Koffi Annan
JF-Expert Member
- Dec 23, 2018
- 2,556
- 7,813
Mwezi uliopita tarehe 29 nilikuwa na safari ya kwenda Tanga, ukizingatia nilikua napasikia sijawahi kufika nikasema ngoja nikaone hizo raha za Tanga,
Safari yangu ilianzia stand ya Msamvu majira ya saa tisa alasiri, nikapanda costa ndogo kwa nauli ya 22k, ndani ya gari nilianza kusikia lafudhi za watu wa Tanga na watu walikua friendly sana kama wanafahamiana ila baadae nikaja kujua sio kwamba wanafahamiana ila ni uchangamfu wa kila aliyekuwa anapanda na kushuka kwenye ile gari ukizingatia ni gari ambazo zinasimama vituo vingi
Saa nne na robo usiku tayari nilishuka Tanga mjini, nikamvuta boda nikamwambia nipeleke sehemu ambayo inachangamka usiku kuliko sehemu zote, haikua mbali na niliposhuka tukaondoka akanishusha Tanga Pazuri, ndani kulikua na live band tamu sana nikaingia huku napishana na watu wanapata kilaji wengine misosi na warembo hapa na pale, nilinyoosha counter nikaagiza chupa yangu nikatulia nikisikiliza live band taratibu
Kwa muongozo wa Google maps nilichagua Lodge nzuri nikapiga simu wakasema room zipo nikamwambia boda anipeleke nikaweka mazaga kisha nikatoka kiaskari nikarudi eneo la tukio
Round hii sikuingia ndani maana lile eneo nje kuna movements nyingi na pub ndogondogo kadhaa, niliagiza msosi nikaenda nikatafuta kona moja ipo nyuma ya Tanga pazuri nikakaa, muda huo nilikua nimemwita kijana kwenye zile pub nikamuagiza cha Arusha hivyo tukawa tunakula na stori za hapa na pale na vinywaji tukaagiza palepale
Kupitia yule kijana niliweza kuielewa Tanga namna ilivyo kwani alinipa ramani ya Mkoa ulivyo na pia haikua ngumu kuelewa sababu maeneo mengi ya Tanga nayasikia kwa majina tokea nikiwa shule, nilipata picha ya muundo wa mji mpaka baharini namna fukwe na bandari zilivyo kwa ramani kuanzia mwanzo hadi mwisho bila kusahau boda za kuingia Kenya
Lakini pia yule kijana alinithibitishia mambo kadhaa ambayo nimekua nikisikia kutoka Tanga hasa tabia na ufundi wa mabinti bila kusahau mapishi na tuliachana muda wa saa tisa Alfajiri nikarudi kulala
Asubuhi saa moja niliamka, hali ya hewa ilikua ya joto kiasi, nikaenda baharini sehemu inaitwa Deep sea, niliona mikoko mingi sana na watoto wengi wa kaa wanatembea kwa makundi kama siafu na huyu star fish
Deep sea kuna soko la samaki na sehemu za mama ntilie wanapika, nilikunywa supu ya samaki na chapati tamu sana nikaondoka saa tatu nikarudi nilipofikia kujiandaa na kilichonipeleka Tanga.
Shuhuli iliyonipeleka ilinilazimu kutembea eneo la CBD hivo nilikatisha kwa Mkuu wa mkoa kuingia roundabout ya Pangani kisha nikaanza kuhesabu barabara za namba, nikaonana na wenyeji wangu mpaka saa saba na nusu mchana nilimaliza kilichonipeleka Tanga
Watu ambao nilibahatika kukutana nao kwenye harakati zangu walikua friendly sana, sikujihisi mgeni hata kidogo, lakini pia huu ndio mji pekee nimeona ngozi nyeupe na nyeusi wanashirikiana kuliko mikoa mingine ambayo kuna mchanganyiko wa race.
Nilirudi lodge nikaagiza msosi nikaletewa ndizi za nazi,mabinti wanajua kupika sio mchezo,
Japokua nilipanga baada ya kumaliza shughuli niondoke baada ya mazungumzo na yule kijana nikasema niongeze siku moja hivyo badala kuondoka alhamisi nikaondoka Ijumaa,
Ndio nilipoamini Tanga waja leo kuondoka majaliwa
Baada ya kumaliza kula nilienda kupumzika saa kumi niliamka kwa kuwa nilikua sijajiandaa kubaki sikua na nguo za kubadili, nilimcheki yule kijana akaja tukaenda soko la nguo lipo pale mjini nikanunua bukta ya mtumba kwa 5k na T Shirt ya spesho kwa 10k mtoko ukawa umekamilika na nikawa nimepata muda mzuri wa kutembea sokoni
Muda tuliorudi saa moja jioni ilikua tayari nkamuuliza mwenyeji ni sehemu ipi nzuri ya kula muda huu, tukatembea kutoka nilipokua mpaka forodhani, ilikua ni umbali wa 1.8km hivyo nilipata mda wa kuona mji wa Tanga unavyokua wakati wa usiku
Baada ya kufika forodhani kila nilichokua nagusa ladha yake sijaipata sehemu nyingine, nilijikuta nakula vitu vingi kuanzia chips, sea food, kuku na bites, kama unapenda kula ukifika Tanga nenda forodhani hutojutia bei zao ni za kitanzania
Tulitoka pale saa nne usiku mwenyeji wangu akarudi kwao nikarudi Lodge, pale Lodge kuna bar nilikuta jamaa wanaangalia masumbwi, hapa nilijua kwa nini Mwakinyo katokea Tanga, ushabiki wa Masumbwi ambao upo Tanga sijauona kwingine na hapo mjini Tanga kuna teams zina mabifu makali.
Asubuhi ya ijumaa niliamka nikafanya mambo yangu palepale lodge nikisindikizwa na hizi chapati hatari sana
Mchana nilitoka breki ya kwanza nikaenda Raskazone, nikatulia pale nikala upepo wa bahari, pale napo nilipata mwenyeji akanielekeza ramani ya bahari kwa uzuri zaidi ndipo nikagundua pia Tanga kuna jeshi la maji.
Nilikaa pale masaa mawili saa tisa nikatoka nikaenda beach inatofuata inaitwa Jet huku nilikuta wenyeji wanaogelea na couple zikiwa zimetulia, moja ya kilichonifurahisha beach na open space za Tanga kulikua na couple nyingi sana na sio vijana tu, hata wazee wapo beach na parks wanakula upepo taratibu iwe mchana iwe usiku.
Saa 11 jioni nilitoka Jet nikarudi forodhani kupata misosi adimu kisha nikatembea na njia ya deep sea nikiangalia bahari na sunset
Ticket nilikua nayo ya saa moja na nusu hivyo nikarudi kubeba virago vyangu niksenda ofisi za bus Mkwakwani tayari kurejea mkoa
Kichwani nikiwa na kumbukumbu nzuri za mazingira mazuri, vyakula vyenye ladha tamu na ukarimu wa wenyeji usiopimika kwenye mizani.
Nilibeba na hii bidhaa nzuri wiki imeisha ila yenyewe haitaki kuisha maana utamu wake lazima uchanganye na maji kisado