Vionjo vya Arsis - Majini ya Kojani- Pemba 6.
Tukaamka kabla ya alfajiri, tukaondoka kabla ya saa 11. Tukafika Airport mapema tu tukawahi ndege vizuri kabisa. Ikaondoka ontime.
Tulipofika Pemba, tukakuta vigari nje, Dokta na wofe walikua washa arrange gari la Karafuu Hotel, Dr. Akawaona anawajua yeye, maana anakuja kuja Pemba mara kwa mara, tyukapelkwa Hotel, ni takriban sio mbali na kati kati ya mji wa Chakechake.
Hotel nzuri sio mbaya. Tukaponeshwa chumba chetu, kilikua hakipo mbali na cha Dokta. Floor hio hio, hii hoteli nadhani ina ghorofa tatu. Nikamwacha wife ndani anapanga panga, nikamwabia mimi nakwenda kunusu upepo wa karafuu nje, huko. Nikatoka kwa nyuma iuna swiming pool ndogo ndodgo na kuna sehemu ya breafst ya nje. Nikaenda kwa mbele nikato nje, ukitoka tu kuna barabata, nikawa natia macho Nuru.
Nikapapenda Pemba, pako green sana, sehemu ile jirabni hakuna yumba nyingi lakini ilizopo zinaonesha ni nyumba nzuri kama popote YTanzania kwenye majengo ya watiu mazuri. Nikatembea tembea kama dakika 45 hivi nikarudi, ile naingia tu resepshen wakanambia, wenzako wako huko wameacha maagizo uende pool.
Nikawakuta washaanzq kupiga breakfast, na mimi wife akaniagizia.
Wife: Mwenzetu ushakua mwenyeji? Tunaambiwa umetoka nje, tunaytoka hatukuoni.
Mimi; Nilikua nanyoosha nyoosha miguu navuta jewa ya karafuu.
Wife; Dokta mueleze kisa na mikasa, mie sijaongea nae lolote.
Dokta: Ngja nianzie kwa Mzee Ali jana, mkeqwe alinipigia simu akaniuliza kuhusu safari, maana nilishaongea kabla nikamjulisha nimepata tiketi na pesa> Simba si unajua walinitumia klaki tano za safari?
Mimi; Hapana sijui.
Dokta; Nisha hujamwambia?
Wife: Sijamwambia, pesa zako nimwambie yeye ya nini?
Dokta' Ungemjulisha tu, hizo ni gharama za safari yetu, mndio zilizokata tiketi yako na gharama za hoteli, kama zitapungua ni juu yangu.
Mimi; Hapana, hizo kama hazijatosha mimi nitatoa zigtazozidi, hilo tulishaongea na Nisha na hio ni closed case, yeye ata take care gharama, mtashirikiana mpaka zitappoishia hizo laki tano, sitaki kua burden yako, sisi tumekuja kutenbea tu Pemba Dokta.
Wife: Si nilikwambaia Dokta hakubali kabisaa Simba, mimi sijamwambia llolote. Wacha tu enjoy Pemba.
Dokta; Sijamaliza jamani, mkewe Mzee Ali akanambia leo iusikiu ndio hio shughuli inaanza kesho nikumalizia tu, tunatakiwa tuwe pale kuanzia mchana tule hukohuko, twende mpka kituo cha Kojani, tukifika tutaonana na mzee Ali haondoki mpaka sisi tufike. Atatuchukua tutaenda nae Kojani. Ni hapo hapo tu tunavuka na ngarawa, sio mbali.
Mimi; Poa.
Doktaa; Na Sheikh...wa unguja alinipatia wenyeji, wae zao walinnipigia simu nikaongea nao, nikawaambia sisi tumeshabook hotel na mimi nitakua kikazi kuanzia Jumatatu, k hio wasijisumbue nikifika nitwajulisha, wakanambia na we Simba waume zao watakupigia tukifika, kwa hio tegemea simu yao.
