Safari yangu ya Botswana na Niliyoyaona huko

Keagan Paul

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
500
3,058
Tukiachana na ule uzi wangu wa “Nilivyokwenda South Africa bila kuwa na ndugu wala rafiki” Leo nitawaelezea safari yangu ya kwanza nchini Botswana na nilioyaona na kujifunza huko.

Kwa mara ya kwanza niliingia Botswana kupitia Boda yake na South Africa, kupitia mji mdogo wa Zeerust.

Nakumbuka tulitoka majira ya saa Sita mchana kwa Bus kutoka Park Station: Johannesburg kulipitia Pretoria hadi saa mbili usiku ndipo tulifika Mji Mkuu wao wa Gaborone, Botswana. Kama kawaida barabara zao ni nzuri na za kuvutia.

Tofauti na nilivyodhani yani Kutoka boda hadi Mji Mkuu wa Gaborone haikuwa mbali sana. Ni mwendo kama wa saa moja au usizidi.

Tofauti na picha niliyokuwa nayo kichwani mwangu, nilidhani Gaborone itakuwa Mji mkubwa sana, wenye magorofa makubwa na mataa mengi, barabara za juu na chini kama ulivyo mji wa Johanesburg, Pretoria au Capetown. Niliona Mji wao ni mdogo sana na usio na mbwembwe zozote zile. Magorofa sio mengi, Barabara zao hazina mambo mengi, hakuna mambo ya mafly over.

Hata mtu aliyejifunza kuendesha gari leo anaweza kwenda nalo hadi Mjini.

Tulishuka kwenye Bus sehemu moja inaitwa Main Mall. Nikatafuta Hotel ya karibu nikafikia hapo, nililipa kwa pesa yao inaitwa Pula. Asubuhi nilikuwa natoka nakwenda zangu kutembea, kutafuta marafiki wapya na kuona mandhari ya mji wao. Mimi napenda sana kuwa na Marafiki wengi nje ya nchi, nikirudi tena ile sehemu nakuwa sio mgeni tena.

Mambo niliojifunza pale kwa muda wa Wiki mbili nilizokaa pale.

1. Gaborone ni mji tulivu sana, watu wake ni watulivu sana. Ni mji umepoa. Mji wao ni mdogo sana. Hiyo Gaborone unaweza kuizunguka kwa masaa machache na ukaimaliza. Huwezi kuufananisha na mji kama Dar. Kwa watu wanaopenda kuishi miji isiyo na mavurugu sana, ujanja ujanja basi naweza kuwashauri kufikiria Gaborone kama Mji mzuri kwao.
2. Watu wake wengi wanaendesha Magari ya thamani sana. Niliambiwa wengi wananunua magari yao kwa kuchukua Mikopo Mikubwa Bank.
3. Pesa yao ina nguvu sana kulinganisha na ya kwetu. Kwa mfano, Elfu 10 yao, kwetu ni wastani wa Milion 1 na Laki 8. Unaweza kuona utofauti mkubwa uliopo.
4. Kwa utafiti mdogo wa siku chache, wengi walisema Botswana haina nafasi nyingi za Kazi, huwezi kufananisha na South Africa. Michongo sio mingi. Harakati sio nyingi, ni kama kila kitu kimenyooka.
5. Mji ni mdogo kiasi kwamba hakuna hata stand kubwa ya Mabus kama ilivyo stand yetu ya Magufuli. Stand yao kubwa haina tofauti sana na ile Stand ya Kibaha. Stand yao haina Mabus mengi kabisa.
6. Kwa upande wa Malls, Wana Malls kubwa kutuzidi, wanazo nyingi, huduma nyingi zinapatikana huko.

Baada ya kumaliza wiki nilitaka kuchukua Bus niende zangu Namibia, Nilikosa Bus za moja kwa moja. Kwa kifupi ukiwa Gaborone hakuna Bus ya kueleweka ya kutoka nje ya nchi yao. Ruti yao kubwa ya kutoka nje ya nchi yao ni kwenda South Africa, Zipo za kwenda Bulawayo Zimbabwe lakini pia ni chache sana. Hivyo lengo langu la kupitia njia ya Gaborone hadi Namibia lilishindikana.

Kama ningetaka kulazimisha ingenibidi nichukue Bus kutoka Gaborone hadi boda yao na Namibia, nishuke hapo, nivuke kisha upande wa pili ndiyo nichukue tena Bus kwenda Mji mkuu wa Namibia. Nikasita nikaachana na hilo wazo.

