kambale mnene
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 271
- 197
CcmKuna masikini wa akili ambao ni viongozi wetu, hawa wamesoma lakini hawana maarifa ya kutuongoza, na masikini wa kipato ambao wengi ni wananchi.
CcmKuna masikini wa akili ambao ni viongozi wetu, hawa wamesoma lakini hawana maarifa ya kutuongoza, na masikini wa kipato ambao wengi ni wananchi.
We mbulula kweli!Serikali imepunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kufidia tozo tuache kulalamika tozo zimesaidia kuimarisha sekta muhimu ya afya na elimu
Baada ya watu kupiga kelele,wasingepiga kelele angeondoa??Anapenda haki ndio maana amepunguza amepunguza na kuondoa tozo
Huo ufukara wa waTz uliouzungumza wameuprogram wao na wataendelea kuuprogram ili kuendelea kutawala. Wanatumia kanuni hii "Ukitaka kumtawala mtu utakavyo mnyime elimu bora ili awe mjinga pia muue kiuchumi". Usitarajie huruma hapo ndugu.Habari Watanzania wenzangu,
Kuna jambo ambalo naamini viongozi wetu huwa wanalipuuza wakifika kwenye viti hivyo.
Japo Tanzania ina utajiri mwingi sana, lakini Watanzania asilimia kubwa ni fukara sana.
Hii ni kuanzia kwa Mawaziri, Makatibu wakuu, viongozi wa Taasisi mbalimbali, Majaji, Bunge na Wabunge, Wawakilishi, Waziri Mkuu, Makamu na Rais; wote hawahisi kabisa magumu wanayopitia wananchi wengi waliopo ktk umaskini wa kutupwa.
Ukitaka kuthibitisha hili, angalia sera mbalimbali zinazotungwa na serikali. Haziakisi kabisa hali ya maisha ya Watanzania wengi!
SWALI: Shida ni nini?
Tuna sera za kijinga sana, tuna maamuzi mengi ya kipumbavu kweli kweli. Nchi imejaa mikorogano tu.
Ukiulizwa hii sera alitungiwa Mtanzania, hadi unahisi uchungu hadi moyo unataka kuchomoka.
Hawa akina Mwigulu, na Rais wetu Mh. Samia wana shida gani hasa?! Au shida ni vile ving'ora, au saluti wanazopigiwa, au misafara mikubwa mikubwa ile, Mbona hawaelewi kabisa uhalisia wa maisha ya WaTz wengi!
Niliwahi kusafiri hadi Bukombe, Geita huko. Nilimkuta Mwananchi mmoja, ameugua kweli, lakini kwa sababu alikuwa na Sh. 2000 tu. Hiyo hiyo anaitegemea kula, kuhudumia watoto, na kila kitu. Yule ndugu alichukua uamuzi wa kwenda kununua paracetamol (dawa za maumivu) za sh. 400/- ili ameze japo atulize maumivu ya mwili.
Watanzania wa aina hii wapo chungu mzima nchi hii. Mtu anaumwa, hana hela ya kumuona daktari, hana fedha ya vipimo, na wala uwezo wa kununua dawa. Anaamua kununua tu dawa za maumivu.
Si kwamba hapendi kutibiwa, la hasha, kipato kinakataa.
Nikuulize Mh. Rais Samia, huyu Mtanzania akitumiwa na ndugu yake sh 25,000/- aende hospital, mtumaji anakatwa tozo, na yeye akienda kutoa ana tozo. Rais wangu na wewe Dr. Mwigulu mnatengeneza Uchumi wa watu gani? Huu sio wa WaTz, labda mna watu wenu wengine mnaowawaza na kuwahudumia.
Ni wakati sasa Mh. Rais Samia ukate matumizi yote yasiyo ya lazima ndani ya serikali yako.
Haiwezekani Waziri, Naibu Waziri, Katibu mkuu, Wakuu wa Taasisi, Mamlaka mbalimbali, mkuu wa mkoa, n.k, atembelee gari ya thamani ya Tsh. 400 million, huku kuna Kijiji kizima hakina Zahanati, Kuna shule haina choo, kuna shule hawana madawati. Halafu unaweka Tozo kwenye sh. Elfu 10, unajiita Mzalendo, na tai ya rangi ya Tanzania unavaa. UNAFIKI!
KATA MATUMIZI YOTE YASIYO YA LAZIMA, KABLA HATUJAKWAMA KAMA TAIFA.
Watanzania ni fukara sana. Isipokuingia akilini hii, 2025 watakulazimisha upishe mwingine.
