wifew; Any obejection daaad?
Mimi: Mimi kwangu poa tu, lakini natamani baby boy.
Wife: Yeyoite ataekuja, mimi naomba awe mtoto mwenye heri, wala sipimi kujua kama wale wengine, uliona nimepima hata siku moja kujua?
Mimi: Mzee si alikua anakwambia ukapime?
wife; Nilimkatalia kabisa tena, hata mama, shangazi yako pia. Nashukuru wewe tu hukunambia.
Mimi; Sasa plan ya leo nini?

Wife; Tushangea na Dokta, leo Mister kwanz atunaenda kiwanda cha mafuta kutazama order ya mama. Halfu Dokta analijua soko la hapa anasema halipo mbali, tukaweke order ya ndizi mkono wa tembo za Pemba na dagaa la pemba orijino anasema siku hizi kuzipata shida kweli mpaka tuweke order, yeye kuna watu anawajua pale sokoni, halafu mchana baada ya kula anataka twende Mkoani, huko anapajua Dokta na kuna madaktari anajuana nao agtawaoigia simu kama watakubali watutembeze mkoni...

Kwa hio jitayarishe for a long day.

Mimi; Kiwanda cha mafuta leo Jumapili kipo?
Dokta; Kile kila siku kipo, wapemba unawajua wee kwa pesa?
Mimi; Okay huko tutaenda wote, soko kama halipo mbali tutaenda wote, lakini huko mkoani mimi mtanisamehe.
Wife; Unajua Mkoani tumepoanga tunaenda na nini? Tunaenda na yale mabasi yao ya mbao, tunaoanda nyuma. yaani yale mume wangu tuke mpaka Pemba tusiyapande?
Mimi; Mtanisamehe, nimeagana na wale wenyeji wetu atanipitia. Tena nawashauri, kwani huko Mkoani hakuna chakula ili tukitroka sokoni muende na mimi niende safari yangu, maana safari yangu ni saa sita inabidi niende.
Dokta; Tena hilo tulilifukiria tukaona tule kabisa kwa sababu yako, sisis hapa makomando, kula na kulala popote. kwa hio basi tukitoaka asubuhi hii kwenda kiwandani haturidii hapa, tuaachana huko huko mitaani?

Mimi; Poa tu, hakuna neno.

Tukakaa stry za haoa na pale kufika saa mbili tukaondoka.
Wife tupande kibajaji tuuone mji, au sio Dok?

Mimi; Poa.

Dokta; basi tutemebeeni mpaka pale barabatra kubwa hatukosi vibajaji.

Ikawa hivyo. tukaenda kiwandani kama Dokta alivyosema yukakuta wapo na wanafanya kazi kiwandani, mimi nilifikiri labda kiwanda, kiwanda cha maana, nikakuta cha kizamani zamni, wakatuelekeza wanavukamua kila aina ya mafuta wakasema leo baadae akija mtaalam mtaona tunavokamua mafuta ya pilipili manga. Nikashangaa. Jaamaa yule akasema usidhngae Ami, mbegu zote haoa tunauwezo wa kutoa mafuta, Huu utaalamu hakuna kabisa chini ya sahara yote hii, kila mbegu na proicess yake na utaalamu wake.

Tukachukua mafuta yaliokuwepo chupa mbilimbili a mama na wao kila mmoja akachukua moja mojamtulipata kama aina tano za mafuta, mafuta ya karafuu, mafuta o ya pilipili manga, mafuta ya haba soda, mafuta ya ufuta, mafuta ya korianda. Jamaa akasema mkitaka kutengezewa aina yoyoyte ya mafuta mnatupa order tu, chukueni namba za simu, hata Dar tunakutumia tu. Tunatuma mpaka Ulaya. Ni vitu adimu hivi. Dokta akaninesha sehemu inaitwa nachomne, akanambia hapa In shaa Allah usiku njooni tule. Vyakula vya Kipemba. Tukaenda sokini chake, sio mbali sN na pale tunapokaa, ndio unaigia chake cenyre hpo halafu unaenda kwa nyuma yake tu , kuna soko lina kila kitu cha Kipemba, nilipenda samaki wa kukausha kila namna, nikamwabia wiife pweza wa kukausha ho, usiwaache.
Wife ; Wewe tuwachie sisi tunataka tuwa surprise nyumbani, hata wewe hujui tutavyonunua vingine, siri yangu na Dk.

