yellow java
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 1,283
- 2,332
Kwani yesu alipandishwa na kushushwa mlimani na nani ? Kama siyo huyo jini..!Kitabu gani aya gani?
Kwani yesu alipandishwa na kushushwa mlimani na nani ? Kama siyo huyo jini..!Kitabu gani aya gani?
Nakupata vyema sana mkuu, nina swali sasa utamtambuaje huyu jini ni mwema maana kigezo cha kukutendea mazuri hakutoshi kuwa bayana ya nia iliyojificha.ASILI YA MAJINI --2
Baada ya kuona kuwa majini wameubwa kwa moto kwa mujibu wa quran nije katika hadithi za bwana mtume muhammad swalalah alaiy wasalam.
Aisha (RA) alieleza kwamba Mtume Muhammad (SAW) alisema: "Malaika waliumbwa kutokana na nuru, majini waliumbwa kutokana na moto na Adamu aliumbwa kutokana na kile kilichoelezwa kwenu."
عن عائشة رضي الله عنه قالت: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «خُلقت الملائكة من نور، وخُلق الجَانُّ من مَارِجٍ من نار، وخُلق آدم مما وُصِفَ لكم».
[صحيح] - [رواه مسلم]
Hadthi hii ni sahihi na imepokewa na muslim, Katika hadithi hii tumeona kuwa Malaika wameumbwa kutokana na nuru , majini kutokana na moto na wanadamu kutokana na kile tulichoelezwa kwa maana hapa mtume alisha waeleza kuwa mwanadamu kaumbwa kutokana na udongo.
Hivyo hakuna shaka kuwa asili ya majini ni mwale wa moto. Tuje katika melengo yao kwanini majini wameumbwa?
LENGO LA KUUMBWA MAJINI.
Imetajwa katika Quran kuwa lengo la wanadamu na majini kuumbwa ni kumuabudu Allah. Kama ilivyokuja katika quran (Adh-Dhariyat 51:56)
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ -- sikuumba majini na watu ila waniabudu.
Hapa tunaona kuwa lengo kuu la kuumbwa majini na sisi wanadamu ni kumuadu Allah, swali linakuja ikiwa ilo ndio lengo la kuumba mbona majini na wanadamu tunafanya mambo ya kumkufuru mungu nadhani umesoma katika kisa cha bwana simba mabalaa ya majini jinsi wanavyokata majii(kunywa pombe), wanavyofanya uchawi na mabalaa mengine, Kuhusu wanadamu apo bwana Battor unajua mabalaa ya mwanadamu uzinzi, wizi, rushwa, chuki, uongo, dhulma, zinaa, mauaji, kukata undugu, kusengenya, ushoga, utapeli n.k kwanini yote haya na Allah anasema lengo ni kumuabudu yeye?
Quran inajibu kwa kusema katika surah Al-Insan (76:3) ''Hakika Sisi tumemwongoza katika njia. Ikiwa atashukuru au akufuru."
إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا
Hapo wamezungumzwa wanadamu kuwa muongozo upo na njia ni mbili tu ushukuru au kukufuru na majini pia imeelezwa katika surat jinn kuwa kuna kundi la majini lilisikia quran nalikakiri kuwaa ni ya ajabu na inaongoza katika haki na hawatamshikisha mola wao.
"قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا * يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَنْ نُشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا"
Lakini pia katika aya ya 11 ya surat jiinn inasema
''وَأَنَّا مِنَّا ٱلصَّـٰلِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَۖ كُنَّا طَرَآئِقَ قِدَدٗا'' -- Na hakika miongoni mwetu wapo walio wema, na miongoni mwetu wapo kinyume na hivyo; tulikuwa njia mbalimbali.
