Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Huko ndiko walikotoa tulio, Lidafo, Etugrul Bey Nourhan na mashehe zao, labda kuelewa au kuto kuelewa.
Kwanini hii elimu imeegamia upande mmoja wa dini?
Wewe mwaga elimu ya upande uujuao.
Simba.
 
Huko ndiko walikotoa tulio, Lidafo, Etugrul Bey na mashehe zao.
Kama hazina sawa, Mimi nishakupa zenye kisa cha adamu.
Muite Arsis ajibu maswali yamekuwa mengi
Hicho kisa cha "adamu" kiko wapi, ulichonipa? Qur'an au Biblia?
Simba.
 
Hoja yako hapo ni nini sasa?
Rudia kunisoma hujaelewa.
Nimefurahi unaanza kupata elimu na kukiri kama hivi "... Ndio quran haijasema kuwa Adam Ni binadamu."

liia hapo na neno "wa kwanza.

Sisi tunaamini kuna adama wengi wametajwa kwwenye Qur'an, sio mmoja, lakini hawakutajwa kama mtu wa kwanza kuumbwa.
Simba.
 
Fikra zako hazipo sawa, sisi tunasema Adam hajatajwa kwenye Qur'an kua ni mtu wa kwanza, mmeyatoa hayo kwenye biblia.

Kua makini ni elimu kubwa sana, usiburuzwe. Unajua maana ya elimu au ngoja nikufahamishe alivyowahi kunifundisha Arsis maana ya elimu "elimu ni maarifa yanayotokana na ushahidi".
Simba.
 
Waislam wengi ni wakristo wa zamani, au wao au wazazi wao. Naamini Mkristo wa kweli ni Muislam.

Sihitaji msaada, haya aliniochia babu yangu soiyatumii. Ukiusoma vizuri huu mjadala utaona hata waliposaidia kutoa matatizo ya watu, mimi nilikuepo tu kwa kua ni marafi zangu. Lakini sijawahi kufanya kazi ya uganga, isipokua nikikutana na mtu ana matatizo na naweza kuyatatua namtatulia. Mwiko kukataa, hata nikikataa wanakuja wao wanasaidia.

Majini wanaotaka uwafanyie na wao vitu vyao, hao sio wema ni wachawi kwa mujibu wa Arsis.

Kama unakumbuka kisa cha Unguja? Baba yule alianza kwa kutoa jogoo ikaenda akaanza mbuzi, ikaenda ikawa ng'ombe, ikaenda ikawa ngamia, ikaenda ikawa nyama na damu za watu, mwisho kamba ikakatia kwa binti yake.
Simba.
 
Thanks for this very interesting thread, please do us a favour, compile all episodes into thread starter.

Nimesoma page one nikavutiwa sana, nilipokuta kuna pages 128!, nikaishiwa nguvu!.
Please do the needful. Hii story ukiiweka kwenye kitabu kitakuwa best seller!.
P
 
Nimefurahi kwa bingwa na gwiji wa uandishi kama wewe kuliona hilo.

Nitawapata wapi publishers, kisa cha kufunguliwa macho ni kirefu sana, ninaishi katika hali hiyo kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

Nimekusoma kuhusu Karma mpaka nilipokuona umeandika hapa, nimemuuliza Arsis, ni nini maana ya Karma? Amecheka sana, jibu alilonipa bado nimepigwa na mshangao, kama ilivyo kawaida yake, elimu yake ina mitazamo tofauti kabisa na majibu yake ni tofauti na matarajio yetu.
Simba.
 
nzaghamba naona na wewe umepigwa na mshangao.

Usishangae, Arsis ana kichwa kinafikiria tofauti na sisi. Hujaliona hilo katika kumsoma hapa?
Simba.
 
Hadithi za Biblia, Quran na Torah; ni myth and legends tu za Middle East.

Theory of ‘legend and myth’ (over time they evolve).

Kwenye evolution ya hizo stories zikaja variation luluki.

