Kite Munganga
Platinum Member
- Nov 19, 2006
- 1,773
- 952
Tafuta ufisadi wake ulio mpya endapo anao, hii tunangoja taarifa ya Mkaguzi wa serikali
Huwa hamkosekani.....utaomba ushahidi sasa hivi.....Hii imekaa kama Mipasho fulani hivi, Mkuu Kevo haya yote ambayo unasema ni tone yalishapita humu labda kama unatukumbushia tuu.
Hivi ni kweli alikuwa anapiga mapanga bili za matibabu?
nimepata info kuwa hatalile CARPET la BUNGENI ambalo lilinunuliwa toka SPAIN alikuwa 10% yake na mbaya zaidi CARPET lilikuwa na bendera ya NCHI ambalo kila siku anaikanyaka
sasay alot about the man right?
sasa kama mytu ambaye yuko heartbeat from Urais ni hivi je kweli twaweza muamini na nchi?
KNasikia hata wakati wa ujenzi wa Bunge alikuwa aningilia mpaka kazi za ma ARCHITECTS kisa hakpata 10%
sasa how do we deal na mtu kama huyu ? maana ukwli ni kuwa hawezi kushitakiwa lakini tunayo freedom ya kuongea au mnasemaje?
Hivi ni kweli alikuwa anapiga mapanga bili za matibabu?
nimepata info kuwa hatalile CARPET la BUNGENI ambalo lilinunuliwa toka SPAIN alikuwa 10% yake na mbaya zaidi CARPET lilikuwa na bendera ya NCHI ambalo kila siku anaikanyaka
sasay alot about the man right?
sasa kama mytu ambaye yuko heartbeat from Urais ni hivi je kweli twaweza muamini na nchi?
KNasikia hata wakati wa ujenzi wa Bunge alikuwa aningilia mpaka kazi za ma ARCHITECTS kisa hakpata 10%
sasa how do we deal na mtu kama huyu ? maana ukwli ni kuwa hawezi kushitakiwa lakini tunayo freedom ya kuongea au mnasemaje?
Hivi ni kweli alikuwa anapiga mapanga bili za matibabu?
nimepata info kuwa hatalile CARPET la BUNGENI ambalo lilinunuliwa toka SPAIN alikuwa 10% yake na mbaya zaidi CARPET lilikuwa na bendera ya NCHI ambalo kila siku anaikanyaka
sasay alot about the man right?
sasa kama mytu ambaye yuko heartbeat from Urais ni hivi je kweli twaweza muamini na nchi?
KNasikia hata wakati wa ujenzi wa Bunge alikuwa aningilia mpaka kazi za ma ARCHITECTS kisa hakpata 10%
sasa how do we deal na mtu kama huyu ? maana ukwli ni kuwa hawezi kushitakiwa lakini tunayo freedom ya kuongea au mnasemaje?
Binafsi nahisi hizo allegations kwa spika ni false. Hasa kwa jinsi unvyo sound..'nasikia'....unasikia toka wapi? Kwa unakitu chenye mshiko mwaga bila konakona, tutaweza elewa.
Spika si ndio alidaiwa kuwa gharama zake za matibabu kwa mwezi Sh.2ml ??? Hawezi kuacha kuwa Fisadi na yeye si uzao ule ule wa Nambari 1??
Hta mimi naona nitasoma vizuri nikiweka bingwa kichwani jioniNimesoma nime elewa lakini sija elewa .Naenda pale bakhresa kutafuta kinywani nirudi cafe .Unasma haya ndiyo maisha ya Samwek Sitta ? Naomba uendelee kumwaga mambo hapa .
Source:MPs' expenses: the demise of Speaker Michael Martin - TelegraphHigh crimes & misdemeanours
October 23, 2000: Elected Speaker amid claims election was stitched up by close friend Gordon Brown
October 30, 2001: Forced to apologise after speaking out in favour of Home Secretary David Blunkett's abolition of voucher scheme for asylum seekers
May 9, 2006: Attacks Press for using the 'hurtful' nickname 'Gorbals Mick'
June 6, 2007: Private Eye says Martin spent £20,000 of public money hiring libel lawyer to challenge negative Press stories
February 17, 2008: Emerges that he used air miles accumulated on official business to fly his children and their families business class
February 23: His spokesman resigns after unwittingly giving 'misleading' details about Mrs Martin spending £4,200 of public money on taxis for shopping trips
March 25, 2008: Speaker's 'shameless' last-ditch legal bid, costing £120,000 of public funds, to cover up MPs' expenses
March 29: Report that refurbishment of Martin's official residence, Speaker's House, cost taxpayer £1.7m over seven years
April 1: Standards Commissioner John Lyon launches sleaze probe into Mrs Martin's taxi trips
November 27: Provokes fury by failing to stop police raiding office of Tory MP Damian Green
May 9, 2009: Report that he claimed £1,400 for chauffeur-driven car trips that included visits to Celtic FC
May 18: Makes disastrous statement apologising for role in expenses fiasco
May 19: Bows to pressure by announcing he will quit on June 21 - first time a Speaker forced out of office since 1695
Sitta achunguzwa
na Happiness Katabazi...TANZANIA DAIMA..28 March 2008
TUHUMA za ufisadi zilizosambazwa katika mtandao wa intaneti zikimlenga Spika wa Bunge, Samuel Sitta, zimesababisha Ofisi ya Bunge kuanzisha uchunguzi dhidi ya kiongozi huyo wa juu wa mamlaka hiyo ya dola.
