Ni Zanzibar ipi wanaitaka?

Rejeeni, mwafaka wa Lancaster House kuhusu matayarisho ya uhuru wa Kenya. Suala la Mwambao kubakia sehemu ya Kenya au Zanzibar lilitatuliwa kwa mabubaliano kati ya Sultani wa zanzibar na Kenya!
 
. Kweli tunayo Jamhuri Moja ya Muungano wa Tanzania said:
Mara nyingi, katika masuala kama haya watu hutumia 'mtima' na sio akili kufikir, .

Mgogoro ni kuwa je sheria na taratibu zinafuatwa wakati wa mrekebisho? kuvunja katiba ya URT ili kufuata matakwa ya SMZ ni halali?
Kinachojadiliwa ni nini, labda wangeulizwa baraza la wawakilishi na SMZ, wana majibu nadhani, ndio ''waliyolianzisha''
Kinachogomba ni mambo kufanywa kinyemela, upendo wa kinafiki, na ''changu ni chetu, chako ni chako''.
 
WaZanzibar wanataka iwepo Tanganyika ,ili kukata mzizi wa fitna ,kama akina Kikwete walithubutu kuidai kurudishwa kwa Tanganyika ,sababu hizohizo ndizo zinazotakiwa ili Tanganyike irudi sasa kama mtabaki kuitwa Tanzzania haya ,lakini hapa kinachotakiwa ni kuwepo kwa Tanganyika au tuseme serikali ya Tanganyika.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ,hivi mnaelewa kuwa hakuna Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hili jina limebambikizwa tu na ndio hata mapolisi wamezuka na mtindi wa kubambikiza kesi.

Serikali ya Tanzania ,hili jamani haipo wala haitakuwepo ,huu ni wizi kuwaibia WaTanganyika na WaZanzibar ,hawa ni wezi wachache wanajirahisishia wizi wao,huu ni wizi tu wanaiba mawazo na kuyabadilisha.

Zanzibar wanahitaji uyakinifu ulio wazi ,iwepo Serikali ya Tanganyika na iwepo Serikali ya Zanzibar (Hii kwa bahati nzuri ipo) ,mambo haya ya kuzinguana yawe yamefikishwa mwisho sasa mtachagua kusuka au kunyoa ,kuburuzana kunafikia mwisho ,naamini kabisa ikirudi Tanganyika ndio utakuwa mwisho wa Utawala wa Sultani CCM na wezi arubaini.
 
katika miaka ya mwanzo wa 1970s Zanzibar walikuwa na uchumi mzuri zaidi ya bara largely kwa sababu ya bei nzuri ya karafuu katika soko la dunia. Akiba yao ya fedha za kigeni ilikuwa mara mbili ile ya huku bara. SMZ walinda independence ya uchumi wao sana.

SMZ badala ya kuinvest kwenye productive economic ventures ikaingia kwenye ku-invest kwenye vitu vya anasa - ndege ya rais, televisheni ya rangi - zanzibar ilikuwa nchi ya kwanza afrika iliyokuwa na television ya rangi - hata South Africa wakati huo haikuwa na television ya rangi; majengo ya flats za ghorofa etc. Social investment zote hizi zilikuwa hazizalishi mali zaidi.

Bei ya karafuu ikaanza kushuka kuanzia mwaka wa 1977 na pia miti ya karafuu Pemba ikashambuliwa na magonjwa largely because of neglect - walikuwa hawa palilii na pia uvunaji ulitegemea sana vibarua toka bara. Pia nchi nyingine zikaanza kulima karafuu - indonesia etc Uchumi wa Zanzibar ukaanza kudorora - akiba yao ya fedha za kigeni walikuwa wameshaimaliza kwenye matumizi ya anasa na wakaanza kutegemea zaidi mainland.

In the 1980s they opened up a freeport ku-import things from Dubai, singapore etc and to re-export the same to the mainland without paying duty. Hii haikuwa sustainable kwa sababu mainland walizuia hii biashara kwa kuimpose duty - this made their Freeport a white elephant. They then turned to Beach Tourism which is now the mainstay of the economy wakishindana na Malindi Kenya. However if TZ mainland wakianza kufungua beach zake baada ya kuimprove infrastructure kuanzia Lunga Lunga mpaka Ruvuma ni kweli kuwa hii italeta ushindani mkubwa sana kwa biashara ya utalii Zanzibar.