Kabla ya dini rasmi kwanza watu wakachagua mtindo wao wa kufanya ibada na version zao za story ambazo zi kubadilika over time (given the theory of undocumented stories).

Japo watu walikuwa na imani ya ‘monotheistic god’ lakini baada ya muda kukawa na mitindo kibao ya kufanya ibada given the version of story ilivyobadilishwa kwenye eneo.

Jews wakawa wa kwanza kurasimisha kitabu maandishi yepi (version ipi inakubalika) kikaundwa kitabu cha Torah.

Wapili nani jibu lake mtihani (but factually most likely were Muslims, given the logic). Kwanini kwasababu hizi dini mbili zinafanana sana taratibu zake na wahusika wengi walikuwa Middle East, hata forms of Christianity za maeneo hayo zinafanana na hizo dini mbili.

Tofauti ya Jews na Islam ni New Testament (kwenye biblia). Jews wanaishia kwenye Old Testament.

Tofauti Islam na Muslims na Christians (Japo wote wanatambua, Old Testament) Iła vitabu vyao vina nyongeza ya New Testament (sehemu ya hadithi zao zinapishana) na waislamu wana nyongeza ya Muhammad.

Kwanini Christianity aiwezi kuwa dini ya pili, promoter wake ni foreigner wa eneo wa msingi wa hizo ‘myth and legends’. Na historia inasema Constantine kabla ya kuamuru kuandika biblia alikuta wenyeji hawajielewi (isipokuwa Jews walikuwa tayari washachagua version ya kitabu) Ila mtindo wa kufanya ilikuwa bado.

Kwa hivyo ilikuwa bado vurugu machi kwenye kufanya ibada na kuchagua version sahihi. Constantine akaamuru mtindo wake wa kufanya ibada na kuchagua version yake ndio ikaundwa biblia na utaratibu rasmi wa kufanya ibada (sasa shughuli ya kulazimisha wengine wafuate huo utaratibu sikia tu).

Halikadhalika wenyeji nao wakaunda kitabu kingine chenye variation ya myth wanazotaka ndio Quran.

Ndio maana utaratibu wa Quran na Turah culturally unafanana sana, it resembles wenyeji, whereas Christianity ina tofauti kubwa sana nao culturally kwa sababu Constantine aliingiza mambo yao ya paganism ya masanamu. Na Ukristo uliokuwa unafanana na Jews na uislamu culturally cha moto walikiona wasiotaka kuelewa kitabu cha Constantine na masanamu yao.

Je hawa ndio sahihi kwenye dini kuliko Buddhist, Hindus na kadhalika (personally I don’t think so) to me those are myth just as Greek Gods, Norse Gods and those of other culture (shida ni kwamba hazikuwa monotheism).



Uhalisia ni kwamba sisi tunaishi kwenye hako kajiwe kadogo sana kwa picha iliyopigwa na rover from mars. Hako kajiwe chetu kina watu kila pembe (kila mtu ana mbingu yake tofauti) ukikakinganisha na Jupiter ni kubwa mara mia. Ukikafananisha na jua kadogo mara million moja. Yaani tunaishi kwenye kajiwe kadogo sana kwenye solar system. Achilia milkway gallaxy (yenye nyota kati billion 1 mpaka mbili na luluki zina solar systems na pengine life). Let alone the universe which is estimated to have trillion galaxies. We are so insignificant in this universe.

Kila mtu akiangalia alipo anaona nyota na galaxy. Hakuna mbingu labda tuamue kwa pamoja mbingu yetu ni jua lilipo.

Sasa aina maana hiki kijiwe chętu hakina maajabu ya kujiuliza binadamu tumetokea wapi. Personally I don’t buy the evolution theory na naamini kwenye spiritual world. Shida zaidi ni kusikiliza huu upuuzi wa dini na kulumbana based on ‘myth and legends’ za M.E now that’s just stupid us.

Dini ni hadithi tupu, aina maana hakuna spiritual world.
 
