Niliyokutana nayo katika safari yangu ya jahazi kutoka Wete(Pemba) mpaka Tanga, vimbwanga vya mabaharia

BARDIZBAH

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
4,789
8,492
Habari waungwana?

Yah, juzi nikiwa natoka Pemba Kaskazini (Wete) nikielekea Tanga nilipanda jahazi kutokana na ufinyu wa usafiri wa meli za kutoka Pemba kuelekea bara, lakini pia si unajua bajeti maana uchumi mgumu bado sijatengamaa.

Basi bwana nikafika bandarini pale Wete asubuhi ya saa tatu hivi. Hali ya hewa haikuwa nzuri sana kulikuwa na mawingu mazito sana yakiashiria mvua itanyesha muda wowote.

Baada ya kukaa kidogo mvua ikanyesha kidogo kisha ikakatika. Muda huo mabaharia waliokuwa na vyombo(Majahazi) walikuwa wawili(2) na kila mmoja alikuwa anatafuta vichwa vya kuondoka navyo muda huo.Basi nikapanda Jahazi la kwanza kuondoka Kwa bei ya elfu 15 mpaka Tanga.

PICHA LINAANZA, Baharia walikuwa kama watatu na vijana wao wa kupakia mizigo na kufanya kazi za kupandisha shuka kama wa 5 hivi. Huyo baharia mkuu ni mzee mmoja hivi anaupara wake Anatukana kama vijana wa Arusha.

Tusi lao kubwa hao wapemba ni KHANITHI. CHOMBONI tulikuwa abiria wengine wengi na ile jinsia yetu Ke walikuwemo pia. BASI chombo iliondoka kwa speed nzuri mwanzo kila mtu akiwa katulia.

Tulipofika kwenye mkondo mkubwa wa maji Chombo ikazimwa Engine pazia likafunguliwa na hapa ndipo KILA MTU aliichukia safari (KASORO MABAHARIA WENYEWE). Tulifika mkondoni wimbi la bahari likawa limekolea, Bahari imechafuka kweli kweli, kuna muda Jahazi linapigwa wimbi mpaka maji yanaingia Chomboni tunaloana.

Ohoo punde si punde watu si tukaanza kutapika tu,, maajabu ni kwamba MABAHARIA wakiona mtu anatapika WANACHEKA sana ,, Na likipiga wimbi kubwa sana WANACHEKA na kusema HILO DOGO tunataka kubwa zaidi😂😂 Mtu unabaki kusema hawa mahabaria wapuuzi kweli.

Ile safari ilifikia kipindi najuta kwanini nimepanda hiki kichombo yaani nailaumu nafsi sana na niliiona ndefu sana. Tulitoka wete saa nne na nusu hivi asubuhi tulifika Tanga saa kumi na mbili jioni. Nilitapika mpaka nikakosa nguvu za kusimama.

Mbali na hayo mateso ngoja nikupe vimbwanga vya hii safari
  1. Ukiwa kwenye mashua huruhusiwi kuvaa viatu, nilikuwa nimekaa na viatu ila niliambiwa nivue viatu tena kwa sauti ya ukali. (Nilijaribu kuuliza hii imekaaje baadae nikaambiwa kuwa watu wanaswali ndani ya mashua so haipendezi kuchafua na viatu, pia niliambiwa kuwa unaweza kutereza ukiwa na viatu ukaumia au ukaangukia kwenye maji).

    Though kuna jamaa aliniambia ni sababu za kiroho na mambo ya kishirikina.

  2. Mabaharia wanastori za kutisha sana, kuna mmoja nilikaa nae akaniambia alishawahi kuzama na chombo aliogelea kwenye mkondo kwa siku mbili akaja akapata msaada siku ya pili.

  3. Kuna muda chombo kina weza kukutana na upepo mkubwa sana kisizame ila kikapelekwa mbali sana mnaweza jikuta hata Commoro.

  4. Mabaharia wamekariri location za bahari mpaka nikamuuliza mmoja hii imekaaje nikaambiwa wanaangalia Jua na kwa usiku wanaangalia Nyota na hawapotei.

HAKIKA ILIKUWA SAFARI KWELI NA NIMEJIFUNZA MENGI KWA WALE MABWANA MAJI.
 
Me nilifika mpaka bagamoyo bandarini ili nipande chombo kwenda Pangani na Tanga kama kuenjoy tu maji, ila roho ikagoma kabisa baada ya kuona yale majahazi, nilichofanya nikageuka nikarudi stendi nikapanda gari za kwenda Tanga so nikatumia njia ya barabara.

Maji yanatisha sana.
 
Ungejaribu moto mkuu kwa kuushika.
 