Tukazunguka zunguka sokoni pale, wakawekesha order zao kwa mtu pale pale sokoni wanajuana na Dok. Akamwambia nipo pale pale ninapofikia siku zote, vifungashe vizuri vitaondoka na boti za kwenda Dar. Jamaa akamwambia poa, najua Dok.

Tukaondoka, tukaenda baraba kubwa wao wakapanda vile vi chai maharage vya mbao, wakanishikilia niwapige picha nikawa[iga piga picha, wakaenda zao Mkoani, mimi nikarudi hoteli ili nikajionee mambo ya Chano cha Kojani. Niliamua siwaambii mpaka tukirudi dar., sikutaka kuwakumbusha majonzi ya Dok alipokua anahadithiwa alichofanyiwa Mzee Ali.

Nikarudi zangu hoteli kujitayarisha tripu ya Kojani, na fuko la machupa ya mafuta.
 
Vionjo vya Arsis - Majini ya Kojani- Pemba 10.

Baada ya kukoga kogas na kujitoa jasho la matembezi ya sokoni. Nikajinyoosha kitandani, nikawa nawaza mkasa mzima huu wa kojani, nikasema nitawauliza maswali mengi sana, sina majibu nayo. Nikaanza kupitiwa kama na kiusingizi cha uvivu nikasikia mlango unagongwa. Nikajua Jini 1, nikamwambia pita, akafungua mwenyewe m;lango, mimi nikawa nimekaa kitandani yeye akaenda kukaa kwenye kiti, baada ya kusaimiana.

Jini 1; Pole sa Simba naona mambo ya Kojani yamekuchosha, unaonesha umechoka.
Mimi' Sio kimwili, kimawazo. Nina maswali mengi sana, lakini sina majibu.
Jini 1: kama maswali ya kujua tu mambo, subiri tumalize zoezi la leo halafu utaulliza maswali yako, nitaloweza kuyajibu nitayajibu, nikishindwa yupo mama, yupo Aris watakupa majibu.
Mimi; Poa, naona sia mawali ya dharura isipokua ya kuelewa tu.
Jini 1; Basi usiwe na hofu subiri. Sasa sikiliza kilichonileta sasa hivi.; Leo kuna mpoango wa sinema ya mwisho, mpoango mdogo tu, umepangwa na Kamanda, ili muweke na kulinda hehima yenu na yao kwa kazi walioifanya.
Mimi; Mpango geni tena, niliyoyaona na kuyasikia ya Dokta yamenitosha jamani.
Jini 1; Ya Dokta ukurasa wake wa Kojani umeshafungwa, wala hautousikia tena. Mmefanya kazi nzuri sana. Dokta sasa yupo fiti kabisa hana tatizo lolote la vijini na wala hatokua na tatizo labda kwa uwezo wa Muumetu. ba w, vivuli na vijini na vijini vya tarasimu vyote vya kijingajinga vya Mzee Ali vimesambaratishwa, vingine vimeuliwa, vingine vimefungiwa kufanya kazi, vinatiwa adabu na wenyewe wakubwa zao, pale pangini, kwa makubaliano na Kamanda.

Mimi; Vimeuliwa? Mbina hili jipya kwangu.
Jini 1; Si unakumbuka Mzee Ali antengez vijini vingine vya rtarasimu? Hivyo alivyomsukumia Dokta vimeuliwa, yule mzee ni mjinga sana, badala ya kutumia ujuzi aliopewa kwa faida, yeye alikuwa anutumia kufanya mambo yakijinga kabisa. Tena ashukuru Mungu sana, bakora kamuombea sana kwa Kamanda na kwa mmku bwa wao, wamuachie lakini akiri kua atafanya toba ya kweli na ataacha mambo ya utapeli na kuumiza eateja wake wanaomfata.

Si unajua majini hawa wakubwa wanaheshimiana sana, Wakaheshimu ombi la Bakora, wakaweka mkataba na Mzee Ali na wakubwa zake, akiponyoka tu ndio anamalizwa kila kitu, sasa hivi atakua mtu wa sadaka sana. Alikua kishakata tamaa, Bakora akamuhurumia, lakini hajamwambia kama ni yeye Bakora aliyemuombea, Ilikua Mzee Ali ahame kabia Dar. Karuhusiwa arudi lakini kwa heshima na adabu. kma kuambiwa ataambiwa na majini yake huko...

..Kwaa hio vijini vya tarasimu vimeuliwa, vivuli, hivi hajavituma kwa Dokta, alikua anaviweka awapchike watu wanaokwenda kwake, navyo vimeuliwa vyote, na kaapishwa kua hatorudia kutumia uchawi wa kijinga ule. Yeye ataruhusiwa kuwatoa kwa wateja wake na kuwaua au wakubwa zake watavyompa maagizo, basi. Umeelewa Simba?

