Ni Zanzibar ipi wanaitaka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Zanzibar ipi wanaitaka?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 14, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Wanaitaka nchi "yao" ya Zanzibar; Wanataka kurudia "utukufu wa Zanzibar" kwa kuwa hapa walipo sasa hawaoni manufaa "yoyote" kwa Zanzibar. Wanasema wanaitaka nchi yao waliyonyang'anywa na Wadanganyika (ati Watanganyika). Wanataka warudishiwe nchi yao waliyonyang'anywa na Nyerere na watu wa bara.

  Ni Zanzibar ipi hiyo wanayoitaka?

  • Zanzibar ya historia ya kale (Zenj - nchi ya weusi?) ambayo ni zaidi ya visiwa vya Unguja na Pemba bali na mwambao wa Afrika ya Mashariki
  • Zanzibar ya Sultani(ambaye naye utawala wake ulizidi mipaka ya Unguja na Pemba)
  • Zanzibar ya Sultani chini ya Mwingereza
  • Zanzibar ya baada ya Uhuru na Sultani akiwa bado ni Mkuu wa Nchi na serikali ya Mseto
  • Zanzibar ya Mapinduzi kabla ya Muungano
  • Zanzibar "mpya" ambayo haijawahi kuwepo yaani ya baada ya muungano
  Ni ipi hasa wanayoitaka? Ni ipi hasa Zanzibar "proper". Isije kuwa ni kama nchi ya ahadi ambayo iko katika fikra za watu tu lakini haijawahi kuwepo; yaani ile nchi imiminikayo maziwa na asali na kwamba watu wa bara na dunia nzima wanataka kuwanyang'anya Wazanzibari.

  Na labda hapa itabidi tulijibu swali pia kuwa Mzanzibari ni nani hasa?
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Tanzania Visiwani
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Aug 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  msimamo wangu mimi mbona uko vile vile tu... sipendi kweli mazingaombwe na ujanja ujanja.. !
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Aug 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  hahaha na wewe ulipotelea wapi duh!! au ndio umeshatangaza nia?
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Aug 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  ni ipi hiyo sasa na inafafanaje? Kwa hiyo ni Zanzibar mpya sivyo.. isiyofanana na yoyote ya zamani?
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  ni maswali magumu sana kujibika, nasema ni magumu kwa sababu wao 'Wazanzibar' siwamoja, na hawajawahi kuwa na umoja wakiwa nje ya muungano, (Kabla ya muungano), wana matabaka ya Rangi na ujuwaji, kuna kundi la watu ni bora zaidi ya wengine ambao wanaamini asili yao ni arabuni, kwa kuangalia vigezo vingi vya Zanzibar, nadhani itatokea Zanzibar mpya ambayo haikuwepo mwanzo nadhani Hiyo Zanzibar inaweza kuwa JAMUHURI YA MUUNGANO YA ZANZIBAR Namaanisha muungano wa Pemba na Unguja, Na huo Muungano utakuwa ni wa serikali tatu, serikali ya Pemba ambayo itakuwa na support ya arabuni na serikali ya unguja ambayo itakuwa na support ya "Tanganyika", pamoja na hayo huo muungano hautadumu miaka 46 kama ya huu muungano wa Tanzania na mwisho wa siku patakuwa na nchi Mbili ambazo si Zanzibar
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  The ZNZ issue always AMAZES me!
  Sijawahi hata siku moja kuelewa nini kinatakikana na kila mhusika na kwa sababu gani!

  SEHEMU MBILI ZIKIUNGANA/KUUNGANISHWA KISHA IKATOKEA KUWA HAZISHIKAMANI - JE NI VEMA KUONGEZA GUNDI KULAZIMISHIA KUUNGANISHA..AU NI KUANGALIA NI VIPI SEHEMU HIZO ZIBAKIE KIVYAKEVYAKE?

  HUENDA GUNDI IMECHOKA, KUONGEZEA ZAIDI HAKUTATUA SABABU INAYOFANYA GUNDI KUACHIA...
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Aug 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Katiba ya sasa ya Zanzibar ndiyo iliyotumiwa wakati wa baada ya Uhuru 1963?
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Aug 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  umoja unaotokana na chuki dhidi ya muungano? au msingi wa umoja wao ni nini?
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Haaa haaa haaa! Nipo Mkuu, naona ulisahau kuwa kuna Tanzania visiwani kama ilivyo Tanzania bara, katika Serikali ya Muungano. Binafsi ninapenda kuwa na Tanzania Visiwani, ambayo inaundwa na Unguja na Pemba. Zanzibar ni jina la mji mkuu wa Unguja.
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Aug 14, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kama wanataka "wawe huru zaidi" na "kutaka maendeleo yao bila kupitia upande wa pili" maana yake wanataka kuvunja Muungano! Kwa nini wanauma sana maneno?
   