Hio hadithi unayosema "mtume amefasiri na kusema ndio binaadam wa mwanzo" iko wapi? hujatuonesha.

Hujioni hapo umejichanganya vibaya sana?
Simba.
 
Vionjo vya Arsis 5 - 1

nilivyokutanishwa na majini ya Kingazija (Comoros) na Kipemba Kojani.

Baada ya kurudi kisa cha Unguja mengi sna yaliendelea lakini kw aufupi nilirudi kwenye maisha yangu kawaida ya kwenda kutengeza magarei na kushughulika na kiduka changa kidogo, kwa siku hizo, cha spare za umeme wa magari.

Tulipoondoka unguja, yule binti na mamake walikuja Dar na mamangu, ilifanywa siri kubwa kuondoka kwao na wakaja kwa ndege ya kukodisha na ndugu wengine ili waweze kujifich kuondoka kwao, kuepusha kujulikana kwani Unguja minong'ono ya kisa ilikua mingi.

Kwa ufupi yule mama nilikuata nae Dar na binti yake lakini hawajakaa sana Dar wakaondoka nchi za nje, walikua hawana kabisa hamu na Tanzania, bara wa Unguja. Mambo yaliwakumba si madogo.

Katika kua nao Dar, yule mama akanihadithia kua mwanamke aliemstua, alikua ni mke wa yule DSheikh wa Unguja tulikua nae siku ya kikao na wahalifu. Akanambia yule Shehe ndio tuna w))wasiliana na kamuomba namba zangiu za simu, nikampa. Tukawa na mimi tuna mawasiliano ya hapa na pale na yule Sheikh.

Siku moja akanambia kwenye simu, Simba, nafahamu ulikua kimya sana kwenye kikao cha siku ile ya hukumu pale nyumbani lakini mimi naelewa wewe ndio ulikua kiongozi wa yote yale ingawa u kijana mdogo sana. Nafahamu kwa pete yako ulioivaa, hio pete sio ya kawaida kabisa na wenyewe waliokipa hio pete wana nguvu kubwa sana. Natamani niwaelewe. Nimeshindwa mbinu zangu zote kuwafahamu.


Mimi; Unafikiria tu hivyo.

Sheikh, mimi nafahamu babu yako na namfahamu yule Sheikh wa Tanga mlikja nae tulikutana nae kwa babu yako tanga miaka si mingi sana nyuma. babu yako ndio mwenye hio pete, naona kakuachia mikoba.
Mimi; hapana, ana yake.
Sheikh: mimi nimeongea na babu yako juzi, kuna tatizo jingine kabisa limetukabili, akanambia niongee na wewe. Toka siku zile mnaondoka mimi nawasiliana na babu yako. Nilifikiri kakujulisha kua tunafahamiana.
Mimi: Nafahamu mnafahamiana, toka nilipokua Unguja.

Sheikh; Sikiliza Simba, kuna dada mmoja niDaktari wa binadam, huyu dada ni mgazija, na yupo huko huko Dar. lakini ana matatizo makubwa sana ya mambo yao ya majini ya Kingazija sijui ya hapa Unguja, maana huyo ameshaolewa mara mbili, zote na madaktari hukohuko dar, lakini zote kaachika, mmoja kazaa nae, mmoja hajawahi kuzaa nae.

Wazee wake walinifata hapa Unguja, ni watu maarufu sana, wakamleta hapa Unguja, tukamshugulikia sna, lakini hayo majini yanatulia anafanya mambo yake vizuri sema ayataki kabisa awe na mahusina na mwnamme. Binti wa Kiislam ana kisomo chake cha juu, ana mtoto wa kike mmoja anakua tena, lakini kawa mlevi, hatoki ma-klabu ya starehe huko na hata akija hapa. Wazee na ndugu zake sio watu wa hivyo kabisa, anawaibisha sana. Simba tunamsaidia vipi huyu ndugu yetu?
Mimi; Kwa jinsi unavyonieleza, huyu mkamate koo babu. Mimi siyajui kabisa mambo haya jamani. Mimi ni kama bendera, nasukumwa na upepo tu, unakovuma ndio huko huko.

