Implies=> Tumseme Raisi tusimseme Kikwete, Tusimseme Lipumba tuseme CUF, Tusimseme Sitta tuseme Bunge (au Spika wa bunge). Mmmm; ati hapo sijui kuna mantiki ipi unataka kutwambia? The president is Mr. Kikwete, what is a difference between critisizing Kikwete and his Presidency? Bunge la Sita na Sita; wapi na wapi?
Inaonekana kuna mgongano kati ufahamu na hapa ndipo tunapokwama katika kujadili ,ila ndi mjadiliano.
Hao akina Kikwete akina Sita Lipumba ,yako mambo ya kusemwa kwao na ni pale wanapozungumza ndio unaweza kuvaana nao ,kama tunavyomuona Sitta akikingia ubavu wanaoulizwa masuala ya papo kwa pao.
Hapa kunajadiliwa viwango vya mishahara katika vyeo vya kiserikali na si vinginevyo ,mfumo mzima wa mishahara ya serikali na viwango vyake ndio lengo kuu ,katika kuvijadili ,aidha hili halimhusi Kikwete wala Sita au Lipumba na wengine tele.
Vyeo na kima cha mshahara haviendani na hali ya WaTanzania walio wengi ,na hawa tunaowataja wameyakuta na wanayaendeleza pengine na kuyazidisha ,sasa faida ya majadala sio kwenda nao mbali sana ,kinachotakikana ni kujenga hoja nzito ambayo itakubalika kwa wadau ambao ni wananchi wapiga kura.Na nini wanatakiwa wafanye.
Pengine tukaona kwa upigaji kura itatuchukua muda mrefu kusahihisha na kuuondoa ufisadi huu kutokana na ukiritimba wa CCM (Hapa hakuna Kikwete hiki Chama kipo zaidi ya miaka 50 wanapokezana vijiti),nini kifanyike ?
Ni kuushawishi umma wa WaTanzania kuingia mabarabarani kupinga mishahara hii mikubwa ya aina yake ,hii ni kazi ya vyama vya upinzani ,labda hilo itaonekana ni kutaka kuleta fujo.Ila ni njia muhimu kwa siku hizi katika ulimwengu wanyonge kupinga au kuipinga Serikali kutokana na ubadhirifu unaovuka mipaka.
Jengine ni kufanya tathmini kwa nchi majirani hata za Ulaya namna watu kama hawa wanavyolipwa ,ikiwezekana tutafute mshauri muelekezi wa kutufanyia na kutuondolea mirija hii.Ila hili nalo litakuwa la ajabu.
La mwisho ambalo linaweza kuzua mvutano ni kwa upande wa vyama vya upinzani ambacho kitaweza kubeba jukumu la kubadilisha na kupitia upya mfumo wa kiwango cha lala salama kinachotumiwa na Sulatani CCM kulipa wafuasi wake wa ngazi za juu kuwarubuni ili ifanye itakavyo kama tunavyoona ,ukienda mabenki wanakwapua kwa ajili ya Uchaguzi ,wakienda kwenye vyombo vya dola tunaona vinavyotumika,wakienda mahakamani hata kama wanamakosa wanaibuka videdea ,bungeni wabunge wanaunga mkono na Spika anashangalia.
Ingawa bado fedha hio ukiibadilisha kwa dola si pesa kitu labda ile ya raisi kidogo inatia homa na akimaliza utamu wa Uraisi anafungiwa nyingine.Hata hivyo inabidi kwanza tujue International salari inasemaje ,sio tunakwenda mbio tu kama tunaozungumzia private busness,mnaweza mkapanga mkakuta Mkuu wa mkoa inabidi apokee laki moja.