Ni Zanzibar ipi wanaitaka?

Mzee Mwanakijiji,
Umesahau Zanzibar ya John Okello ndio ya Mapinduzi kabla ya Muungano!

hapo napo kwenye bold ndipo lilipo bomu la kuwagawa hawa jamaa (Pemba na Unguja), Wapemba mpaka kesho hawayakubali kabisa haya mapinduzi kwa sababu yamewatenganisha na Ndugu zao wengi, lakini kwa wa unguja hayo mapinduzi ulikuwa ni ukombozi wa kuwapa usawa na haki kwa wote

kitu cha pili ambacho ningependa kuchangia ni kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwa muungano kuvunjwa na watu wa BAra, maana asilimia kubwa ya wabara wamechoshwa na kelele za tunataka nchi yetu, inafikia point wa Bara wanaanza kuhoji faida za muungano wakati hiyo haikuwa desturi yao,
 
... sipendi kweli mazingaombwe na ujanja ujanja.. !

Mbona siku moja zamani ulitunduka mada kuhusu Nyerere kufufuka na hotuba yake aliyoitoa baada ya huko kufufuka...nikaifungua kwa shauku kumbe ulikuwa wewe mwenyewe umeiigilizia sauti yake....

Lol...wewe bana aaah eti hupendi ujanja ujanja....
 
well.. u got me patna! Ila labda niseme sipendi kutawala kiujanja ujanja..
 
Ishu ya Zanzibar iko very complicated na kama ilivyo maswala mengi ya kisiasa ni vigumu kujua nia na madhumuni haswa ukiwa nje una angalia ndani. Una lishwa chakula ambacho huji kipe pikwaje na kama tujuavyo hata chakula chenye sumu chaweza kuwa na ladha tamu. Sasa kama hujui kime pikwaje hata uambie kina sumu utabisha. Cha kujiuliza hapa ni what's the inside story?

Humu JF kuna Wazanzibari wengi tu na wengi wao ni watoa hoja wazuri (japo ni vigumu kutambua hilo linapo kuja swala la Zanzibar maana ni hisia zaidi ya hoja). Wao wana tetea wanacho ona ni kwa manufaa kwao. Ila swala la kujiuliza ni kwamba interest za viongozi wa Zanzibar ni nini hapa? Je haya mabadiliko ya katiba viongozi (au wasaka madaraka) wana tarajia nini na Mzanzibari wa kawaida ana taka nini?

Ukiangalia historia ya mfano vita (na hapa simaanishi tupo kwenye vita...at least siyo vita ya silaha) wanajeshi walitumwa vitani kwa kuambiwa wana tetea vitu fulani. Mfano ni kwenye crusades the dini ambazo watu walitumwa kupigana wakiambia wana tetea dini zao na Mungu wao bila kujua kwamba hao walio watuma nia yao haikua kutetea dini bali maslahi yao ya kisiasa na kiutawala.

Kwa hiyo my point hapa kwa Wazanzibar ni kwamba sawa waweza wakawa wana tetea kitu ambacho kwa ni kitakatifu lakini wajiulize je ni kweli viongozi wao wana taka kitu sawa na wao? Au wana tumika tu kama wanajeshi na kutolewa kafara? "Chakula" kina pikwa nyuma ya mapazia bila Wazanzibari wenyewe kujua vikolombwezo gani vinaingizwa (japo wengi wata kuambia wanajua). Sawa eventually chakula hicho kitaiva na Wazanzibar wata kila. Baada ya kula ndiyo wata jua nia ya hicho chakula. Ubaya ni kwamba ukisha kula saa nyingine hata uji tapishe sumu haitoki. Ni bora Wazanzibar waanje mapema kuwauliza wapishi wao ni nini haswa kina wekwa kwenye hicho chakula na je kama ni kweli ndiyo chakula waki takacho.

Otherwise bwana tuna watakia kila la heri haswa Wazanzibari wa kawaida ambayo nia zao zaweza kuwa za kweli bila kujua nia za viongozi wao. Politics is a game of tricks. Mwanasiasa mwenye kipaji ana kuaminisha kwamba anacho kitaka yeye ndicho uki takacho wewe na ndicho chenye manufaa kwako. Let's wait and see. Time will tell.
 