Sheikh: sasa huo upepo umevumia kwa huyo binti Daktari, wacha ukupeleke utakavyo. babu yako kasema tuongee na wewe, anakijua hiki kisa chote.

Mimi: Sheikh mimi nakushauri huyo mchukueni tu mumpeleke kwa babu, mkimfikisha pale babu hachomoi, itabidi amshughulikie tu. Lakini mimi binafsi siyajui yote hayo.

Sheikh; Nimekuelewa sana Simba, wacha tuone tunafanya nini maana huyo binti ukimuona wala huwezi kujua mambo yake, anaishi vizuri tu anapoata kazi nzuri nzauri tu, lakini atishi maisha ya kihuni mpaka lini? Aliekua mumewe ni Daktari mkubwa sana na mwenye heshima sana Tanzania. Yeye mwenyewe anafahamiu tatizo lakini anashindwa kujizuia hio hali. Anajishangaa.

Tutaongea tena Simba ikiwezekana, wacha niendelee kumrai na kumsihi babu yako atusaidie. Kumwendea ghafla itakua si vizuri, na hatujui hata kama huyo binti atakubali kwenda, babu yako kasema Dar hawezi kuja kwa sasa, tuongee na wewe.

Mimi; Ongeeni nae tu, babu mtaalamu, mimi sina nilijualo.

Tukaagana kwenye simu. Siku kama tatu kupita babu yangu akanipigia siimu. Tukasalimiana, kama kawaida yetu tukataniana kidogo, mtu na wajina wake. Akalianzisha...

Babu; Simba, vipi unakataa kusaidia watu?
Mimi; Vipi tena babu? (Ingawa nilijua anamaanisha nini).
Babu; Sheikh... wa Unguja kanipigia simu, kanambia aameongea na wewe, lakini anachokwambia unamsukumia kwangu, usifanye hivyo Simba, huyo binti yupo Dar, itakua wepesi sana wewe kumuona, tena Sheikh anasema kuna bwana mmoja wa Kipemba yupo hapo Buguruni si mbali na kwenu, anajaribu kumsaidia huyo binti kimatibabu, lakini Sheikh anasema, hata huyo binti atakata tamaa maana muda unazidi kwenda, haioni ile tija anaoitarajia.

Mimi; Buguruni ya wapi hio, babu usifikiri kila buguruni ni karibu na kwetu, buguruni kubwa.
Babu: Cha msingi sio hicho Simba, hata iwe mbali vipi, nyie mna magari huko, hamtembei kwa miguu, halafu buguruni si ndio njia ya kwenda na kurudi kazini kwako Tabata?
Mimi; Babu, ukitaka lako unajidai profesa. Niache nipambane na magari huku, wewe pambana na binadamu. Hizo kazi zako zinatisha, kasheshe la Unguja halikua dogo.

Babu; Simba, kwani wewe unafanya nini zaidi, wewe wawachie wenye kazi zao, mimi nataka wewe ujifunze ya dunia, ujionee mwenyewe ndio kuna siku utaona ni heri usaidie watu kuliko kusaidia magari.