Duh! Pole sana nikiwaza wale mabiliionea walioenda chini ya bahari Kwa mita elfu nne 4000m naona uchawi upo
 
Wale jamaa ukiwakuta wana furaha sana. Ila yale madude kuyapanda mi sidhani labda niwe nina msala mkubwa sana na napaswa toroka ndiyo nitatumia yale madude
 
Habari waungwana?

Yah, juzi nikiwa natoka Pemba Kaskazini (Wete) nikielekea Tanga nilipanda jahazi kutokana na ufinyu wa usafiri wa meli za kutoka Pemba kuelekea bara, lakini pia si unajua bajeti maana uchumi mgumu bado sijatengamaa.

Basi bwana nikafika bandarini pale Wete asubuhi ya saa tatu hivi. Hali ya hewa haikuwa nzuri sana kulikuwa na mawingu mazito sana yakiashiria mvua itanyesha muda wowote.

Baada ya kukaa kidogo mvua ikanyesha kidogo kisha ikakatika. Muda huo mabaharia waliokuwa na vyombo(Majahazi) walikuwa wawili(2) na kila mmoja alikuwa anatafuta vichwa vya kuondoka navyo muda huo.Basi nikapanda Jahazi la kwanza kuondoka Kwa bei ya elfu 15 mpaka Tanga.

PICHA LINAANZA, Baharia walikuwa kama watatu na vijana wao wa kupakia mizigo na kufanya kazi za kupandisha shuka kama wa 5 hivi. Huyo baharia mkuu ni mzee mmoja hivi anaupara wake Anatukana kama vijana wa Arusha.

Tusi lao kubwa hao wapemba ni KHANITHI. CHOMBONI tulikuwa abiria wengine wengi na ile jinsia yetu Ke walikuwemo pia. BASI chombo iliondoka kwa speed nzuri mwanzo kila mtu akiwa katulia.

Tulipofika kwenye mkondo mkubwa wa maji Chombo ikazimwa Engine pazia likafunguliwa na hapa ndipo KILA MTU aliichukia safari (KASORO MABAHARIA WENYEWE). Tulifika mkondoni wimbi la bahari likawa limekolea, Bahari imechafuka kweli kweli, kuna muda Jahazi linapigwa wimbi mpaka maji yanaingia Chomboni tunaloana.

Ohoo punde si punde watu si tukaanza kutapika tu,, maajabu ni kwamba MABAHARIA wakiona mtu anatapika WANACHEKA sana ,, Na likipiga wimbi kubwa sana WANACHEKA na kusema HILO DOGO tunataka kubwa zaidi😂😂 Mtu unabaki kusema hawa mahabaria wapuuzi kweli.

Ile safari ilifikia kipindi najuta kwanini nimepanda hiki kichombo yaani nailaumu nafsi sana na niliiona ndefu sana. Tulitoka wete saa nne na nusu hivi asubuhi tulifika Tanga saa kumi na mbili jioni. Nilitapika mpaka nikakosa nguvu za kusimama.

Mbali na hayo mateso ngoja nikupe vimbwanga vya hii safari
  1. Ukiwa kwenye mashua huruhusiwi kuvaa viatu, nilikuwa nimekaa na viatu ila niliambiwa nivue viatu tena kwa sauti ya ukali. (Nilijaribu kuuliza hii imekaaje baadae nikaambiwa kuwa watu wanaswali ndani ya mashua so haipendezi kuchafua na viatu, pia niliambiwa kuwa unaweza kutereza ukiwa na viatu ukaumia au ukaangukia kwenye maji).

    Though kuna jamaa aliniambia ni sababu za kiroho na mambo ya kishirikina.

  2. Mabaharia wanastori za kutisha sana, kuna mmoja nilikaa nae akaniambia alishawahi kuzama na chombo aliogelea kwenye mkondo kwa siku mbili akaja akapata msaada siku ya pili.

  3. Kuna muda chombo kina weza kukutana na upepo mkubwa sana kisizame ila kikapelekwa mbali sana mnaweza jikuta hata Commoro.

  4. Mabaharia wamekariri location za bahari mpaka nikamuuliza mmoja hii imekaaje nikaambiwa wanaangalia Jua na kwa usiku wanaangalia Nyota na hawapotei.

HAKIKA ILIKUWA SAFARI KWELI NA NIMEJIFUNZA MENGI KWA WALE MABWANA MAJI.
Duh
 
Chai
 
Akili yako mbovu
20230624_123545.jpg
 
Wale jamaa ukiwakuta wana furaha sana. Ila yale madude kuyapanda mi sidhani labda niwe nina msala mkubwa sana na napaswa toroka ndiyo nitatumia yale madude
Yaan hawanaga wasiwasi kabisa
 
Back
Top Bottom