Unajua kiini cha uzanzibari kutaka kutambulika unakuwa driven na umaskini unaoendelea huko zanzibar. Wazanzibari wengine maisha yao na maendeleo yamekuwa yakiporomoka kadiri siku zinavyoenda mbele. Pia hata zile ajira walizokuwa wanazitegemea zimekuwa zikiyoyoma kila siku. In short mzanzibari wa kawaida amekosa matumaini ya kuishi nchini zanzibar. Sasa wakivuka barabara kuja Dar wanaona maendeleo kwa kiwango kikubwa kinachopelekea wajione wametengwa na serikali ya muungano.

Niliwahi kuwaambia wazanzibar wamejipanga kulinda rasilimali zao mkaona nawatania sasa mnajionea wenyewe. Na zaidi imepata nguvu baada ya sasa hivi kufahamika kwa uhakika kuwa kuna uwezekano wa zanzibar kukwamuka kiuchumi kama wakiwa kama nchi. Hilo ndio linalopekea wazanzibar kuona hakuna faida yeyote kuwa na muungano na bora waamue kutoka kivyao pengine itawasaidia.

Kuhusu swali la mmwanakijiji Zanzibar ya sasa hivi mzee imebadilika kuliko ulivyokuwa unafikiria au nyerere anavyofikiria. Social division zilizoletwa na waingereza zimeshatoweka hakuna mwarabu wala muhindi wala mswahili. Wapemba wameoa wazanzibar na wazanzibari wameoa wapemba na wamezaana. Kuna mawaziri wengine wahindi na mama au baba zao wengine wahindi. Hivyo basi zanzibar ya sasa hivi si ile zanzibar ya zamani unayoijua wewe. Kuhusu utawala wa zanzibar nje ya muungano hilo swali ni gumu kulijibu kwasababu halijatokea. Hizi scaremongering statements zinatolewa na baadhi ya watu ni za kukemewa kwani swali moja nawauliza wewe ulikuja ukafikiri Uingereza watakuja kuunda serikali ya umoja? Waachiwe waunde serikali yao na maendeleo yao kwani sisi wenyewe Tanganyika tunawaumiza kwa namna moja au nyengine. Wakilikoroga then watajua wao na wananchi wao.
 
hahahah, labda wanaitaka zanzibar iliyofungua kituo cha kwanza cha tv ya rangi, afrika
 
Mkuu Mdondoaji asante kwa jibu lako sasa twende taratibu.

Unajua kiini cha uzanzibari kutaka kutambulika unakuwa driven na umaskini unaoendelea huko zanzibar. Wazanzibari wengine maisha yao na maendeleo yamekuwa yakiporomoka kadiri siku zinavyoenda mbele. Pia hata zile ajira walizokuwa wanazitegemea zimekuwa zikiyoyoma kila siku. In short mzanzibari wa kawaida amekosa matumaini ya kuishi nchini zanzibar. Sasa wakivuka barabara kuja Dar wanaona maendeleo kwa kiwango kikubwa kinachopelekea wajione wametengwa na serikali ya muungano.

Hizo sehemu mbili nilizo highlight mkuu ndizo zime niinterest sana na zinaonyesha kwa kiasi kikubwa nini nilicho taka kusema. Hiyo sehemu ya kwanza ya umasikini mkuu nakubaliana na wewe ndiyo sababu kuu ya haya yote yanayo endelea. Je hapa hauoni kwamba viongozi na serikali ya Zanzibar imeshindwa kuwa letea maendeleo Wazanzibar kwa hiyo wana tumia kisingizo cha kulaumu umasikini huo kwa muungano ili kutwishwa mzigo wa lawama na kuishushia Muungano? Na ndiyo maana nikasema chakula kikipikwa huwezi jua kime pikwaji na mpishi ana nia gani. In short the Zanzibar government has failed to deliver and they have no other excuse to give it's people except to blame it on the Union.

Kuhusu sehemu ya pili mkuu ya kusema wanavuka bahari na kuona maendeleo huku Bara mkuu with all due respect let's be serious. Tanzania Bara ina maendeleo makubwa kiasi gani kiasi cha kuona wao wameachwa sana? Je wakija Bara ni sehemu gani hizo wanazo tembelea maana ina wezekana hawaja fika Manzese, Kariako, Keko au vijijini huko. Isije ikawa wanaishia Posta au Oysterbayna kuona kieneo kidogo tu waka chukulia hiyo ndiyo hali kote Tanzania bara.