Mimi; Sawa hakuna tatizo.
Simu yangu hapo hapo ikaita, kupokea Jini 1;
Jini 1; Tafuta sehemu nzuri tuongee sasa hivi.
Nikawaambia, jamani nisameheni kidogo nakwenda kuongea na simu, nitarudi nisubirini, nikapanda juu nikaenda chumbani kwetu, ile naingia tu, mlango ukagongwa uulivoigongwa nikajua Jini 1, niamfungulia tukasalimiana.
Jini 1: Sitaki kukupotezea muda, nisikilize kwa makini sana...
Usikubali kufatana na yeyoite huko, nendandeni nyinyi m,msiende hata na hao wenyeji ala wasijue mnaenda wapi. Mtaonana nao kesho mkimaliza hii shughuli. Sawa?
Mimi; Sawa.
Jini 1; Halafu, tupo mimi, mama na Bakora tutakutana hapo kituoni tutavuka wote na tutakua kama mtu yoyote yule na mjulishe Mzee Ali kua hawa nimefatana nao mimi. Usijali kitu gtukiwepo sisi wataweka heshia kubwa sana kwako kwa sababu wakubwa zao watawaambia sisi ni kina nani na tumeshajulishwa nao na Kamanada. Umefahamu?
Mimi; Nimefahamu.
Jini; La mwisho hili, huko itabidi leo vijini vyao vilivukua vina mzoinga Dokta viachiwe, kwa hio mtatoka pale mtafikia kwa Mzee Ali mtaenda kama kilomita moja na nusu, sio mbali kwa kutembea, ndio kuna mizimu ya hayo majini,ukifika utawaambia, kabka ya kuwawachia lazima mzee Mzee aLI Akuahidi kua mkirudi tu leo, kwa kua shughuli inaanza usiku tatu, basi kazima akufundishe njia zake anazofanya kuwapa wati vijini vyake. Zipo njia tatu, zote atakuonesha. akisha kuonesha huko ndio kamanda atawawachia lakini pale mkiend atawaweweka wawaone wao, lakini watakua chini ya ulinzi wake, mpaka wewqe ukisema. Sisi tutafanana na nyinyi kote huko na mtatuona wote msiwe na shaka.
Mimi; Sasa wakinuliza mke wangu an Dokta kna nani hawa?
Jini 1; Waambie kweli kuwa sisi tunajuana kutokea Tanga kwa babu yako na tumekuja na sisi kushuhudia shughuli.
Mimi: Mzee Ali si alisema, kua alisha leta list ya wageni?
Jini 1; Muongo yule, hana cha listiu wla nini, sema hiviu vijini vyake kama havijaachiwa leo, atanyang'anywa ukubwa, unajua yule ndio mkubwa wa shughuli hizi za majini wote wa Kojani? Waganga na wachawi wote wa Kojani yeye ndio Kinara wao, hawafanyi kitu bila yeye kujua. Ni cheo kikubwa akinyang'anywa hicho ni aibu kubwa sana, na hicho wanapewa ukoo wao tu, ndio makubaliano yaliopo toka babuzake...
Sasa hakuna maongezi mengi kama umesahau kitu, utajua namna ya kutuuliza, haya nenda kwa wenzako wasingie wasiwasi, tugtaonana kituo cha Kojani.
Nikarudi.
Wife; Eeeh Simba ulikua na mkutano wa kwenye simu? Muda wite huu?
Mimi; Usijali, yalikua mambo muhimu kidogo. Saa ngapi tunakwend huko.
Dokta; hicho kituo cha Kojanikwa gari kama nusu saa tu, wale wanawake wenyeji wamanipigia tena wanasema watutumie gari, na huyu anaseam mumewe anakupigia hupokei.
Mimi; Ngoja niwapigie niwasikilize, nikanyanyuka.
Nikapiga simu nimekuta miss callas kama tanoi hivi.