 12. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Duuh, imebidi nikugongee senks! Maana haya ndiyo niliyotaka kuyaandika, lakini naona umeyaandika vizuri zaidi ya ambavyo ningeliandika!
   
 13. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Duuh, Mkuu Kibs, kwa hiyo muungano uliopo ni kati ya Tanganyika, Pemba na Unguja?!
   
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Aug 14, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Kuna contradictions sana katika siasa za Zanzibar leo, hata hivyo kosa kubwa sana ni watanzania wenyewe waliochagua kiongozi goigoi kama JK.

  Wazanzibari wanapopinga Muungano ulioasisiwa na Karume, huwa pia wanapinga mapinduzi yaliyoletwa na Karume kwani yote hayo yalipangwa bila ya kuwapo kwa kura ya maoni. Nilitegemea kuwa pamoja na kuwa tulikuwa na mwanzo mbaya ilikuwa ni jukumu letu kuuonyoosha leo kama ambavyo wakati wa chama kimoja mwaka 1977 ASP na TANU viliungana na kuwa na chama kimoja ili kuondoa tofauti za kisera. Ndoto ilikuwa ni kuwa miaka ijayo tutafikia mahali ambapo tofauti zetu za uzawa zitakuwa hazina maana tena ila tutakuwa tutaangalia utaifa wetu zaidi na kuwa na serikali moja, lakini naona wazi kuwa hili ombwe la uongozi linatupeleka kwingineko.

  Ninavyotabiri, naona kabisa kuwa siyo CCM wala CUF itakayokuwa hai katika miundo yake ya leo hii katika miaka saba ijayo kama haya mabadilioko ya katiba yataendelea.
   
 15. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wacheni wafu wawazike wafu wenzao
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Yap, Baada ya uhuru wa Zanzibar 1963, kulikuwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Unguja. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa ikiandikwa katika nyaraka za serikali hiyo. Baada ya Mapinduzi ndio jina la Pemba likaanza kusikika na kuwa maarufu baada ya Muungano na Tanganyika.
   
 17. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #17
  Aug 14, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa Sheria za sasa neno Mzanzibari limetafsiriwa kama ifuatavyo kulingana na The Zanzibari Act, 1985 (No. 5 of 1985):

  3. (1) Any person who is a citizen of Tanzania in accordance with the laws relating to Citizenship, and that he has been residing in Zanzibar before and up to 12th January, 1964 shall be a Zanzibari.
  (2) Any person who, as from the 26th day of April, 1964 is a Citizen of Tanzania and that he was born in Zanzibar shall be a Zanzibari if both of his parents or his father or his mother is a Zanzibari in accordance with this Act.
  (3) Any person who is a citizen, and that before the 26th day of April, 1964 was a Zanzibari shall be a Zanzibari if he has lost his Tanzanian citizenship.
  (4) Any person who is a citizen of Tanzania and that both of his parents or his father or his mother is a Zanzibari in accordance with subsections (1), (2) and (3) above shall be a Zanzibari.


  Pia kifungu cha 4 cha Sheria husika kinafafanua kama ifuatavyo:

  4. Any person who is a Citizen of Tanzania in accordance with the laws relating to citizenship and:-
  (a) he has been residing in Zanzibar for a consecutive period of fifteen years; and
  (b) he has sufficient knowledge to write and read kiswahili; and
  (c) that he is of good character; and
  (d) that he has lawfully entered Zanzibar and has obeyed all prevailing laws and regulations of Zanzibar; and
  (e) that he is of full age; and
  (f) that he intends to continue residing in Zanzibar, may be eligible to be a Zanzibari.
   
 18. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Sawa, ahsante Kibs! Je, pia kuna mkataba wowote baina ya Unguja na Pemba ili kupata Zanzibar, kama ilivyo Tanganyika na Zanzibar ili kupata Tanzania??
   
 19. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hakuna mkataba wa aina yoyote, zaidi ya historia kuwa Zanzibar visiwa vya Pemba na Unguja, zaidi Zanzibar ilikuwa ni pamoja na kisiwa cha Mafia.
   
 20. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #20
  Aug 14, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Vyema kabisa mkuu Kibs! Labda niulize swali jingine; je, hamna historia yoyote ile kwamba Tanganyika, Pemba, Unguja na Mafia ni wamoja na waweza kuwa jamii moja kama nchi?!
   
Loading...