Niliwahi kuwaambia wazanzibar wamejipanga kulinda rasilimali zao mkaona nawatania sasa mnajionea wenyewe. Na zaidi imepata nguvu baada ya sasa hivi kufahamika kwa uhakika kuwa kuna uwezekano wa zanzibar kukwamuka kiuchumi kama wakiwa kama nchi. Hilo ndio linalopekea wazanzibar kuona hakuna faida yeyote kuwa na muungano na bora waamue kutoka kivyao pengine itawasaidia.

O.k. fair enough kama hivyo ndivyo wanavyo dhani. Kama wanaona Muungano hauna faida yoyote na wana taka kuwa nchi basi kwa nini wana fall short ya kudai uhuru kamili? Kwa nini waji nga'tenga'te kusema wana taka Muungano na kuirekebisha na wengine mnakuja na kusema Muungano hauna maana na mna taka nchi? Hapa ndipo ninapo sema wananchi na viongozi mna nia tofauti hamjui tu maana wananchi wanasema wana taka Zanzibar nchi na Muungano hauna manufaa lakini huto sikia kiongozi wa Zanzibar hata mmoja akiwa that direct.
 
hahaha duh umenikumbusha.. nilishasahau maana BinMgen anaitaka hiyo! Itabidi sijui wamjengee mnara wa kumbukumbu Field Marshall Okello?

Hakuna kitu kiliwahi kuniachia maswali mengi kichwani kama historia ya huyu Mganda Field Marshal Okello na mchango wake katika mapinduzi ya Zanzibar na jinsi alivyoachwa solemba.Ujasiri wake na mkwara aliokuwa nao wa kutamba nchi zote tatu za Afrika mashariki.....hadi Zanzibariiii!! Mkjj, na wengineo wenye kujua undani wa hii ishu naomba mnipatie ilmu zaidi maana nilivutiwa kujua zaidi.Nitaomba ukiweza uanzishe thread mpya on this.
 
Labda wanaitaka Zanzibar hii !

mapzanzibar.gif
Sultanate of Zanzibar !
Kaazi kweli kweli !
 
mimi kwa mtazamo wangu naona kabisa kama wanajitutumu tu hasa kwa pupa
maana tangu asili Wazanzibar hawajawahi kuwa na maendeleo zaidi ya waliyo nayo, tena pengine wana afadhali na muungano kwa mtazamo unaweza kuona kuwa hauwanufaishi,
kinacho waangusha zaidi hawa jama mpaka wajione kuwa wametengwa ni ile tabia yao ya asili ya
kutokuwa na umoja wao kwa wao na kujipanga kuviendeleza visiwa na maisha yao,

nijamii ya watu wanaopenda kukaa saana vijiweni, mfano kule Kisonge n.k na kucheza mabao na
kuendekeza majungu na ughafidhuna juu ya asasi zao wenyewe, kupaka hina mabarazani
na mambo mengi ambayo kwa kweli ni ya kizamani siku hizi mtu ni kujikuza kiuchumi yeye
binafsi kwa kujituma zaidi,

hawa wabara hata kama wamepiga hatua hawakupewa mitaji ama kuongezewa nguvu na
serikali ya muunguna zaidi ya kujituma kufanya kazi, kujiendeleza kielimu mpaka baadhi yao kujiinua kiuchumi na kisha kuijenga baara yao,

majungu na ujinga tu ndivyo vilivyo irudisha nyuma Zanzibar, wala si kwa sababu ya kujiingiza kwenye muungano, humo kwenye muungano ndimo ambamo wamepata ahueni kwa namna flani, na kkujitambua kuwa wao ni wazanzibar.
 