Ya kwanza ikawa kwa huyo mwenyeji wetu ytukatambuana pale akanisihi sana aje. Nikamwabia utanisameh Sheikh wangu tutaonana Jumatatu, kuna ndugu lazima niwatembelee watakuja kunichukua. Tukamalizana, kua tukimaliza mambo yetu tuawasiliana nao.
Ya pili ikawa mwenyeji mwengine katika hao hao, nikamjulisha nishaongea na fulani wasijihangaishe,akanambia Sheikh basoi chakula cha mchana nyumbani leo. Nikamwambia leo haiwezekani kabisa, tukakubaliana Jumatatu.
Ya gtatu, mkewe Mzee Ali, nikaongea nae, sisi trumeshafika Kojani, nikamwabia wasiliana na Dokta atakupa maelezo yote. Akajibu sawa, nikamwabia kwaheri.
Ya nne na ya tani ikawa zote za kina Mzee Ali, naona mkewe kaona simu hyake haipokelewi na mimi kwa wasiwasi ule akatafita namba zingine. Nikajua anatiwa presha na Mzee Ali maana nilishambia aiwasiliane na mimi wala Dokta, anaogopa kuukosa ukubwa..
Nikatrudi nikawaeleza nimeongea na jamaa na nimewakatalia kuhusu garo lao na ugeni wao mpaka Jumatatu, tukimaliza kesho shughuli ya hawa jamaa inabidi tupumzike kesho, matembezi na wao Jumatatu. Wakanielewa.
Wife; Mimi naona tuondoke hapa saa sita kamili, nusu saa ya kufika, nusu saa tutatazama mandhar, mchana tutasali hukohukom Pemba hii hapakosi msikiti hapo, Tukitoka kusali tutakutana na Mzee Ali tuvuke. Mnaonaje?
Mimi; Dokta unaonaje?
Dokta: naona good idea na wewe simba unasemaje?
Mimi; Poa tu. Tutaenda na gari ya hoteli au?
Dokta" Gari hapa unawajulisha dakika 15 tu kabla ya kuondoka wana madereva wengi wanafanya nao.
Nikajua huu kama mpango wa Unguja.
...
Vionjo vya Arsis - Majini ya Kojani- Pemba 7.
... Muda ulipofika tukaondoka kama walivopanga wife na Dokta.
Tukafika kituo cha Kojani, tukashuka nikwambia drereva wewe nenda tu tukikuhitaji tutapiga simu. Tukaagana akaenda zake.
Tukatembea kidogo kuna kama nyumba nyumba mbili tatu, moja ina kama kiduka hivi kutaka kuingia nasika Sheikh Simba, kutazama nani ananitta nikaona Mzee Ali. Tukasalimiana wote. Nikamwabia wife huyu Ndio Mzee Ali, nikamwabia huyu mke wangu, Nikamhizi Mzee Ali anajaribu kujiweka kawaida lakini hana raha kabisa na sisi, inabidi afanye.
Mzee Ali; Sheikh karibu sana, naona pale kuna wageni wako ndio nilikua naongea nao hata mliposhushwa na gari sikuwaona, wametokea Tanga, wanasema na wao wamekuja kwenye sherehe zetu, uliwaambia waniulize mimi bahati na wao walikuja duka hilihili kuniuliza, hilo duka ndio kitu cha wageni wote. Twende tukawaone wageni, tukaenda wote walikua wamesimama upande wa pili, hilo duka lilikua kwenye kona, ya kushukia chini kupanda boti au ngatrawa, kuvushwa kwenda Kojani, tukjasalimiana na Bakora na Jini 1 na Jini 2, walikua kama mtu na mamake kabisa. Nikamwabia Sheikh Ali mtatambuklishana wenyewe lakini kweli hawa wageni wangu wapo na sisi.