Babu; Wewe arrange siku tu na huyo Sheikh wa Buguruni ukamjue, ni vizuri, utajionea wanavyofanya tiba zao, ni elimu hio. hakikisha tu siku unayokwenda na huyo Dada awepo anashughulikiwa, wewe uwepo kama mtazamaji tu, tuanzie hapo Simba.
Mimi; babu mbona unanipa kazi ngumu?
Babu: nenda, unaweza kukuta toto la Kingazija jisomi hilo, limenona, ukajipaytia mke wa Kunguja. Muhimu wewe nenda, yule Shjheikh hatojua umeenda kufanya nini, mimi nimemwabia huyu Sheikh wa Unguja rafiki yake, asimwambia kabisa unaenda kufanya nini, yeye amwambie, wewe unaenda kwa mabo yakohuyoi Sheikh, lakini yeye mwenyewe Sheikh atanuelea, hatomueleza chochote kuhusu kazi zetu, maana hawa waganga wengi waoo wachawi tu, hatopenda kuingiliwa himaya yake.
Mimi: babu mimi sitaki, kwanza umeshanitisha hapo, yamalizeni wenyewe.
Babu; Usiwe hivyo, usikatae mwito kataa uliloitiwa.
Mimi: Si nimeshajua ninaloitiwa babu?
Babu; Simba wacha niende, tutaongea kesho, naona leo hatuelewani lugha.

Nikacheka, babu na yeye akacheka, akanichomekea, huyo mtoto ukimuona na sifa zake nilizopewa natamani nije huko Dar, toto, toto kweli, si mchezo. Unamuogopa sana mkeo?
Mimi; Njoo wewe babu.
Babu; Natamani kuja, lakini umri ushakimbia tena.
Mimi: babu kawahi kusali, wacha na mimi nikawahi. Kwa heri

Tukaagana pale. Nikaendelea na mambo yangu.
Simba.

... 5.2
 
Nyingi hapo ni fikra zako au za kujikusanyia kwa wengine wasioamini Mungu.

Umeshaisoma Qur'an?
 
Hayo maneno.
 
Nyingi hapo ni fikra zako au za kujikusanyia kwa wengine wasioamini Mungu.

Umeshaisoma Qur'an?
Soma vizuri post yangu uone msingi wa Torah, Bible na Quran.

Ukipata msingi wa foundation zake ndio utaelewa source ya tofauti zake kutokana na watu walioamua ku-accumalate information wanazotaka.

Au wewe kweli unaamini Quran ilishushwa kutoka mbinguni kitabu kizima?
 
Simple question: Umeshaisoma Qur'an?
Before I answer that who wrote the Quran and its source.

Quran imeshuka kutoka mbinguni au ni maandishi yaliyokusanywa na watu.

Baada ya hapo ndio twende kwenye merit ikibidi nitakushushia ‘Al Baqarah’ yote ushangae, haya kwa haya.

Sampuli ya watu mnaoamini mtume Muhammad alikuwa akichezea mabaya ya malaika wakati anashushiwa Iqra akikosea kusoma.

Dini za Abraham ‘Jew, Islam na Christian’ ni full of tales. Zote zinakubali ‘Old Testament’ ambayo aina ushahidi,

Plato lived 428 B.C.E ushahidi upo, kwanini hakuna ushahidi wa historia ya ‘Old Testament’ kipindi hiko kama sio story ya kutunga tu.

Pythagoras 500 BCE, Tutankamahau sijui 1300 B.C.E bado wazazi wake, Haya ushahidi wa hadithi za hakina Moses/Musa mbona hakuna. Hadithi tu za waarabu on monotheism ambazo watu wamezitumia
Kututawala,
 
Sasa sikila jini hapo ulionalo safi
 
Mkuu anzia mwanzo 2:7
“Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.”

Ukija kwenye Mwanzo 1:27
Hapo tunaona mtu tayari alikuwa ameshaumbwa(mwanaume na mwanamke) inform of spirit ila hakuwa katika mwili wala nafsi.

Ndipo akafanyika katika mwili na kupuliziwa pumzi ya uhai.

Huyo mtu akaitwa Adam, sasa ukifuatilia asili ya neno Adam kwa umakini kabisa utaweza kutofautisha kati ya Mtu na binadamu. (Aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu ni mtu).

Hapo biblia imethibitisha mtu wa kwanza kuwepo duniani inform of spirit, soul, body ni Adam. Kama kulikuwa na mtu mwingine siwezi kupinga moja kwa moja lakini ni dhahiri hakuwa katika form ya mwili, nafsi na roho.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…