Unajua kiini cha uzanzibari kutaka kutambulika unakuwa driven na umaskini unaoendelea huko zanzibar. Wazanzibari wengine maisha yao na maendeleo yamekuwa yakiporomoka kadiri siku zinavyoenda mbele. Pia hata zile ajira walizokuwa wanazitegemea zimekuwa zikiyoyoma kila siku. In short mzanzibari wa kawaida amekosa matumaini ya kuishi nchini zanzibar. Sasa wakivuka barabara kuja Dar wanaona maendeleo kwa kiwango kikubwa kinachopelekea wajione wametengwa na serikali ya muungano.

kaka sikubaliani na wewe kuwa umasikini wa wazanzibar umeetwa na watu wa bara, hii ni sawa na CCM inavyowafanya watanzania kuhamini kuwa umasikini tulio nao ni wakuzaliwa, Kwahiyo basi zitakuwepo sababu nyigine za huo umasikini wao na kwangu mimi ipo wazi kuwa sababu ni UTAWALA MBOVU WA CCM NDIO UMEWEAFIKISHA HAPO WAZANZIBARI.

Niliwahi kuwaambia wazanzibar wamejipanga kulinda rasilimali zao mkaona nawatania sasa mnajionea wenyewe. Na zaidi imepata nguvu baada ya sasa hivi kufahamika kwa uhakika kuwa kuna uwezekano wa zanzibar kukwamuka kiuchumi kama wakiwa kama nchi. Hilo ndio linalopekea wazanzibar kuona hakuna faida yeyote kuwa na muungano na bora waamue kutoka kivyao pengine itawasaidia.

Kuhusu swali la mmwanakijiji Zanzibar ya sasa hivi mzee imebadilika kuliko ulivyokuwa unafikiria au nyerere anavyofikiria. Social division zilizoletwa na waingereza zimeshatoweka hakuna mwarabu wala muhindi wala mswahili. Wapemba wameoa wazanzibar na wazanzibari wameoa wapemba na wamezaana. Kuna mawaziri wengine wahindi na mama au baba zao wengine wahindi. Hivyo basi zanzibar ya sasa hivi si ile zanzibar ya zamani unayoijua wewe. Kuhusu utawala wa zanzibar nje ya muungano hilo swali ni gumu kulijibu kwasababu halijatokea. Hizi scaremongering statements zinatolewa na baadhi ya watu ni za kukemewa kwani swali moja nawauliza wewe ulikuja ukafikiri Uingereza watakuja kuunda serikali ya umoja? Waachiwe waunde serikali yao na maendeleo yao kwani sisi wenyewe Tanganyika tunawaumiza kwa namna moja au nyengine. Wakilikoroga then watajua wao na wananchi wao.

Pia hapa sikubaiani na wewe Mbaya wao si WATANGANYIKA mbaya wao ni Serekali walio nayo ya CCM ambayo imewafanya wawe wabaguzi na huku ikiwatumbukiza kwenye umasikini.
 
mimi kwa mtazamo wangu naona kabisa kama wanajitutumu tu hasa kwa pupa
maana tangu asili Wazanzibar hawajawahi kuwa na maendeleo zaidi ya waliyo nayo, tena pengine wana afadhali na muungano kwa mtazamo unaweza kuona kuwa hauwanufaishi,
kinacho waangusha zaidi hawa jama mpaka wajione kuwa wametengwa ni ile tabia yao ya asili ya
kutokuwa na umoja wao kwa wao na kujipanga kuviendeleza visiwa na maisha yao,

nijamii ya watu wanaopenda kukaa saana vijiweni, mfano kule Kisonge n.k na kucheza mabao na
kuendekeza majungu na ughafidhuna juu ya asasi zao wenyewe, kupaka hina mabarazani
na mambo mengi ambayo kwa kweli ni ya kizamani siku hizi mtu ni kujikuza kiuchumi yeye
binafsi kwa kujituma zaidi,

hawa wabara hata kama wamepiga hatua hawakupewa mitaji ama kuongezewa nguvu na
serikali ya muunguna zaidi ya kujituma kufanya kazi, kujiendeleza kielimu mpaka baadhi yao kujiinua kiuchumi na kisha kuijenga baara yao,

majungu na ujinga tu ndivyo vilivyo irudisha nyuma Zanzibar, wala si kwa sababu ya kujiingiza kwenye muungano, humo kwenye muungano ndimo ambamo wamepata ahueni kwa namna flani, na kkujitambua kuwa wao ni wazanzibar.