Mimi; Nimeelewa kuhusu mzee Ali, lakini...

Jini 1; Subiri Simba, sikuja kwa haya lakini mradi tumeyaanza wacha nimalizie kwa ufupi.

Jini 1; hapa ndio patamu; Unajua Dokta alitupiwa vivuli na mama mkwe wake wa mumewe wa kwanza ili asithaminike kwa mumewe, yaani amuone kama kero tu, sasa hata alivyoachika hivyo vivuli vilikuwepo. Hivyo havikuwa shida sana itmpata aliyevitengeza alikuwa hai, Mzee mmoja wa Kigunya, wa Kenya huko, kishakua mzee sana, sasa anafanya toba anaagua tu, sema alikua na kasoro moja...

Alishaingia mikataba zamani na majini wa kumletea vivuli, ikawa kila mwaka anachinja kafara ya wale wakubwa zao, na wale wakiwepo ama hawajatolewa kwa mgtu aliepachikwa nao, ikitolewa kafara kwa wakubwa zao wanawaambia andeleeni na kazi mliopewa, vikawa mara kwa mara vinamzonga hata kazini anaonekana kama nuksi na mkporofi kaingia. Ndio ikawa mchezo huo huo miaka na miaka. katika hivyo hivyo ndio vilimfanaya asimalizie shahada yake ya juu kabisa. lakini sasa kwisha hivyo.

Jini 1; Vilivyowapa tabu kina mama na Bakora mpaka ikabidi waongee na Kamanda na kamanda ikabidi alete majini wa kuchunguza, sio hivyo. Hivyo vingine vya kutengenezwa, alisukumiwa kutokea Tanga, na mke mwenzie kwa mumewe wa pili, na huyu mumewe wa pikli ni Dokta vile vile, lakini sio mkubwa kama yule wa kwanza.

Hivi kama nilivyokwambia, vilikua vijini vya kutengeza, na yule alievitengeneza kafa muda tu, na alivificha vitu vyake akavimwagia uchawi visionekane, vilikua bya vya watu wengi tu, sio Dokta peke yake, maana alipoanza kuummwa yule akajua haponi yale maradho yake. Sasa waliomrithi hawajui kavificha wapi vitu vingine, kumbe alivichimbia makaburini, akamwaga na dawa zake juu, hilo kaburi la zamani sana, hata wenye marehemu aliezikwa pale wakienda kumuombea dua marehemu wao, kaburi hawalioni...

Hivyo ndio vilivyoleta kasheshe kiasi, lakini vikapatikana, hilo lilifanyika Dokta aliporudi tu kutoka Unguja, wala hajaambiwa hayo ya mkwewe wala ya huyo mke mwenzie yataleta chuki, yalifanywa kimya kimya tu.

Na wewe usimweleze lolote Dokta kuhusu hayo, Ndio ujue kutunza siri za watu. kwa ufupi na vyenyewe vimeuliwa. Ukitaka kujua zaidi mambo hayo muulize Arsis.

Jini 1; Sasa kilichonileta; Leo unatakiwa uende Kojani ukiwa umejificha kwa pete yako, kuanzia juu huko kabla hujavuka, utanikuta mimi nitavuka na wewe. Bakora hatokuwepo kivukoni. Tutaenda moja kwa moja, utaenda kukaa alipokaa Bakora lakini usifichue kabisa, mpaka Bakora atapokwambia, hata Bakora utamuona wewe tu, hakuna jini waa bunadam mwengine atakaemuona. baada ya hapo utafata maelekeso ya Arsis. Hauna kazi yoyote leo, kazi yako ni kujificha tu, utaelewa kwanini zoezi lisha. Umeelewa?

Mimi; Nimeelewa.
Jini 1; haya kwaheri, uwahi huko hakifanyiki kitu bika ya wewe kuwepo.

Mimi; Kwaheri.

Nikaona nikilala hapa nitachelewa, nikaona nitoke tu, niliona maji ya miwa barabarani kule nitatembea tembea ninywe maji ya miwa nikisha sali ndio nitaenda Kojani, kama kuchelewa wacha wachelewe, niliuona msikiti pale barabarani. Nikatoka zangu.

...
 