Mzee Ali; Kareubuni karibuni, twendeni tuvuke. Dokata, wife wangu yupo nyumbani alikua anawatayarishia chakula, yeye kashindwa kuja kuwapokea.
Dokta; Hakuna neno.
Mimi; kqwa kua Mzee Ali kaja mapena kidogo hatruna haja ya kusubiri, naiona Kojani yenyewe si ndio hiyo mbele yetu? Tutasali hukohuko mchana.
Mzee Ali; Ndio hiyo, ukifika hapa ndio ushafika Kojani, hii kuvuka haicuhukui hata dakika tano, maji ya kikupw tubatenbea kwa miguu.
Tukaenda ytukapanda ngarawa kubwa hivi, wote tukaingia, sisi na kina Bakora.
Tuliposhuka tukaanza kuingia mitaani, ni vichochoro vidogo vpdgo nyumba kwa nyumba kama dakika kumi hivi tukafika kwake, nyumba yake ndio ilikua na hadhi naona, lakini hata sijui imejengwa nadhani kwa mikoko lakini sina uhaki, akatukarib9sha ndani mkewe akaja akawakaribisha kina mama ndani. Mzee Ali sisi tuwahi msikitini jamani, poamesha adhiniwa, tukaenda tukasali dhuhr tukarudi.
Kurudi tukakuta chakula wali w maana, samaki wa cchukuchuku lkini samaki kweli wa kula wageni na wengine wamekaangwa. Tukaanza kula wanaume wote wanawake walichukuliwa ndani huko. Tulipomaliza Mzee Ali akaleta kahawa kina mama nao wakawa wameshakuja tukakaa nao kama ukumb lakini una kitanda, tumeenea wote.
Bakora: Sasa Masheikh trusipooteze muda kwa kua sote ni wahusika na hakuna mgeni hakuna siri tufanye kilichotuleta ambacho ni muhimu kabla ya sherehe.
Mzee Ali; Sawa, basi tungeanza safari si mbali ni hapo juu kidogo, kule ndio sehemu za juu za kisiwa cha Kojani, tutatembea kidogo, wote mpo sawa kutembea? Mkewe Mzee Ali akasema, mimi nipo siendi, wageni zangu mtanisamehe.++Bakora: hayta sisi tuanze safari, tuatoka, wakati tupom njiani.
Bakora: Mimi na Mzee Ali tumekutrana kabla hamjaja na kishafahamishwa na wakubwa zake kuwa mimi nipo na wenzangu tupo na wewe DSheikh Simba, sote ni wageni kwa sshughuli hio hio, au sio Mzee Ali?
Mzee Ali; Naam, Sheikh, mimi nashkuru kua mmeacha kazi zenu kuja tuyamalize mambo ya huyu binti na yangu, maana leo ndio shughuli imeshaanza, pale tuliposhuka tumekuja huku kushoto, tungeenda kwa kule kulia mngeona ng'ombe walivojaa kwa shughuli hii hii ya leo usiku na kesho. na bila kumaliza hili jambo letu inakua ugumu sana kwangu. Nawashukuru san tena sana...,
Tena Dokta tumetoka haraka nyumbani kunamzigo wako ilikua nikukabidhi kabla hatuja huku ninao hapa bora nikupe kabisa mzigo wako. Mzee Ali akajisachi akatoa bahasha ya kaki nzito tu. Hii Dokta amana yako.
Dokta; Amana ipi tena?
Bakora: Mimi naona ishike kwanza Mzee Ali, tukifika hapo kabla ya kuanza shughuli mtaeleweshana, hapa njiani haina haja, au sio Sheikh Simba?
Mimi; kweli, maana tunatembeana maongezi haya haipendezi.
Mzee Ali, ni hapo mbele kidogo tu, tumeshafika, sema leo huku kutakua na wageni wengi wankuja kwa ajili ya hii shughuli.