Hapa utaona kuwa majini wenyewe wanasema kuna wema na wabaya hivyo suala linabaki kwa mwanadamu au jinn kuchagua njia ya kufuata na watakao mtwii Allah malipo yao ni pepo na watakao kufuru na kumuasi ALLAH ni motoni kama ilivyo katika quran
"قَالَ ادْخُلُوا فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ فِي النَّارِ"
(Allaah) Atasema: Ingieni motoni pamoja na ummah zilizokwishapita kabla yenu miongoni mwa majini na wana Aadam”. [Al-A’araaf: 38]
Toka nimeanza kuelezea mpaka hapa kuna mambo utagundua kuwa kwa mujibu wa uislamu:-
Hivyo basi, Ushirikiano wowote wa mwanadamu na majini katika kumuasi Allah ni makosa na imekatazwa katika uislamu hilo halina mjadala, ni KUFRU.
- Malaika wameumbwa kwa nuru, Majini kwa moto na wanadamu kwa udongo
- Lengo la majini na wanadamu ni kumuabudu Allah.
- Watako fanya kinyume na kumuabudu Allah malipo yao ni Moto.
Mjadala unabaki Je ni sahihi mwanadamu na majini kushirikiana katika wema mfano bwana Arsis alivyoshirikiana na Simba katika kumuokoa msukule huko unguja na mifano kama hiyo Je yafaa?
Inshaalah, Nitalieleza pia kwa kadri ninavyoelewa, Hapa hapataki muhemko maana pana mambo mtu anaweza ona yafaa kumbe haifai na mengine kuona hayafai kumbe yafaa.
Nitarudi kuelezea maisha ya majini, kuzaana kwao, tabia zao, na kubwa zaidi kwanii wanasumbua wanadamu.
Haya ni maneno yako, Biblia haisemi hivi.Kwani yesu alipandishwa na kushushwa mlimani na nani ? Kama siyo huyo jini..!
mambo gani?Kwa sababu wewe ni jini mkubwa sana, sema yale mambo yanakuondolea ukubwa wako.
Simba.
Clear Mbwai mbwai tu, simba hataki masiara na dm , apa simba kanyooka kama rula yaniWana ukumbi,
Kabla sijaendelea kujibu hoja na kumalizia kionjo cha Arsis cha kojani na Comoro. Naomba mnisome ka umakini yafatayo;
1) Maswali na msaada kwa watu qanaokuja Private.
ka sasa sijibu mtu private, iwe kwa msaada au maswali mengine. Sababu kubwa ni mbili; ya kwanza, tunaweza kujibu swali au msaada kwa mmoja PM lakini ikawa ikawa ni ya wengi tukilijibu jukwaa la wai, kuna wengi hata kuitumia hio PM hawajui na kuuliza wanakua wagumu, wengine hawajajiunga kabisa wao wanasoma tu na kutamani kuuliza lakini hawawezi, ni kibinadamu tu.
La pili, ni kua kuna watu wameshanijaribu mara kwa mara kuniuliza maswali ya kimtego PM kutaka kujaribu kufahamu naishi wapi na tuonane au wanione vipi, sifahamu nia zao.
Cha ajabu na kushangaza, kuna watu wananiofa pesa, wengine wanani ofa asilimia za biashara zao. Wengine wameniofa mpaka penzi. Hawa ni zaidi ya mmoja, wa kutokea Tanga, Dar, Mwanza na Unguja. Waislam kwa wasio Waisla., sijapokea ombi kam hilo nje ya mikoa hio. Au wanasema kweli kuhusu mikoa au wanasema uongo, au wanasema kweli kuhusu dini na imani zao au wanasema uongo. Sipo kuchunguza mtu, lakini nawaambia sitoi majibu Private waka sitaki kujibizana na mtu Private.
Naomba wote muelewe, mimi sio mganga wa kienyeji, sio mchawi, sio kazi yangu kufanya tiba. Hata jukwaa la wazi ninaloweza kulifanya ni kushauri tu ninachokielewa, sina zaidi ya hapo. Kama mlidhani huu ni uzi wa mganga wa kienyeji au "Shehe" au mchawi, mmekosea sana. Huu ni zui wa kuongelea niliopitia na itafikia ninaopitia mpaka leo ili wengi tuielewe dunia.
Arsis yupo kweli, kama ni jini ni mtu na wasaidizi wake wapo kweli majini wawili wa kike, Jini bakora yupo kweli na ana hekima kubwa sana na anaijua miti shamba kuliko tunavyofikiria, tumieni fura ya kuuliza tiba zenu kwa miti, mizizi, matunda, na hata chakula kii ule vipi. Mtashanagaa uwezo wake. Yote nayajibu kupitia JF kwa idhini yao.