Mkuu Arsis shikamoo nina shida nimekuwa ninashida ya usikivu tangu utoto ilinitokea nikiwa na miaka 8...sijui nimerogwa ila inawezekana, kadri siku, mwezi na miaka inavyosonga ndio nakuwa sisikii kiasi kwamba sahivi mpaka niangalie mdomo wa mtu ndio nielewe japo kwa shida sana je kuna tiba mkuu? msaada tafadhali mkuu wangu

Shida nyingine ni nina severe curve scoliosis(uti wa mgongo kupinda) siwezi kutembea niko kitandani mwaka wa nne sasa..pia vidole vya mguuni vinauma sana ata ukivishika tu kingine nimekonda sana ata nile vipi sinenepi pia mishipa ya mwili imesinyaa nakuwa sina nguvu kabisa

Naomba msaada wako mkuu ninataka kupona tena mkuu mana tiba nyingi zimeshindikana from hospitalini to ugangani mpaka sina hamu ya kuishi na haya mateso nayopitia lakini nimepata tumaini naweza kupata msaada

Mwambie Arsis I want to be his friend just like you.....I really do
 
Yaani nimechekeaaa mbavu sina mzee na kitambo anapiga samasoti....bwana Simba Arsis je ni jini wa asili Gani huyo anapiga sarakasi?

Kuna mahali ulisema aidha huzijui sura za jini 1 yaani unaona mtu ila sura haipo au ...namna hiyo. Sasa mlivoenda kojani ulikuawa unawaonaje? Bado sura hazionekani?

Jini 1 alisoma mwaka Gani mlimano?
Mkristo mwenzio kaandika hakuna jinni Mkristo, nimemkubalia 100%.

Imekuwa kosa?
So wakristu hawapatwi na majini? Bali yanawapata Islamic tu, na kama sivyo yanafuata nini kwa Christian ?

Simulizi imeonesha yapo majin mengine yanapenda kula maisha ikiwa ni pamoja kunywa Pombe, kinyume kabisa na kanuni za Islamic, utadhibitishaje kwamba ayo hayana vina saba vya Christian.

Dawa yako ni kupigishwa samasoti
 
Vionjo vya Arsis - Majini ya Kojani- Pemba 10.

Baada ya kukoga kogas na kujitoa jasho la matembezi ya sokoni. Nikajinyoosha kitandani, nikawa nawaza mkasa mzima huu wa kojani, nikasema nitawauliza maswali mengi sana, sina majibu nayo. Nikaanza kupitiwa kama na kiusingizi cha uvivu nikasikia mlango unagongwa. Nikajua Jini 1, nikamwambia pita, akafungua mwenyewe m;lango, mimi nikawa nimekaa kitandani yeye akaenda kukaa kwenye kiti, baada ya kusaimiana.

Jini 1; Pole sa Simba naona mambo ya Kojani yamekuchosha, unaonesha umechoka.
Mimi' Sio kimwili, kimawazo. Nina maswali mengi sana, lakini sina majibu.
Jini 1: kama maswali ya kujua tu mambo, subiri tumalize zoezi la leo halafu utaulliza maswali yako, nitaloweza kuyajibu nitayajibu, nikishindwa yupo mama, yupo Aris watakupa majibu.
Mimi; Poa, naona sia mawali ya dharura isipokua ya kuelewa tu.
Jini 1; Basi usiwe na hofu subiri. Sasa sikiliza kilichonileta sasa hivi.; Leo kuna mpoango wa sinema ya mwisho, mpoango mdogo tu, umepangwa na Kamanda, ili muweke na kulinda hehima yenu na yao kwa kazi walioifanya.
Mimi; Mpango geni tena, niliyoyaona na kuyasikia ya Dokta yamenitosha jamani.
Jini 1; Ya Dokta ukurasa wake wa Kojani umeshafungwa, wala hautousikia tena. Mmefanya kazi nzuri sana. Dokta sasa yupo fiti kabisa hana tatizo lolote la vijini na wala hatokua na tatizo labda kwa uwezo wa Muumetu. ba w, vivuli na vijini na vijini vya tarasimu vyote vya kijingajinga vya Mzee Ali vimesambaratishwa, vingine vimeuliwa, vingine vimefungiwa kufanya kazi, vinatiwa adabu na wenyewe wakubwa zao, pale pangini, kwa makubaliano na Kamanda.

