Wanaitaka nchi "yao" ya Zanzibar; Wanataka kurudia "utukufu wa Zanzibar" kwa kuwa hapa walipo sasa hawaoni manufaa "yoyote" kwa Zanzibar. Wanasema wanaitaka nchi yao waliyonyang'anywa na Wadanganyika (ati Watanganyika). Wanataka warudishiwe nchi yao waliyonyang'anywa na Nyerere na watu wa bara.
Ni Zanzibar ipi hiyo wanayoitaka?
- Zanzibar ya historia ya kale (Zenj - nchi ya weusi?) ambayo ni zaidi ya visiwa vya Unguja na Pemba bali na mwambao wa Afrika ya Mashariki
- Zanzibar ya Sultani(ambaye naye utawala wake ulizidi mipaka ya Unguja na Pemba)
- Zanzibar ya Sultani chini ya Mwingereza
- Zanzibar ya baada ya Uhuru na Sultani akiwa bado ni Mkuu wa Nchi na serikali ya Mseto
- Zanzibar ya Mapinduzi kabla ya Muungano
- Zanzibar "mpya" ambayo haijawahi kuwepo yaani ya baada ya muungano
Ni ipi hasa wanayoitaka? Ni ipi hasa Zanzibar "proper". Isije kuwa ni kama nchi ya ahadi ambayo iko katika fikra za watu tu lakini haijawahi kuwepo; yaani ile nchi imiminikayo maziwa na asali na kwamba watu wa bara na dunia nzima wanataka kuwanyang'anya Wazanzibari. Na labda hapa itabidi tulijibu swali pia kuwa
Mzanzibari ni nani hasa?
Zanzibar inayozungumzwa ni kama ilivyoanishwa na katiba yetu mpya na kama ilivyo katika mkataba wa muungano.Simple as that!
@Kibunango
Nenda kasome tena historia kama unajidanganya kuwa Zanzibar haikuwa nchi ilikuwa ni sehemu ya Tanganyika.Nadhani fuatilia zaidi historia ili ujue taifa la Tanganyika lilianza lini na taifa la Zanzibar lilianza lini.Ukimaliza hapo nadhani utagundua kuwa Tanganyika si nchi yenye natural boarders. Haswa upande wa kaskazini karibu na wamasai utaona ni mstari ulionyooka umepigwa na mzungu na kukata kabila ya la wamasai kati-kati.
Hili la natural boarders ndio haswa tatizo la watu wa Tanganyika kutokufahamu.Hivyo kesi ya mtanganyika kutokukuona umuhimu wa kupotea taifa lake ni logic hapo, kwani taifa lenyewe halikuwapo tokea awali kama si wazungu.
Aidha kwa Zanzibar ni tofauti, hadi leo mimi sitaki hata kusikia neno linaitwa Tanzania.Bado nimebakia mzanzibari, na nitakufa mzanzibari.Huo muungano munaopigia kelele, kwanza nadhani mungelianzia na kutafuta ratification documents kutoka Zanzibar.Mukiweza pata ushahidi huo kuwa Zanzibar ilikubali muungano, then ndio tuendelee hapo.
Lakini kwa Mwanakijiji na wengi ambao ni short-minded, hutaka kuanzia na katiba mara Mapinduzi!.Acheni kujichanganya, Mapinduzi yalifanywa na Nyerere akipatikia watu kutoka pale Tanga kupeleka watanganyika kupindua Serekali halali ya watu wa Zanzibar.
Sasa hapo watakuja wengine na kudai ni dhana za ubaguzi.Naona wengi wenu munazungumza pumba tupu, inawezekana hata hamujawahi kufika Zanzibar.Mumeisoma Zanzibar kwenye kitabu cha Nyerere :confused2:
Anyways, long story short kwa mtazamo wangu Zanzibar haina matatizo yoyote...Wenye matatizo ni watanganyika, na ndio tatizo liliopo.Tokea asubhi Tanganyika inakodolea macho visiwa hivyo kuwa ni sehemu yake...but thats just a dream of yours I guess!