Nikasema hapa naenda Zambia. Njia ya kwenda Zambia nikakuta napo hakuna Bus, pale Stand waliambia kama unataka kwenda Zambia itakubidi uchukue Bus unapita francis Town mpaka Boda ya Kazungula bus zinaishia hapo.

Halafu pale Boda uchukue gari ndogo kama Noah, mnapanda wengi hadi upande wa pili wa Zambia.

Hapo utachukua Bus kupitia Mji wa Livingstone, Mazabuka hadi Lusaka.Nilitumia njia hii kufika Lusaka Zambia.

Ni njia ndefu sana, Kwa mfano, tulitoka Gaborone saa mbili usiku na kufika Boda ya Kazungula saa kumi na mbili Asubuhi. Hapo tukavuka, saa mbili asubuhi tukachukua Bus hadi Lusaka, tulifika saa moja jioni. Ni safari ndefu na ya kuchosha sana.

Ushauri wangu kwa mtu anayetaka kufanya safari kutoka hapa kwetu kwenda South Afrika, mpaka sasa njia nzuri na uhakika ni kutumia njia ya Zambia hadi Harare Zimbabwe ndo uingie South Africa kupitia Beit Bridge. Hizi njia nyengine hazina usafiri wa kueleweka sana. Mambo yanakuwa mengi njiani.

Imeisha
 
Welldone mkuu ILA ukweli utamalaki kwenye mada kama hizi, JF ina members hadi Bogota, Alaska, Accra,GABBS etc etc, kutoka Gabbs kuna bus hadi LSK (Zambia),wafanya biashara wengi kutoka Lusaka wanatumia hizi bus (wengi wanaagiza TVs,na wengi wananunulia Francis Town au GABBS),facts kuna mabus kati ya Gaborone na Lusaka ,na elewa kutoka kazungula border hadi Lusaka ni 550km,na barabara ni top class except kipande cha Monze hadi Mazabuka (40km),mabus mengi yanatumia less than 7hrs to cover that distance, kutoka 8am na uingie Lusaka 1900 mmmmm unless ulipata breakdown ya bus, Nami nafuatilia hili ila facts zibaki hivyo mkuu
 
Hapo kwenye pesa yao inaitwa pula na pula 10k ukiichange kwenda tsh ni karbu milioni na ushee ......hiyo kwenye ualimu tunaishia kuifundisha kwenye somo la Basic Mathematics Topic ya rate and variation ya kidato cha tatu kila mwaka hahahaha.

Basi inabidi uwachekeshe watoto kwa kuwambia kule kwetu Denmark pesa yetu inaitwa kronor na tukifunga likizo nitarudi ila nitapitia kwanza germany kwa mjomba ambayo pesa yap inaitwa euro basi watoto wataguna(wanakataa kamba) na kucheka life linasonga.
 
WIVU DETECTED.
 
Tukiachana na ule uzi wangu wa “Nilivyokwenda South Africa bila kuwa na ndugu wala rafiki” Leo nitawaelezea safari yangu ya kwanza nchini Botswana na nilioyaona na kujifunza huko.

Kwa mara ya kwanza niliingia Botswana kupitia Boda yake na South Africa, kupitia mji mdogo wa Zeerust.

Nakumbuka tulitoka majira ya saa Sita mchana kwa Bus kutoka Park Station: Johannesburg kulipitia Pretoria hadi saa mbili usiku ndipo tulifika Mji Mkuu wao wa Gaborone, Botswana. Kama kawaida barabara zao ni nzuri na za kuvutia.

Tofauti na nilivyodhani yani Kutoka boda hadi Mji Mkuu wa Gaborone haikuwa mbali sana. Ni mwendo kama wa saa moja au usizidi.

Tofauti na picha niliyokuwa nayo kichwani mwangu, nilidhani Gaborone itakuwa Mji mkubwa sana, wenye magorofa makubwa na mataa mengi, barabara za juu na chini kama ulivyo mji wa Johanesburg, Pretoria au Capetown. Niliona Mji wao ni mdogo sana na usio na mbwembwe zozote zile. Magorofa sio mengi, Barabara zao hazina mambo mengi, hakuna mambo ya mafly over.

Hata mtu aliyejifunza kuendesha gari leo anaweza kwenda nalo hadi Mjini.