Mimi; Vimeuliwa? Mbina hili jipya kwangu.
Jini 1; Si unakumbuka Mzee Ali antengez vijini vingine vya rtarasimu? Hivyo alivyomsukumia Dokta vimeuliwa, yule mzee ni mjinga sana, badala ya kutumia ujuzi aliopewa kwa faida, yeye alikuwa anutumia kufanya mambo yakijinga kabisa. Tena ashukuru Mungu sana, bakora kamuombea sana kwa Kamanda na kwa mmku bwa wao, wamuachie lakini akiri kua atafanya toba ya kweli na ataacha mambo ya utapeli na kuumiza eateja wake wanaomfata.

Si unajua majini hawa wakubwa wanaheshimiana sana, Wakaheshimu ombi la Bakora, wakaweka mkataba na Mzee Ali na wakubwa zake, akiponyoka tu ndio anamalizwa kila kitu, sasa hivi atakua mtu wa sadaka sana. Alikua kishakata tamaa, Bakora akamuhurumia, lakini hajamwambia kama ni yeye Bakora aliyemuombea, Ilikua Mzee Ali ahame kabia Dar. Karuhusiwa arudi lakini kwa heshima na adabu. kma kuambiwa ataambiwa na majini yake huko...

..Kwaa hio vijini vya tarasimu vimeuliwa, vivuli, hivi hajavituma kwa Dokta, alikua anaviweka awapchike watu wanaokwenda kwake, navyo vimeuliwa vyote, na kaapishwa kua hatorudia kutumia uchawi wa kijinga ule. Yeye ataruhusiwa kuwatoa kwa wateja wake na kuwaua au wakubwa zake watavyompa maagizo, basi. Umeelewa Simba?

Mimi; Nimeelewa kuhusu mzee Ali, lakini...

Jini 1; Subiri Simba, sikuja kwa haya lakini mradi tumeyaanza wacha nimalizie kwa ufupi.

Jini 1; hapa ndio patamu; Unajua Dokta alitupiwa vivuli na mama mkwe wake wa mumewe wa kwanza ili asithaminike kwa mumewe, yaani amuone kama kero tu, sasa hata alivyoachika hivyo vivuli vilikuwepo. Hivyo havikuwa shida sana itmpata aliyevitengeza alikuwa hai, Mzee mmoja wa Kigunya, wa Kenya huko, kishakua mzee sana, sasa anafanya toba anaagua tu, sema alikua na kasoro moja...

Alishaingia mikataba zamani na majini wa kumletea vivuli, ikawa kila mwaka anachinja kafara ya wale wakubwa zao, na wale wakiwepo ama hawajatolewa kwa mgtu aliepachikwa nao, ikitolewa kafara kwa wakubwa zao wanawaambia andeleeni na kazi mliopewa, vikawa mara kwa mara vinamzonga hata kazini anaonekana kama nuksi na mkporofi kaingia. Ndio ikawa mchezo huo huo miaka na miaka. katika hivyo hivyo ndio vilimfanaya asimalizie shahada yake ya juu kabisa. lakini sasa kwisha hivyo.

Jini 1; Vilivyowapa tabu kina mama na Bakora mpaka ikabidi waongee na Kamanda na kamanda ikabidi alete majini wa kuchunguza, sio hivyo. Hivyo vingine vya kutengenezwa, alisukumiwa kutokea Tanga, na mke mwenzie kwa mumewe wa pili, na huyu mumewe wa pikli ni Dokta vile vile, lakini sio mkubwa kama yule wa kwanza.

Hivi kama nilivyokwambia, vilikua vijini vya kutengeza, na yule alievitengeneza kafa muda tu, na alivificha vitu vyake akavimwagia uchawi visionekane, vilikua bya vya watu wengi tu, sio Dokta peke yake, maana alipoanza kuummwa yule akajua haponi yale maradho yake. Sasa waliomrithi hawajui kavificha wapi vitu vingine, kumbe alivichimbia makaburini, akamwaga na dawa zake juu, hilo kaburi la zamani sana, hata wenye marehemu aliezikwa pale wakienda kumuombea dua marehemu wao, kaburi hawalioni...

Hivyo ndio vilivyoleta kasheshe kiasi, lakini vikapatikana, hilo lilifanyika Dokta aliporudi tu kutoka Unguja, wala hajaambiwa hayo ya mkwewe wala ya huyo mke mwenzie yataleta chuki, yalifanywa kimya kimya tu.

Na wewe usimweleze lolote Dokta kuhusu hayo, Ndio ujue kutunza siri za watu. kwa ufupi na vyenyewe vimeuliwa. Ukitaka kujua zaidi mambo hayo muulize Arsis.