Pia All geological indications are that ukanda wa bahari una gas na sio mafuta. Mafuta yako zaidi kwenye njchi kavu - mkuranga; lindi; mtwara etc. Kwa hiyo kabla hawa jitenga kwa hope ya mafuta ambayo hawana hakika nayo wangefikiria sana.

The important thing about Zanzibar is that they have to recognize kuwa uchumi wao ni mdogo sana na unategemea zaidi hali ya uchumi wa mainland. Wakijitenga lazima wakubali kwa watakuwa nje ya Tanzania na watakuwa treated that way. They cannot have their cake and eat it. K

Uchumi wao ukiwa matatani hawa wanaweza kuanza kwenda kwenye extremist politics na kuchukuliwa na Al Queda!

Kwani Zanzibar ilipoingia katika Muungano ilikuwa ikitafuta kukuza uchumi wake??????
Kabla ya hizo karafuu walikuwa na nini???? Hata wakafikiria kuanzisha zao hilo?????
Kwa nini washindwe kubuni mbinu nyengine za kiuchumi ??????

Kwa nini baadhi yetu ya sisi Watanganyika HASA WAKRISTO tunapigania sana huu muungano kwani una faida gani kwetu sisi?????

Hawa si watoto wadogo wamekuwa nasi zaidi ya miaka 40 na wameona wanaangamia si waacheni tu na maamuzi yao????
 
Wanachotaka Wazanzibari ni Zanzibar mpya. Haidhuru na iendelee kuwa ndani ya Muungano, lakini Zanzibar ambayo itakuwa haiminywi, kudharauliwa, na kubezwa ndani ya Muungano huo. Zanzibar itakyojulikana kama Partner katika Muungano huo. Zanzibnar yenye haki na fursa sawia na Patner wake katika Muungano huo. Zanzibar ambayo wananchi wake watakuwa wanajinasibu kwa Uzanzibari wao kwanza, na halafu ndiyo kujieleza kuwa ni Watanzania. Zanzibar yenye mshikamano ambao utadumisha ushirikiano bora na wenzao wa Tanganyika katika kuendeleza Jamhuri yetu ya Tanzania.
 
.......... Na huo Muungano utakuwa ni wa serikali tatu, serikali ya Pemba ambayo itakuwa na support ya arabuni na serikali ya unguja ambayo itakuwa na support ya "Tanganyika

Kwa nini umeona Pemba ndio lazima ipate support ya Uarabuni? Naona wewe huijui historia ya Unguja na Pemba. Unguja kuna Waarabu "asilia" wengi kuliko Pemba, ambapo asilimia kubwa sana wamechanganya. Hata ukiangalia kwa sasa hivi tu misaada ya ndugu kutoka Arabuni ni mingi zaidi kwa upande wa Unguja wakati Wapemba wako hoi wanaendelea kulima karafuu.

If at all kutatolewa misaada basi hao "waarabu" watatoa zaidi huko Unguja kuliko Pemba. Na hao waarabu wanarudisha tu kile ambacho walikivuna huku visiwani, kwani wao wamesoma kwa fedha za karafuu za huku.
 
Kwani Zanzibar ilipoingia katika Muungano ilikuwa ikitafuta kukuza uchumi wake??????
Kabla ya hizo karafuu walikuwa na nini???? Hata wakafikiria kuanzisha zao hilo?????
Kwa nini washindwe kubuni mbinu nyengine za kiuchumi ??????

Kwa nini baadhi yetu ya sisi Watanganyika HASA WAKRISTO tunapigania sana huu muungano kwani una faida gani kwetu sisi?????

Hawa si watoto wadogo wamekuwa nasi zaidi ya miaka 40 na wameona wanaangamia si waacheni tu na maamuzi yao????