Tulishuka kwenye Bus sehemu moja inaitwa Main Mall. Nikatafuta Hotel ya karibu nikafikia hapo, nililipa kwa pesa yao inaitwa Pula. Asubuhi nilikuwa natoka nakwenda zangu kutembea, kutafuta marafiki wapya na kuona mandhari ya mji wao. Mimi napenda sana kuwa na Marafiki wengi nje ya nchi, nikirudi tena ile sehemu nakuwa sio mgeni tena.

Mambo niliojifunza pale kwa muda wa Wiki mbili nilizokaa pale.

1. Gaborone ni mji tulivu sana, watu wake ni watulivu sana. Ni mji umepoa. Mji wao ni mdogo sana. Hiyo Gaborone unaweza kuizunguka kwa masaa machache na ukaimaliza. Huwezi kuufananisha na mji kama Dar. Kwa watu wanaopenda kuishi miji isiyo na mavurugu sana, ujanja ujanja basi naweza kuwashauri kufikiria Gaborone kama Mji mzuri kwao.
2. Watu wake wengi wanaendesha Magari ya thamani sana. Niliambiwa wengi wananunua magari yao kwa kuchukua Mikopo Mikubwa Bank.
3. Pesa yao ina nguvu sana kulinganisha na ya kwetu. Kwa mfano, Elfu 10 yao, kwetu ni wastani wa Milion 1 na Laki 8. Unaweza kuona utofauti mkubwa uliopo.
4. Kwa utafiti mdogo wa siku chache, wengi walisema Botswana haina nafasi nyingi za Kazi, huwezi kufananisha na South Africa. Michongo sio mingi. Harakati sio nyingi, ni kama kila kitu kimenyooka.
5. Mji ni mdogo kiasi kwamba hakuna hata stand kubwa ya Mabus kama ilivyo stand yetu ya Magufuli. Stand yao kubwa haina tofauti sana na ile Stand ya Kibaha. Stand yao haina Mabus mengi kabisa.
6. Kwa upande wa Malls, Wana Malls kubwa kutuzidi, wanazo nyingi, huduma nyingi zinapatikana huko.

Baada ya kumaliza wiki nilitaka kuchukua Bus niende zangu Namibia, Nilikosa Bus za moja kwa moja. Kwa kifupi ukiwa Gaborone hakuna Bus ya kueleweka ya kutoka nje ya nchi yao. Ruti yao kubwa ya kutoka nje ya nchi yao ni kwenda South Africa, Zipo za kwenda Bulawayo Zimbabwe lakini pia ni chache sana. Hivyo lengo langu la kupitia njia ya Gaborone hadi Namibia lilishindikana.

Kama ningetaka kulazimisha ingenibidi nichukue Bus kutoka Gaborone hadi boda yao na Namibia, nishuke hapo, nivuke kisha upande wa pili ndiyo nichukue tena Bus kwenda Mji mkuu wa Namibia. Nikasita nikaachana na hilo wazo.

Nikasema hapa naenda Zambia. Njia ya kwenda Zambia nikakuta napo hakuna Bus, pale Stand waliambia kama unataka kwenda Zambia itakubidi uchukue Bus unapita francis Town mpaka Boda ya Kazungula bus zinaishia hapo.

Halafu pale Boda uchukue gari ndogo kama Noah, mnapanda wengi hadi upande wa pili wa Zambia.

Hapo utachukua Bus kupitia Mji wa Livingstone, Mazabuka hadi Lusaka.Nilitumia njia hii kufika Lusaka Zambia.

Ni njia ndefu sana, Kwa mfano, tulitoka Gaborone saa mbili usiku na kufika Boda ya Kazungula saa kumi na mbili Asubuhi. Hapo tukavuka, saa mbili asubuhi tukachukua Bus hadi Lusaka, tulifika saa moja jioni. Ni safari ndefu na ya kuchosha sana.

Ushauri wangu kwa mtu anayetaka kufanya safari kutoka hapa kwetu kwenda South Afrika, mpaka sasa njia nzuri na uhakika ni kutumia njia ya Zambia hadi Harare Zimbabwe ndo uingie South Africa kupitia Beit Bridge. Hizi njia nyengine hazina usafiri wa kueleweka sana. Mambo yanakuwa mengi njiani.

Imeisha
Nenda Namibia hasa Windhoek ni mji mzuri sana na pia safi magaribi hasa mji wa Swakopmund utapenda mji huo wa kishua sana kwenye fukwe wa Atlantic Ocean. Namibia wanafanana mengi sana na Botswana.
 
kwahiyo ni bidhaa gani naweza kutoa huko kuleta bongo nikapata hela?
 
Back
Top Bottom