Jini 1; Sasa kilichonileta; Leo unatakiwa uende Kojani ukiwa umejificha kwa pete yako, kuanzia juu huko kabla hujavuka, utanikuta mimi nitavuka na wewe. Bakora hatokuwepo kivukoni. Tutaenda moja kwa moja, utaenda kukaa alipokaa Bakora lakini usifichue kabisa, mpaka Bakora atapokwambia, hata Bakora utamuona wewe tu, hakuna jini waa bunadam mwengine atakaemuona. baada ya hapo utafata maelekeso ya Arsis. Hauna kazi yoyote leo, kazi yako ni kujificha tu, utaelewa kwanini zoezi lisha. Umeelewa?

Mimi; Nimeelewa.
Jini 1; haya kwaheri, uwahi huko hakifanyiki kitu bika ya wewe kuwepo.

Mimi; Kwaheri.

Nikaona nikilala hapa nitachelewa, nikaona nitoke tu, niliona maji ya miwa barabarani kule nitatembea tembea ninywe maji ya miwa nikisha sali ndio nitaenda Kojani, kama kuchelewa wacha wachelewe, niliuona msikiti pale barabarani. Nikatoka zangu.

...

Vionjo vya Arsis - Majini ya Kojani- Pemba 11.

Nikpigiga juisi ya maji ya miwa, nikaenda kuali nilipotoka, pale pale Masjid nje nikapata Kibajaji kikanipeleka kituo cha Kojani, nikamlipa kabisa mwenye Kibajaji nikiwa ndani ya Bajaji kabla hatujafika. Lengo likiwa nikishuka tu nijifiche, nisionekane.

Kufika tu nikaiminya pete kabla sijashuka, nikawa najisemea mwenye Kibajaji akigeuka kuatazama akiona hakuna mtu kazi kwake.

Niliposhuka nikamuona Jini 1 kwenye kona karibu na kiduka cha pale kivukoni, akaja, akanambia haya Sima tuwahi, umefanya vyema kabisa, mimi ningekua sina pete zetu hizi tusingeonana.

Tukavuka bila mimi kuonekana, Jini 1 pale hakijificha, alikua anaonekana yeye tu, maana yeye ndio alilipa alilipa pesa zaidi akamwambia Mwenye ngarawa, hizo zako, weka tu. Alikua hajui analipwa na nauli yuangu.

Tyulipofika viwanja vya chano, watu wanacheza, kama kawaida wakubwa wapo ndani, watu wamejaa vumbi, nikashangaa, nikaona leo walijipaka rangi nyeupe usoni, wengine zina mistari mekundu, wengine zina mistari meusi, wengine nyeupe tupu. Kufika meza kuu nikaona Bakora yupo pale na pembeni yake kuna nafasi ya kukaa, akanisharia nikakae pale. Nikamuona yule Mzee alioaibishwa na Bakora kwa kunyamazishwa na kukalishwa chini kiajabu yupo pale lakini alikuwa kawaida tu hana ile muonekano wa kugtamba tena, kanywea.

Watu wakaanza keleke tunachelewa tunachelewa. Mzee Ali akasimama akayamaZisha kila kitu, ngoma ile ya pale ndani ikasimama, nje uwanjani huko kulikua na ngpma zaidi ya moja, kama vikundi vikundi hivi hivi.

Mzee Ali; Endeleeni kushereheka, tunangoja wakuu waturiuhusu tuanze kumalizia ngwe ya mwisho ya shughuli yetu, anaeona anachelewa aondoke.

Bakora akaninong'oneza jifichue tu, na yeye akajifichua. Mzee Ali inageuka tu kuongea kutazama akae, akatuona, akashikwa na butaa, akatuuliza, tuendelee na shughuli wakuu au kuna maagizo yoyote. Nikaona hata meza kuu wote wameshangaa kutuona tumekaa pale.

Bakora: Endelea tu.

Mzee Ali; Akasimamisha tena ngoma kwa ishara tu, watu wakawa kimya; Shughuli yetu inaanza kama kawaida vyano vitapita nje hapo kama ada, na wakishapita watu wa chano wote ndipo sisi tutawafata nyuma. haya twendeni nje tukawapokee.

Mzee; Ali; Wakuu naomba twendeni, hapo mez kuu yote wameanza kushuka kuwahi nje.

Bakora: Nendeni, lakini msikipeleke chano mpaka sisi tufike, tangulieni, sisi tutakuja mwisho. Akshuka Mzee Ali akatoka nje ukumbi ukawa mytupi.