Serekali ya mapinduzi ni yakulahumiwa daima kwani hii ndio imewafikisha hapo, wamekuwa wakiwabagua wapemba miaka yote na mimi nawapongeza sana wapemba kwani wakati wanabaguiwa wao waichofanya ni kujituma kwenye biashara na masomo, tunao wengi huku bara na nje ya nchi wapo wanasoma na wengine wanafanya biashara kwa juhudi zao zote mimi sijawahi kukutana na muunguja au hao wanamapinduzi wanaojituma kama wapemba wao waichokaia ni ubaguzi tu, sasa nchi imewashinda wanasingizia muungano mimi nazani waache kutuhandama sisi watanganyika a.k.a wadanganyika kwani yetu wenyewe yanatushinda huku. CCM NDIO MBAYA WAO NA HATA KAMA WAKISEMA CCM INATOKA BARA KAMA WANVYOSEMAGA BASI WAJUE ATA SISI HUKU WEGINE HATUITAKI HIYO CCM NA NDIO MAANA TUNATAFUTA VYAMA MBADALA.
 
..wajuzi wa historia na sheria za kimataifa naomba maoni yenu kuhusu mahusiano na haki za Zenj kwa kisiwa cha Mafia na eneo la Mombasa.

..nimekuwa nikisikia minong'ono kwamba maeneo hayo yaliwahi kuwa chini ya utawala wa Zenj. je, ni nini kilitokea yakaangukia mikononi mwa Tanganyika[mafia] na Kenya[mombasa].
 
Nimekuwa nikifuatilia mjadala huu juu ya Zanzibar uliosababishwa na marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar. Mawazo mengi yameshatolewa, mengine yakirejea nyuma kwenye historia ya Zanzibar na mengine yakiangalia hali ya kisiasa ilivyo hapa nchini, na mgawanyiko wa kijamii ulivyo huko unguja na kijamii, kuwepo au kutokuwepo kwake.

Mimi nataka nitoe mchango wangu kidogo katika masuala mawili, la kwanza ni dhana zinazotumika/au zilizotumika katika katiba na mjadala huu, na pili historia ya nchi inayoitwa Zanzibar na hii wengi wanaojadili wanaiita Tanganyika.

Nianze na dhana: katika mjadala wa marekebisho haya humu JF na kwingineko maneno NCHI, TAIFA, JAMHURI (REPUBLIC), STATE (DOLA) yamekuwa yakitumika. Na wengi wetu tumekuwa tukiyatumia na kuonesha hisia zetu bila kutafakuri mfanano au utofauti wa maana za dhana hizo. Nchi kwa mfano, ni pande la ardhi, lenye mipaka inayotambulika, wenye nchi yao wakaitambua hivyo na majirani zao na walimwengu wengine wakaitambua hivyo. Ukiangalia maana ya dhana hii - pengine tusingekuwa na ubishi sana juu ya Zanzibar kuwa nchi au si nchi - kwa maana hii hapana shaka kuwa Zanzibar ni nchi. Na kwa kuangalia historia, Tanganyika tunayoizumngumzia imekuwa Nchi baada ya ukoloni, kumbuka Berlin Conference, mipaka yake tunayoililia imewekwa na mkoloni. Hapakuwa na Tanganyika kabla ya hapo (wajerumani walipotutawala). Na kama kutawaaliwa na wageni ndio kunatupa nchi, basi Zanzibar imekuwa NCHI awali zaidi ya Tanganyika. Hilo mosi.

Pili, kuna suala la Dola - mamlaka inayotawala katika pande la nchi, mamlaka hiyo ina vyombo vyake ambavyo ni Serikali, Bunge na Mahakama. Sasa tujiulize hapa je Zanzibar ni dola kwa maana hii, tunaweza kubishana pia, lakini kilicho wazi ni kuwa kabla ya Muungano, Tanganyika na Zanzibar zilikuwa Dola kamili zenye mamlaka katika masuala yote ya ndani na nje ya nchi zao pamoja na suala la Uraia. Baada ya Muungano, kinadharia, Tanganyika iliachia mamlaka yake yote na kuikabidhi dola ya Tanzania, na Zanzibar ilikabidhi baadhi tu ya masuala, yale yanayoitwa ya Muungano (yalikuwa 11 1964 sasa yako 22).