Embu kaitafute historia ya Zanzibar halafu urudi hapa !utaona nani ni wakuja hivi kwa kukumegea tu unaelewa kuwa Tanzania ilikuwa pori na watu kama nyie ni wakuja tu mkishukia milima ya na mambonde ya Congo wengine wakitokea Kusini mwa Afrika ,yaani baada ya kuwinda mlipotea na kutojua mtokako na kubaki hapa leo panapoitwa Tz ,angalia ni lini ilianza kuitwa Tanganyika na lini ilianza kuitwa zanzibar.
 
wanataka zanzibar ambayo raisi wake atachaguliwa zanzibar na sio dodoma, na pia raisi ambaye atakuwa na nafasi na heshima ya kiongozi wa nchi katika serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanganyika na sio kuwa waziri tu asiye na wizara maalumu
 
..wajuzi wa historia na sheria za kimataifa naomba maoni yenu kuhusu mahusiano na haki za Zenj kwa kisiwa cha Mafia na eneo la Mombasa.

..nimekuwa nikisikia minong'ono kwamba maeneo hayo yaliwahi kuwa chini ya utawala wa Zenj. je, ni nini kilitokea yakaangukia mikononi mwa Tanganyika[mafia] na Kenya[mombasa].
Utumwa kitu kibaya sana hawa jamaa walitolewa bara kwenda kufanya kazi ya Utumwa leo hii wanasahau asili yao na kutukuza utumwa! naona Somalia ndogo ipo njiani!
 
ni maswali magumu sana kujibika, nasema ni magumu kwa sababu wao 'Wazanzibar' siwamoja, na hawajawahi kuwa na umoja wakiwa nje ya muungano, (Kabla ya muungano), wana matabaka ya Rangi na ujuwaji, kuna kundi la watu ni bora zaidi ya wengine ambao wanaamini asili yao ni arabuni, kwa kuangalia vigezo vingi vya Zanzibar, nadhani itatokea Zanzibar mpya ambayo haikuwepo mwanzo nadhani Hiyo Zanzibar inaweza kuwa JAMUHURI YA MUUNGANO YA ZANZIBAR Namaanisha muungano wa Pemba na Unguja, Na huo Muungano utakuwa ni wa serikali tatu, serikali ya Pemba ambayo itakuwa na support ya arabuni na serikali ya unguja ambayo itakuwa na support ya "Tanganyika", pamoja na hayo huo muungano hautadumu miaka 46 kama ya huu muungano wa Tanzania na mwisho wa siku patakuwa na nchi Mbili ambazo si Zanzibar

Duh! kumbe kuna nchi nyingine zitakuja?
 
Jasusi,

..hili suala, haswa la Zenj na Mombasa, siyo la kuhitaji nguvu za kijeshi.

..nadhani suala hili linaweza kufanana na lile la Bakasi ambapo Nigeria na Cameroun walikuwa wanaigombea.

..suala hili ni la mikataba na sheria za kimataifa na linapaswa kuamuliwa na mahakama ya kimataifa iliyoko The Hague.

..tatizo sina uhakika na facts zilivyo, lakini suala la Zenj na Mombasa ni la miaka ya karibuni sana.

..mwenye kuelewa nini kilitokea mpaka Mafia ikawa sehemu ya Tanganyika, na Mombasa wakapewa Wakenya, naomba tafadhali atueleze.

NB:

..kwa jinsi Maalim Seif na CUF wanavyoitukuza ile Himaya ya Sultani iliyokuwa kinara wa biashara Watumwa, nina wasiwasi kuna siku watakuja kuibua suala hili.
 
Mkuu hii ni songombingo hivi reference line kwa maana ya taifa la Zanzibar ni ipi?
 
Nimefurahi kuwa munajadili Zanzibar ikijitenga. Hivi aliyewambia kuwa zanzibar itajitenga na tanganyika ni nani?. Hivo kudai haki yao katika muungano imekuwa ni noma?. Kama alivyosema mwanasheria mkuu, baraza la wakilishi halijakwenda kintume kabisa bali wamechukua hatua ambayo inawaruhusu kikatiba kabisa.
sisi wazanzibari tumesema tangu mwanzo, NIA yenu twende kwenye serikali moja haikubaliki kabisa na maadamu haikubaliki, tunawahakikishia tu kuwa zanzibar ni nchi kamili na hii nong'o nong'o yenu yakutaka kuiuwa zanzibar imekwisha.Sasa tutakuwa na muungano wa kuheshimiana na sio wa kunyanyasana.
Zanzibar ni nchi kamili licha ya muungano.
 