Hatukwenda sana tukafika sehemu kama ina uwanja hivi halafu kwa mbele kuna kama lango la pango hivi,. kuna watu watu pale.
mzee Ali; Ni hapa jamani, lakini naomba twendeni pale pembeni tukamalize kukabishiana amana yetu.
Tukaenda pembeni kuna kivuli cha miti moiti pepee chini tukakaa pale, Mzee Ali akaitoa tena bahasha, akaanza.
Mzee Ali; kwanza ndugu zangu mliopo hapa wote, kwa kuijutia nafsi yangu na jina langu nakuomba sana Dokta unisamehe sana makosa yote niliokufanyia, unayoyajua na usio ya yajua.
Dokta: hakuna kosa ulilonifanyia lakini binadam hatujijui tusameheanae sote pengine tunakoseana bila kujua.
Bakora; Kwanza naomba niongee kidogo msione vibaya, nyinyi hamnifahamu, mimi ni trafiki yake sana babu yenu wewe Simba na wewe Nisha, nyie mnanijua, Nisha umenina ona tu kwa babu yako unanijua klakini sio sana, Simba swahiba yangu hapa ananifahamu vizuri sana. Mimi nimekuja kwa sababu mbili hapa Kojani, ya kwanza ni hii iliotulet hapa sasa hivi na hii ni ya msingi ya lili na mimi miaka mingi naisikia sherehe ya kila mwaka ya Kojani nikaona ndio fursa na mimi nije kuiona>Umenikumbuka Nisha, mimi rafiki ya Simba?
Nisha ; Sasa nakukumbuka tokea mdogo nakujua kwa babu, tunakuita Mzee Bakora, Bakora yako hio kama ya babu na mume wangu.
Bakora; Ndio wote wananita hivoi hivo Bakora ndio imekua jina langu kwa sababu siiachi hii imekua ndio alama yangu. Akacheka.
Sasa Mzee Ali tusizungushe maneno muda unakwenda, bira uingee moja kwa moja kama kuna mtu analake atasema, hakuna siri, sisi sote wamoja hapa. Tuokoe muda tufanye mengine, au unasemaje Sheikh Simba?
Mimi: Unayosema kweli.
Mzee Ali; Dokta, mimi nimekufanyia makosa, tena makosa makubwa sana ambayo hata kuyakiri inakua vigumu lakini inabidi niyakiri ili niishi kwa amani, sitokua na mani maisha...
Mimi Dokta nimekukosea namna tatu kuu. Kwanza ulipoojulishwa kwangu na baada ya kukutazama noilijua kua voiumbe uliokua navyo mimi siwezi kukuagua lakini nikakuficha, nilijua kua wewe unasumbuliwa na viumbe aina ytatu, kimpja ndio huyo aliekupenda, nililiona hilo, halafu ulikua na viumbe amabyo ni kizimu ya kikwenu ya kibuki ya upande wa kuumneni kwa na kukeni kwako. Ndio maan nikashikilia sana uende ukawaone wau wa vibuki ndio aliekujulisha mikamwambia kwa nia njema kabisa atagfute huko Unguja ndio kuna wataalaam wa vibuki, ikaonekana vibuki wako, wapo wanaoweza kutulizewa Unguja na wengine wa uonade kikekeni kwamkoi ni laima uende kwenye shina huko kwenu Anjuani, Ngazija huko. Hayo yalikua ni ukweli nililokudanganya ni kua tunaweza kuyashughulikia sisi. La pili nililokukosea, ni sisi katika kazi zetu huwa tunavitumia vijini viwe na wewe ili viwe vinatupa habari zako zote ndio maana ulipokua unakuja kwangu niliweza kukwambia mambi yako, wala sio siri niliwaweka mimi hao viumbe muda wote. Lingine mama nililkusoea nile kukutapisha amaba nilisema uchawi, ile mama ni mchezo tunacheza wa mazingaombwe hata utazame vipi kama hujui tunachokifanya huwezi kuelewa wala kuona. Kwa hio mama hakunauchawi tuliokutapisha wala chocote, Nisamehe sana kwa hilo mama. Ni hayo mama.