Bakora: Sikiliza, Simba, sisi tunakwenda kabla yao wakati wao wanapokea wenye kuleta Chano hapo nje, tutaingia kwenye maji ya tumbo, trunajificha kuanzai sasa wasituone, wakifika huko, tutajifichua kwenye maji watatuona sisi tunatokea baharini. Tukajificha tukaondoka.

Nje pale ndio nikaona kumbe zile rangi na walizojipaka na bendera zake na mwari wao aliebeba chano na kundi lao la ngoma. Ndio nikajoionea wapo watu wa kila aina hapo, taani waarabu, wazungum wahindi, na wakojani ndio wengi. Kila mmoja na kundi lake, wemye kucheza, wenye kulia, wenye kutingisha vichwa, yaani zaidi ya nusu waliokuepo pale nje wamepandisha mashetani.

Tukaingia kwenye maji kama Bakora alivinambia, hivyo hivyo na nguo zetu.

Nikaona wanakuja, Mzee Ali akaongea kitu na mbeba chano kikubwa. Lilikua sinia kubwa kweli, nikaona wamesimama ufukweni, yule binyti kasimama na chano Arsis akanambiajifichue tutoke. Nikasikia watu wanguna, haiwahi kuwatokea watu kutokea ghafla bahatini. Mzee Akawa anakodoa tu macho na wenzake wa meza kuu. Tukatoka tukasimasima pembeni kidogo, wakati tunatoka Bakora akamwambia endeleea na shughuli yenu. Maee Ali akaanza kupaza sauti...

Mzee Ali; Maini na mizimu ya pemba, na majini wote kutoka nchi na sehemu mbali mbali mliohudhuria, sasa kama ada ya hapa, kitatangulia chano kikubwa kupelekwa wengine wote mtabaki na vyano vyenu mpaka atoke mjumbe wa kupeleka chano. Aliebeba chano Kikubwa akaanza kuingia kwenye maji taratibu, huku Chano kipo kichwani.

Alipokua anaingia, wenye kushangulia wana shangilia, wenye kulia wanaliza, eengine wanapiga kelele za kufuru " mzimu mkuu wa kojani, gtutalie shida setu" mwengine nitatuiea shida zangu, yaani kila namna ya maombi anaombwa shetani. Mie nikawa naomba toba tu kimoyomoyo. Na hapo ndio nikajua kua yule mwari alikua akfungwa kanga tu kiustadi zilikuasio nguo zile, maana khanaga zilipoanza kuingia maji zikawa zinapanda, akaingia akatembea baharini mpaka maji takamfunika kabisa ikawa kanyua mikono kulibeba lile sinia, akaendelea kidogo mpaka likabaki sinia tu juu ya maji, naona akaliahcia lkakini ikawa kama analisuma kwa chini kuelkea baharini, yeye haonekani linaonekana sinia tu linakwenda, kufika sehemu, nikaona aja kutokea maji amabayo imetokeza shingo, na sinia lianenda zakw lenyewe.

Mie nikawa na shangaa na sinia linazidi kwenda tu lenyewe.

Bakora mchezo wa kuigiza tu huo, mazingaombwe tu hayo atakufahamisha Jini 1 baaadae.

Yule mnbeba chano aktoka moka nje Khanga zimerowa zimemnganda mwilini, ni binti kashibew wa haja kweli kweli, alipotoka tu.

Mzee Sli haya mpeni khanga zake mpya hizi hazirudiwi tena.

Kuna kina mama wakamletea kumfunga kanga mpoya wakafanya kama pazia hivi na khanga, walipotoa pazia ikawa yupo fresha na khanga zake kavu zimefungwa kiustadi kabisa.

Mzee Ali; Chanoi kikubwa kishapokelewa, haya sasa nyie pelekeni kwa mstari. Asiwafate asie na chano, kabisa tena, madhara yake makubwa.

Mabinti wakaanza kuelekea kama alivyofanya yule lakini hawa ikawa kila wakifika maji ya kiuno mooja anaenda kushoto mmoja kulia, yaana wanapanua wigo mpaka walipokaa mstari kwa baharini, wakaanza kuingia kama mpoka maji ya kunyatu mikono, kama alivonya yuule wa mwanzo mcheo ukawa huo wakaanza kutoka, sasa kila anaetoka kikundi chake akishatoika nje ndio kinafanya pazia anavikwa khanga mpya. Dah, hawa wabeba nikajua wanachaguliwa kweli kweli, yaani ni ushetani. Hakuna mwanamme rijali ataevumilia kuwamezea mate. Vile wanavyotoka zile khanga zingine zimepanda juu na zilivyogana mwilini show zote nje, si nyuma si mbele. Naona wanavotabasamu ni kama wamefundishwa kwa kina, waumize mioyo ya marijali.