Taarifa za kuanza kwa uchunguzi huo zilitangazwa na Katibu wa Bunge, Damian Foka wakati alipofanya mahojiano na gazeti hili, ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.
Kwa mujibu wa Foka, madai ambayo atayafanyia uchunguzi ni yale yanayomhusisha Spika na tuhuma za kuwasilisha katika ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Bunge risiti za kughushi za matumizi yake.
Ofisi za Bunge hazina taarifa za Spika kughushi risiti, nipeni muda niwasiliane na wakuu wa vitengo husika, ili tutafute ukweli kuhusu tuhuma hizo, na iwapo tutabaini lolote tutatoa majibu. Ile ni ofisi ya umma na mali zake zinatakiwa zitumike kwa matumizi yanayopaswa na si vinginevyo, alisema Foka.
Pamoja na hilo, Foka alikiri madai yaliyoandikwa katika mtandao wa intaneti yanayoeleza kuwa, Sitta aliwasilisha risiti ya shilingi milioni mbili aliyonunulia dawa kutoka katika duka moja la dawa lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Aidha, alisema baada ya kuwasilisha risiti hiyo, alimwelekeza alete pia cheti cha daktari kilichokuwa kikionyesha kuwa alitakiwa kutumia dawa zenye gharama hizo kutokana na matatizo yake ya kiafya katika kipindi cha wiki moja.
Ni kweli kuwa mwezi uliopita, Spika Sitta alilipwa shilingi milioni mbili katika kipindi cha wiki moja kwa ajili ya kununulia dawa katika duka la dawa la Oysterbay, alisema Foka.
Alisema malipo hayo ni halali kwa sababu Ofisi ya Bunge ina taarifa kuhusu matatizo ya kiafya ya Spika Sitta ambayo hata hivyo hakutaka kuyaweka bayana kwa madai kuwa maradhi ya mtu ni siri yake na daktari wake.
Hata hivyo taarifa ambazo gazeti hili linazo zinaeleza kuwa, Spika amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya miguu ambayo kimsingi ndiyo aliyokuwa akiyatibu kupitia dawa alizonunua katika duka hilo la dawa.
Kuhusu madai kwamba Spika amekuwa akijihusisha katika matumizi mabaya yasiyotambulika kisheria na kikanuni kwa madaraka yake, ya magari mawili ya Bunge aliyopewa kwa shughuli zake binafsi, Foka alisema hana taarifa hizo na kuongeza kuwa uwezekano wa kuwepo kwa jambo hilo ni mdogo.
Wakati Foka akitoa taarifa hizo, maofisa kadhaa wa Bunge waliozungumza na Tanzania Daima wanaeleza kuwa, siku chache zilizopita ofisi ya Katibu wa Bunge ilipata kumhoji Sitta kuhusu kuwapo kwa madai hayo yanayomhusisha na matumizi yasiyofaa ya magari ya umma.
Foka pia alikanusha madai kwamba Ofisi ya Bunge imekuwa ikilipa gharama za umeme na maji kwa baadhi ya watu walio na uhusiano wa karibu na Spika, ambao kimsingi hawastahili kupata malipo hayo.
Pia alikanusha madai kuwa, kamati moja ya kudumu ya Bunge iligundua kuwepo mapungufu katika matumuzi ya fedha yaliyofanywa na Spika, lakini wajumbe wake walinyamazishwa na Sitta mwenyewe baada ya kuwatisha kuwa, iwapo wangeweka hadharani upungufu huo, wangekabiliwa na adhabu ya kunyimwa posho pamoja na kutopangiwa safari za nje.
Akizungumza madai kwamba Sitta amekuwa akilipwa kiasi kikubwa kwa ajili ya safari anazofanya ndani na nje ya nchi, na pia kujilimbikizia deni kubwa linalotajwa kufikia sh milioni 60, Foka alisema anachofahamu, Spika anasafiri nje na huwa analipiwa huduma ya maradhi na nusu ya asilimia 20 ya posho kama fedha za matumuzi na si zaidi ya hapo.
Naye Mkurugenzi wa Elimu ya Umma na Uhusiano wa Kimataifa wa Bunge, Jose Mwakasyuka ambaye alikuwapo wakati Foka akihojiwa, alisema mali za Bunge zipo salama na kwamba tuhuma zinazoelekezwa sasa kwa Spika zina kila dalili ya kuwepo nia ya makusudi ya kumchafua.
Hizi tuhuma ni za kupakana matope na kuchafuliana majina, kwani tuhuma zenyewe hazimtaji nani aliyezitoa. Nadhani kuna watu wanataka waandishi waache kuandika mambo ya msingi kwa ajili ya maendeleo ya nchi na badala yake wajielekeze kwenye tuhuma dhidi ya viongozi, alisema Mwakasyuka.
