Nilimuheshimu sana kama kaka, leo hii ananitaka

Nilimuheshimu sana kama kaka, leo hii ananitaka

Kwahiyo hili nalo la kuleta jf?? Au yuko humu unataka asome? Hebu copy hii umtumie huko, usituchoshe sie, kwani huyo ndio wa kwanza kukutongoza?? Kaka yako mmezaliwa tumbo moja huyo?? Mxiiiiuuuuuuu!! Sasa tukianza kuleta ya kila anayetutongoza humu kweli patatosha humu??
Msipotongozwa mnamlilia Mungu, mkitongozwa mnalalamika, sasa what do you want??

haka kanaonesha ni katoto kabisaa, haiwezekan et namuheshimu so sitegemei anitokeee....ssa anataka atokewe na kka jambaz au??? aache ujima na kuanzisha nyuzi za kitoto...

<umeeleweka mama>
 
Mimi nakushukuru kwa kumtega kaka wa watu sasa anapo kwambia umtegue ndo unaanza vitendawili.... Wanawake jamaaaaaaani.
Sijawahi kumtega hata sikumoja yaani
 
Kwa jinsi unavyo elezea inaonekana hyo Kaka anakomalia co umkubali ila usex nae ndo maana unayemheshim kama Kaka mara anabadilika unamuona kama baba!.. Sa cjui kama ni hilo kwann unaogopa kulisema direct?
 
Sijawahi kumtega hata sikumoja yaani

Mimi kwa upeo wangu najua kama umekuwa nae karibu hata kwa wiki moja basi kuna pahala uliteleza na ikawa sababu ya kumshawishi kaka wa watu haya unayo yafanya kwa sasa ni mateso kwake. wewe mchepukie tu.!!!!!!!!!
 
Umri wako bado mdogo na hujaanza kujitambua!

Mwanamke ukishakuwa karibu na mwanaume asie ndg yako tegemea kutongizwa 90%...and if the guys is serious and strictly halafu yupo mbioni ku-divorce, that's your golden chance!

Leo unalalamika kutongozwa, subiri miaka michache uanze safari nyingi za Bagamoyo kwa 'babu' utakakokuwa unakesha kutafuta mtu wa kukutongoza???

tungekuwa mahali ningelipia meza yako...huyu dogoa anachezea nafas nyeti mno yaan daaah....angekuwa mdogo wangu nambamiza mabanzi tu.
 
Nimegundua wengi wanaojibu ni wanaume na ndio zao loly kama unasubiri majibu ya faraja hapa hupati wao wanaona nikawaida mwanaume mwenzao alivyofanya
 
Nimegundua wengi wanaojibu ni wanaume na ndio zao loly kama unasubiri majibu ya faraja hapa hupati wao wanaona nikawaida mwanaume mwenzao alivyofanya

Hiyo ni zaidi ya kawaida dada yangu Chokochoko, kutongozwa wanawake mmeumbiwa, ni.Mwanamke mpuuzi ndo anaweza kulalamika kutongozwa....tena jamaa yupo single, hata huyo rafiki yake atakuwa anamshangaa sana kukataa uwifi!
 
Last edited by a moderator:
sio wote wanaume wenye tabia hizo za ajabu😡 mind your language....
 
Nashindwa kuelewa umri wako! We una miaka mingapi. Kutongozwa jambo la kawaida kwa mwanamke. Na siku zote siyo lazima atakayekutongoza ndo huyo unataka afanye hivo. Kuna siku unayemtaka utataka akutongoze kama anavyofanya huyu jamaa lakini itakuwa ngumu. Hapo utamkumbuka huyu anayekutongoza kwa sasa.

Heshima gani unayoisema kwa huyu mwanaume? Ni kaka yako huyo? Jipime uchukue hatua. Kama humpendi acha kupokea hata misaada yake.

Mkuu umeongea yote...humtaki pia misaada yake achana nayo. Hutamwona tena akikutongoza.
 