Bakora: bado, sema kweli, mimi ninz(azo habari zote si unaju akua nimekutana na wakubwa zako? Au niseme ka unajifanya umesahau?
Mzee Ali; Nisamehe, mambo mengi kichwani kwa sasa.
Bakora: nakuonya kwa mara ya mwishi, unakumbuka siku huyu binti aliokuapa shillingi millioni moja?
Mzee Ali; Nimekumbuka sana, mnisamehe mimi hilo lilinitoka kabisa, kweli mniamini siwezi kudanganya kuna wakubwa zangu wanayaona na kuyasikia haya mambo.
Bakora; haya jielezee, tumekuelewwa kua ulisahau, sasa umekubuka.
Mzee Ali; Siku ile vile vile ilikua ni azingaimbwe tu, yale machupa mahirizi tuliofukua yalikua ni yetu wenyewe wala htukufukua pale tulipochimba. Tulikua tundanganya ytujipatieiea pesa tu. Niasamehe sana mama.
Bakora; kuna ingine?
Mzee Ali; mengine ni ya kusema sema uongo tu kwa ninayiambiwa na majini walikuwa kwake, najifanya kama ni mtu wa ajabu sana ninayajua majina mpaka ya ndugu zake, mpaka watu wa kazini kwake, kwa ufupi kila kitu hake, majini yalishikwa ndio yalikua yananiletea habaro hizo zote. Ni ujanja wa kawaida wa ma,bo yetu ya shirki.
Bakora: baado hujamaliza, nakukumbusha najua hili huwezi kulikumbuka kwa kua hili lilikua bado mnalipika halijatendeka. Sema tumalizane.
Mzee Ali; Nimekuelewa. Bwana Bakora; Dokta kumradhi mama nisamehe sana tulikua tunakutengenezea sihri iliukirudi safari yako ya Unguja yukunyweshe, ilikua ya mambi maiwili, moja tunakutia ugonjwa mdogo tu, wa kuumwa na kis)chwa na kila ukiumbmwa na kichwa lazima uje kwangu ndio nikupe tiba ya kukutuliza. Hilo mama tulikua tunalifanya ili kujipatia kipato cha mara kwa mara. Ni dhulma mama. Nisamehe sana lakini halikujaaliwa kufanyika, toma siku aliokuja huyu bwana na babake nyumbani kwangu, sikudhania kama wao ndio wenye nguvu ya kuharibu mambo, mpaka mlivokua Unguja ndio nikawa siwaoni majini nilowapa kazi yako, ndio wakubwa zangu katika kuwatafuta wakasema wamefungwa lakini hatuwezi kuwaona mpaka atake Simba hapa. Ndio hayao mama.
Dokta na mke wangu nikawaona wameanza kulia.
Bakora; Sasa sikilezeni kna mama apoleni sana ndio ulimwengu na waliwengu walivyo. bado, hayo yako mama madogo sana. Utayajua mengi ya wengine kenye hii safari, hii ni fsagari ya kufungua macho yetu wote. Haya kuna mwenye swali?
Mimi; Ndio, mimi nina swali au maswali. kwanza nagtaka kujua mmzee Ali majini unayoyatuma unayatoa wapi. Sitaki kudanganywa, kila kitu kipo wazi sasa.
Mzee Ali; naapa sitodanganya. Nimeshaona nikidanganya au nikificha neno najiharibia mwenyewe. Mimi bwana simba najua kutuma majini aina tatu.
Aina ya kwanza ni hawa wakuleta habari, hao tunawita saatulkhabar, kai yao ni hio tu, na hao ni majini wa hapa gtulipo, Mimu wao na wakubwa zao wapo hapa, na hivi navyokwambia wapo na wengine wamefungiwa humo ndani hawawezi kufanya kazi yangu wala ya mwengine.