Hivi karibuni, Spika Sitta alizungumza na gazeti hili kuhusu tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwake na kueleza kuwa, hawezi kuzizungumzia kwa sababu zinatolewa na wahuni wenye lengo la kumchafulia jina lake mbele ya jamii.
Mbali ya hilo, Sitta alilielekeza Tanzania Daima kuwasiliana na maofisa wa Bunge ili kupata ukweli wote kuhusu madai hayo yaliyoandikwa katika mtandao mmoja wa intaneti.
Basil Msongo
Daily News; Sunday,June 01, 2008 @00:01
Spika wa Bunge, Samuel Sitta amesema yeye si fisadi na hana hata senti moja nje ya nchi. Mbali na hilo, Sitta amesema ni vema sasa suala la mgombea binafsi likaamuriwa.
Pia alizungumzia serikali kuwasilisha mapendekezo ya Richmond pamoja na ya uchunguzi wa kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu (BoT) bungeni katika kikao kitakachoanza wiki moja ijayo.
Sitta aliyasema hayo Dar es Salaam jana alipozungumza na watendaji wakuu wa vyombo vya habari, wahariri, waandishi waandamizi, na waandishi wa habari za Bunge ikiwa ni mwanzo wa utaratibu wake wa kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari kila mwezi.
Kiongozi huyo wa Bunge amesema Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali atatoa taarifa kuhusu tuhuma zinazomhusu yakiwamo matumizi mabaya ya fedha za umma. Alisema wabaya wake wamekosa hoja hivyo wameamua kumgonga kwa kutoa tuhuma za kipuuzi za kijamii ikiwa ni pamoja na kuihusisha familia yake.
Sitta alisema anaamini yupo katika mstari mzuri katika kuliongoza Bunge na kwamba wabunge na wananchi katika jimbo lake la uchaguzi wanamuunga mkono. Mimi sibadiliki hata kidogo ..kama tunavyoelewa katika siasa ukiwa unapika kwa kuni usiogope moshi, alisema na kuongeza kuwa katika umri wake, amepita katika changamoto nyingi.
Naamini hata wabunge wananiunga mkono, alisema Spika wa Bunge na akatoa msimamo wake pia kuhusu masuala yanayogusa maslahi ya taifa ukiwamo uamuzi kuhusu kuwapo au kutokuwapo kwa mgombea binafsi, uchunguzi kuhusu wizi wa fedha za EPA na utekelezaji wa mapendekeo ya Bunge katika mkataba wa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond.
Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, alisema kuna haja ya kufikiwa kwa uamuzi wa mwisho kuhusu suala la mgombea binafsi kwa kuwa limeshajadiliwa kwa muda mrefu. Tufike mwisho, tukubaliane au tusema haiwezekani, alisema katika mkutano huo wa kwanza na vyombo vya habari ulioonyeshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha serikali, TBC 1.
Kama jambo limeamuriwa na majaji watatu, na bado hujaridhika, unaweza kukata rufaa likaamuriwa na majaji saba, alisema Sitta akizungumzia suala hilo ambalo serikali imekata rufani Mahakama ya Rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kuruhusu mgombea binafsi katika uchaguzi.
Kuhusu Richmond, alisema atashangaa kama serikali haitawasilisha taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuhusu mkataba huo uliozua utata na kusababisha kujiuzulu kwa mawaziri mawili pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, Februari mwaka huu.
Alisema pia anatarajia kuwa katika Mkutano wa 12 wa Bunge utakaoanza Juni 8, mwaka huu, serikali itawasilisha taarifa kuhusu maendeleo ya uchunguzi wa wizi wa fedha za umma kupitia EPA.
Spika Sitta alisema katika mkutano huo wa bajeti, atatoa uamuzi kuhusu kauli ya Mbunge Nazir Karamagi, kuwa uamuzi wa kuongeza mkataba wa Kitengo cha Makontena katika Bandari ya Dar es Salaam (TICTS) ulifanywa na Baraza la Mawaziri.
Alisema Karamagi amewasilisha ushahidi kwake, lakini isingekuwa busara kutoa maelezo ya suala hilo nje ya Bunge kwa kuwa suala hilo lilizungumzwa bungeni. Sitta alisema katika mkutano huo unaotarajiwa kumalizika Agosti 25, mwaka huu, Ofisi ya Bunge itaanza kuwadhibiti wabunge watoro wakiwamo wanaoingia kusaini asubuhi na kuondoka kisha wanarudi baadaye kuchukua posho.
Kwa mujibu wa Spika, miongoni mwa mipango yake hivi sasa ni kubadilisha jina la Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma kwa kuwa kwa sasa inahusika na mashirika yenye hisa zaidi ya asilimia 50 za serikali, lakini kuna mashirika mengine serikali ina hisa chini ya hizo.
Alisema atakapofanya mabadiliko hayo, kamati hiyo itaitwa Kamati ya Bunge ya Mitaji ya Umma. Spika pia alitetea azma ya wabunge kuongezewa mishahara akisema kuwa kiwango wanacholipwa kinajumuisha mahitaji yao yote zikiwamo gharama za usafiri na mishahara ya madereva.