Kila mkasa unaotokea unakufanya uonekane katika picha halisi ya namna ulivyo bt ni kawaida mambo kama hayo kutokea kwa mwanamke,sasa kazi kwako kuuza utu au kumkubalia
 
natamani kufanya hivyo ila hachelewi kukanusha nakusema nimemsingizia maana hakuna anaeona wakati akianza kusema hayo mambo yake nikiwa Mimi na yeye tuu ndio anasema naakitokea MTU ghafla anabadilisha mada, nilishamwambia haitawezekana anasema nilazima iwezekane hata gharama yaani sasahivi hata ishu alikua akinisaidia haikomalii kama mwanzo nilienda kumuona story nihilo swala lake mpaka muda unaisha naambulia kurudi namawazo mdogo wake anajua kuna msaada napata kumbe kaka ameshabadilika kweli shetani achagui mkuyu

Mrekodi sauti kwenye simu yako mkiwa nae au akikupigia na uitumie kama ushahidi. Au kama kuna texts anazokutumia pia, zinafaa kama ushahidi. Kuwa makini kwa sababu inaelekea huyo yuko obsessed na wewe, anaweza kufanya kitendo cha kijinga hasa ukirefer kauli yake kuwa ni lazima iwezekane kwa gharama yoyote. Hiyo ni kauli ya mtu asie sawa.
Unaweza pia kuandaa watu ambao watajificha kwenye chumba ambacho utamwita aje ili mzungumzie hiyo proposal yake. Hao watu ndio wawe mashahidi na ikiwezekana akiwa hapohapo, wajitokeze ili awaone na kujua kuwa wamemsikia.
Kingine ni kuwa, wewe nawe una tatizo, hivi ni lazima uishi kwa kusaidiwa tu? Ni kipi hicho usichoweza kukifanya mwenyewe mpaka upate msaada wake huyo? Kwa kukusaidia hivyo, inaelekea yeye amejijengea uhakika kuwa hustahili kwenda kwa mtu mwingine isipokuwa yeye tu, ni kama anajihisi kuwa anakumiliki hivi.
 
Kuna rafiki yangu mmoja alinikutanisha na kaka yake kama mwaka moja sasa kulikua kuna ishu flani hivi akaniambia kaka yake anaweza kunisaidia basi nikashukuru sana.

Uzuri alinisaidia kweli nikaka anaeonekana makini sana kwenye mambo yake.

Na ni very strictly namuheshimu kama kaka kama baba naajua namuheshimu na ni mtu anayependa kunionya mengi nakunihasa sana huwa namuona nizaidi yakaka wakati mwingine.

Sasa chakushangaza sasa hivi ananitokea sikutegemea kabisa nasiwezi, nasitoweza, namuheshimu mno .

Kila mara huwa nampotezea najifanya simuelewi lakini yeye ndio kwanza yupo serious naogopa kumwambia rafiki yangu maana hataweza kuamini kabisa maana kama kukutana na totoz anawaona wengi na wala hana tyme.

Sasa leo hii nikimwambia sinitaonekana mzushi, nikijidai kumkaushia anakuwa mkali kwa mdogo wake ambae ni rafiki yangu.

Hadi ananiamba kwanini kaka anakupigia hupokei amekwambia umpigie sasa. Mimi naona aibu kwavile namuheshimu mno yeye ananiambia maneno mazito mazito kwenye simu naona aibu sana.

Hivi wanaume mkoje hamna cha dada kwanini msiwe na heshima mkiheshimiwa?

Na hapo kakuheshim sana akaamua kukupa airtime ya kukutongoza, maana alikuwa pia na uwezo wa kukubaka kwa jinsi ulivojipeleka kwake na njaa zako.
 
pole sana mdogo wangu, mweleze kwamba hicho kitu hakiwezekani kisha achana nae,poteza mawasiliano nae kabisa
 
Back
Top Bottom