Ati "issue sio tozo" na "tusaidie kufanikisha mapinduzi ya kilimo"! Eti unampongeza Rais...nk. Naona ungejisemea tunajipongeza ss viongozi kama ulivotuomba "tuwasaidie" kufanikisha.Umezungumza kwa hisia. Kuhusu hoja ya umasikini vijijini; tunakubaliana kimsingi ni tatizo kubwa. Rural poverty ni tatizo kubwa si tu Tanzania bali ktk devoloping countries, hasa za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Chanzo kikubwa; ni kutokufanya mapinduzi ya kilimo. Kwa sababu rural economy ktk hizo nchi inategemea kilimo, lakini poor teknoloji, black market na ukosefu wa mitaji na utaalamu umefanya kilimo cha kujikimu, hivyo mnyororo wa umasikini tena wa kurithi (generational poverty) kuzidi kukua. Umasikini wa kurithi yaani masikini anazaa masikini hadi vijukuu. Kwa msingi huo, issue siyo tozo bali kufanya mapinduzi makubwa ya kilimo. NDICHO ANACHOKIFANYA MHE. RAIS SAMIA. Nampongeza sana Mhe. Rais.
Rais anafanya mapinduzi ya kilimo. Tusaidie mawazo kufanikisha mapinduzi ya kilimo maana ni mfumo endelevu wa uchumi na wa kukata mnyororo wa umasikini vijijini, kuhakikisha food security, kujenga taifa la watoto wenye lishe bora hivyo kuondoa udumavu wa akili na mwili. Tumsaidie Mhe. Rais SSH.🙏🙏🙏
Hii kauli huwa inaniboa kinoma yaani imekaa kubembelezana sana, yeye kama mkuu wa nchi lazima atambue mamlaka aliyonayo na atoe maelekezo/amri ya nn kifanyike na kwa muda gani. Siyo kutoa kauli zenye loopholes au general general kama hiyoMh. Samia apaswa kujua eti, mwanangu na hilo nendeni mkalitizame, sio kauli ya kiuongozi.
vyoteHivi ni kweli kina Mwigulu hawana akili au hawajui waongoze vipi? Kweli?
Utakuwa unakalia kichwa sio makalio. Huwezi kuandika upuuzi huu hapa au na wee ni mlaji.Serikali imepunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kufidia tozo tuache kulalamika tozo zimesaidia kuimarisha sekta muhimu ya afya na elimu
Nashaka na elimu yako. Alafu FAKIRI utamuita nani. Kama masikini ni mlemavu basi wee ni wakwanza coz una ulemavu wa akili, maana hujui kutofautisha kati ya FUKARA NA MASIKINIMasikini ni mtu mlemavu asiye jiweza kwa lolote.
Usitutie umasikini wako mkuu maana sisi tunajielewa na tunajiondoa katika hali hiyo kifikra na kimatendo.
Wewe ni masikini tu. au Ka bima kana kuwambia we umepata maisha.Masikini peke yako.
Mimi nimeshatoka huko shimoni uliko, tena kwa nguvu zangu alizonijaalia Mola.
Usifikiri tuko sawa.
Kabla ya Tozo mambo yalikuwaje?Serikali imepunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kufidia tozo tuache kulalamika tozo zimesaidia kuimarisha sekta muhimu ya afya na elimu
Una matatizo kichwaniMasikini ni mtu mlemavu asiye jiweza kwa lolote.
Usitutie umasikini wako mkuu maana sisi tunajielewa na tunajiondoa katika hali hiyo kifikra na kimatendo.
Na bado wanasema ttcl imepata hasara.. aseeeeKuna kiongozi mmoja alipiga picha na bibi mmoja ameweka umeme wa Tanesco kwenye nyumba ya udongo. Hawa viongozi hawana muda wa kumkwamua mtu wa chini ili awe na maish mazuri bali kumdidimiza ili awe masikini. Kuna Clip mmoja ya yule mzungu. Nilimuelewa sana. Yule bibi kazi aliyobakiza sasa hivi ni kusafiri tu mara yupo Kenya, yupo Uingereza kwa kodi na tozo za watanzania.
Sasa hivi bei ya bidhaa na huduma zipo bei juu mara 2 ya zamani. Ukitaka kuona hii serikali ya kinyonyaji kaangalie vifurushi vya TTCL halafu wanajiita wazalendo. Leo matumizi ya internet yapo juu kwa hela gani walizonazo watanzania?
Wewe ndio una matatizo makubwa zaidi.Una matatizo kichwani
Ikiwa masikini ni mlemavu!
Unapoiita nchi yetu kuwa ni masikini, huwa mnamaanisha nchi yetu ni lemavu?
Pumbavu kabisa!
Ukisha ukubali uamsikini katika maisha yako, hutoboi katika lolote.Wewe ni masikini tu. au Ka bima kana kuwambia we umepata maisha.
Semantics hazikusaidi kma bado wewe ni masikini.Nashaka na elimu yako. Alafu FAKIRI utamuita nani. Kama masikini ni mlemavu basi wee ni wakwanza coz una ulemavu wa akili, maana hujui kutofautisha kati ya FUKARA NA MASIKINI
Hahaha, nafikiri wanatekeleza matakwa yao na rafiki zao tu, kuliko ya Umma.vyote
Napata wasiwasi kwamba si yeye anayeongoza!Hii kauli huwa inaniboa kinoma yaani imekaa kubembelezana sana, yeye kama mkuu wa nchi lazima atambue mamlaka aliyonayo na atoe maelekezo/amri ya nn kifanyike na kwa muda gani. Siyo kutoa kauli zenye loopholes au general general kama hiyo