Majini na mizimu ya Kisimba ipo kweli na ni ya jadi ya kwetu ya pande zote za baba na mama lakini mimi binafsi nimeachana nayo kabisa, haina ugomzi na mimi kwa kua sikuachana nayo kwa vibaya, mke wangu nae kaachana nayo, mamaya gu kaachana nayoi kwa kiwango kikubwa lakini bado yupo huko kwa siri, Babagu nae bado yupo huko kwa dhahiri kabisa ingawa umri hamuungi mkono lakini hajaacha vituko vya usimba kila vinapomtokea. Nawaombea wazazi wangu usiku na mchana waachane na usimba wa kishenzi. Arsis amesema usiongee nao kuhusu hilo mpaka wa kuhusishe usianze kuwauliza au kuwiangilia, anasema yeye ana dili na hao masimba wenyewe, wote ni rafiki zake na wengi wao washakaa sawa, sielewi anamaanisha nini kwa hilo, hasemi zaidi.
kama una swali, maswali, tatizo au chochote kile uliza jukwaa la wazi iwe faida kwa wengi.
Simba.
Simba nasubili majibu ya maswali haya kutoka kwa ArsisHapa mimi nina swali kwenye hoja ya kwanza ya Jini.
Kama jini ni kiumbe cha Allah wameumbwa ili wamuabudu Allah, je majini wanatumia kitabu gani?
Je majini ni dini gani?
Je majini wanaswali wapi?
Je kuna ukweli wowote kwamba kuna binadamu wanatengeneza majini na kuyafuga na kuyatuma?
Naomba na Arsis atie neno kwenye haya maswali yangu yanayonitatiza.
Asante.
Find a quite Room or empty space and call them while being in a meditation mode. Call them by whatever name they used in your dream.How?
They didn't mention their name so far...Find a quite Room or empty space and call them while being in a meditation mode. Call them by whatever name they used in your dream.
Hakuna neno "kulifukuza" kwenye hayo maandishi, hayo umeongezea chumvi yako.Nimesoma mpaka mstari wa 10 Yesu alipomfukuza Ibilisi.. haya nipe mfano halisi wa mtu aliyewahi kulifukuza jini lililomkumba
mmh!naona mada imeshavamiwa na wazungu.!Find a quite Room or empty space and call them while being in a meditation mode. Call them by whatever name they used in your dream.
Arsis anasema "lisan" au hujamsoma?Hapa sasa tunazungumza lugha moja... Tuendelee kupata darsa🤝
Leta andiko hapa .Haya ni maneno yako, Biblia haisemi hivi.
Inachosema Biblia Yesu alipelekwa jangwani na Mungu mwenyewe ili ajaribiwe na Ibilisi na alifunga usiku na mchana kwa siku 40, na huu ulikuwa ni mtihani wake kutoka kwa Mungu.
Habari za jini umezitowa wapi?
Kwahiyo nawe unakubaliana na hiyo hoja kwamba tunatumia ukristo kufundisha uislamu,upo serious kabisa?Mfano mzuri sana huo, nimemuelewa sana Arsis, Waislam imewaingia sana hiyo.
Nawashauri Waislam wenzangu tuanze kutumia Qur'an kufundisha Uislam.
Qur'an haina shaka ndani yake.
Leta andiko hapa .
Na ukiona mungu mwenyewe anampeleka yesu kwa shetani (jini) basi ujue shetani ni kiumbe cha hatari sana ambacho hakina mfano na kiumbe ambacho kinakaa na kupiga story na mungu nini wafanye .N k
Hakuna Jini Mwema wala Binadamu Mwema.Nakupata vyema sana mkuu, nina swali sasa utamtambuaje huyu jini ni mwema maana kigezo cha kukutendea mazuri hakutoshi kuwa bayana ya nia iliyojificha.
Na imeelezwa huko juu kuwa moja ya sifa zao kubwa ni uongo. Kama tujuavyo muongo haaminiki.