Ni kweli kabisa tatizo ni muundo wa muungano. Kinachodaiwa sio kuuvunja muungano bali kubadili muundo wake. Kwa ujumla, Wazanzibari wanataka 1 + 1 = 3 na 'Watanganyika' wanataka 1 + 1 = 1. Sasa ili kutatua tatizo hilo Mwalimu Nyerere akaamua kuwa katika kipindi cha mpito kuelekea 1 + 1 + n = 3 + n = Umoja wa Afrika Mashariki basi tutakuwa na hicho tulicho nacho sasa, yaani 1 + 1 = 2. Kwa maneno yake mwenyewe Mwalimu alisema hivi katika kijitabu chake cha UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA:

"Nchi mbili zinapoungana na kuwa Nchi Moja mifumo ya kawaida ya miundo ya Katiba ni miwili: Muungano wa Serikali Moja, au Shirikisho la Serikali Tatu. Kwa mfumo wa kwanza kila nchi itafutwa na Nchi mpya inayozaliwa itakuwa ni Nchi moja yenye Serikali Moja. Katika mfumo wa pili kila nchi itajivua madaraka Fulani ambayo yatashikwa na Serikali ya Shirikisho, na itakuwa na Serikali ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yaliyobaki.
Mambo yatakayoshikwa na Serikali ya Shirikisho ni yale ambayo yakibaki katika mamlaka ya nchi zilizoungamana, basi kwa kweli nchi hizo zitakuwa hazikuungana kuwa Nchi Moja, bali zitaendelea kuwa Nchi Mbili zenye ushirikino mkubwa katika mambo fulani fulani.

Nchi za Afrika Mashariki zilikuwa katika hali kama hiyo kabla ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Zilikuwa Nchi Tatu zenye ushirikiano mkubwa, lakini hazikuwa Nchi Tatu zilizoungana kuwa Nchi Moja yenye muundo wa Shirikisho. Shirikisho halisi la nchi mbili litakuwa ni Nchi Moja yenye Serikali tatu, Serikali ya Shirikisho, na Serikali mbili za awali zilizoungana kuzaa nchi mpya moja.

Tanganyika na Zanzibar zilipoamua kuungana na kuwa Nchi Moja, tungeweza kufuata mmojawapo wa mifumo hiyo ya kawaida. Lakini tulishindwa kufanya hivyo ka sababu ya udogo wa Zanzibar na ukubwa wa Tanganyika. Zanzibar ilikuwa ina watu laki tatu (300,000) na Tanganyika watu milioni kumi na mbili (12,000,000).

Mungano wa Serikali moja ungefanya ionekane kama Tangayika imeimeza Zanzibar. Tulikuwa tunapigania Uhuru na Umoja wa Afrika; hatukutaka tudhaniwe, hata kwa makosa, kwamba tunaanzisha ubeberu mpya! Kwa hiyo mimi nilipinga mfumo wa Serikali Moja. Shirikisho la Serikali Tatu lingekuwa ni gharama kubwa mno kwa Tanganyika. Zanzibar ingeendesha Serikali yake na kuchangia gharama za Serikali ya Shirikisho; na Tanganyika ingefanya vivyo hivyo. Lakini ni dhahiri kwamba mchango wa Tanganyika ndio hasa ungeendesha Serikali ya Shirikisho. Kwa hiyo Tanganyika ingeendesha Serikali yake ya watu 12,000,000 na pia ndiyo ingetoa sehemu, kubwa ya ya kuendesha Serikali ya Shirikisho la watu 12,300,000.

Ni watu wanaofikiri kwa ndimi zao wanaodhani kuwa gharama ya Serikali yoyote kati ya hizo ingekuwa ndogo, hata bila ya mambo yasiyo ya Shirikisho. Na pia gharama zote hizo zingebebwa na Tanganyika.

