Ngoja ni kwambie dada angu, huyo mwanaume siku ya kwanza tu alipo kusaidia tayari ulikuwa kwenye hesabu zake, wanaume ni waoga na alikuwa anatafuta mazingira sasa naona amediriki kukwambia na hapo hawezi kuacha kupress. halafu wewe umekosea, wewe ndiye uliye yaendekeza kwa kuonyesha sitaki nataka bila kuwa na msimamo halisi halafu unakuja kulalamika huku, ungetaka yaishe bila ya yeye kuendelea na mbakie kuheshiana alipokutokea tu ulitakiwa utafute mda mzuri umueleze msimamo wako na namna unavyo muona kama kaka, najua yangeisha vizuri na mungeendelea kuwa marafiki.
ila hujachelewa bado unaweza mkalisha kikao mkaongea vizuri bila kumwaibisha yataisha.
Tatizo la vijana wa sasa hivi dadangu si wawindaji, muwindaji kama mimi nilivyofundishwa na wazee unatakiwa uende porini mbali usiko fahamika katafute wanyama huko! wanaume wa sasa ni mapaka shume kama linalogeuka na kuanza kula vifaranga vya nyumbani badala ya kwenda kuwinda panzi na ndege porini! wanaume wa sasa wanatamani vya kunyonga, wanatamani shemeji zao, dadazao, mahousegirl, binam etc. impact yake heshima huisha nyumbani wadada wanamdharau baba kwa sababu ameshawahi waomba, hata wewe unaweza dhihirisha jinsi ulivyo mshusha baada ya kukutokea. wanaume wenzangu tubadirike.