Suala la kuachia mamlaka yote au sehemu ni la kawaida katika aina zote za muungano, Mathalani, tukiwa na sarafu moja ya Afrika Mashariki, tutakuwa, kama dola ya Tanzania tumekabidhi baadhi ya mamlaka na maamuzi kuhusu fedha kwa mamlaka ya juu ya Afrika Mashariki (ndio maana kwenye EU baadhi ya nchi kama Uingereza kwa kutaka kubakia na Sarafy yao hawawa sehemu ya Euro japo wao ni wana EU). Hoja yangu hapa ni kuwa hata Zanzibar wanayo dola, japo haina mamlaka juu ya mambo ya siasa za nje, usalama na ulinzi wa nchi, kati yamambo mengine.

Utaifa, nayo ni dhana nyingine, Taifa ni kundi kubwa la watu - wenye historia moja, lugha moja, utamaduni mmoja, uchumi mmoja, na pande la ardhi (nchi) yenye mipaka inayotambulika. Mwalimu alitambua kuwa Tanganyika haikuwa bado Taifa ndio maana akaanza juhudi za Ujenzi wa Taifa, ili sote tulio Tanzania tujihisi kuwa tu Watanzania na tujitambue na kujitambulishaa hivyo. Mradi huu umeachwa na watawala wa baada ya Mwalimu na baadhi ya hoja zinazotolewa ni kielelezo cha kutokukamilika kwa mradi wa Ujenzi wa Taifa.

Hoja yangu hapa ni kuwa hata Watanganyika, kama Mwalimu alivyokuwa akisema, bado si wamoja kwa maana hiyo ya utaifa. Hebu tuvunje muungano halafu tuone. Rwanda pale ile Genocide ilitokeaje (hili ni suala jengine kabisa japo muhimu kwetu kutafakari). Kuna dhan hii nyingine, ya Republic (Jamhuri), hii ina maana ya utawala ambao msingi wa mamlaka yake ni watu na Mkuu wa Nchi ni Rais wa kuchaguliwa na watu. Dhana hii chimbuko lake ni karne nyingi zilizopita ambapo Ulaya kwa sehemu kubwa iliamua, baada ya mapambano makali, vita na mapinduzi kuachana na utawala wa kifalme (ambapo chimbuko la mamlaka haikuwa watu bali mfalme).

Sasa Tanzania, na pengine Zanzibar katika zipo katika hadhi hiyo katika hali halisi. Kweli tunayo Jamhuri Moja ya Muungano wa Tanzania, yenye mamlaka juu ya masuala yote ya iliyokuwa Tanganyika na baadhi ya Zanzibar. Sasa mgogoro uko wapi katika marekebisho haya ya katiba? Kinachojadiliwa ni nini hasa U-Nchi wa Zanzibar, U-jamhuri wake, U-Taifa wake, au U-dola wake? Ni nini haswa kinagomba?

Mara nyingi, katika masuala kama haya watu hutumia 'mtima' na sio akili kufikir, matokeo yake huwa ni kufikia hitimisho zisizo na mantiki ambazo madhara yake huwa yenye gharama kubwa. Rai yangu, marekebisho haya yameleta suala la kutufanya tujadili masuala na mustakabali wa nchi yetu, lakini tukiongozwa na ufahamu usio shaka wa kile tunachokijadili. Vinginevyo tutajikanganya tu.
 
katika miaka ya mwanzo wa 1970s Zanzibar walikuwa na uchumi mzuri zaidi ya bara largely kwa sababu ya bei nzuri ya karafuu katika soko la dunia. Akiba yao ya fedha za kigeni ilikuwa mara mbili ile ya huku bara. SMZ walinda independence ya uchumi wao sana.

SMZ badala ya kuinvest kwenye productive economic ventures ikaingia kwenye ku-invest kwenye vitu vya anasa - ndege ya rais, televisheni ya rangi - zanzibar ilikuwa nchi ya kwanza afrika iliyokuwa na television ya rangi - hata South Africa wakati huo haikuwa na television ya rangi; majengo ya flats za ghorofa etc. Social investment zote hizi zilikuwa hazizalishi mali zaidi.

Bei ya karafuu ikaanza kushuka kuanzia mwaka wa 1977 na pia miti ya karafuu Pemba ikashambuliwa na magonjwa largely because of neglect - walikuwa hawa palilii na pia uvunaji ulitegemea sana vibarua toka bara. Pia nchi nyingine zikaanza kulima karafuu - indonesia etc Uchumi wa Zanzibar ukaanza kudorora - akiba yao ya fedha za kigeni walikuwa wameshaimaliza kwenye matumizi ya anasa na wakaanza kutegemea zaidi mainland.