Majini aina ya pili nyoweza kutuma mimi ni ambayo wengi wanayaita ya kutengeneza, lakini kiukweli huwa hatutengezi isipokua hao ni majini ya kishetani yapo kial kabila lakini ni yale maovu kabisa yenye ushetani yaliogoma kabisa kutubu, Sisi tunatengeneza mawasiliano nao na kwa kutumia njia zao wenyewe waliotufundisha na katika hayo mawasiliano tunawaahidi tutawatimia wayatakayo na tunamtafiuta yule wa ile kazi tunayoitaka sisi kwa funi tunaweka majina ya huyo anaetakiwa ashulikiwe nayo basi inakua ndio tumemaliza kulitengeneza.
Majini aina ya tatu, hivi ni vivuli tunanunua aidha iwa watu wenye kazi hizo au kwa majini wenye kazi hizo, lakini kwa kuepuka mashrti mengi ya majini, ndio tunavinunua hoivo vivuli kwa wagtu, hawa wa namna hii kazi yao kubwa kuaharibu kufanya mambo machafu.
Mfano kumuharibia mtu mvuto wake, na ndio ukenda kwa mganga anakwambia nyota imechafuka, hakuna cha nyota wala nini, inakua kishajua ni vivuli tu hivyo, ukimlipa naviondosha kama anajua namna zake, na yeye anavichukua anaviuza tena kwa wengine.
Ndio hivyo ninavyovijua kuvifanya mimi kuhusu majini.
Dokta alikua analia tu, kimya kimya lakini kwa kwikwi.
Wife: laanatullah aleik, mzee Ali, tazama kitambi chakula haramu tu.
Mimoi; Tulia mkwe wangu ndio yamekwisha tena.
Bakora; Haya ulikua unagtaka kumpa nini?
Mzee Ali, hii bahasha ina oesa nimejaribu kupiga hesabu nilizoshukua kwake nimepata kama millioni tatu, nilimpa laki tano kwanza na hizi kwenye bahasha millioni mbili na nusu. Naomba sipokee Dokta nihaki yako, unisamehe sana.
Dokta: Mimi sikusamahe duniani na akhera, yaani shida zangu nimekutaji bado unanitumia vijini, na unataka kuniroga juu ili niwe knakuchumia wewe tu? Unafikiri hovyo vi milioni tatu vyako ndio vitanitusha roho nikusamehe, wewe umeoiga hesabu ya ulizopopkea wewe tu, umepiga hesabu ya muda wangu, umepiga hesabu y asafari zangu za nenda rudi? Umepiga hesabu ya mawazo yangu kwa kujidai kunipa faraja kumbe unanimaliza zaidi. Sikusamehi na hivyo vijini vyako.
Bakora; Ali leo hii utatafuta millioni kumai utampa huyu binti, sisi tumeshawawka vijini vyenu hapo kwenu kabla hata hamjaja hapa, lakini tumevufunga kufanya kazi yoyote na leo kama hukuleta millioni kumi, usiku ndio kazi yako sijui utaifanyaje, ndio mwisho wako leo.
Mimi; haya twendeni jamani, kama tumemaliza hakuna cha kungoja.
Wife; kama yamekwisha na hio sherehe yao ya kishetani hatuna haja ya kukaa kuiona, twendeni zetuni.
Mzee Ali; Akapiga yuwe kama siku ile pale kwake akapiga smasolti na kitambi chake, mimi nikashidwa kujizuia nikacheka, m0aka dokta na wife wakacheka,
Wife; Nini tana jamani?mbina imekua sarakasi?
kitu kimojawapoi nnachopendea mke wangu, hana uoga kabisa kabisa, yupo straight firwarda na manweza kua na mawazo au mmekasirika yeye akaleta utani kwa kuwatuliza. Ni kama Zee tu au babu tu. Hata mimi hiuwa nastuka na kuogopa saa zingine, wao sijawahi kabisa kuwaona wakiopa jambo.
