TRUST NO ONE...
Hii ni formula unayotakiwa kuitumia popote pale si online au katika maisha halisi
Hasa unapokua na shida,tembea kwa machale na umakini uongezeke hasa unapo
hitajiwa kutoa pesa ili tatizo lako litatulike,sijawahi ona mtu anaesaidia mtu mwingine
mwenye shida akimuhitaji atoe pesa,sijawahi shuhudia msaada wenye Gharama,nadhani
maana halisi ya neno Msaada ni BURE,ndio maana ikaitwa MSAADA.. Anaetaka kukusaidia
hakuombi chochote,hatohitaji chochote toka kwako na ukiona yanatokea hayo yakuombwa
chochote kitu basi ni haki yako kutumia Akili iliyo ndani ya UBONGO wako kuamua jambo sahihi.
Pole Mkuu,siku nyingine Usiongozwe na shida na taabu zako,Hakunaga mwanadamu aliyeumbiwa
Mateso milele,Usikubali kuendelea kutumika kama daraja la mtaji kwa hao wasio na huruma na wenye matatizo.