In the 1980s they opened up a freeport ku-import things from Dubai, singapore etc and to re-export the same to the mainland without paying duty. Hii haikuwa sustainable kwa sababu mainland walizuia hii biashara kwa kuimpose duty - this made their Freeport a white elephant. They then turned to Beach Tourism which is now the mainstay of the economy wakishindana na Malindi Kenya. However if TZ mainland wakianza kufungua beach zake baada ya kuimprove infrastructure kuanzia Lunga Lunga mpaka Ruvuma ni kweli kuwa hii italeta ushindani mkubwa sana kwa biashara ya utalii Zanzibar.

Pia All geological indications are that ukanda wa bahari una gas na sio mafuta. Mafuta yako zaidi kwenye njchi kavu - mkuranga; lindi; mtwara etc. Kwa hiyo kabla hawa jitenga kwa hope ya mafuta ambayo hawana hakika nayo wangefikiria sana.

The important thing about Zanzibar is that they have to recognize kuwa uchumi wao ni mdogo sana na unategemea zaidi hali ya uchumi wa mainland. Wakijitenga lazima wakubali kwa watakuwa nje ya Tanzania na watakuwa treated that way. They cannot have their cake and eat it. K

Uchumi wao ukiwa matatani hawa wanaweza kuanza kwenda kwenye extremist politics na kuchukuliwa na Al Queda!
 
jokaKuu,'
No problem. Zenj na Mombasa na wakati mmoja ukanda wote wa mashariki mwa Tanzania ikiwa pamoja na Kilwa kivinje ilikuwa himaya ya
Sultan wa Oman. Katika majadiliano ya uhuru wa Kenya na kwa kuwa Kenya ingekuwa haina bahari, Uingereza ikakubaliana na Sultan wa Zanzibar, ambaye naye wakati huo alikuwa chini ya British protectorate, kuiweka Mombasa chini ya Kenya mpya, kwa makubaliano kwamba Mombasa itaendelea na utamaduni wake ikiwa pamoja na mahakama ya kadhi. Sasa kama Wazanzibari wanataka kurejesha utawala wa Sultan, najua Kenya hawatarudisha Mombasa. Najua pia Tanganyika haitakubali kusikiliza upupu wa enzi za Zenj empire. jokaKuu, hata Roman Empire ilishaanguka. Hujawahi kusikia mtu anadai maeneo yaliyokuwa chini ya himaya hiyo. Jumamosi njema.
 
JASUSI.....hapo umenena...nchi ambazo zilishindwa ama kuingia mikataba .....kurasa hizo mpya zilizingatiwa na kuheshimiwa .....hata pale utengano mwingine unapotokea pale ndo panapojadiliwa na si kama ilivyokuwa awali....REFER SOVIET DISSINTERGRATION & CHINA/TAIWAN SAGA!
 
Mimi nadhani watakuwa na haki siyo tu kuidai lakini kuichukua kwa nguvu tu. Kwa sababu "Zanzibar" katika historia haijawahi kumaanisha visiwa vya Pemba na Unguja TU!. Zanzibar ilikuwa ni kubwa kuliko visiwa hivyo viwili. Labda ndio maana ningependekezwa nchi hii mpya iitwe "Unguja na Pemba" kama ilivyo "Trinidad and Tobago"
 
Rudieni au wacheni uvivu someni historia kwa kina ,sehemu ya Mombasa ilikodishwa kwa mkataba maalum ambao upo na kwa miaka fulani ambayo ikitimia Kenya itabidi iilipe Zanzibar kiasi fulani ,kitu ambacho hawajafanya.
Madai yatawezekana ikiwa kuna hati zilisainiwa ,je hati hizo zipo au hazipo ?

,,,,...The British took control of Mombasa in 1895, after the sultan of Zanzibar leasedthe town to the British.....!!
 
Sawa, sasa tuwaone na jeshi lenu mje kuziteka Mombasa, Darisalama na Kilwa Kivinje. Si mnataka kujenga himaya? Tuwaone basi.
 
Back
Top Bottom