Mzee Aki akaongeza yome wakapiga samasolti nyingine kama mbili.
Mzee Ali; Salaam Salaam Salaam, wageni mnisamehe sana, leo mmekuja kwangu kwa amani lakini mimi nikasirishwa sana na huyu Ali, katutia aibu Kojani nzima. Samhani sana, mimi naondoka nilija kuwasalimia hapo kwenye hio mlango ndani ndio kwangu. Karibuni sana. Msee Ali akajibwga chini, nikajua jini samasolyti limeshakitoa.
Mzee Ali akaaa chini pale kapigwa na butaa kama dakika tatu, kimya kabisa akaanza kutazama kote, akaanza kulia alipomaliza kulia.
Mzee Ali: jamani mimik ndio basi tena, leo hii sasa hivi nakwenda kuwapa millioni kumi na hizi chukueni jamani, sasa hivi nyumbani kwangu ninazo. twendeni jamani, mimi nimeambiwa nisiguse humo pamgoni mpaka nimalizane na nyinyi, mpka nihakikishe mnaondoka Kojani salama kabisa. Twendeni tukamalizane mimi jipagte kurudi huku.
Tukaondoka pale pangini krudi kwa mzee Ali, kufika kwake nje tu, Dokta akasema mimi siingii ndani kwa huyu mchawi, handbag na bag langu nitoleeni asije akalishindilia ma uchawi yake mbwa huyu.
Wife; na mimi siingii toni vitu vyetu wote jamani.
Tukaingia mimi na bakora hata jini 1 na 2 wakabaki, mkewe akatoka.
Mkewe: Kuna nini jamani mboina Mzee a)Ali anasema mmegoma kuingia kwangu jamani, njooni jamani, nawaomba mimi.
Kinamama kimya hawajamjibu kigtu akrudi ndani, Mzeae Akaingia wapi sijui huko ndani hakuchelewa akatoka na bahasha nyingine nene zaodo na ile ya kwanza anayo.
Mzee Ali; Naomba nbwana Bakra uingilie kati mnisamahe sana, nagfafahamu makosa yangu si madogo ni makosa ya kuuliwa kabisa, natoa ahadi moja kwenu kuanzia leo nitanya tiba za halali tu na nafanya toba, hii kazi mimi basi tena na hio sherehe yao potelea mbali. Hizi mama Millioni kumi kawa shinda nilizokupa, nafahamu, shida zako hazina thamani ya kuzilipa, lakini hii inakua kua ni kifuta machozi na tushuku Mwenyezi Mungu kuwa kupitia kwangu umejiposesha wewe na umeniokoa mimi nianze kufanay toba, na kilinge cha Buguruni kuaniza sasa kimefungwa rasmi. Mimi sina zaidi Bwana Simba, Sina zaidi Bwa na Bakora, mshikieni hizi huyu bibi twendeni niwasindikize maanake hata nyinyi mmeisikia amri iliotoka nihakikhshe mnatoka Kojani salama.
Tukaanza kuondoka yeye tukamwabia pita mbele utuonhgoze niia, akapigta mbele huku bado analia,
Tukafika kivukoni tukapanda nae ngafrawa kama tulivokuja hatujakaa sana, kumbe wakati tunaondoka kwa Mzee Ali mkw)e wangu alipiga simu, kukawa kuna gari haipo mabli sana sisi ikaja kutuchukua, Tukaagana pale Bakora akasema nyinyi nd)endeni, Dimba chukua pesa hizo, msiogope, kama alivosema za kufutia machozi.
Mimi nikachukua bahasha zote mbili, nikamwambia mzee Ali nakuomba kauli yako ya toba iwe ni kweli, hio ni ahadi kwa Mwenyezi Mungu. Tukarudi zetu hoteli.
..