Nilimuheshimu sana kama kaka, leo hii ananitaka

Nilimuheshimu sana kama kaka, leo hii ananitaka

Loly

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Posts
522
Reaction score
232
Kuna rafiki yangu mmoja alinikutanisha na kaka yake kama mwaka moja sasa kulikua kuna ishu flani hivi akaniambia kaka yake anaweza kunisaidia basi nikashukuru sana.

Uzuri alinisaidia kweli nikaka anaeonekana makini sana kwenye mambo yake.Na ni very strictly namuheshimu kama kaka kama baba naajua namuheshimu na ni mtu anayependa kunionya mengi nakunihasa sana huwa namuona nizaidi yakaka wakati mwingine.

Sasa chakushangaza sasa hivi ananitokea sikutegemea kabisa nasiwezi, nasitoweza, namuheshimu mno.Kila mara huwa nampotezea najifanya simuelewi .

Lakini yeye ndio kwanza yupo serious naogopa kumwambia rafiki yangu maana hataweza kuamini kabisa maana kama kukutana na totoz anawaona wengi na wala hana tyme.

Sasa leo hii nikimwambia sinitaonekana mzushi, nikijidai kumkaushia anakuwa mkali kwa mdogo wake ambae ni rafiki yangu.Hadi ananiamba kwanini kaka anakupigia hupokei amekwambia umpigie sasa.

Mimi naona aibu kwavile namuheshimu mno yeye ananiambia maneno mazito mazito kwenye simu naona aibu sana.

Hivi wanaume mkoje hamna cha dada kwanini msiwe na heshima mkiheshimiwa?
 
Ameoa?kama hajaoa namshauri akaze buti tu soon utalainika,hamna mkate mgumu mbele ya chai.

Ameoa ila yupo single kwa sasa, ile heshima ndio najiuliza haoni?? Akiwa namdogo wake ananiheshimu mdogo wake akisogeza tuu mguu anaanza kuniambia maneno yaajabu namimi najikaysha kama simuelewi sasahivi anaongea maneno makali kabisa hadi najuta
 
Ameoa ila yupo single kwa sasa, ile heshima ndio najiuliza haoni?? Akiwa namdogo wake ananiheshimu mdogo wake akisogeza tuu mguu anaanza kuniambia maneno yaajabu namimi najikaysha kama simuelewi sasahivi anaongea maneno makali kabisa hadi najuta


Kwani wewe una mpenzi??
 
Mmmh mueleze jinsi ulivyomchukulia na wasi wasi unaouona mbeleni mara nyingi mwishoni huwa ni pagumu kutabiri. Umesema ameoa na yuko single kwa sasa kivipi??
 
Back
Top Bottom