Kwa hiyo ilitupasa tujiulize kwa nini tunataka kuibebesha Tanganyika gharama zote hizo; na hasa kwa nini tunataka Serikali ya Tanganyika? HIvi tuna hofu ya kwamba Tanganyika, bila ya kuwa na Serikali yake, itaonekana kuwa imemezwa na Zanzibar? Hofu yetu ni kwamba tukiwa na Serikali Moja Tanganyika itaonekana kuwa imeimeza Zanzibar. Basi na tutafute muundo ambao utaiondolea Zanzibar hofu hii ya kumezwa, bila ya kuibebesha Tanganyika mzigo wa kuendesha Serikali mbili zenye uzito unaolingana.

Hivyo ndivyo tulivyofanya, na hiyo ndiyo asili ya ya muundo wa Serikali Mbili. Badala ya kutungua mfumo uliopo kama wapumbavu, tulitazama hali halisi yetu ilivyokuwa, na tukabuni mfumo utakaotufaa zaidi."

katika miaka ya mwanzo wa 1970s Zanzibar walikuwa na uchumi mzuri zaidi ya bara largely kwa sababu ya bei nzuri ya karafuu katika soko la dunia. Akiba yao ya fedha za kigeni ilikuwa mara mbili ile ya huku bara. SMZ walinda independence ya uchumi wao sana.

SMZ badala ya kuinvest kwenye productive economic ventures ikaingia kwenye ku-invest kwenye vitu vya anasa - ndege ya rais, televisheni ya rangi - zanzibar ilikuwa nchi ya kwanza afrika iliyokuwa na television ya rangi - hata South Africa wakati huo haikuwa na television ya rangi; majengo ya flats za ghorofa etc. Social investment zote hizi zilikuwa hazizalishi mali zaidi.

Bei ya karafuu ikaanza kushuka kuanzia mwaka wa 1977 na pia miti ya karafuu Pemba ikashambuliwa na magonjwa largely because of neglect - walikuwa hawa palilii na pia uvunaji ulitegemea sana vibarua toka bara. Pia nchi nyingine zikaanza kulima karafuu - indonesia etc Uchumi wa Zanzibar ukaanza kudorora - akiba yao ya fedha za kigeni walikuwa wameshaimaliza kwenye matumizi ya anasa na wakaanza kutegemea zaidi mainland.

In the 1980s they opened up a freeport ku-import things from Dubai, singapore etc and to re-export the same to the mainland without paying duty. Hii haikuwa sustainable kwa sababu mainland walizuia hii biashara kwa kuimpose duty - this made their Freeport a white elephant. They then turned to Beach Tourism which is now the mainstay of the economy wakishindana na Malindi Kenya. However if TZ mainland wakianza kufungua beach zake baada ya kuimprove infrastructure kuanzia Lunga Lunga mpaka Ruvuma ni kweli kuwa hii italeta ushindani mkubwa sana kwa biashara ya utalii Zanzibar.

Pia All geological indications are that ukanda wa bahari una gas na sio mafuta. Mafuta yako zaidi kwenye njchi kavu - mkuranga; lindi; mtwara etc. Kwa hiyo kabla hawa jitenga kwa hope ya mafuta ambayo hawana hakika nayo wangefikiria sana.

The important thing about Zanzibar is that they have to recognize kuwa uchumi wao ni mdogo sana na unategemea zaidi hali ya uchumi wa mainland. Wakijitenga lazima wakubali kwa watakuwa nje ya Tanzania na watakuwa treated that way. They cannot have their cake and eat it. K

Uchumi wao ukiwa matatani hawa wanaweza kuanza kwenda kwenye extremist politics na kuchukuliwa na Al Queda!

I like this analysis!
Pia wasisahau wafanya biashara wao wakubwa wenye ari na nguvu na kasi ( Wapemba) wamajisimika bara kwa kiwango kikubwa. Wakijitenga itakula kwao! Pia bara ni soko lao na source ya karibu na ya bei poa ya mazao ya chakula ( viazi, mchele, matunda na mboga etc ) hata wakiwa na jeuri ya kusema wata import fom elsewhere bado itakula kwao.
 