Walipokwisha toka wote;

Mzee Ali; haya jamani, chano chote kimepokelewa, sasa kama kawaida yake mwenye lake aseme, mwenye chochote cha kupeleka baharini apeleka, na nawashauri sote tyujiyie kwenye maji japo mwili mzima upate maji, kila mtu kwa raha zake. Tukitoka hapa, karamu yetu kama kawaida kiwanjani, wale wapishi na wandalizi wawahi kutoka majini.

Bakotra; Haya simba wakati wanaingia bahatrini, jifiche tuondoke zetu.

Mzee Ali ndio alikua kaoingoiza msafara akaanzq yeye ne meza kubwa yote kuingia baharini, wakaftatia watu wote, wkubwa, wadogo, wazee, vijana, wanaume kwa wanawake. Mimi na bakora tukatazama kidogo oirika zao, wenye kwenda maji ya kina huko wenye kuongelea, waliobaki maji ya mwanzo mwanzo wanajizamisha haya.

Tukaondoka na Bakora akanambia, shughuli yao ndio imeisha, sasa wanapoakuliwa pilau, tukapita pale, hakuna watu uwanjani ndio nikaona masufuria makiubwa zaidi ya 20.

Bakora: Utangoja kula Simba?
Mimi; nani ale nyamafu hizo zilizochinjwa kwa ajili ya kafara za majini, twende etu bwana. Nimeshajionea shughuli zote za kishirikina za Kojani, inatosha. Bakora, haya twende, mengine atakuja Jini 1 kukueleza ukihitaji.

Bakora; Tulivofika karibu ya nbandari ya ngarawa akanambia jifichue tu. Tukapanda ngarawa na Bakora, upande wa pili tukakuta vibajaji kibao, tukaagana na bakora, nikapanda kimoja nikamuelekeza tukaondoka zetu.

Hoiteli, nikauliza resepshen kama Dokta amaesharudi, nikaambiwa bado. Nikapanda kwangfu nikakoga vizuei, nikasali. Nikakaa kuwasubiria, Niakapiga simu nyumbani kwa mama, baada ya kusalimian...

Mama; habari zote nazipata hapa, mkeo na mapoicha ananitumia. wanaonesha wamepapenda mkoani vijini huko.

Tukaagana nikapiga simu kwa wife. baada ya kusalimiana.

Wife; Nimekupigia sana simu inaita tu, umeshaoa Pemba mume wangu, hatiuambizani?
Mimi; Niliizima sauti msikitini nikasahau kuiongeza z)sauti. Vipi huko?
Wife; Ndio nilitaka kukuuliza muda mrefu, hapa madaktari wa Kipemba mashiga zake Dokta wa metuzuwia mpaka tule chakula cha usiku, sasa mume wangu, tutachelewa kurudi, si unajua vyakula na maongezi, tukichelewa usiwe na wasiwasi kama kuna choxxhote tutakujiulihsa. Hiwa wasi youer dayt?

Mimi; Siku nzuri nimetembea tembea nimeend mabli kidogo, nimerusi si muda mrefu. Vipi Dokta? Wife yupo, nimemwacha anaingea na wenzake, mimi nimetoka kidogo kuongea na wewe na simu. Njoo basi D. nikamwabia aah poa nyie endeleeni, sitaki kuwekwa mtu kati na wanawake watupu huko.

Wife; Unajifanya umesahau, ungesema hayo siku zile?
Mimi; Mke wangu tuombe tba tu, wala tusiyakubuke ya ushetani wa zamani, tulikua kizani.
Wife; Amiin, mimi naomba usku na mchana mume wangu kila nikisali, naomba sana Mwenyezi Mungu atutoie kabisa kizani.

Wife alikua kama mimi, haongei kabisa na simu zake mbele za watu, au kukaa, kua bize na meseji wakati anaongea na watu. Naona hio tabia, wote nyumbani tunayo.

Mzee anasema simu na wakati wake, nyinyi mushukuru sasa hivi tunapiga na lupokea simu wakati wowote. Zamani sisi ilkua hakuna hayo. Kupiga simu mpaka mtu aende posta ndio akapige. Nyinyi jopangieni, wakati wa simu n zisiwapotezee muda wenu, sana sana zinazidisha umbea tu. Tukawa tunamuelewa sana.

Nikawa sina budi, ni kuwasubiri tu.

...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom