Inatokea post namba 304.
Tulipomaliza tukatoka nje na babu, akanambia haina haja ya kwenda kilingeni, saa hizi hakuna atakaekuja hapa, watu wamechoka wanakwenda kulala. Wewe bwana mkubwa huendi kulala? Kisa kirefu.
mimi; bbu nikikukosa leo naweza nisikupate mpaka msimu mwingine, mwanao anaweza kutimua kurudi Dar wakati wowote, gereji siku hizi akiwa yeye yupo mimi naweza kusafiri, nikiwa mimi nipo yeye anasafiri, Hivi imebidi jana njiani ampigoie msomi aende pale mpka yeye au mimi nirudi, nasikia wanabishana siku ya kurudi.
Babu; haondoki kesho huyo kwa sababu kesho kutwa kuna gari inakuja kuchukua nazi, shambani kwake.
Mimi: hajanambia.
Babu; Atakwambia kesho akisha kua na uhakika, lakini mimi niliongea na wale watu, kesho hawawezi kuja, wanakuja keshoi kutwa. labda akuwache wewe uwapakilie nazi.
Mimi; kama kina pesa haondoki, namjua mwanao mimi, anapenda pesa kama Mpemba.
Babu: Hio kachukua kwa bibi yako, mimi sina hio. Vipi wewe?
Mimi: Mimi nakurithi wewe babu, nakumbiuka simo ulinambia kama mali inakuja jhakuna wakuizuia na kama haiji hakuna wakuileta.
Babu; Hio ni kweli kabisa babu. Tulifikia wapi bwana mkubwa?
Mimi: Plae unasema umetupwa chini pangoni.
Babu; babu nadhani nilizimia, maana nakumbuka kurushwa na kuanguka na kingine nakumbuka nimesimama pale nilipoangukia na Jini la Mzee Mgunya limenisimamia, mimi mpaka hapo nilikua najua ni Mzee Mgunya mwenyewe, kumbe ni jini wake, alikuja kunambia baadae.
Babu; Ikawa kama nimepagawa kidogo, nasikia joto, ule moto unawaka kweli kweli tuliouwasha sisi, kulikua kuna magogo yapo pale akanambia yote tuyaweke kwenye ule moto, tukayaweka na manyasi yote tukayaweka, akanambia haya twende nje, kutoka nje akanambia wewe pumzika hapo mchangani, mimi nakwenda zangu tutaonana mjini ukija. Nikakaa mbali kidogo na ule mlango wa kuingilia pangoni, pale ambapo siku hizi tunachoma choma samaki na kamba wakija wageni.
Babu; Basi bwana mkubwa nikakaa nikapiwa pigwa na upepo nikaanza kupata fahamu vizuri , muda wote nimekaa nasoma QAAur'an tu. Nikaanza kuwaza huyu mzee mgunya usiku wa manane huu peke yake saa hizi akatize hili pori, siku hizo babu hili pori ni kubwa kweli kweli, miti mikubwa manyasi mengi, wanyama na wadudu wengi sana. Kumbe ilikua muda wa alfajiri sio mbali. Kidogo akatoka Jini Bakora.
Tukauliza hali zetu, akanambia wewe soma Qur'an hapa mpaka ukisha sali alafjiri uende Tanga lakini usiende nyumbani kwako nenda moja kwa moja kwa Mgunya, mimi mtaniita baadae. Kazi imefanikiwa. Nilikua nataka kumuuliza lakini nikahisi hataki kuongelea lolote kuhusu kazi iliotuleta pale, basi baada kusali alfajiri nikatwang mpaka barabarani, zikukaa sana nikapata gari ya kwenda Tanga, nimeingia Tanga jioni, zamani barabara mbaya sio kama sasa.
Babu; Kufika Tnaga moja kwa moja kwa mgunya, muda wote babu nasoma Qur'an kimoyo moyo. Kufik pale nikapumzika baadaya ishaa akaitwa Jini Bakora akaja, pale ndio nikajua kua yule alikuwa jini niliekua nae pangoni hakua Mgunya, tulishinda nae toka mchana tunavita magogo na walewagiriama wa bindeni kule niwachukua asubuhi wanisaidie kujaza manyasi na magogoya kuni, Tulifanya kazi nzuri sana babu.
Ndio pale sasa jini Bakora akatueleza kua yule mtu tumwfanikiwa kumtoa kifungoni ndio huytu Ramses, alikua kifungoni mda nrefu, utamuuliza mwenyewe atakwambia. Siku ile babu sikuruhusiwa kwenda nyumbani, mkewe Mzee Mgunya akamfata mke wangu mimi nikakaa pale mpaka ule moto tuliouwasha kule ukachima magogo yote pakwa jivu tupu, lile jivu babu tulilipakia kwenye ngarawa tukaenda kulimwaga baharini mpaka pakawa hakuna hata jivu kabisa pakabaki mchanga mgtupu kama palivyokua mwanza, hayo ndio tuliyafanya baadae lakini.
Nikakaa pale kama nipo saba ya harusi ikawa kazi yetu kula kulala siku tatu ya nne nikaondoka na mke wangu nikasindikiwa na Sheikh Mgunya mpaka nyumnai tukafanya dua. Sheikh Mgunya akasema siku ya saba atafanya sadaka ya chakula pale kwake, tukale pale watu wa nyumba nima, basi ikawa hivyo babiu.
Siku tuliomaliza takrima ya Sheikh Mgunya, kurudi nyumnani usiku akaja Jini Bakora, kaja kafurahi kweli kweli nikajua mambo mazuri. Akanambia nimekuletwa mgeni wako, utaongea nae mwenyewe lakini hutiweza kumuona isipokua mtaongea kama kawaida. Kwa hio chumba kile chako tunachokutana nikiondoka mimi ukisikia unasemesha usistuke mgeni wako alietoka kifungoni, Mtaingea wenyewe mimi sitaki kuingilia maongezi yenu. Jini Bakora akaondoka.
Itaendelea.
Ombi zuri sana.
Kwa sisi wa koo za simba, hilo ni jqmbo dogo sana na dawa zake zipo, tena tunakulekeza uzifanya mwenyewe.
Tiba ya nguvu za kiume ina mlolongo wa kufatiliwa kwa watu wa kisasa.
Kwanza ulijuaje hauna nguvu za kiume?
Una mke?
Kwa muda gani sasa?
Una watoto?
Wa ngapi?
Una umri gani?
Unajichua (punyeto)?
Unatembea na wanawake zaidi ya mkeo au ya wale aliokuruhusu mkeo?
Una lawiti au kulawitiwa (ushoga). -?
Unatumia sigara?
Unatumia bangi? Elezea unaitumia vbipi na kwanini?
Mkeo ndiye mwenye kulalamika kua huna nguvu za kiume?
Au ni wewe mwenyewe yeye hajawahi kulalamika?
hayo ni baadhi wa maswali ya awali, unaweza kuyajibu kwa faida ya wengi au unaweza kuja PM kama hutopenda kuwa muwazi.