Mimi nadhani watakuwa na haki siyo tu kuidai lakini kuichukua kwa nguvu tu. Kwa sababu "Zanzibar" katika historia haijawahi kumaanisha visiwa vya Pemba na Unguja TU!. Zanzibar ilikuwa ni kubwa kuliko visiwa hivyo viwili. Labda ndio maana ningependekezwa nchi hii mpya iitwe "Unguja na Pemba" kama ilivyo "Trinidad and Tobago"
hakuna haja ya kuongeza chumvi...unaonekana unakereka sana wa Zanzibari wakidai haki zao...Kwasababu ,kichwa chako kimejaa kasumba za kwamba Zanzibar ni semehu ya Tanganyika... hili ndio tatizo kubwa hapa, yule mzee Nyeree aliwaharibu sana watu kwa kasumba ambazo imefikia wakati watanganyika kumuona kama nabii... Zanzibar iliungana na Tangayika na sio Tanzania Bara. Wakati ule hapakua na T,bara...
Na hili jina halitambuliki official... Lazima tuuweke ukweli wazi, hakuna Tanzania bara , ipo Tanganyika...tusione aibu kukubali jina letu...Wenzetu wana Zanzibar ,tangu enzi na enzi .
 
Utumwa kitu kibaya sana hawa jamaa walitolewa bara kwenda kufanya kazi ya Utumwa leo hii wanasahau asili yao na kutukuza utumwa! naona Somalia ndogo ipo njiani!

kweli kuna waZanzibari wenye asili ya Tanganyika, lakini hii haina maana lazima wakubali muungano na Tanganyika... ukweli wa mambo ni kuwa waZanzibari ni watu mchanganyiko...Watu wenye asili ya sehemu mbali mbali ikiwemo, India,Iran,Yemen,Oman,Pakistan,Kenya,Uganda,Somali,Ethiopia,Malawi,Zambia na Comoro. Wamekua na utamaduni wao ambao influenced by Islam (brought by Oman)... Wanzanzibari wana ukana muungano kwa sababu za kisiasa,uchumi na maendeleo...Makubaliano ya muungano yamekiukwa na Tanganyika na kuwafanya wazanzibari wapoteze baadhi ya haki zao...Tanzania sio nchi masikini lakini inaongozwa na watu au system ambayo haijali maslahi ya raia wake. Kwahilo Zanzibar wanaona wanaweza kujikwamua kutoka katika janga la umasikini bila ya muungano... kwani huu muungano ndio umekua kipingamizi kikubwa cha maendeleo ya Tanzania yote. Watanganyika wanataka mafuta yawe ya muungano, wakati hizi mali za hapa Tanganyika hakua raia yoyote wa kawaida anaepata faida...Wazanzibar ni kidogo lakini mimi naamini ndio watakao tukomboa sisi waTanganyika... kwasababu ,mabadiliko ya kiuchumi yanaweza kua haraka sana Zanzibar , na hicho ndio kitakacho peleke sisi kudai maendeleo na hawa viongozi kuona aibu.
 
Sawa, sasa tuwaone na jeshi lenu mje kuziteka Mombasa, Darisalama na Kilwa Kivinje. Si mnataka kujenga himaya? Tuwaone basi.

hakuna haja ya ku-panic. Wazanzibar hawataki muunganona Tanganyika, lakini wakikubaliana wanaweza kufanya muungano na Kenya...

haya ni mambo ya makubaliano...WE MISS TREATED ZANZIBARIS ,THAT WAS THE ISSUE...WE TOOK THEM JUST LIKE ANY PART OF TANGANYIKA...ZANZIBAR IS A NATION...We need to learn to accept the facts.
 
Hivi Zanzibar wangependa kuwa na pasi zao za kusafiria kwenda ng'ambo kwa sababu wao ni nchi vile vile na hakuna sababu ya kutumia pasi ya Tanganyika?
 
Hivi Zanzibar wangependa kuwa na pasi zao za kusafiria kwenda ng'ambo kwa sababu wao ni nchi vile vile na hakuna sababu ya kutumia pasi ya Tanganyika?
Mtu mzima wacha ujinga ,hivi kuna pasi za Tanganyika ? au ndio wataka tuburuza sie tusio na pasi ?
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom